Ilipoishia “Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadi  jioni sawa” Alisema Mama 

“Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauli  ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,  kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama Osman  angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiria  pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwa  kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatu  vyangu. Endelea 

Kumbe yule Mdada msaidizi wa Osman alikuwa akiniangalia tu,  alienda kumwambia Osman, nilitembea kwenye mvua nikiwa  natetemeka, kufika nyumbani kwetu kwa mguu ni zaidi ya masaa  matatu. Kwa jinsi mvua ilivyokuwa ikinyesha ilionesha wazi  kuwa isingelinyamaza kwa muda huo, basi niliendelea kutembea.  Osman alipopata taarifa kuwa natembea kwenye Mvua aliacha  kazi zake, alichukua Mwamvuli akaingia kwenye gari yake  akaanza kunifukuzia 

Ilifika mahali baridi lilinizidia, nilitembea kwa maumivu  makali huku nikimfikiria sana Mosses, kwanini hakunitumia  hiyo pesa? Kwanini alikuwa hapokei simu zangu, nilijikuta  nikilia njiani sababu moyo wangu nilimpa Mosses, niliulaumu  umasikini ambao Baba yangu alituachia, nilimlaumu Mungu  kwanini alimchukua Baba wakati akiwa masikini?

Mara nilisikia Honi ya gari, niliipisha ipite lakini  haikufanya hivyo, alikuwa ni Osman. Nilipogundua ni yeye  niliondoa mikono yangu kifuani, nilitabasamu ili asione kama  kutembea kwenye mvua kumetokana na kutokuwa na hela bali ni  mazoezi tuu. Alishusha kioo akaniambia 

“Ingia kwenye gari nikusogeze Jacklin” Alisema kwa busara na  hekima ya hali ya juu sana, pesa alizonazo Osman hakustahili  kuninyenyekea namna ile 

“Hapana nafurahia maajabu ya Mungu” Nilisema huku nikiwa  napiga hatua huku Osman akiendesha taratibu. 

“Hapana mvua ni kubwa sana Jacklin, twende nikupeleke kwenu”  Alisema tena Osman 

“Usijali Osman, nitachukua Tax mbele, nafurahia mvua kwanza”  Nilisema nikiwa nimeshikilia viatu vyangu mkononi, Basi Osman  alifunga kioo ili aondoke zake, kiukweli hali yangu haikuwa  nzuri, lile baridi lilinitesa sana, njaa ilikuwa ikinikwangua  vibaya mno, nilijikuta nikianguka kwenye mvua. 

••••••••••••••••••••••••••••••••• 

Nilipokuja kurudisha fahamu zangu nilijikuta nikiwa  Hospitali, Osman alikuwa amekaa kitandani, Mama yangu alikuwa  pembeni yangu 

“Mama!” Nilimuita Mama 

“Jacklin Mwanangu, nesi Mwanangu ameamka” Alisema Mama,  alinifanya nitabasamu sana, Upendo wa Mama ulikuwa Mkuu sana  kwangu, niligeuza macho na kumtazama Osman 

“Asante sana Osman” Nilisema nikiwa natabasamu japo  nilipoteza fahamu ila nilijuwa tu aliyenisaidia alikuwa ni  Osman, kabla hajanijibu Chochote nesi alikuja kwa ajili ya  kuangalia hali yangu, Osman alimwambia Mama 

“Naomba tuongee kidogo Mama” Basi Mama na Osman walitoka huku  Daktari akiwa ananiangalia kwa makini na kiniuliza baadhi ya  Maswali ili kujuwa nilikuwa najisikiaje. 

Osman alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo, alimuuliza  Mama 

“Huyu ni Binti yako wa kumzaa?” Mama alitabasamu kisha  alimjibu Osman

“Ndiyo, ndiye Mtoto pekee ninayemtegemea, nakushukuru sana  Baba japo sijakufahamu maana umenipigia tu simu na kunieleza  kuhusu hali ya Binti yangu, kwa jinsi nilivyokuwa  nimechanganikiwa wala sikuwa na muda wa kukuuliza” Alisema  Mama 

“Naitwa Osman, Mimi ndiye mmiliki wa kampuni ambayo Binti  yako alikuja kuomba kazi” Alijitambulisha Osman kwa Mama  yangu 

