IlipoishiaScola nijibu alikuja Mgeni si ndiyo?” Nilimuuliza tena baada  ya kuona alikuwa hanipi jibu 

“Lakini Dada..” alisema Scola, nikahisi kuna jambo 

“Sitaki cha lakini nataka uniambie ukweli ni nani alikuja  hapa?” Nilimkazia sauti na jicho 

“Baba alisema nisiseme unanipa wakati mgumu Dada Jacklin”  Nilimshika mkono Scola nikamuingiza chumbani kwangu  nikamwambia 

“Tupo Mimi na wewe naomba unieleze ukweli ni nani alikuja  hapa”  Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA NNE

“Kusema ukweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumuona ila  nakumbuka Baba alisema nisikwambie wewe, aliniambia niandae  chakula chenye hadhi ya kuliwa na Bilionea. Aliniambia kuwa  ni Mtoto wa tajiri Mkubwa sana anaitwa Dhabi” Alisema Scola 

“Basi inatosha, Asante!!” Nilimkatisha Scola, nilifungua  mlango na kumpa ishara kuwa atoke, alikuwa ameniambia ukweli  ambao nilifichwa na Lidia na Dokta Simon. 

“Dada naomba Usimwambie Baba” alisema Scola 

“Usijali Scola siwezi kufanya hivyo, nenda nahitaji  kupumzika” Basi Scola aliondoka zake 

Unajuwa yale maumivu ya kuchomwa na msumari mguuni? Ndiyo  ambayo nilikuwa nikiyapata kwenye moyo wangu, kulia haikuwa  tiba, kukaa haikuwa tiba, nilitamani nipate sehemu yenye  utulivu nipige ukunga hadi sauti yangu iishe. 

Basi siku mbili zilipita, ilikuwa ni tarehe 25/09 ndiyo siku  ambayo iliandikwa kwenye ile kadi, moyo wangu uliniambia kuwa  ndiyo siku pekee ya kuonana na Osman, nilisoma muda ambao  Harusi ilikuwa ikifanyika, ilikuwa ni saa 2 Usiku katika  Hoteli ya nyota tano ya BAMOL DE HOTEL, muda nawaza yote  ilikuwa ni mchana 

Nilijaza jina langu kwenye ile kadi, nilijuwa tukio  litawashangaza wengi lakini ili moyo wangu utulie ni lazima  nionane na Osman na sehemu peke ilikuwa ni kwenye harusi  yake. 

Niliandaa gauni langu zuri jeusi, mishale ya saa moja  nililivaa, nilijitazama kwenye kioo niliona jinsi  nilivyopendeza ila nilipofunua gauni nilipata huzuni sana,  sikuwa na mguu mmoja wa kuvalia kiatu, mkononi nilikuwa  nimeshikilia kiatu cheusi cha kupanda 

Nilikitupa pembeni, nilikusanya magongo yangu, nilimpita  Scola akiwa anaingia jikoni, niliondoka nyumbani Usiku huo  ili nielekee Hotelini, niliita Tax nikaanza safri huku moyo  wangu ukiwa na maamuzi mawili ya kuacha au kuendelea na  safari, niliazimia ni bora niende tu. Nikiwa kwenye Tax Lidia  alinipigia simu akaniuliza nipo wapi, nilishangaa sana 

“Nipo njiani narudi nyumbani” nilimjibu 

“Ulikuwa wapi?” Aliuliza

“Nilikuwa kwenye matembezi kidogo nilichoka kukaa tu  nyumbani” 

“Sawa ukifika nipigie niongee na Scola” 

“Sawa!” Alikata simu 

Niliona ni bora niizime simu sikutaka tena kufikiria kuhusu  wao. 

Nilifika Hotelini mishale ya saa tatu kasoro, palikuwa  pamepambwa sana kwa nje, ulinzi ulikuwa wa kutosha sana  sababu aliyeko ndani alikuwa ni Bilionea Mkubwa sana. 

Niliangalia kadi yangu, niliongoza kuelekea kwenye lango kuu  ambalo lilikuwa na walinzi, kumbe nyuma yangu alikuwepo Dokta  Simon alafu sikushtukia ila kwakuwa alikuwa na pirika nyingi  wala hakuniona, nilimshtukia aliponipita. 

“Kumbe mpo hapa Mjini eeh! Kitakachotokea hamtoamini, kama  hamtotaka kuishi na Mimi tena ni sawa tu” nilijisemea ndani  ya moyo wangu! Nilionesha kadi yangu pale mlangoni  nilikaguliwa kisha niliruhusiwa kingia ndani ya Hoteli,  nilielekezwa mahali ambapo harusi ilikuwa inafanyika. 

