Ilipoishia “Sikia Dokta Simon, naomba hili jambo liwe siri Baina yetu.  Baba yangu asijuwe chochote wakati ambao tunatafuta Figo kwa  ajili ya kunipandikiza” Alisema Osman 

“Naweza kulificha lakini hali yako inaweza ikaniumbua mbele  ya Baba yako, vyote nitafanya lakini vipi kama Jacklin  akazikataa hisia zako huoni kama utakuwa umekula hasara wewe?” Alimuuliza swali gumu sana, Osman alikunbuka namna  tukivyogombana kule Dubai, aliona Swali la Dokta Simon  lilikuwa na mashiko sana. Endelea

SEHEMU YA SITA

“Tuachane na hilo, naomba ufanye siri asijuwe Mtu yeyote na  pia tangaza dau kwa ajili ya kupata figo nyingine” 

“Sawa kama unavyotaka” Alijibu Dokta Simon, Osman alitoa pesa  akampatia Dokta Simon kisha aliondoka hapo na kurudi nyumbani  kwake. 

Mimi nilikuwa nikifanya kazi zangu kama ambavyo Mama alikuwa  amenisihi nifanye ili nisimvunje moyo Osman, nilichapa kazi  hadi mida ya Jioni, muda wa kazi ulipoisha niliondoka nikiwa  nimechoka sana, nilimtafuta Mosses kisha alinielekeza wapi  natakiwa kwenda, nilipitia Benki kabla ya yote, nilitoa kiasi  kidogo kisha nilienda huko. 

Nyumba ilikuwa nzuri sana, ilikuwa kubwa na yenye viunga  vizuri vya kupumzika. Tuliikagua kwa pamoja, pesa  zilizotakiwa kulipwa pale zote zilikuwa ni pesa zilizotokana  na Osman, baada ya kuwa tayari tumemaliza kuikagua, nilifanya  malipo kwa kutumia huduma za kibenki kwa simu. Malipo  yalikamilika, tuliandikiwa mkataba pale kisha zoezi  lililokuwa limebakia lilikuwa ni kununua fenicha zote za  ndani ili nyumbani ipate kuitwa nyumba wanayoishi Watu. 

Baada ya kuona nina pesa nyingi vile Mosses aliniomba pesa ya  mtaji ili afungue biashara, nilimwambia nitampatia baada ya  siku tatu, kuhusu Mosses nilikuwa sikifirii chochote kile  bali hisia za mapenzi ndizo zilizokuwa zikinisukuma kufanya  kila kitu kwake. 

Nilipomaliza kila kitu ndipo nilikumbuka kuwa nilikuwa na  maua ndani ya gari ambayo nilitakiwa kumpatia Osman ili  nimuombe msamaha, basi nilimdanganya Mosses kuwa naelekea  nyumbani, kwa vyovyote asingeliweza kusema anisindikize maana  alikuwa hapatani na Mama yangu. Nilimuacha hapo kisha  niliingia kwenye gari nikawasiliana na Osman, alinielekeza  mahali anapoishi, lengo langu lilikuwa ni kumuomba msamaha  kama ambavyo nilimuahidi Mama, 

Safari ya kuelekea kwa Osman ilianza nikiwa ndani ya gari ya  kukodi, nikifikiria ni jinsi gani nitaongea na Osman ili  nipate kumuomba msamaha. Alionekana kunisubiria sana sababu  alikuwa akinipigia na kuniuliza nilikuwa nimefika wapi,  mwendo wa saa moja na nusu nilifika nyumbani kwa Osman,  alikuwa akiishi kwenye Bonge la Kasri, ndioo niliamini kuwa  Mwanaume huyu alikuwa tajiri sana.

Jumba lilikuwa likiwaka taa nzuri zenye kuvutia sana, ilikuwa  ndiyo mara ya kwanza nafika kwa Osman, nilivuta picha ya  nyumba aliyotununulia japo ilikuwa ya kifahari ila niliona  haiifikii hata theluthi nyumba ambayo Osman alikuwa akiishi,  nilimpigia simu kisha aliwapa taarifa walinzi kuwa kuna ugeni  nje, nilifunguliwa geti kisha gari liliingia mara moja,  ilikuwa ni mishale ya saa moja kasoro. 

Alikuja Mdada mmoja kunipokea, tena alinipokea kwa bashasha  zote kama alikuwa akinifahmu vile, vile nilikuwa muelewa  nilijuwa tu ni kazi yake ya kupokea wageni ndiyo inayomfanya  awe mchangamfu, nilimruhusu dereva aondoke, Mimi pamoja na  yule mdada tuliongozana kuelekea juu ambako Osman alikuwepo,  jumba lake la kifahari lilikuwa la ghorofa tatu tu lakini  lilikuwa la kisasa mno, ilinifanya niwe na hamu ya kumuona  Osman. 

“Osman yupo chumba hiki” Alisema Yule Mdada kisha akaongeza  kwa kusema 

“Ingia tuu” Yule Mdada aliondoka zake, niliangaza huku na  kule kabla ya kufungua mlango huo ambao ulikuwa na kitasa  chenye mg’ao wa Almasi, ilikuwa ni kwenye floo ya mwisho ya  ghorofa. Nilipofungua mlango nilihisi kama nilikuwa nikiingia  kwenye bustani fulani hivi, Osman aliidizaini nyumba yake  mithiri ya Bustan ya Eden. 

