IlipoishiaMama umemyoosha sana” 

“Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kile  sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufunguka  kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo Msichana  Mshikilie hadi mwisho.” 

“Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno” 

“Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena” 

“Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatu  kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,  akaingia Mwanaume mmoja.. Endelea 

 

SEHEMU YA TISA

“Nimebwana, naomba kujisaidia” Akasema Matilda huku akianza  kujikojolea, Mlinzi akamwambia Matilda 

“Nenda haraka” Akasema na kumsindikiza hadi chooni, choo  hicho kilikua cha ndani. 

Alipoingia huko alikua tayari ameshasoma ni namna gani  anaweza akaondoka hapo, akapanda juu ya sinki kisha akapita  katika kitundu kidogo ambacho kilikua juu kilichotumika kama  Dirisha la Choo, akadondokea chini, yule Mlinzi akaendelea  kusubiria hapo huku mwenzake akiwa anamwita. Matilda akapata maumivu kadhaa, jua lilikua linaanza kuzama, akatazama mbele  yake akaona ukuta ambao haukua mrefu sana, akafikiria kutumia  ukuta ili atimke hapo, akaparamia ukuta. 

Mlinzi akaona dakika zinasogea akagonga mlango, akajibiwa na  ukimya huku akianza kupata mashaka juu ya uwepo wa Matilda,  ikabidi afungue mlango, hakumkuta Matilda, akatazama pale  kwenye kitundu akaona dalili za Mtu kupitia hapo, akapanda  kwenye sinki akamwona Matilda akiwa anamalizia kuteremka  ukuta, akagongana naye macho. Matilda akajiachia, Yule Mlinzi  akatoka chooni akampa taarifa yule Mlinzi mwingine kisha  wakaelekea nje kwa ajili ya kuhakikisha wanamkamata Matilda  jioni hiyo. 

Matilda akajikuta yupo Msituni, akaanza kukata nyika  kuwakimbia walinzi hao ili asalimishe maisha yake, Walinzi  wakiwa na mbwa wakawa wanamfukuzia Matilda ambaye alionekana  kua na spidi kubwa sana, alikua kilomita kadhaa kutoka walipo  walinzi. Akaendelea kukata nyika huku giza likiwa linaingia,  akawa amechoka sana, alikua hajui ni mahali gani alipo, hivyo  alikua akikimbia kama mwendawazimu tu.

“Mama nilitereza naomba unisamehe kwa hili, nilikosea kabisa,  nipo tayari kulipa kwa hili, nakiri Mimi ni Mtoto mpumbavu  sana” Alisema James akiwa mbele ya Mama yake ambaye alikua  amekunja uso wake, watu kadhaa walikua wameshafika hapo kwa  ajili ya Msiba wa Patra. Chozi na makamasi yalikua yakimtoka,  Mama Naomi akamwonea huruma sana, akamtazama Mama James  lakini hakua na nguvu ya kusema chochote 

“Mamaaaaa!” akaita James huku akizidi kudondosha chozi, Mama  yake alikua kimya sana akiwa anatazama pembeni, kwa hasira  aliyokua nayo hakutaka kabisa kumtazama James 

“Mama James, rudisha moyo wako nyuma, huyu ni Mtoto,  ameteleza” Akasema Mchungaji George ambaye alikua bega kwa  bega na familia 

“Tunazungumzia Maisha ambayo hayawezi kurudi, yule Binti,  hawezi kurudi kwa namna yoyote ile, na Mama yake pia  asirudi?” akauliza Mama yake James huku akiwa amekaza macho  yake kwa Mchungaji George, Mchungaji akameza funda la mate,  swali aliloulizwa lilimfanya akae kimya. 

Chozi na jasho vilikua vikivuja kwa pamoja, James alijitahidi  sana kumwomba Mama yake amsamehe lakini Mama James  akashikilia msimamo kua hawezi kumsamehe hadi Matilda  aonekane. James akaondoka hapo Usiku

Hekaheka ndani ya Msitu ilikua ikiendelea, Matilda aliendelea  kuwakimbia wale walinzi wa Neema, alichoka akaamua kujibanza  nyuma ya Jiwe kubwa, walinzi nao walikua wameshachoka huku  wakihimizana kua kabla ya jua kuchomoza wahakikishe kua  wamempata Matilda. 

