IlipoishiaUnaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huwezi  kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza ni kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili ya  upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta Simon 

“Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikana  Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” Aliuliza  Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao. 

“Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko,  tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko wa  Osman” 

“Unamaanisha nini?”  Endelea 

SEHEMU YA NANE 

“Tumaini la Osman lilikuwa kwa Jacklin, aliweka moyo na akili  yake kwenye tukio la kumvisha pete, ili apone ni lazima  atimize lengo hilo, akili yake haifanyi kazi sawa sawa,  analitaja jina la Jacklin tu” Alisema 

“Oooh Mungu wangu, sasa Binti hamuhitaji Osman, amemkataa  mbele za Watu unafikiria ni rahisi kukubali?” Aliuliza Mama  yake na Osman 

“Hakuna jambo zuri linaloweza kuja kirahisi Mzee Dhabi, wewe  ni shahidi hata kwenye ubilionea wako haukuja kirahisi,  ulihangaika, mtafuteni Jacklin, kama Osman aliweza kuokoa  Maisha ya Jacklin kwa kumtolea figo basi Jacklin aokoe Maisha  ya Osman kwa kukubali kufunga ndoa na Osman” Alisema Dokta  Simon kisha aliongeza 

“Kisaikolojia Osman anahitaji kuona alichokiwaza kinakuwa  kweli, tunaweza kumsaidia kupandikiza figo lakini tukampoteza  kwa mfadhahiko, ni lazima tuuwe ndege wawili kwa jiwe moja” 

“Kwenye hili jambo sidhani hata kama pesa niliyonayo inaweza  nisaidia, nitajaribu kufanya hivyo Dokta lakini kwa upande  wako hakikisha unafanya kila liwezekanalo zipatikane figo  mbili au moja kwanza” Alisema Bilionea Dhabi kisha waliondoka  Hospitalini sababu hawakuruhusiwa kumuona Osman kwa wakati  huo hadi kesho yake asubuhi. 

Usiku huo ulikuwa ni Usiku wenye Hekaheka sana, Bilionea  Dhabi alimpeleka Mke wake Nyumbani kwa Osman kisha alitoka na  Mlinzi wake akaenda nyumbani kwetu, alihitaji kuniona Mimi. 

Alimkuta Mama akiwa bado yupo macho, ilikuwa ni mishale ya  saa 7 Usiku, Mama alipomuona Bilionea Dhabi alijuwa tu  alikuja kwa ajili yangu Mimi. Waliketi na kuanza kuzungumza,  swali la kwanza alilouliza Bilionea Dhabi lilikuwa

“Jacklin yupo hapa nyumbani?” Aliuliza kwa sauti iliyopoa  sana, Mama alitikisa kichwa kuashiria kuwa sipo nyumbani 

“Tangu alipoondoka ule muda hajarudi tena” Alijibu Mama kwa  sauti iliyopoa iliyojaa maumivu ndani yake 

“Ulijaribu kumpigia simu?” Aliuliza Bilionea Dhabi 

“Amezima simu yake” Alijibu Mama, Bilionea Dhabi alishusha  pumzi zake 

“Ulikuwa unamuhitaji? Vipi hali ya Osman?” 

“Hali ya Osman ipo katika hatari sana, Alikuwa na tatizo la  figo moja, figo hilo hilo lililokuwa zima alilitoa kwa ajili  ya kunusuru Maisha ya Binti yako Jacklin, hivyo anakabiriwa  na tatizo la figo na mfadhahiko ambao ameupata baada ya  kilichotokea, anahitajika Binti yako kwa ajili ya kuokoa uhai  wa Osman” Alisema Bilionea Dhabi 

“Jacklin anatakiwa kulitoa hilo figo ampe Osman?” Aliuliza  Mama huku akiwa mwenye wasiwasi sana 

“Hapana, anatakiwa kuondoa mfadhahiko wa Osman vinginevyo  tunaweza kumpoteza. Jacklin anatakiwa kukubali kuolewa na  Osman ili Osman aamke tena” Alisema Bilionea Dhabi 

Mama alikuwa kinywa wazi kwa alichokisikia, alishusha pumzi  zake alizozivuta kwa mkupuo. 

“Kwanini Maisha yananipa machaguo magumu hivi? Jacklin uko  wapi Mwanangu” alijiuliza Mama yangu. 

