Ilipoishia Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwa  na tabia ya wivu sana 

“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanja  kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwa  ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bila  kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianza  kujichukia Mwenyewe. 

Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, nami  nilitoa tabasamu 

“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadi  kulipopambazuka. Endelea 

 

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatatu iliyoanza kwa jua kali la  mvua, nilimuaga Mosses, nilirudi nyumbani kujiandaa kwa ajili  ya kwenda kazini japo Mosses aliniambia niache kazi, hata  Mama aliniuliza 

“Ulilala wapi na unaenda wapi?” Aliniuliza nikiwa tayari kwa  ajili ya kutoka nyumbani kuelekea kazini 

“Shikamoo Mama!!” Nilimsalimia kwanza 

“Marahaba! Siku hizi unaamuwa tu kulala unapopajuwa wewe,  kufanya unachowaza wewe si ndiyo?” Aliniuliza, niliutupa  mkoba kwenye sofa kisha niliketi Mama akiwa amesimama 

“Mama nililala Hotelini” Nilimjibu Mama huku Moyo ukinisuta “Na unaenda wapi?” Aliniuliza

“Naenda kazini” Nilimjibu Mama nikiwa ninafinya vidole  vyangu, Basi Mama alisogea kisha aliketi kando yangu 

“Jacklin ningekushauri usiende huko sababu ile ni kampuni ya  Osman na Baba yake, kilichotokea baina yetu na ile Familia  hakiwezi kuleta picha nzuri endapo tutaendelea kujihusisha na  ile Familia” Alisema Mama 

“Mama chochote kilichotokea hakina mahusiano ya moja kwa moja  na kazi ninayoifanya kwao, hii ni kazi ambayo  

tumeandikishiana mikataba labda waamuwe kuvunja mikataba”  Nilisema 

“Inatosha Jacklin, usiende huko Mwanangu” Alisema Mama lakini  sikutaka kumsikiliza, moyo wangu uliniambia kuwa napaswa kuwa  karibu zaidi na Osman japo yupo Hospitalini lakini kuwa  ofisini kwake kungefanya moyo wangu utulie 

“Mama najuwa ninachokifanya, usijali kila kitu kitaenda sawa”  Nilisema kisha nilinyanyuka na kuondoka zangu. 

Nilizongwa na mawazo kichwani, nilizongwa na hisia kali ndani  ya moyo wangu, hisia ambazo zilinikosesha raha kabisa.  Niliingia ofisini kwangu na kuanza kazi, nilitekeleza  majukumu yangu ndani ya kampuni ya JM Motors. Siku hiyo Mzee  Dhabi alikuja kwenye kampuni kukagua utendaji wa kazi  unavyoendelea, hakujuwa kama Mimi ni mmoja wa wafanyakazi,  aliponiona aliniuliza 

“Wewe ni miongoni Mwao?” Akimaanisha hao Wafanyakazi “Ndiyo Baba” Nilimjibu tukiwa wawili tu ofisini 

“Usiniite Baba, Niite Mzee Dhabi inatosha” Alisema Mzee  Dhabi, hapo ndipo nilipokumbuka maneno ya Mama kuwa siyo  busara sana kurudi kufanya kazi ndani ya kampuni ya Bilionea  Dhabi kutokana na kilichotokea kati yangu na Kijana wake 

“Mbona katika orodha ya Wafanyakazi wewe haupo, Osman  alikuajili vipi?” Aliuliza Mzee Dhabi kisha aliketi,  niliiyona chuki ndani yake, nilijawa na kigugumizi 

“Mbona nilishajaza mkataba na kupewa hii Ofisi” nilijibu 

“Hapana, Mimi ndiye Mwenye hii kampuni, Osman anasimamia  sababu ni Kijana wangu! Sikutambui, hakuna mkataba ulio mbele  yangu” Alisema Bilionea Dhabi tena kwa sura kavu sana

“Lakini mbona nilifanya usahili hapa na kujaza mkataba wa  kazi iweje leo nisitambulike” Niliuliza 

“Ni huruma ya Osman ambayo imemteketeza ndiyo iliyokufanya  wewe kuwa hapa lakini hukupaswa kuwa hapa, nikiwa kama  Mmiliki wa hii kampuni, sihitaji kukuona hapa kuanzia muda  huu, kusanya kila kilicho chako” Alisema Bilionea Dhabi kama  vile hakuwahi kuniona kabla, ujuwe nilichoka sana kuanzia  roho hadi mwili, ningesema nini na aliyesimama mbele yangu  alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo 

Nilifanya kama alivyosema tena akiwa amenisimamia, niliondoka  kwenye kampuni ya JM Motors, nilijuwa chuki aliyoionesha Mzee  Dhabi ilitokana na jinsi nilivyokataa kuokoa uhai wa Kijana  wake japo dakika za mwisho niliufungua moyo wangu ila  nilikuwa nimeshachelewa, Chozi lilinibubujika. Tayari mvua  ilikuwa imeanza kunyesha. 

Nilitembea kwenye mvua huku nikikumbuka siku ya kwanza kabisa  ambayo Osman alinisaidia kwenye mvua, nilipofika nyumbani  nilimsimulia Mama kile kilichotokea. 