Matilda akalala hapo Msituni hadi siku iliyofuata, alipoamka  akaendelea na safari ya kutafuta msaada wa kutoka hapo  Msituni, akakatiza vijito na majabari makubwa na madogo huku  akiwa hajui ni wapi anaelekea. 

Moyoni mwake akawa anasema na Mungu wake kua amlinde Binti  yake, Masikini hakujua kua Binti yake alikua ameshafariki,  ghafla akasikia sauti za Mbwa akajua anapaswa kuongeza mwendo  wa kuendelea kuutafuta Msaada, akakimbia umbali mrefu akiwa  na njaa na kiu ya Maji akajikuta akianguka baada ya kuhisi  kizunguzungu. 

“Eee Mungu nilinde” Akasema Matilda, akahisi giza kisha  akapoteza fahamu. 

“Babu kinachofuata ni kitu gani?” Akauliza Neema, Babu na  Mama yake wakiwa mbele yake 

“Mtoto akizikwa habari yake itakua imeisha pia, James anaenda  kua mali yako bila kipingamizi chochote kile, hili ndiyo  jambo kubwa” Akasema Babu yake Neema, wakafurahi sana 

“Yaani Babu kama tutafanikisha hili nakuahidi kua nitakupa  zawadi ambayo hutonisahau” Akasema Neema 

“Huna haja ya kuahidi sababu wewe ni Mjukuu wangu Neema,  kikubwa upate unachohitaji, ukipata wewe Mama yako amepata,  basi ndiyo furaha yangu hiyo” 

“Pamoja na hayo Babu nitahakikisha nakujengea nyumba ya  kifahari, nitakua na pesa nyingi” Alisema Neema. Mama Neema  alikua Mtu wa kutabasamu tu akimwangalia Mwanaye na Babu yake  wakiwa wanazungumza, kicheko chao kilikua kilio upande wa  Mama James ambaye kila alipofikiria jinsi mambo yalivyoenda  alijikuta akiangusha kilio cha Mtu mzima. 

Moyoni alijua kua kuendelea kuzuia Mtoto kuzikwa ni sawa na  kumtesa Mtoto huyo lakini moyoni pia alikua akiumia Mtoto  kuzikwa bila Mama yake kuwepo, aliona ni sawa na kuzuia haki  ya Msingi ya Mama Patra, lakini hakuna aliyejua kilichokua  kikiendelea, Matilda alikua akipigana vita Msituni.

“Nipo wapi?” Akauliza Matilda baada ya kujikuta akiwa kwenye  nyumba moja ambayo ilikua imeezekwa makuti, hakuna aliye  mbele yake bali kitanda na ukuta uliojengwa kwa udongo wa  kugandika. Akakohoa kidogo, haraka akaingia Mzee Mmoja ambaye  alikua na ndevu ndefu, chafu zenye Mg’ao wa fedha, alikua na  rasta pia, Matilda akaogopa sana, wakati anajisogeza pembeni  akajikuta shuka ikiwa inamvuka, ndipo akagundua kua alikua  hana nguo yoyote ile, akarudisha macho kwa mzee kwa Mshangao 

Mara, akaingia Bibi mmoja ambaye alionekana wazi kua ni Mke  wa Mzee huyo. 

“Usiogope Binti, Nilikukuta ukiwa hujitambui nikakusaidia”  Akasema Mzee huyo, Bibi akaketi pembeni 

“Na wale watu waliokua wakinifukuzia?” Kwanza Bibi akacheka “Walishambuliwa na jeshi langu” Akasema Mzee huyo “Jeshi lako, unamaanisha nini?” 

“Siafu waliwashambulia walipotaka kukuchukua, wakakimbia  ndipo nikakusaidia” Hadithi hiyo ikamshtua sana Matilda. 

“Umepoteza fahamu kwa zaidi ya masaa matano, unahitajika  kupumzika zaidi ili kuvuta nguvu, lakini kwanini wale Watu  walikua wakikufukuzia?” Akauliza Bibi 

“Ni stori ndefu sana” Akasema Matilda baada ya kuona watu hao  si wabaya kwake, akawasimulia kilichotokea 

“Pole lakini unaonekana bado una tumaini kwa hayo unayopitia,  bado una Muda wa kurekebisha mengi” Akasema Babu huyo,  Matilda akaketi vizuri 

“Unamaanisha nini Babu” 

“Ulipokua umelala nilifanikiwa kuyaona yanayokuzunguka,  usishtuke sababu ipo Dunia isiyoonekana, ni Dunia ambayo  mambo huenda haraka mno, huyo Mtoto unayemzungumzia hapa yupo  kwenye usingizi mzito sana, hawezi kuamka kirahisi sababu  nguvu kubwa imetumika kumlaza” Akasema Babu huyo, Matilda  akashtuka sana

“Usingizi?, kwanza niko wapi hapa nataka kwenda kumwona Binti  yangu” 

“Hapa ni Mkata” 

“Mkata?” 

