Ilipoishia “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, muda siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendelea kumuuliza, nilimwambia
“Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu” Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishi Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. Hadi naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana na kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. Endelea
SEHEMU YA SABA
Ila ndani ya moyo wangu nilihisi amani sababu tayari nilikuwa nimeshamuomba msamaha Osman, na pia nilikuwa nimeweka mambo sawa kwa Mama yangu. Siku zilipita, niliendelea na kazi, Mapenzi yangu kwa Mosses yaliendelea bila tatizo lolote tena alikuwa akininyenyekea sana tofauti na mwanzo, kazi ziliendelea kule kwenye kampuni ya Osman, niliendelea kupata uzoefu huku ukaribu kati yangu na Osman ukizidi kuongezeka. Osman alikuwa akiumwa sana ila alikuwa akijikaza mno mbele yangu ila sura yake ilionesha wazi kuwa alikuwa akiumwa, sikutaka kumuuliza sana sababu kama ningekuwa na unuhimu wa kulijuwa hilo angelikuwa ameshaniambia muda mrefu.
Alinipeleka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Nchi, alinifundisha vingi sana Osman. Namna tulivyokuwa tumezoeana kama ikitokea umetuona kwa mara ya kwanza ingekuwa rahisi kuhisi ni wapenzi, Osman alikuwa akijaribu kunionesha hisia zake lakini hakusema kwa kinywa chake, nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa alininunulia gari aina ya Cadilac, aliniandalia kila kitu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa, nilimuarika Mosses kwasababu ndiye Mwanaume aliyekuwa akinipa furaha.
Mama aliniita pembeni, akaniuliza
“Hivi Jacklin unatumia ubongo wako vizuri kuwaza?” Aliuliza kwa sauti ya Juu sababu kulikuwa na kelele za Mziki, wakati huo Watu ndio walikuwa wakifika nyumbani kwetu kwenye hiyo sherehe ya siku ya kuzaliwa
“Mama! Nimefanya kitu gani kibaya?” Nilimuuliza
“Mosses amefuata nini hapa? Hii ni sherehe yako wewe, Osman amefanya kila kitu bado unashindwa hata kumuheshimu?” Alisema Mama ilinibidi nishushe mzuka wangu
“Hivi Mama kwanini tunaishi kwa kuhofia fulani atasema nini? Osman ni rafiki yangu, na Bosi wangu. Kuniandalia sherehe haimaanishi mimi na yeye ni wapenzi Mama, Nitasherehekea vipi siku yangu ya kuzaliwa bila Mosses?” Nilimuuliza Mama
“Huyo Mosses anajulikana na nani? Amekusaidia nini hadi hivi sasa kama siyo kula pesa yako ambayo imetokana na Osman? Jacklin, hujui kilichopo kichwani kwa Osman na hujui kwanini aliandaa hii sherehe yako ya kuzaliwa. Unaiyona ile gari pale? Ile ni zawadi kutoka kwa Osman, huyo Mosses wako anaweza kukununulia japo Pikipiki?” Mama alisema na niliona wazi alikuwa amepaniki.
“Samahani Mama” Nilisema, nilikuwa sipendi kumuona Mama yangu akiwa katika hali ya kuhuzunika kisa Mimi
“Mwambie huyo Mosses aondoke hapa kabla Osman hajafika, Osman ni mfadhili wetu hivyo ni lazima tuheshimu hisia zake” Mama alisema Maneno ya mwisho kisha aliondoka pale, aliniacha na mawazo lukuki sana nikajiuliza maswali mengi ambayo sikuwa na majibu yake
Nikiwa nimesimama alikuja Mosses akiwa ameshikilia glasi yenye kinywaji, aliniuliza
“Mama alikuwa anasemaje? Nimewaona kama mlikuwa mkigombana hivi” nilimtazama Mosses kisha nilitabasamu tu nikamwambia
“Hapana kuna jambo alikuwa ananielekeza ndio tukawa hatuelewani, lakini usijali” nilisema
“Mlisema Sherehe inaanza saa moja usiku, sasa inakimbilia saa mbili, anasubiriwa nani?” Aliuliza Mosses, nilikosa cha kumjibu. Mara zilisikika honi za gari huko nje,
“Wageni hao hebu twende” Nilisema lakini Mosses alinishika mkono akanivuta pembezoni kwenye mnazi. Alitupa glasi pembeni, akaanza kunila mate yangu. Nilishindwa kujizuia nikajikuta namba sapoti Mosses, eneo ambalo sisi tulikuwa tumesimama lilikuwa na mwanga hafifu sana.
