IlipoishiaLakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?  Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishi  wapi?” Nilimuuliza Mosses 

“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pambo  la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi ni  Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, sura  yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishana  naye nilimkubalia 

“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.  Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Nilimuamini sana Mosses, nilijuwa nitaipata hiyo pesa ila  sasa huo muda ambao alisema atanipa nilifikria tutaenda  kuishi wapi Mimi na Mama yangu? Nilipoongea na Mama  sikumwambia kuhusu zile pesa istoshe alikuwa hajui kama kuna  pesa hiyo. Aliniuliza tu nina akiba gani, kiukweli sikuwa  hata na hamsini mbovu, maana nilijuwa na tumaini kubwa kwenye  zile milioni 60 zilizo kwa Mosses, niliona aibu hata kumjibu  Mama kuwa sina pesa, nilikaa kimya japo Mama alinielewa 

“Mimi nina Milioni moja Jacklin, tufanye mpango wa kutafuta  chumba kimoja” Alisema Mama huku akitabasamu kwa maumivu  makali, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kukielezea. 

“Itabidi tutafute mahali pa kuishi Jacklin, imeshatokea ni  lazima tukubaliane na hali halisi” Alisema Mama, nilitamani  sana kumwambia tukaishi nilipompangishia nyumba Mosses lakini  nilihofia kwa jinsi wawili hao walivyokuwa hawaivi chungu  kimoja 

“Sawa Mama haina shida” Huzuni ilitanda kwenye nyumba yetu. 

Siku iliyofuata Mzee Dhabi alituma Watu, tuliwapa funguo za  magari yote kuanzia na lile jipya na mengine ambayo hata  nilikuwa sijui kuendesha, yaliondoka yote. Nilianza harakati  za kutafuta chumba cha kupanga ili niishi na Mama yangu,  bahati nzuri nilipata japo uswazi huko ila ndiyo Maisha  ambayo tulishayaishi hivyo haikuwa shida sana kurudi  Uswahilini huko. 

Baada ya muda ambao Mzee Dhabi aliusema, alirudi kwa ajili ya  kuchukua funguo za nyumba, Mama alijitahidi tena kuongea naye  ila Mzee huyo hakusikiliza kabisa. Tulihama kwenye jumba la  kifahari ambalo Osman alitununulia, msichana wa kazi  aliondoka kwao, hatukujuwa maamuzi hayo yalitoka kwa mwenyewe  Osman au Mzee Dhabi aliamuwa kutumia hasira zake tu.

Tuliacha kila kitu ndani ya Jumba hilo, nguo pekee ndizo tulizoondoka  nazo. Hatukuwa na godoro, tulinunua baadhi ya vitu kidogo ili  pesa itusaidie kwenye mahitaji ya hapa na pale, tumaini  lilibakia kwa Mosses japo kila nilipo mpigia simu  alinizungusha kuonana naye, nilipoenda anapoishi nilikuta  pamefungwa, niliishi kwa tumaini tu kuwa Maisha yale  yasingekuwa ya muda mrefu. 

Siku zilipita, tuliishi kwa matumaini, tulilala kwenye mkeka,  niliona jinsi Mama alivyokuwa akiteseka roho iliniuma sababu  chanzo cha yote nilikuwa ni Mimi. Namba za Osman  hazikupatikana kabisa, hatukujuwa kama alikuwa mzima au  alikuwa amekufa, mwisho tulifuta namba zake. Miezi ilisonga,  Mosses hakupatikana kwenye simu kabisa, hata alipokuwa  anaishi alihama na sikujuwa ningempata vipi, moyo wangu  ulijawa na maumivu makali sana, pesa zilianza kuisha,  tulishauriana Mimi na Mama tufanye nini kwa pesa iliyobakia,  kila nilipojaribu kwenda kuomba kazi nilikosa, Mama alishauri  tuanze biashara ya Mboga mboga 

Tulikuwa tunaamka asubuhi mapema tunaenda Bustanini,  tunanunua mbogamboga tunaenda kuuza, Waliotujuwa  walitushangaa sana, waliosikia kilichotokea walitucheka na  kutuona hatuna akili, ningefanya nini zaidi ya kukubali  masimango yao ili mkono uwende kinywani, Mimi na uzuri wangu  na usomi wangu niliishia kutembeza mbogamboga Mitaani. 