Ndani ya chumba hicho kulikuwa na mandhari za kuvutia sana,  hewa safi na upepo mwanana, mwenyewe Osman alikuwa amekaa juu  ya Kiti akicheza na samaki walio kwenye bwawa dogo la  kutengeneza. Aliponiona aliacha kila kitu kisha akaweka macho  yake yote kwangu, najuwa moyo wake ulimwambia kuwa Jacklin ni  mrembo sana, maana alinitazama kutoka juu hadi chini kisha  chini hadi juu kabla ya kunisemesha chochote. Nilitabasamu tu  huku nikiwa nimeficha Mauwa nyuma kwa kutumia mkono wangu wa  kushoto, alinifuata kama vile mzimu, alinisalimia kwa  kuhangaika kama si yeye aliyekuwa akiumwa 

“Ooh Jacklin! Karibu” Yaani Osman aliongea kama zuzu fulani  hivi asiyejuwa nini kinaendelea au kama Mtu ambaye hakuwa na  taarifa kuwa ningefika pale wakati nilikuwa nikiwasiliana  naye kuwa naenda. 

“Asante!!” Nilisema kwa tabasamu murua, Osman alihangaika  kutazama ni wapi tungekaa. 

“Kama hapa si sehemu nzuri tunaweza kwenda chumba kingine  chenye sinema tukaangalia filamu mpya” Alisema Osman

“Hapana Osman hapa pazuri panatosha, hewa yake ni safi sana”  Nilisema 

“Basi tukae pale” Alinionesha mahali ambapo alikuwa  amepaandaa kwa ajili ya Mimi na yeye, hapo palikuwa na meza  ya mawe na viti vya mawe, juu yake kulikuwa na juisi mbili  ambazo ziliwekwa pambo la Ndimu, moyoni nikijikuta nikisema  “Wow” 

Kusema ukweli Osman alikuwa romantic sana, alijuwa nini Maana  ya mapenzi, dakika chache tu za kuwa pale nilianza kuhisi  kumpenda Osman lakini nilimkumbuka Mosses nilisema na moyo  wangu 

“Hapana Jacklin, hapana una Mpenzi” Nilijisemea kisha  nililazimika kufanya haraka, hata sikusogea kuketi  alipopasema bali nilimwambia 

“Osman! Lengo langu la kuja hapa kwanza ni kujuwa  unaendeleaje lakini pili ni kukuomba msamaha kwa kile  kilichotokea jana, haikuwa dhamira yangu. Nimejisikia vibaya  sana tena zaidi ya sana” Nilisema kisha nilimuona Osman  akionesha kama vile tukio la jana halikumuumiza chochote kile 

“Aah usijali Jacklin, yameshapita hata hivyo wala sikuweka  akilini sana, karibu tukae” Alisema Osman, nilitoa mauwa  nyuma yangu nikampatia, alikuwa ameduwaa mithiri ya  Mwendawazimu aliyeona jalala lenye chakula, alikosa hata neno  la kusema, Mauwa ni ishara ya upendo hivyo ndivyo ilivyoingia  katika akili yake 

“Ja…jac…Jacklin” Aliniita kama Mtu asiye na uhakika wa  jina langu 

“Samahani na pia ugua pole” Nilisema kisha niligeuka na  kuondoka nyumbani kwa Bilionea Osman, nikiwa nje nilimuona  akichungulia dirishani wakati huo giza lilikuwa limeingia.  Ilipita Bajaji niliita kisha niliitumia kurudi nyumbani. 

Osman nilimuacha akiwa na furaha ambayo aliipoteza muda  mrefu, furaha ambayo Zahra aliichukua kwake lakini haikuwa  kwamba ndiyo nilikuwa naanza mapenzi na Osman japo  nilimuonesha ishara ya kumpenda, bado akili na mawazo yangu  yalikuwa kwa Mosses. 

Kabla hata sijafika nyumbani Osman alimpigia simu Mama na  kumwambia kuwa nilienda kwake, Mama na Osman walikuwa  wameivana sana kiasi kwamba Mama alikuwa akinitaka niwe na  Osman. Waliongea kuhusu malengo na mawazo yao, nilipoondoka 

Hali ya Osman ilibadirika akakimbizwa Hospitalini, alikuwa  mgonjwa japo ugonjwa wake alikuwa hajausema popote zaidi ya  kwa Dokta Simon. 

Nilipofika nyumbani nilishangaa kwa hali ambayo ilikuwepo  jana kati yangu na Mama yangu, nilistaajabu kumkuta akiwa ni  mwenye furaha sana tena akiimbaimba nyimbo za kabila letu, ni  muda mrefu Mama hakuwahi kuwa kwenye furaha namna hiyo. 

Nililazimika kumfuata na kumuuliza kuliko alikuwa mwenye  furaha sana. 

“Nina furaha sababu Maombi yangu yanaenda kutoa majibu muda  siyo mrefu, nilichokiwaza kinaenda kudhihirika hivi karibuni”  Alisema Mama akiwa bize 

“Mh! Mama uliomba nini na ulikuwa unawaza nini?” 

“Siku zote Mama humuombea Mtoto wake na kumuwazia yaliyo  mema, ni furaha kwa Mama kuona Alichokiwaza kinaenda  kutendekea kwa Mtoto wake” Maneno ya Mama yalinipa tabasamu  japo yalijaa mafumbo, mimi ndiye Mtoto wake wa kipekee  niliwaza atakuwa ameomba nini au kuniwazia nini 

“Mama unaniwazia nini Mwanao?” Nilimuuliza 

“Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, muda  siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendelea  kumuuliza, nilimwambia 

“Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”  Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishi  Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. Hadi  naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana na  kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA Ya PUMZI YA MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

15 Comments

  1. Admin upewe maua yako… unajua bhan…ila t tunaomb isiwah kuish…ivute vute had tuone jacklin na osman wamependan na kuoan

  2. Kwa kweli jack ni muuaji kabisa kupenda gani huko anakompenda Moses mwanaume aliesema bora afe lakini yeye maisha yaendelee kwake

Leave A Reply


Exit mobile version