Ilipoishia “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Macho angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisema Dokta Simon
“Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twende Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra, waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simon
Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman, aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa. Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuona Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmke ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio. Endelea
SEHEMU YA KUMI
“Zahra?” Aliita Osman akiwa anaendelea kumuangalia Zahra ambaye alikuwa akitembea taratibu kuelekea kilipo kitanda alicholala Osman, alitikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa ni Yeye
“Baba! Huyu ni Zahra?” Osman alimuuliza Baba yake
“Ndiyo Osman huyu ni Zahra” Alijibu Mzee Dhabi, Chozi lilimbubujika Osman, Dokta Simon alikuwa akiangalia kilichokuwa kinaendelea kwa kutumia mlango
Zahra alisogea na kumkumbatia Osman akiwa analia, Osman aliweka mikono yake kwenye mgongo wa Zahra. Muda huo Mimi na Mama tulikuwa tumeingia wodini, tulikuta hali hiyo. Ilitubidi Mimi na Mama kusizi kwa dakika ili kuangalia kilichokuwa kikiendelea, walipoachana Zahra aligeuka nyuma alimtazama Mzee Dhabi aliyekuwa akipepesa macho yake baada ya kuniona Mimi
Macho yangu yaligongana na Macho ya Zahra, nilimtambuwa kuwa ndiye Mwanamke aliyekuwa akiuendesha moyo wa Osman lakini nilijiuliza aliweza vipi kurudi tena katika Maisha ya Osman, roho iliniuma sababu alirudi wakati ambao nilikubali kumsaidia Osman
Osman alinitazama, ukimya ulitawala huku kila Mtu akiwa kwenye taharuki ya kilichokuwa kinaendelea pale.
“Baba! Nimerudi” Alisema Zahra akiwa analia, jinsi nilivyomtazama niligundua alikuwa na jambo zito lililomfika ambalo lilimrudisha kwa Osman
Nilihema sana nikihisi maumivu makali sana kifuani, niliondoka nikaenda nje ambako nilijikuta nikiwa nimekaa peke yangu usiku ule.
Mama hakuwa na neno la kuzungumza ilimbidi aangalie tu kilichokuwa kinaendelea pale
“Zahra” Osman aliita, mara moja Zahra alimgeukia Osman
“Ulikuwa wapi siku zote, nimekutafuta kila kona ya Dunia hii bila mafanikio yoyote” Alisema Osman, Zahra alidondosha chozi akasema
“Nisamehe Osman, najuta kwa Ujinga wangu, najuta sana. Nimerudi kukufuta chozi lako” Alisema Zahra kisha alipiga magoti akiwa analia, hata Mama alidondosha chozi lake
“Niambie nifanye nini Osman ili uamini kuwa nimerudi kwa ajili yako, nimekukosea sana” Alisema Zahra akiwa anaendelea kulia, Bilionea Dhabi alimsogelea Zahra na kumyanyua kisha alimfuta chozi kwa kutumia mkono wake, akamwambia
“Osman anaumwa sana, hakuna tumaini la yeye kupona isipokuwa kupata Figo na kumuondolea mfadhahiko” Alisema Mzee Dhabi kwa sauti yenye kunong’oneza masikio ya Zahra, hii ilimshtua sana Zahra alimfuata Osman alipolala kisha akamwambia
“Utapona Osman” Zahra alimshika mkono Bilionea Dhabi wakatoka ndani, walinipita mahali nilipokuwa nimekaa, walielekea ofisini kwa Dokta Simon
“Baba kama kutoa kiungo changu kutamfanya Osman awe salama nipo tayari hata sasa hivi, pimeni figo zangu zikifaa mnitoe” Alisema Zahra mbele ya Dokta Simon na Bilionea Dhabi ambao walijawa na mshangao, chozi lilimtoka Bilionea Dhabi
“Zahra!” Aliita Bilionea Dhabi kwa sauti ya Chini sana, Zahra alitikisa kichwa ishara kuwa alichokisema ndicho alicho kimaanisha.
Mzee Dhabi alimkumbatia Zahra kwa Uchungu sana, alikuwa ameshakata tumaini, Ujio wa Zahra ulimfanya Osman arudi katika hali ya kawaida hata ile hali ya kunitaja ilikata. Mama alimuuliza Osman kule Wodini
“Huyu Mwanamke ni nani?”