Wakati magari yanaingia sisi tulikuwa bize kupeana mate pale kwenye mnazi, bahati mbaya Osman aliangalia tulipo japo hakunitambua kutokana na lile giza. Alikuwa ameingia na Baba na Mama yake, Zilipokuja kuwashwa taa zote ndipo tuliposhtuka tukaacha ule mchezo, ila mashine ya Mosses ilikuwa imesimama. Tuligawana njia, mimi nilipitia upande wangu na Mosses upande wake, nilipowaona Wazazi wa Osman nilishangaa sana sababu wao walikuwa Dubai au inamaana walikuja kwa ajili ya Sherehe yangu ya siku ya kuzaliwa tu au kulikuwa na jambo lililowaleta pale? Nilisimama kwa sekunde kadhaa kabla ya kujitokeza huku bado mawazo yakiwa yananizonga kichwani kwangu, sikuamini Sherehe yangu ya kuzaliwa ihudhuriwe na Bilionea Mkubwa kama Baba yake Osman?
Nilipojitokeza sikuonesha dalili yoyote kuwa nilikuwa nimetingwa na mawazo, nilienda kumsalimia Baba yake Osman, alikuwa akinipenda sana na mara zote alikuwa akisema natembea na kiungo chao japo alikuwa akisema kama utani ila ilikuwa ni kweli nilikuwa natembea na figo ya Osman, tulicheka pamoja, nilipogeuka nilikutana na Mama yake Osman naye alitabasamu, tulisalimiana vizuri sana, ilikuwa ni sherehe ndogo iliyobadilika na kuwa kubwa tena yenye heshima sana hadi Watu tuliowaarika walishangaa. Walinionesha mahali alipo Osman, alikuwa amesimama na rafiki zake, nilienda kumsalimia huku macho yangu yakimtafuta Mosses alipo, Osman alinikumbatia kisha alinishika mkono huku akiendelea kuniuliza maswali ya hapa na pale
Punde shughuli ilianza, Mama yangu sikumuona kabisa licha ya kupepesa macho huku na kule. MC wa shughuli aliniita katikati ya Watu waliokuwa wamesimama, nilitembea taratibu sababu nilivalia gauni refu lenye rangi ya Dhahabu. Nijisifie tu maana ukisubiria kusifiwa hapa Duniani utazeeka, nilipendeza mno.
“Leo ni siku nzuri na nyenye baraka kutoka kwa Mungu, ndugu yetu Jacklin leo ametimiza miaka 28. Bahati ilioje kwake ni kwamba sherehe yake imehudhuriwa na Bilionea ambaye ndiye Baba wa Osman ambaye pia ameandaa shughuli hii kwa ajili ya Jacklin” Alisema MC kisha Watu walipiga makofi mengi sana, bado nilikuwa nikiangaza macho yangu kumtafuta Mosses, bahati nzuri nilimuona akiwa amesimama nyuma akiwa anaangalia tukio lilivyokuwa likiendelea.