Siku moja nikiwa nauza Mbogamboga nilimuona Mtu aliyefanana  sana na Mosses, nilitamani kumuona kwa ukaribu zaidi. Ndio!!  Alikuwa ni yeye, alikuwa ameongozana na Mwanamke mmoja.  Niliona kama vile nimeokota Almasi kwenye zizi la ng’ombe  nilimkimbilia Mosses na kumkumbatia. Hakuonekana kunifurahia  kabisa, yule Mwanamke aliuliza 

“Wewe Dada vipi unakichaa au?” Nilijitoa mwilini mwa Mosses 

“Ndio! Mimi ni kichaa sababu Sijamuona huyu Mtu kwa muda  mrefu, Mosses haujui ni jinsi gani nimekutafuta” Nilisema,  beseni la mbogamboga lilikuwa limeanguka pembeni na mboga  zote zilikuwa chini kwa jinsi nilivyokuwa nimefurahi 

“Kutokumuona muda mrefu na kumkumbatia mbele ya Mke wake kuna  husiana nini? Mosses huyu ni Nani?” Aliuliza yule Mwanamke 

“Simjui Mimi” Nilishtuka 

“Mosses hunijui Mimi Jacklin? Au kwasababu nimebadilika?”  Kiukweli nilikuwa nimebadilika, sio Jacklin yule ambaye  alikuwa akimfahamu, kutembea kwenye jua ilikuwa ndiyo Maisha  yangu hadi ngozi yangu ilibadili rangi.

“Sikujui kabisa, nimeshangaa sana unakuja kunikumbatia mbele  ya Mke wangu” Alisema Mosses, nilisogea nyuma, niliokota  mboga zangu na kuzirudisha kwenye beseni langu. 

“Samahani nilikufananisha na Mosses wangu, mmefanana,  Samahani Dada” Nilisema kijasiri sana kisha niliondoka zangu.  Mbele ya macho yangu nilidondosha chozi, nilienda kukaa chini  ya Mti nililia mno tena kwa kusaga meno. Niliumia kwa mambo  mawili kwanza kudharirika na pili kupoteza tumaini la kuipata  ile Milioni 60 ambayo Mosses aliichukua kwenye akaunti yangu  ya Benki. 

Jua lilikuwa langu, mvua ilikuwa yangu, nilichotakiwa ni  kuhakikisha napata pesa itakayoendesha Maisha yetu Mimi na  Mama yangu, nilijiuliza kitu kimoja kama nitaendelea kulia  nini kitabadilika kwenye Maisha yangu? Hakuna, basi  nilinyanyuka na kuondoka zangu, nilirudi nyumbani maana mboga  nyingi nilikuwa nimeshaziuza iliyobakia niliipigia mahesabu  nitakaporudi iwe ndiyo Mboga maana siku hiyo Mama hakwenda  kuuza mboga alikuwa hajisikii vizuri. 

Mdogo mdogo nilifika nyumbani, kulikuwa na mmama anaitwa Mama  Amina alikuwa ni Mpangaji mwenzetu. Alinisimamisha kabla hata  sijaingia ndani alinipa taarifa kuwa Mama yangu alikuwa  ameanguka chooni hivyo amekimbizwa Hospitalini, nilishtuka  sana 

“Hospitali gani?” Nilimuuliza beseni likiwa chini 

“Wamempeleka Kwa Dokta Simon” alipomaliza kunielekeza  nilitimua mbio kuelekea Hospitalini. Mama yangu alikuwa ndiye  Mtu pekee aliyebakia na Mimi, alikuwa ndiye tumaini langu,  taarifa ilinichanganya sana. Nilikuwa katika hali ya  kuchanganikiwa sana, nilijikuta nikigongwa na Pikipiki nikiwa  nakaribia Hospitalini. 

Nilipoteza fahamu zangu kutokana na ile ajali mbaya ya  Pikipiki, nilipokuja kurudisha fahamu ilikuwa ni siku  iliyofuata, nilijikuta nikiwa Hospitalini, nilihisi maumivu  makali sana ya Mguu wa kulia, kulikuwa na wepesi sana na  ubaridi hadi nilishangaa, nilipeleka mkono ili kuugusa mguu  wangu!! Nilishtuka sana, nilikuwa nimeshakatwa Mguu, nililia  sana. 

Dokta Simon alikuja kuniangalia maana mara nyingi alikuwa  akipita kukagua Wagonjwa, ndipo aliponiona, alinijuwa  kutokana na ile iliyotokeaga kati yangu na Osman, alishangaa  sana, nilikuwa katika maumivu makali na majonzi, alinipa pole  kisha aliniambia

“Pole sana kwa kilichokupata na kilichomfika Mama yako” Mwili  ulisisimka ghafla sana, wazo la Mama kuwa alikuwa Hospitalini  lilinijia 

“Mama yangu anaendeleaje Dokta?” Nilimuuliza huku Kidonda cha  Mguu kikiwa na maumivu makali sana 

“Mama yako alishafariki tokea jana” 

“Nini?” 

“Ndiyo Pole sana Jacklin, Mwili wa Mama yako umechukuliwa leo  kwa ajili ya mazishi, umezikwa na Manispaa sababu hakuna  ndugu aliyejitokeza!” Alisema Dokta Simon, moyo uliloa chozi  la Maumivu, Nilijihukumu sana kwa kilichomfika Mama yangu,  Nililia sana. 