Nilitembea na Magongo yangu kwa tahadhari sana maana kama  nitakutana na Lidia au Mume wake mpango ungekufa. Watu  walikuwa wamependeza sana, ile nakaribia nilimuona Mzee Dhabi  akizungumza na Simu basi niligeuza haraka kama narudi  nilipotoka maana kama ningeendelea mbele angeniona, bahati  nzuri kulikuwa na chemba upande wa kushoto niliingia huko  hadi pale alipomaliza kuongea na kurudi Ukumbini. 

Nilijitoa na kuelekea Ukumbini, kweli ilikuwa ni harusi ya  Kifahari ambayo hata kwnye Filamu sikupata kuishuhudia, roho  iliniuma sababu nilipaswa kuolewa mimi, ilipaswa Mama yangu  awepo kwa ajili ya furaha ambayo aliipigania. 

Nilitafuta Kiti cha nyuma kabisa ili nisije onekana na  wanafamilia, Muda ambao nilikuwa nimefika ndio kwanza ilikuwa  inaanza. Matajiri wenye rangi nyeupe walikuwa wengi mno,  nilijitahidi kuangaza huku na kule ili nimuone Osman. 

Kweli nilimuona Osman, huwezi amini nilijikuta nikisimama  bila kurajia, nilimtazama Osman akionekana kuwa mwenye furaha  sana, pembeni yake alikuwepo Zahra naye akiwa mwingi wa  tabasamu. Nilishuka na kuketi bila kutaka, Shughuli ilianza  kwa kutambulisha baadhi ya Watu wakubwa waliohudhuria pale,  Dokta Simon na Lidia walikuwa wakizungumza jambo huku wakionekana kupiga simu bila kupokea majibu, nilijuwa tu  walikuwa wakinipigia Mimi kujuwa niko wapi naona hata wao  hofu iliwaingia maana Scola sikumuaga kabisa. 

Nilisubiria muda sahihi wa kuonana na Osman bila kubuguzi mtu  yeyote wala kuharibu chochote kile ila kadili muda ulivyozidi  kwenda ndivyo nilivyogundua kuwa hali yangu ya kuhitaji  kuonana na Osman ilikuwa ikipanda. 

Muda wa Osman kumvisha pete Zahra ulipowadia roho ilizidi  kuniuma, wengi walisimama na kupiga makofi kwa ajili ya  tukio, ila macho yangu yalikuwa yakibubujikwa na machozi  mfululizo, nilijitahidi kujizuia nilishindwa, nilitamani  kuondoka pale Ukumbini pia nilishindwa. Katika hali isiyo ya  kawaida nilihisi kuguswa kwenye bega langu, nilipogeuka  nilikutana na Lidia. Nilishtuka sana huku chozi likiendelea  kunibubujika 

“Jacklin umefuata nini hapa?” Aliniuliza Lidia kwa sauti ya  Chini ambayo hakuna aliyesikia maana wengi akili yao ilikuwa  kule mbele. Nilimpiga kofi Lidia 

“Muongo Mkubwa wewe, kama ni furaha kusema uwongo na kuficha  kilicho kizuri basi furaha yako haiwezi kudumu Lidia, wewe ni  Muongo na mnafiki Mkubwa” Nilisema kwa sauti ya kawaida  ambayo baadhi waliisikia 

“Jacklin naomba tutoke tukaongee tusije haribu shughuli ya  Watu” Alisema Lidia 

“Tayari imesha haribika Lidia, unafikiri nitakubali kuondoka  bila kumwambia Osman kuwa nipo hai, kumwambia kuwa Mimi ni  kilema wa Mguu, kumwambia kuwa Mama yangu amefariki,  kumshukuru na kumuomba Msamaha?” Watu wa karibu walianza  kututazama, Lidia alishtukia hilo akasema 

“Nakuelewa Jacklin, naomba tukaongee hilo halina shida”  akaanza kutaka kunitoa pale kitu ambacho sikukubaliana nacho 

“Niacheeee! Niache Lidia Niache…” nilisema kwa sauti ya Juu  ambayo ilimshtua kila Mtu, macho yote yalikuja upande wetu.  Bahati nzuri nilikuwa nimeonesha mgongo kule waliko akina  Osman hivyo aliyeonekana vizuri alikuwa ni Lidia, Dokta Simon  haraka alikuja baada ya kumuona Mke wake 

“Jacklin hukupaswa kuja hapa kabla mambo hayajaharibika  nakuomba urudi nyumbani, yote tutayaongea kule” Alisema Dokta  Simon