“Ndiyo, kilomita kadhaa kutoka hapa kuna barabara ambayo  inaelekea huko ulikotoka” 

“Umesema kuhusu Usingizi, sijakuelewa” 

“Namaanisha Mtoto wako amekufa katika Dunia hii lakini  anaishi kuzimu” Matilda akazidi kushtuka, aliyokua akiambiwa  yalimpa Mshtuko mkubwa sana, chozi likaanza kumtoka 

“Mtoto wangu amekufa?” 

“Ndiyo lakini usilie sababu bado hajaondoka, mwili umekufa  lakini nafsi inaishi kuzimu, kikubwa unatakiwa kuwahi kabla  hajazikwa” 

Wazee hao wakamwambia mengi sana Matilda, wakampa chupa ya  Maji, wakamwambia kua akifika anyunyize maji kwenye mwili wa  Binti yake, ataamka na kua sawa kabisa. 

Haikuishia hapo, wakampa nauli ya kurejea Dar.

“Mchungaji, naona namtesa Mjukuu wangu, hakuwa na kosa lolote  sitaki aendelee kuteseka zaidi. Kesho Patra azikwe” Akasema  Mama yake James, alizungumza mbele ya James 

“Asante Mama, najiona nimepoteza thamani kubwa sana katika  Maisha yangu. Nitamtafuta Matilda kadiri ya uwezo wangu Mama”  Akasema James, Siku iliyofuata 

Taratibu za Mazishi zikafanyika, mwili wa Patra ukawekwa  kwenda sanduku, vilio vilitawala, familia ilizizima, James  alilia sana mbele ya sanduku la Patra, alijutia sana  kumkataa, akatamani hata aamke ili amuombe msamaha Binti  yake, kila aliyefika aliona ni jinsi gani James alikua katika  hali mbaya sana 

Mchungaji George akaongoza maombi ya ibada ya mazishi ya  Patra, hatimaye sanduka la Patra likawa linashuka taratibu  kuelekea chini, ikasikika sauti ikisema

“Patraaaaaaaa” Ilikua ni sauti iliyotambulika kwenye masikio  ya walio wengi, vilio vilikoma, hakuna aliyeamini, walimwona  Matilda akiwa ameshikilia chupa aliyopewa kule Msituni 

“Msimzike Binti yangu bila kumwona” Alisema Matilda,  Mchungaji akawaamuru waliokua wakishusha sanduku kulirudisha  juu, Matilda akakimbia hadi kwenye sanduku la Patra, kisha  akageuka na kuwaambia 

“Patra hajafa msimzike” Alisema akiwa anatokwa na mchozi 

Ni kama watu walipigwa Bumbuwazi, hakuna aliyesema chochote  zaidi ya Mchungaji George ambaye alimuuliza Matilda 

“Unasema nini Matilda, Mtoto amekaa kwenye jokofu kwa siku  tatu. Ulikua wapi?” Akauliza 

“Mchungaji, moyo wangu unaniambia nimwone kwanza Mtoto ndipo  nieleze kilichotokea, chozi la James lilijikuta likikauka  lenyewe kutokana na Mshangao ambao alikua nao, minong’ono  ikaanza kusambaa miongoni mwa waliofika Kwenye mazishi. 