“Ni Mwanamke niliyampenda sana lakini alinikimbia na kwenda Ughaibuni” Alijibu Osman
“Osman Mwanangu, Jacklin amekuja kwa ajili yako, yupo tayari kufunga ndoa na wewe” Mama alisema kwa uchungu sana, Osman alitikisa kichwa chake ishara ya kukataa huku akisema
“Jacklin hanipendi Mama, hawezi kukubali nimuowe”
“Tafadhali sana Osman, Jacklin anakupenda na yupo tayari” Alisema tena Mama wakati huo Mimi nilikuwa ninachungulia mlangoni, niliumia sana. Sikuona umuhimu wa kubakia pale Hospitali niliondoka zangu. Mama alijitahidi sana kumbembeleza Osman lakini haikusaidia, kilichomtesa Sana Mama yangu ni ule wema ambao Osman alitutendea na jinsi ambavyo Mimi niliulipa wema huo kwa ubaya sana, Mama alilia sana hadi Mzee Dhabi aliporudi akiwa ameambatana na Dokta Simon na Zahra, Mzee Dhabi alimwambia Mama yangu
“Nashukuru kwa msaada na Mchango wako Mama Jacklin lakini kwasasa wewe nenda”
“Lakini Mzee Dhabi…” Mama alikatishwa na Mzee Dhabi kisha alipewa ishara ya kuondoka, chozi lilikuwa linamvuja Masikini Mama yangu, aliondoka zake.
Mama alilia njia nzima hadi anafika nyumbani nguvu zilikuwa zimemuishia, bahati nzuri nilikuwa sebleni. Nilipomuona Nilimkimbilia na kumdaka asianguke, mwili wake ulikuwa wa moto sana, jasho lilikuwa likimtoka, sikupata kumuona Mama akiwa katika hali hii hata siku moja, nilimlaza kwenye Kochi nikawasha Feni ili apate ubaridi kisha niliketi pembeni, ukimya ukatawala huku nafsi yangu ikiwa imejaa majuto makubwa sana, niliamini hali ya Mama ilitokana na makosa yangu.
“Jacklin” Mama aliita kwa Maumivu makali kisha alisema
“Tumechelewa lakini Mama yako nakupenda sana, Dunia nzima inaweza ikakuona mbaya lakini Mama yako nitahangaika kukusafisha. Osman amekataa kufunga ndoa na wewe” Alisema Mama huku chozi likimbubujika, kusema ule ukweli niliumia mno ndani ya nafsi yangu.
Moyo wangu nilishaufungua kwa Osman lakini niliufungua nikiwa nimechelewa, nilijuwa Zahra ndiye aliyeharibu kila kitu, nilimyanyuka na kuondoka nyumbani kwa hasira na maumivu makali, sikutaka kujuwa kuhusu Hali ya Mama tena, kichwa changu ni kama kilijaa moshi mkali sana.
Nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa 6 Usiku, nilimpigia simu Mosses, zaidi ya mara sita mara ya saba ndio alipokea simu yangu ikionesha kuwa alikuwa amelala. Aliniuliza nataka nini? Nilimwambia nahitaji kuonana naye, aliniambia niende kwake, nilianza safari ya kuelekea huko Usiku huo.
Nilipofika kwa Mosses kuna hali nilianza kuihisi ndani ya nafsi yangu, niliona kabisa mapenzi kwa Mwanaume huyo yalianza kuondoka ndani yangu, niliigiza tu na kumwambia kuwa nammiss sana ila ukweli ni kwamba akili yangu ilikuwa kwa Osman, kila nilipomfikiria Osman nilijikuta nikiumia tena kibaya zaidi nilipofikiria kuwa Zahra amechukua nafasi yangu ndani ya moyo wa Osman ndiyo nilizidi kupagawa, hali hii Mosses aliiona kwangu kwasababu mara nyingi nilikuwa nikitoka kifikra akaniuliza
“Unawaza nini? Haupo kabisa” Aliuliza Mosses, huwezi amini tulikuwa katikati ya tendo lakini akili yangu hata haikuwa hapo, Mosses alishuka kisha alielekea Bafuni aliporudi alihitaji majibu kutoka kwangu.
“Sijui Mosses! Najikuta tuu” Nilimjibu nikiwa ninavuta Shuka, kweli mapenzi yanaumiza sana Aisee kumbe Osman aliumia hivi? Sikuwahi kuumia kama ambavyo nilikuwa naumia
“Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwa na tabia ya wivu sana
“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanja kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bila kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianza kujichukia Mwenyewe.
Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, nami nilitoa tabasamu
“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadi kulipopambazuka.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MOJA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
14 Comments
Dah fupi sana admin tuma mbili Leo Jana hukutuma hii pumz ya mwisho ni 🔥🔥🔥
Waoooow 🥰💯
Admin nyingn jmn 🔥🔥🔥🔥
Admini hii ni ya jana bado ya leo
Atleast sasa nimeanza kufurahi zahra kuwepoo
Jana hujatumia na leo ndio imeishia hapa
Admin umerudia mbn 😭😭😭😭😭ila 🤣jack kaulambaaaaaaa akome ingekua mm toka kitamb san nihsaolewana huyoooo osman🤣hata hila kusem yy ungekuta nishamtongoza zangu🤣🤣🤣🤣🙌
Hiyo ndo dawa ya wanawake kama kina jacklin….😏
Akomee huyu dada ..pumbaf
Adimin unasikia oja za ndugu zako tuma nyengne
Kusema ukwel j kayatimba hapo
🌝🌝 Lakini atajua mwenyew cz aliyataka
Leo n 11 jamn
admn vp ten tuma ya 11 Leo bwan
Admin umezinguwa see ya 11 pumzi ya mwisho hujatuma ,