“Siwezi kuondoka hapa bila kuongea na Osman, hamjui ni jinsi  gani naumia Mimi, hamjui ni jinsi gani Maisha yangu yamejaa  majuto, ili moyo wangu uwe sawa ni lazima nionane na Osman  leo” nilisema kwa sauti ya Juu, Osman alinisikia, sauti yangu  aliijuwa, alipiga hatua tatu mbele akiwa ameshikilia pete,  Zahra alimshika mkono kumzuia asije upande wangu! Hakuna  aliyeshtuka kuwa nilikuwa ni Mimi 

Upande wa Familia ya Osman wote walisimama, taa ililetwa  kwangu ili nionekane. Ilibidi nigeuke kutazama mbele ambako  Osman na Watu wengine walikuwepo, Mzee Dhabi alishtuka sana  kuniona, Osman alitumbua macho yake kwa Mshangao, hakutegemea  kama angeniona tena katika Maisha yake. 

Dokta Simon na Mke wake walitazamana ni wazi hawakufurahia  Mimi kuwepo pale, chozi lilikuwa likinivuja, nilimtazma Osman  ambaye naye alikuwa bize kunitazama, Zahra aliuacha Mkono wa  Osman. Ukumbi mzima ulikuwa kimya sana 

Nilichukua magongo yangu nikaanza kujongea kuelekea  aliposimama Osman, nilimuona akiwa mwenye mshituko mkubwa  baada ya kugundua kuwa nilikuwa kilema wa mguu, hata Mzee  Dhabi na Mke wake nao walishangaa sana. 

Nilisogea karibu na Osman nikiwa natabasamu kwa maumivu  makali sana, Osman alidondosha chozi lake 

“Jacklin?” Aliniita, niliitika kwa kutumia kichwa maana mdomo  ulikuwa mzito sana 

“Upo hai? Ulipatwa na nini, umepoteza Mguu?” Aliniuliza kwa  hisia kali sana, nilitoa tabasamu lenye maumivu nikamwambia 

“Nilipata ajali” nilitokwa na machozi nilishindwa kujizuia  kabisa 

“Mama yupo wapi?” 

“Mama amefariki Osman” 

“Mungu wangu! Mlienda wapi?” Aliuliza Osman, nilitaka moyo  wangu uwe safi, nilimuonesha kidole Baba yake 

“Baba yako alitufukuza kwenye ile nyumba, tulirudi Mtaani  ndipo yalipotukuta haya yote, naomba unisamehe Osman,  nilihitaji kukusaidia sana ila nilichelewa” Watu wote  walimtazama Mzee Dhabi, ilitosha kuidhihirishia Dunia kuwa  Baba yake Osman alitutendea Unyama!! Osman alimgeukia Baba  yake akamuuliza

“Baba ni kweli?” Aliuliza Osman akiwa anatiririkwa na  machozi, Mzee Dhabi hakuwa na jibu zaidi ya kuinamia chini. 

“Baba ulisema waliuza kila kitu na kuhama Mji, ulisema  haijulikani kama wapo hai au wamekufa, walikukosea nini Baba?  Kumbe mkatili kiasi hicho Baba yangu! Mungu ameamua  kukudhihirisha mbele za Watu wanaokuheshimu na kutaka kuwa  kama wewe, ulitaka iwe hivi si ndiyo?” Alisema Osman kwa  hisia kali ambayo hakuna aliyeweza kumzuia 

“Osman imeshatokea! Hayo yamepita, nahitaji msamaha wako tu”  Nilisema. 

“Jacklin nilishakusamehe tokea ile siku ambayo ulikataa kuwa  Mke wangu, niliheshimu maamuzi na mawazo yako” Alisema Osman,  huzuni ilitanda pale ukumbini, wenye mioyo midogo walilia 

“Baba ulitaka nimuowe Zahra kwasababu alikubali kutoa figo  yake kwa ajili yangu? Ukasahau ndiye aliyesababisha jeraha  ndani ya Moyo wangu, aliniacha katika wakati ambao nilikuwa  sina chaguo lingine. Maumivu na mateso niliyoyapta ameyalipa  kwa kutoa Figo lake, Hata Moyo wangu Baba unajuwa kuwa  nampenda Jacklin, namuhitaji ila ulijaribu kumuweka mbali na  Maisha yangu!” Alisema Osman kisha alinikumbatia, Huwezi  amini Zahra alilia sana pale chini, alitoka mbio akakimbilia  nje 