Muda huo nilikuwa nimekumbatiwa na Mosses ambaye alikuwa  ndiyo Mwanaume niliyempenda sana. Akili yangu ilikuwa  ikimuwaza sana Mama yangu sababu ndiye Mzazi pekee aliyenizaa  na kunilea kwa shida sana, kwa ajinsi anavyonipenda kwa  vyovyote atakuwa analia Usiku kucha, nilimuamsha Mosses  nikamwambia 

“Nahisi Mama ananiita Mosses” Nilisema nikiwa nimekaa  kitandani 

“Unahisi anakuita kwani wewe ni jini au, unaweza kuhisi jambo  ambalo huna uhakika nalo, jinsi ulivyoondoka pale unafikiria  Watu wanakuchukuliaje? Bado wana hasira na wewe Jacklin hebu  tulale” Alisema Mosses, basi nilijilaza kitandani.

Sikujuwa kilichokuwa kinaendelea huko nje, sikujuwa kuhusu  hali ya Osman na jinsi ambavyo Mimi nilikuwa nikitafutwa na  Familia ya Bilionea Dhabi, Asubuhi Mapema nilimuuliza Mosses  alikuwa anataka kuniambia nini kutakapo pambazuka, alikuwa na  usingizi hivyo nilimuacha alale hadi atakapo amka, Mama na  Bilionea Dhabi walinitafuta kila kona bila mafanikio yoyote,  hakuna aliyekuwa anapajuwa mahali ambapo Mimi na Mosses  tulikuwa tumepanga nyumba 

Mosses alipoamka tuliketi ili tuongee, Mosses alinipa wazo la  kuacha kazi kwa Osman kwasababu pesa ilikuwepo kisha  aliniambia kuwa tuishi pamoja kama Mke na Mume tena  ikiwezekana tufunge ndoa haraka sana ili kumkata tumaini  Osman, wazo lake lilikuwa zuri ila nilimuwaza sana Mama  yangu, alikuwa akinipenda sana na kwa vyovyote alikuwa akilia  tu, nilishusha pumzi nikamjibu Mosses 

“Najuwa unanipenda nami nakupenda sana Mosses, kufunga ndoa  na kuishi na wewe ni jambo zuri na ndiyo ndoto yangu ila  nikimfikiria Mama yangu huko alipo naishiwa nguvu. Naomba  niwashe simu kwanza” Nilisema, Mosses alinisogezea simu  yangu, niliiwasha, ilikuwa ni majira ya saa mbili asubuhi  njua angalau siku hiyo lilikuwa limechomoza maana kilikuwa  kipindi cha masika, jua lilikuwa likionekana kwa nadra sana 

Sekunde chache za kuwasha simu ziliingia meseji nyingi sana,  papo hapo Mama alinipigia simu. Mosses alikuwa amekasirika,  nilipomtazama aliondoka pale chumbani. Niliisikilizia simu ya  Mama kwa sekunde kadhaa kisha niliipokea, niliisikia sauti ya  Mama akiwa analia akiniuliza nipo wapi tena alikuwa  akiniuliza kwa kilugha chetu, ilitosha kutambuwa kuwa Mama  yangu alikuwa katika hali ya huzuni sana 

“Mama nipo” Nilisema 

“Upo wapi Jacklin, kwanini unanitesa Mama yako?” Aliuliza  Mama akiwa analia, taratibu chozi lilikuwa likinidondoka  kwenye macho yangu. 

“Mama usilie sasa Mimi nipo salama tu wala Usijali” Nilisema  huku nami nikiwa ninalia, jinsi ambavyo niliishi Maisha na  Mama yangu ilikuwa ni rahisi sana kuhisi maumivu yake ndani  ya Moyo wangu, niliumia sana kujuwa Mama alikuwa akilia 

“Sasa Jacklin huwezi hata kunionea huruma Mimi Mama yako?  Nimehangaika tokea jana usiku, simu yako ilikuwa haipatikani,  nimekutafuta kila kona bila Mafanikio yoyote, sijala tokea  jana…” nilimkatisha Mama ili asizidi kuongea Maneno ambayo  yangeongeza maumivu katika Moyo wangu, Jamani Mama alikuwa  akilia kwa kwikwi

“Nakuja Mama” nilisema kisha nilikata simu, nilijiinamia huku  moyo ukizidi kuniuma, Mama yangu alikuwa ndiye Mzazi pekee  niliyebakiwa naye, alinilea katika mazingira magumu sana  ambayo yalinifanya nimpende sana Mama yangu. Nilinyanyuka  nikatafuta kibanio cha nywele kilipo, Mara alikuja Mosses  akiwa katika hali ya hasira 

“Unaondoka si ndiyo?” Aliniuliza 

“Ndiyo Mpenzi kwa ajili ya Mama ila nitarudi” Nilimjibu  nikiwa mbele ya kioo nikiwa nabana nywele zangu. 