Nilitabasamu ili tu mambo yaende ila nilipoteza uwezo wa kujiamini kabisa, MC aliendelea
“Namkaribisha Osman Dhabi aje mbele atuambie siku ya leo amemuandalia nini Jacklin” Makofi mengi yalipigwa, Bilionea Mzee Dhabi naye alikuwa akifurahi pamoja na Mke wake hapo ndipo nilipomuona Mama yangu akiwa amesimama kando ya familia hiyo ya Kitajiri, Mama alinipa ishara ya kukubali kitakachotokea pale, nilishindwa kumuelewa ni kwanini nikubali kwasababu sikujuwa kilichotaka kwenda kutokea. Osman alipofika karibu na Mimi alisema
“Wakati nakutana na Jacklin kwa mara ya kwanza nilimuona ni Mwanamke Msumbufu, asiyejali, mkorofi lakini nilivyokuja kumuelewa niligundua ni Mwanamke wa tofauti sana” Alisema Osman, wote walipiga makofi hata Mimi nilitabasamu maana nilikumbuka jinsi nilivyokutana na Osman kuanzia kwenye Pikipiki hadi kwenye mvua, nilicheka.
“Kwa muda mfupi anenitengenezea kumbukumbu zisizofutika katika Maisha yangu, leo kwenye siku yake ya kuzaliwa nilifikiria ni zawadi gani naweza kumpa ili afurahi, niliona nimnunulie gari aina ya Cadilac escaled ya Mwaka 2021” Shangwe ziliibuka pale, makofi yalipigwa sana
“Gari hii ina thamani ya Milioni 600, ni zawadi ambayo moyo wangu umeridhia kwake lakini pia napenda kumuomba Jacklin” Alisema Osman kisha alipiga magoti akanitazama, nikaiyona ishara kuwa anataka kunivika pete kidoleni, nilishtuka nilipomuona Akitoa pete kwenye mfuko wa koti lake la suti
“Nipe ruhusa niwe Mumeo Jacklin, maneno haya si rahisi Mtoto akayazungumza mbele ya Wazazi wake lakini nimeshindwa kufikisha hisia hizi kwako, nimeona leo ni wakati sahihi wa kufanya hivi” Nilimtazama Osman kama vile nataka kumuuliza maswali ambayo hata sikujuwa niulizaje, nilipogeuza macho nilikutana na Mosses, Mama na Wazazi wa Osman, wote walikuwa kimya kusikiliza nitasemaje. Niliishiwa nguvu jamani
Osman alinishika mkono akawa ananivisha ile pete taratibu, nilikuwa kama Mgonjwa wa koma, ghafla nilishtuka nikasema
“Hapana Osman, siwezi” nilisema kisha niliivua ile pete nikamtupia Osman, Watu walijawa na mshangao mkubwa sana, Chozi lilimbubujika Osman
“Jacklin tafadhali, fanya kwa ajili ya Wazazi wangu nakuomba” Alisema Osman
“Siwezi Osman, siwezi kuidhurumu nafsi yangu, siwezi kuuza upendo wangu Osman, unajuwa fika nina Mtu wangu” Nilisema, Watu walikuwa kimya sana kusikiliza maongezi yetu
“Jacklin, hili ni ombi langu kwako, baada ya hapa sitakuwa na uwezo wa kukuomba chochote tena, tafadhali” Alisema Osman kisha aliushika mkono wangu ili anivishe tena ile pete, nilimsukuma kisha niliondoka pale, nilikimbilia nje kabisa, Mosses alinifuata huko nje, tulichukua Bajaji na kuondoka pale nyumbani. Nilipomsukuma Osman alianguka, hali yake ilibadilika alikimbizwa Hospitalini, Hekaheka ilikuwa kubwa pale nyumbani, Watu walikuwa wakijiuliza kulikoni, Mzee Dhabi alihangaika kwa ajili ya Mtoto wake. Muda mchache watu waliondoka pale nyumbani, alibakia Mama akiwa analia tu, nami nilikuwa nikilia ndani ya Bajaji, siyo kwamba nilikuwa simpendi Osman ila tayari nilikuwa na Mwanaume niliyempenda ambaye ni Mosses.
Nilikuwa nimeshabadilisha hali ya hewa, nililia sana nikiwa ndani ya Bajaji, Mosses alinibembeleza hadi tulipofika kwake.
Tukiwa chumbani aliniuliza
“Nini kinaendelea Jacklin?” Aliniuliza akiwa amekaa pembeni, chozi lilikuwa likinibubujika, nilimuwaza Mama yangu, nilijuwa nimemkosea sana.