“Usilie Jacklin, Maisha ndivyo yalivyo. Kwasasa unaishi  wapi?” Aliniuliza, nilijawa na kwikwi sana sikuweza kumjibu  mwisho alisema 

“Tutaongea utakapokuwa sawa Jacklin, pole kwa Msiba na pole  kwa yaliyokufika” Alisema kisha aliondoka, niligumia 

“Mamaaaaa! Umeniacha kilema Mwanao!! Mamaaa umeondoka  umeniacha na Nani Mimi” Aaah! Chozi lilikuwa ndiyo rafiki  yangu, nililia sana, sikuwa na uwezo wa kunyanyuka wala  kutembea. 

Baada ya wiki mbili kupita Dokta Simon alikuja tena kisha  aliketi kando yangu, angalau nilikuwa nimetuliza maumivu  yangu! Alinipa pole kabla ya kuanza kuzungumzia kilichokuwa  kimemleta 

“Kwanza pole sana Jacklin, Dunia yako imekugeuka lakini  ndivyo ilivyo sababu siyo Watu wote wanakuwa na simulizi tamu  za Maisha yao, yako chungu sana. Osman alikutafuta sana,  ilisadikika kuwa Mlikuwa mmeuza kila kitu na kuondoka”  Alisema Dokta Simon, stori yake ilikuwa ngeni masikioni  mwangu 

“Tuliuza kila kitu?” Nilimuuliza 

“Ndiyo! Mzee Dhabi pia alihangaika kuwatafuta bila mafanikio,  mwisho alikata tamaa baada ya kupata taarifa kuwa mliuza  nyumba na kuondoka wewe na Mama yako!” 

Haraka niligundua kuwa Mzee Dhabi alifanya yote pasipo Osman  kujuwa 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA TATU Ya PUMZI YA MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

  

18 Comments

    • Hamza Mwalyawa on

      Hujakosea upo sawa kabisa brother dunia ina zunguka. Ulipo anzia wakati fulani ndipo unapoishia.
      Mara hutokea sivyo. HEBU TUANGALIE KIJACHO………

    • Mmmh!! Usiombe yakukute kaka au dada sijui
      Tuulize sisi yalotukuta
      Jacklin hana tofauti sana na mm sema yeye mwanaume alompenda alimpa uhuru sana wa mali zake
      Wanaume wa siku hisi wanapenda sana misaada kutoka kwa wanawake wakifanikiwa wanasahau kila kitu.

  1. Siwezi mlaumu sana Jackline, mana story yake inaendana kidg na yangu
    Mimi Tulipendna sana na mkaka flan ambaye huyo mkaka alikuwa na rafk ake na huyo rafk ake Tulikuwa Majirani nando Mwanaume wa kwanza kunitongoza, Wote tulisoma Pamoja Standard 3, bc nikadate na huyo mkaka Takriban miaka 12
    Lakn lafk ake akiwa bado hajakata tamaa ya kunipenda, nilikuwa nikiumwa kwa haraka sana anafika Hospital nilipo lazwa, Nikiumwa hata kichwa, haraka alifika nyumbn lakn bado sikumkubalia, nilizidi kudate na rafk ake na sio yeye

    2021 nikaumwa Ugonjwa wa MOYO nikalazwa Jakaya Kikwete Cardinal Institute (Muhimbili) Nikafanyiwa Operation da!! Yule Mpenzi wangu Akaniacha na wala hakuwahi kuja hospital wala Nyumban But yule anaye nipenda alikuja kila cku na cku zingne alivuta cku moja tu
    Ndg zangu wakasema wanichangie Damu naye pia akaungana na ndg zangu kunichangia Damu.
    Lakn bado sikumkubalia
    Mwaka jana Mwishoni Nikajikuta nayatafakar Mengi aliyo yafanya kwangu da! Niliumia sana why nimemtenda hivo kwa muda mrefu toka tukiwa watoto wa darasa la 3
    Basi nikajikuta naomba appointment bc tukakutana nikamwambia sorry kwa usumbufu wa miaka yote
    NAKUPENDA NAOMBA TUOWANE TUWE MKE NA MME
    Da!! Akasema Wewe ni msichana pekee niliye kupenda katika hii dunia na niliishi kwa kujipa moyo kuwa wewe ni mke wangu lakn Moyo wangu ukachoka sana baada ya wewe kutoka hospital bado ukawa unampenda mtu aliye kufanyia ukatili hivo ni Mwezi sasa toka niingie kwenye mahusiano na binti niliye muona ananipenda kwa dhati
    Guys nililia sana na bado mpka leo naumia cz Kadi za mwaliko zimesha anza kugawiwa ANAFUNGA HARUSI DECEMBER

  2. Pole kwa yaliyokupata, haya maisha ni fumbo, laiti tungejua yajayo huenda maisha yetu yangekuwa na raha, yule unaempenda hakupendi,. Usiye mpenda ndie anakupenda, kwa kweli maisha ni kitendawili, Mungu pekee ndie ajuaye mwisho wetu, SS niwakupokea tu

Leave A Reply


Exit mobile version