“Unaenda kuolewa na huyo Mjinga eee?” Aliuliza Mosses,  ilinibidi niache kubana nywele maana nilijuwa ana hasira  zaidi 

“Hapana Mosses! Mama yangu alikuwa akiongea kwa kilio,  nimeumia sana, naenda kuweka mambo sawa ili tufunge ndoa”  Nilisema 

“Sawa nenda lakini kumbuka nina video zako Jacklin, chochote  utakachoamua kufanya nami nitafanya kwa upande wangu” Alisema  Mosses, nilijuwa ni video gani alikuwa akizizungumzia, ni  zile ambazo alinirekodi tukiwa tunafanya Mapenzi 

“Nakuahidi Mosses siwezi fanya ujinga, siyo kwasababu ya  video bali ni kwasababu Nakupenda sana” Nilisema kisha  nilimbusu shavuni nikaondoka zangu. 

Hali ya Osman ilizidi kuwa mbaya alikuwa akiendelea kutaja  jina langu kila wakati, alikuwa akichomwa sindano za usingizi  ndipo anaacha kunitaja. Bilionea Dhabi aliitwa Hospitalini 

Dokta Simon alimueleza Bilionea Dhabi kuwa kuna hatari ya  kumpoteza Osman kutokana na hali yake sababu kadili  anavyozidi kunitaja Mimi ndivyo mfadhahiko unavyoongezeka  kwake 

“Sasa tufanye nini Dokta, tumehangaika Kumtafuta Jacklin  tokea jana usiku hadi sasa hakuna dalili ya kupatikana kwake”  Alielezea Mzee Dhabi 

“Cha msingi mjitahidi apatikane huyo msichana, muongee naye  ikiwezekana haraka iwezekanavyo aletwe” Alisema Dokta Simon,  Ubilionea wa Mzee Dhabi haukuwa na kazi ili kuokoa Maisha ya  Mtoto wake Osman, Mimi niligeuka kuwa Lulu, mara simu ya  Bilionea Dhabi iliita, aliyempigia alikuwa ni Mama yangu,  alimpa taarifa kuwa nimerudi nyumbani.

“Dokta nimeelezwa kuwa Jacklin amerudi nyumbani kwao, sasa  cha Msingi ngoja niwahi huko kusudi nipate kumueleza hili  jambo, nina imani atatusaidia” Alisema Mzee Dhabi, mara moja  aliondoka Hospitalini akaja nyumbani 

Muda huo nilikuwa nimekaa na Mama akiwa ananiuliza kuhusu  kilichotokea 

“Mama mimi sikuwa na kosa lolote lile, kama wewe ulijuwa  uwepo wa tukio lile kwanini usinishirikishe na Mimi? Mlijuwa  fika siwezi kukubali ndiyo maana mlifanya kuwa siri” Nilisema 

“Sawa Jacklin hilo limeshatokea lakini hali ya Osman tokea  jana hadi hivi sasa nilipozungumza na Baba yake bado ni mbaya  mno, ipo hatari akapoteza Maisha yake” Mama alinieleza kwa  mara ya kwanza kuhusu hali ya Osman 

“Osman anaumwa? ” nilimuuliza Mama 

“Ndiyo baada ya tukio la jana alipelekwa Hospitalini na  kugundulika kuwa amepata mfadhahiko, ila kibaya zaidi ni kuwa  alikuwa na matatizo ya figo moja, alilolitoa kwa ajili yako  ndilo lilikuwa zima hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji ila  Daktari ameshauri utoe msaada katika hali ya Osman” Alisema  Mama, ilinibidi nikae vizuri ili nipate kumuelewa 

“Unamaanisha nini kusema Msaada!” Nilimuuliza Mama 

“Mfadhahiko wa Osman unapaswa kuondolewa, muondoaji wa  mfadhahiko wa Osman ni wewe hapo Jacklin” 

“Mimi nitaweza kuondoa vipi Mama” Nilimuuliza Mama, alisogea  kisha alinishika mikono yangu. 

“Kukubali kuolewa na Osman” Alisema Mama 

“Nini?” Niliuliza 

“Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone na  afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauli  yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, maneno  aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yangu  kwake 

“Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile,  wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu,  Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia,  chozi lilikuwa likinivuja.

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA Ya PUMZI YA MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

  

13 Comments

  1. Irene Liwaya💞 on

    Mambo ni moto🔥🔥🔥…!admin rusha kingine maaana siku hukurusha simulizi jaman huyu dada mbona ni muuaji aiseee karne ya sasa itokeee mie naopoa nitaenda kumpenda mbele kwa mbele hivi wapo kama kina osman sikuhizi kweli maaaana naona hawapoooo kabisaaaa

Leave A Reply


Exit mobile version