“Ooh! Asante sana Baba” Alisema Mama 

“Sasa Mama! Pamoja kwamba hali ya Binti yako unaiyona ipo  sawa lakini kuna tatizo kubwa sana katika mwili wake,  inaoneka figo zake zote mbili hazifanyi kazi ipasavyo,  inatakiwa kubadilishwa, kama zitapatikana mbili au moja iliyo  imara sana” Alisema Osman, Mama alishindwa hata kusimama  aliomba akae kwanza, akiwa kama Mama alichanganikiwa sana  kusikia nina tatizo la figo zangu 

“Unasemaje?” Aliuliza Mama akiwa anakaribia kuanza kulia 

“Ndiyo maana Mama nimekuita hapa iliniweze kuzungumza na wewe  kuhusu hali ya Jacklin, ana siku 30 za kufanyiwa matibabu”  alisema Osman 

“Sasa mimi na umasikini huu nitaweza vipi Baba yangu? Mungu  kwanini ananipa mtihani mzito kiasi hiki niimemkosea nini  Mimi?” Alisema Mama akiwa analia, Osman aliketi na kumwambia  Mama 

“Mimi nina safari ya kwenda Dubai kesho, gharama zote  nitazifanya. Mnapaswa kutafuta Mtu wa kumtolea figo Jacklin”  Alisema Osman, angalau Mama alifuta mchozi wake 

“Nitakuunganisha na daktari Bingwa wa hii Hospitali,  mtasaidiana itakapopatikana hata moja imsaidie Binti yako”  Alisema Osman, Mama alimtazama Osman akamwambia 

“Wewe ni Binadamu mwenye moyo wa peke yako Mwanangu, Mungu  azidi kukubariki kwenye kila hatua” Alisema Mama 

“Ila Mama naomba hili liwe siri yako, Jacklin hapaswi kujuwa  kama ana tatizo la figo sababu akijuwa inaweza leta shida  zaidi” Alisema Osman, walipomaliza kuzungunza walirudi  wodini, walinikuta nikiwa ninafakamia vyakula maana njaa  niliyokuwa nikiisikia haikuwa ya kawaida, sura zao  hazikuonesha dalili ya tatizo lolote lile 

“Jacklin!” Aliniita Mama kisha aliketi kitandani

“Kama kuna Binadamu ana roho nzuri katika hii Dunia basi huyu  Kijana ni namba moja, namshukuru kwa kuokoa Maisha yako”  Alisema Mama kisha alitabasamu, kumbe Osman alikuwa  amewasiliana na Mosses na kumwambia kuwa nilikuwa nina umwa  sababu namba ya Mosses nilisave kama Mume wangu, alikuja muda  huo, alinikumbatia na kunipiga busu mbele ya Mama na Osman,  Mama alishangaa sana sabahu alikuwa hamfahamu Mosses 

“Mama!! Huyu anaitwa Mosses, ni..ni…ni” nilishindwa  kumtambulisha Mosses mbele ya Mama na Osman, Basi muda huo  huo Osman aliaga na kuondoka zake 

“Mama huyu ni Mchumba wangu anaitwa Mosses…..Mosses huyu ni  Mama yangu” Nilijitahidi hadi kumtambulisha Mosses kwa Mama  yangu, japo niliona Mama hakufurahia ila alijikaza tu 

“Oooh!! Sawa, basi mpate muda wa kuongea Mimi naenda kwa  daktari” Alisema Mama, kumbe alikuwa anataka kumuwahi Osman  nje, kweli alimkimbilia Osman kabla hata hajapanda kwenye  gari akamuita, alipomfikia alimwambia Osman 

“Baba upo sawa?” Aliuliza Mama 

“Ndiyo Mama nipo sawa, naenda kuendelea na kazi” Alisema  Osman, ila Mama alihisi kuna jambo lipo ndani ya Osman kwa  jinsi alivyoaga pale wodini. 

“Nakuomba Mwanamgu, msaidie Jacklin apone na Mungu atakulipa  zaidi” Alisema Mama, Osman alimsogelea Mama akamwambia 

“Ni jukumu nililokuahidi Mama, Mwanao atarudi kuwa sawa tu  wala usijali, hii hapa ni kadi yangu ya Biashara” alimpatia  Mama kadi yenye mawasiliano yake, Osman aliingia kwenye gari  yake na kuondoka. 