“Mosses, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Osman, nimeshangaa ameita wazazi wake kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa istoshe hakuwahi kuongelea kuhusu mapenzi nimeshangaa alipotaka kunivesha pete” Nilisema huku nikiwa najifuta mchozi, simu yangu ilikuwa ikiita sana na aliyekuwa akinipigia alikuwa ni Mama yangu, niliamuwa kuizima kabisa.
“Yule ndiyo amebadilisha Maisha yenu?” Aliniuliza “Ndiyo Mosses, ni yeye”
“Haiingii akilini Mtu aje tu atake kukuvesha pete, lazima kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kati yenu”
“Mosses tafadhali naomba uniamini, nisingelimkimbia kwa ajili yako, ile ni familia ya kitajiri sana. Kama siyo wewe ningelikuwa nimekubali lile jambo ila upo wewe Mwanaume nikupendaye Mosses” nilisema kisha nilimuona Mosses akitafakari jambo, kilio changu kilikata nikawaza labda alikuwa anataka aniache
“Hebu tuliza akili yako Jacklin, kesho asubuhi tutaongea jambo moja” Alisema Mosses, nilipata muda wa kupumzika.
••••••••
Mama yangu hakulala, hakula chakula, alikesha kunipigia simu bila kupokea majibu yoyote. Usiku ulikuwa mwingi ilimbidi aingie ndani, Usiku huo taarifa kutoka maabara zilisema hali ya Osman inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya miezi mwili kutokana na figo lingine kufanya kazi kwa kiwango kidogo sana. Taarifa hii ilikuwa mbaya na isiyopendeza kabisa, Mzee Dhabi na Mke wake walihuzunika sana, walimuuliza Dokta Simon
“Kwanini hukusema kabla Osman hajachukua uamuzi wa kuondoa figo moja?” Ilikuwa ni sauti yenye maumivu sana iliyotoka kwenye kinywa cha Bilionea Dhabi
“Niliongea naye kabla ya kuchukua uamuzi huo, cha ajabu alimuhamisha mgonjwa na kwenda kufanya upasuaji India, aliniomba nisiwaambie chochote kwasababu alikuwa na uhakika wa kupata figo haraka iwezekanavyo. Tukio lililotokea leo siyo tu limemletea mshituko bali mfadhahiko mkubwa ndani yake” Alisema Dokta Simon, Chozi lilimbubujika Mama yake Osman, alikuwa ndiyo Mtoto wao wa pekee hawakubatika kupata Mtoto mwingine
“Laiti kama mioyo ingekuwa inahamishika basi ningehamisha moyo wa Osman, mara zote tuliamini tukimpa pesa nyingi Mtoto wetu itampa jeuri na kuondoa mapenzi katika Moyo wake lakini Osman amekuwa dhahifu sana linapokuja suala la Mapenzi” Mzee Dhabi alimtuliza Mke wake
“Dokta inahitajika huduma gani kwa Mtoto wangu, Hospitali gani Duniani, Pesa Kiasi gani? Nipo tayari kutoa nusu ya utajiri wangu kwa ajili ya Osman” Alisema Mzee Dhabi, Dokta Simon alimwambia Mzee Dhabi
“Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huwezi kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza ni kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili ya upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta Simon
“Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikana Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” Aliuliza Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.
“Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko, tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko wa Osman”
“Unamaanisha nini?”
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
12 Comments
Duh ya moto sana.
Duuuuh….. Si mchezoooo🙆🔥
Hadithi tamu Sana
Pumzi ya mwisho kipande kimoja Ni kitamu sana, ladha haiishi, ongeza viwe viwili kwa siku chief
😊😊 mpka kieleweke
Huyo dada anatia hasira 😤😣😠hv ana akili zote mpuuzi huyoooo
Aise imenigusa sana dah
Hadithi tamu balaaa
Kwan adinimi story unatowa wap mbon kama muvi iv tunaangalia jamani
Admin nikutmie shingap unitmie vipande vyote
😂😂😂
Nzurii