“Nilikwambia Mwanangu lakini hata Usijali sana sababu umesoma  utapata kazi sehemu nyingine na Maisha yataendelea” alisema  Mama 

“Lakini Mama, natamani sana kulipa fadhila za Osman,  amebadilisha Maisha yetu kutoka kwenye Umasikini, ameokoa  Maisha yangu kutoka kifo, nilichelewa kuiyona thamani ya  Upendo na huruma yake” Nilisema nikiwa nimeegemea ukuta 

“Usijutie kwa chochote sababu anayepanga kila kitu ni Mungu  pekee, Maisha lazima yaendelee” Alisema Mama, mara tulisikia  honi ya gari. Mama alichungulia, aliona gari ya Mzee Dhabi  ikiingia, 

“Baba yake Osman anakuja” Alisema, nilikuwa nimelowa kutokana  na ile mvua hivyo nilihitaji kubadilisha nguo haraka,  nilielekea chumbani kwangu kubadilisha nguo, nilipotoka  niliwakuta Mama na Bilionea Dhabi wakiwa wameketi hapana  shaka walikuwa wakinisubiria Mimi. 

Niliketi kwa utulivu sana, nilimtazama Bilionea Dhabi ambaye  alikuwa ameongozana na Mke wake. 

“Shikamoo Mama” Nilimsalimia Mama yake Osman ambaye hata  hakuitikia, nilipata ishara kuwa hawakuja kwa lengo zuri,  alianza Bilionea Dhabi kusema

“Tumekuja kwa ajili ya mambo mawili makubwa, moja ni kuchukua  magari ambayo Osman alikununulia, mbili ni kuchukua nyumba  hii ambayo mnaishi” Alisema Mzee Dhabi kwa sura kavu sana.  Mama alishtuka sana 

“Unasemaje?” Alihoji 

“Pesa iliyotumika hapa ni pesa yangu Mimi, maamuzi  ninayoyatoa yanatoka kwangu Mimi pia. Iwe mlipewa hati au  hamkupewa Hati ya Hapa, mnaondoka na jeuri yenu” Alisema  Bilionea Dhabi 

“Baba tafadhali sana hebu fikiria tutakwenda wapi sisi?  Fikiria kwa kipindi hiki tutafanya nini?” Alisema Mama akiwa  analia, nilizidi kuumia ndani ya nafsi yangu 

“Kwani zamani mlikuwa mnaishi wapi? Mlikuwa mnaishi vipi  kabla ya kuanza kutumia pesa za Osman?” Aliuliza Bilionea  Dhabi, nilikaa kimya bila kusema chochote sababu sikuwa na  cha kusema 

“Nionee huruma Mimi, Mimi ni mtu mzima nitaishi vipi Baba,  fikiria hilo ina maana makosa ya Binti yangu yanatufanya tuwe  maadui?” Aliuliza Mama akiwa katika hali ile. Ile ya kilio 

“Siyo maadui tu bali ni maadui wa Maisha, adui wa Maisha ya  Kijana wangu ni adui yangu pia, mna siku mbili za kuhakikisha  mnahama hapa, gari zinaondoka sasa hivi” Alisema Bilionea  Dhabi kisha yeye na Mke wake walinyanyuka, Mke wa Bilionea  Dhabi hakusema chochote kama ambavyo Mimi sikusema chochote,  Mama na Bilionea Dhabi ndio ambao walikuwa wakirushiana  maneno 

“Nakuomba tuonee huruma sisi, tutaenda wapi, siku mbili  jamani Aaah” Mama alisema lakini hakukuwa na maelewano, Mzee  Dhabi aliondoka bila hata kuchukua Funguo za Magari. Nililia  sana, nilikumbuka kuwa Kulikuwa na pesa kwenye akaunti ya  Benki zaidi ya Milioni 60 ambazo Osman alinipatia, kadi  ilikuwa kwa Mosses, haraka nilimpigia na kuhitaji kuonana  naye. 

Alinielekeza alipo niliondoka na kumuacha Mama akiwa analia,  nilienda kuonana na Mosses. Nilimsimulia kilichotokea,  nilihitaji Milioni 40 ili kununua nyumba ya kuishi Na Mama  ila majibu ya Mosses yalinigandisha damu, alisema Pesa zote  aliziweka kwenye Biashara yake ya Mazao hivyo nisubirie ndani  ya mwezi mmoja angenipatia pesa hizo.

“Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?  Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishi  wapi?” Nilimuuliza Mosses 

“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pambo  la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi ni  Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, sura  yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishana  naye nilimkubalia 

“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu. 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MBILI Ya PUMZI YA MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

13 Comments

  1. Mambo ni Fire ooooooh🔥🔥🔥🔥🔥 amechezea bahati ona anavyopata tabu…! Hivi dunia ya sasa wapo watu kama kina jack maaaana oh mie weeee mapema na kwa haraka sana ningemkubalia osman I don’t care na mahusiano yangu🤪🤪👌🏼👌🏼👌🏼👌🏼

Leave A Reply


Exit mobile version