Mchungaji akawaambia walifungue sanduku ili Matilda amwone  Mtoto wake, sanduku likafunguliwa, Matilda akafungua chupa ya  Maji akanyunyiza kwenye sanduku 

“Unafanya nini?” Akauliza Mchungaji George 

“Patra ataamka sasa hivi” Alisema Matilda, Mchungaji akaona  Matilda amechanganikiwa, akawaamuru wannaume kumshika Matilda  ili Sanduku lifungwe 

“Mchungaji mwanangu ni mzima naomba Msimzike” alisema  Matilda, ukimya ukatawala kwenye sanduku, alichotegemea  Matilda kilikua ni sawa na njozi ya mchana, Patra hakuamka  kama alivyofikiria, akaanza kuona wale wazee walikua  wamemuongopea, alilia sana huku utaratibu wa kulifunga  Sanduku ukifanyika, Mama Naomi akamwambia Matilda 

“Mtoto amekufa Matilda hawezi kurudi” Mchungaji akamsogelea  Matilda akamwambia 

“Huu ni mwisho wa Patra lakini siyo mwisho wa Maisha yako,  pole kwa msiba” 

Katika hali ambayo kila mmoja alistaajabu, Patra akaamka  kwenye sanduku na kukaa kitako kitu ambacho si tu kilimfurahisha Matilda bali kilimshtua, tokea amezaliwa  hakuwahi hata kukaa lakini aliamka na kuketi kiisha akaanza  kushangaa watu. Wasio na moyo wa ujasiri walikimbizana  Makuburini, wachache wakabakia. 

Muda huo Babu yake Neema alikua amepata ishara mbaya  akamwambia Neema 

“Nenda Muhimbili kaokote kile kitu kakitupe jalalani haraka  sana” 

“Babu kwanini unasema hivyo?” Akauliza Neema 

“Nenda Neema fanya haraka sana” Akasistiza Babu yake Neema,  haraka Neema akakodi Pikipiki ili awahi Muhimbili,  haikuchukua muda mrefu, akawa amefika Muhimbili, akakimbilia  mahali ambapo alitupa kile kitu, kabla hata hajakiokota  kikawaka na kumwingia machoni, akawa anapiga kelele  akilalamika kua haoni, haraka akasadiwa kupelekwa Kwa  Daktari. 

Familia ikawa imekaa, kila mmoja akistaajabu maajabu ya Mtu  aliyekufa kurejea tena kwenye Maisha, ukimya ukawa mwingi  sana. Matilda akaanza kuwasimulia kila kitu, siku hiyo ndiyo  ikawa siku ya kumwona Mama yake James, huwezi amini Patra  alikua ni Mtoto mrembo sana, akitabasamu ni James Mtupu,  James akaomba Msamaha na kuahidi kua atafunga ndoa na Matilda  na kumlea Mtoto. 

Zikapita siku tatu mambo yakawa shwari, furaha na amani  ikazidi kutamaraki, kwa shukurani, James akampatia Mama Naomi  ile nyumba aliyokua akiishi Matilda, akampa pesa pia kwa  ajili ya kuanza Biashara. Siku moja akiwa ofisini akapokea  simu ya Mama Neema, alivyopokea akaambiwa kua Neema amepofuka  macho, James akamwambia kua ataenda kumwona. 

Baada ya kazi akaenda Hospitalini kumwona Neema, Mama Neema  akiwa analia sana kwa kile kilichomfika Binti yake. 

“Mama huna haja ya kulia, Mimi nimelia sana, Matilda amelia  sana, Mama yangu amelia sana. Siku zote Mshahara wa dhambi ni  umauti Mama” 

“Lakini James, Neema ana Mtoto wako tumboni, hupaswi  kumhukumu moja kwa moja”

“Namshukuru Mungu sababu amefumbua fumbo zito sana, sikuwahi  kuwa na thamani kwenu hata kwa yale makubwa niliyowafanyia,  nilikua mjinga sijui hata nilikwama wapi hadi nikamkataa  Mtoto wangu wa damu” Akasema James kisha akataka kuondoka 

“James, naomba msaada kama Mama, Neema anatakiwa kwenda  kutibiwa India, sina pesa hiyo Mwanangu, msaidie kwa hilo tu” 

“Siwezi kumsadia adui anayewinda Maisha yangu, alie mbele ya  Mungu wake, amwombe amsamehe” Akasema James kisha akaondoka,  Mama Neema akalia sana huku akijilaumu kwa kusema ni ujinga  wake kwani yeye ndiye aliyekua akimshauri vibaya Binti yake,  akaona ni bora kufa kuliko kuendelea kumwona Neema akiwa  kipofu, akaondoka Hospitalini na kumwacha Neema akiteseka  kwenye kutanda cha Hospitalini ya Muhimbili. 

MWISHO

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

 

18 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version