Mzee Dhabi na Mke wake walilia kwa maumivu makali sana.  Nilivyomkumbatia Osman nilihisi akiwa anapumua kwa shida  sana, alikuwa akitaka kusema neno ambalo nilitamani  kulisikia, neno ambalo hadi hivi leo sijui alikuwa anataka  kuniambia nini, alisizi kwenye mwili wangu bila kuhema tena,  ilikuwa ndiyo Pumzi ya Mwisho ya Osman katika hii Dunia,  hakuna aliyejuwa kuwa Osman alifia kwenye mwili wangu. Mzee  Dhabi alisogea na kupiga magoti akasema 

“Osman! Nisamehe Mwanangu,,nisamehe kwa yote, nilifanya kwa  hasira baada ya kuona amekataa kusaidia Maisha yako, nimekupa  hasara Jacklin umempoteza Mama yako na Mguu wako naomba  mnisamehe” Alisema Mzee Dhabi, ukimya wa Osman ulianza kunipa  wasiwasi, nilimuacha lakini cha ajabu alienda chini kama  Mzigo, haraka gari ya wagonjwa ilifika, Osman alipelekwa  Hospitalini. Sote tulienda kusubiria hatma ya Osman, kila  mmoja alikuwa kimya, nilikuwa mwingi wa kulia tu. 

Masaa matatu Baadaye Dokta Simon alitoka chumba cha Wagonjwa  mahututi, alitupa taarifa iliyoondoa uhai wa Bilionea Dhabi  pale pale, Ndio, Osman alikuwa amefariki kwa mshituko na  mfadhahiko. Mzee Dhabi na Osman walizikwa nyumbani kwa Osman,,,nilimshukuru Mungu kwa kila jambo lililonifika kwenye  Maisha yangu. Nilipoteza kila kitu lakini Mke wa Bilionea  Dhabi aliniambia kuwa ananipa Nusu ya mali zote za Bilionea  Dhabi. 

Nilipewa kila kitu nilichoahidiwa, japo havikuwa na thamani  ya kuzidi uhai wa Osman, Bilionea Dhabi, Mama na Mguu wangu.  Nilijiapiza kuwa sitokuja kupenda tena katika Maisha  yangu.,,,,Miezi mingi ilipita, maumivu ndani yangu yalianza  kupona, niliwekewa mguu wa Bandia. 

Siku moja asubuhi nikiwa naelekea JM Motors nikiwa kama  mmiliki wa kampuni hiyo ya Uuzaji wa magari, nilijikuta  katika foleni eneo lile lile ambalo nilijikuta kwenye Foleni  siku ya kwanza kabisa ambayo nilikuwa naenda JM Motors kuomba  kazi, ndiyo siku ambayo nilikutana na Osman. Moyo wangu  uliingiwa na maumivu makali sana, nikiwa nasubiria gari  zianze kutembea, Mtu mmoja ambaye ni ombaomba aligonga kioo  cha gari yangu! Nilikuwa ni Mtu ninayezijuwa shida sana  kutokana na Maisha niliyopitia, nilifungua kioo, moyo  uliniripuka sana. Aliyegonga kioo alikuwa ni Mosses Mwanaume  niliyekuwa nampenda sana katika Maisha yangu, alikuwa haoni  yaani kipofu wa macho yote mawili hivyo yeye hakujuwa alikuwa  akimuomba pesa nani, sikujuwa alikuwa amekutwa na nini ila  hata vidole vyake vilikuwa vimekatika. 

Nilimpa noti ya Shilingi Elfu tano, kisha aliondoka zake,  unajuwa kwanini nilimpa noti ya Elfu tano? Ni kwasababu ile  siku aliniahdi kunitumia pesa ya pikipiki alafu hakunitumia  wakati huo Elfu tano yangu nilimpa marehemu Osman, nilisema 

“Malipo ni hapa hapa Duniani Mosses, Kwaheri ya kuonana”  Nilifunga kioo kisha niliondowa gari yangu. 

••MWISHO•••

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kununua SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho

  

19 Comments

  1. So sad 😢
    Mapenzi ni ugonjwa usio na dawa
    Eeee Mwenyezi Mungu naomba unipe atakae nipenda kwa dhati kama mapenzi ya Osman kwa Jacklin.
    Stori ya kuhuzunisha yenye Mafundisho tosha na maumivu makali ndani yake.😭

  2. Kaka mkubwa KWELI wewe ni kaka mkubwa umeumba ulimwengu wa kufikirika mpaka basi……. SASA WATENGENEZA FILAMU MPOWAPI? HAMONI MNANGOJA NINI?…SHIRIKIANENI NA KAKA MKUBWA!!! MTUTENGENEZEE DUDE JAMANIEE

Leave A Reply


Exit mobile version