Mosses alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana katika Maisha  yangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu, nilimuuliza 

“Kwanini ulikuwa haupokei simu yangu?” 

“Samahani Mke wangu, unajuwa muda ule nilipatwa na dharura  nikaenda kumuona Mdogo wangu alikuwa ana tatizo” Alisema  Mosses 

“Ooh pole sana, anaendeleaje” 

“Yupo sawa, hivi huyu jamaa aliyekuwa amekaa hapa ni nani?  Mbona baada ya kukupiga busu aliaga?” Aliuliza Mosses

“Mmmh! Jamani Mosses, ni rafiki tu, ndiye aliyenisaidia”  nilimjibu Mosses, kitu kilichokuwa kikinivutia zaidi kwa  Mosses ni wivu wake kwangu, yaani nisisimame na Mwanaume au  kuongea naye 

“Anhaa! Sasa sitaki hayo mazoea na huyo jamaa sawa?” Alisema 

“Mmmh! Sawa” Nilimjibu, Mama aliporudi alitukuta tukiwa  tumemaliza mazungumzo, basi alimuita Mosses pembeni na  kumueleza kilichokuwa kikinisibu sababu alikuwa Mtu wangu wa  karibu sana. 

Mosses alipoambiwa hivi kuwa nina tatizo la Figo alimuuliza  Mama 

“Mama unajuwa matibabu ya Figo yana gharama kubwa sana na  kama hivyo umesema yanahitajika ndani ya siku 30 tu,  itakuwaje? 

“Sasa unafikiria nitafanya nini Kijana? Japo yupo  aliyejitokeza kugharamia matibabu ila hatuwezi kumuachia yeye  kila kitu ndiyo maana nimekueleza na wewe ili nione kwa  upande wako utajitoa vipi maana Jacklin ni wako wewe” Mama  alisema, maneno ya Mama yalijaa uchunguzi sana 

“Mama naomba siku moja ya kutafakari kisha nitakupa mrejesho  wa nini ambacho mimi nitafanya, ila nakuahidi kuwa tupo  pamoja” Alisema Mosses, basi siku hiyo niliruhusiwa kurudi  nyumbani ila nilikuwa nahisi maumivu kiasi fulani kwenye  mbavu zangu, jinsi Mama alivyokuwa akinifanyia kila kitu  ilinitia shaka sana nilimwambia 

“Mama Mimi nipo sawa huna haja ya kunifanyia kila kitu” “Nafanya sababu nakupenda Jacklin” alisema Mama 

“Najuwa kuwa unanipenda lakini nilianguka sababu ya baridi tu  Mama hakuna kingine, nipo sawa” Mama hakusema chochote kile  kuhusu tatizo nililokuwa nalo la figo, siku iliyofuata Osman  alienda Dubai kama alivyomwambia Mama. 

Usiku wa siku hiyo, kilikuwa kipindi cha mvua hivyo kulikuwa  na baridi sana, Mama alikuja na kuniambia kuwa Osman alikuwa  ameshaondoka, ilinishangaza sana namna ambavyo Osman na Mama  awalikuwa karibu kiasi hicho hadi kuanza kujuwa kuhusu safari  

za Osman, nilicheka kwanza 

“Mmh! Mama nawe, yote hayo umeyajuaje? “

“Si kaniambia mwenyewe jana kule Hospitali, alafu Jacklin  ngoja nikuulize swali, unamuonaje Osman?” 

“Mh! Mama hebu liweke vizuri hilo Swali, namuonaje kivipi  tena?” 

“Hujausoma Moyo wake? Hujahisi kitu ndani ya moyo wa yule  Kijana?” 

“Sasa Mama naanzaje kuusoma moyo wa Mtu ambaye sina ukaribu  naye? Alafu hata kama akiwa na kitu moyoni mwake mimi tayari  nina Mtu wangu..” 

“Sijamaanisha eti uwe naye hapana ila nimekuuliza tuu  Jacklin, anaonekana ana upendo sana yule Kijana” Mama  aliendelea kusema mafumbo ila niliijuwa nia yake 

“Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasi  hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyo  nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?” 

“Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniacha  na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbuka  kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya Mosses  kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada ya  kuchukua namba kwenye simu yangu.  

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tatu Ya PUMZI YA MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

 

15 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version