Ilipoishia “James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni Mtoto  wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”  alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibu  walishtuka 

“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanya  kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni Mtoto  wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyo  vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”  alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua na  hasira sana. 

Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, Mama  Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakini  ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James naye  aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,  aliondoa gari haraka sana.  Endelea 

SEHEMU YA TATU

Mama Naomi akamkimbilia Matilda kujua kwanini James alifikia  uamuzi wa kumpiga, hakuna alichokizungumza Matilda sababu  bado alikua akilia kutokana na kilichotokea, Mwanaume  aliyesababisha akatoroka kwao, akawapa Mawazo wazazi wake  aliishia kumpiga na siyo kujali hali ya Mtoto kisa tu ulemavu 

“Matilda usilie hebu nieleze kimetokea nini hadi akakupiga?”  aliuliza Mama Naomi 

“Niache Mama Naomi, ilipofikia nimechoka na mateso ya hii  Dunia ni bora hata nife tu” Alisema kwa hasira Sana Matilda  huku akilia kwa uchungu sana.

“Huo ni uamuzi wa kijinga sana Matilda, ukifa Patra atazidi  kuteseka, angalia jinsi anavyoteseka sasa hivi je ukifa  itakuwaje?” 

“Sasa nitakaa nikimwangalia Binti yangu akifa mbele ya macho  yangu alafu Baba yake akiwa na uwezo wa kumsaidia lakini  hafanyi hivyo, ni bora kufa kuliko kumwangalia Patra akifa”  Alisema Matilda. 

“Nakuomba Matilda kwasasa turudi nyumbani tutafakari jinsi ya  kuipata pesa ya Matibabu, hebu nyanyuka” Mama Naomi  alimnyanyua Matilda kisha aliondoka naye. 

******** 

“Mimi nina wao wazo Matilda, kwanini usiende kanisani kwenu  ukaomba Msaada kwa waumini wakakusaidia?” alisema Mama Naomi,  yalipita Masaa matatu baada ya kurejea nyumbani 

“Wataweza nisaidia kweli?” 

“Ndiyo nina imani kubwa watakusaidia sababu wewe ni Muumini  mwenzao” 

Ushauri wa Mama Naomi aliufanyia kazi, jioni ilipoingia  alienda kanisani, wengi walimshangaa maana baada ya  kujifungua hakuonekana tena kanisani, aliofahamiana nao  walikua wakimuuliza jinsia ya Mtoto, Maswali ya kuhusu Mtoto  yalizidi kumfanya Matilda ajisikie vibaya sana. 

“Mbona unalia?” aliuliza Mchungaji mara baada ya Matilda  kufika ofisini kwa mchungaji wa kanisa 

“Mchungaji Mtoto wangu” Alisema Matilda, Mchungaji alishtuka  akamuuliza 

“Mtoto wako amefanyaje?” 

“Mchungaji Mtoto wangu Mimi” Sauti ya kilio ya Matilda  ilisikikika na kumfanya Mchungaji aingiwe na maswali mengi  kichwani 

“Matilda Mtoto wako amefanya nini, hebu punguza kulia  uniambie” Alisema Mchungaji kwa sauti iliyojaa upole wa Hali  ya juu sana, kwikwi ilimshika sana Matilda kila alipotaka  kusema alijikuta akishindwa, kilio kilimuandama katika kila  neno alilohitaji kuzungumza, Mtandio wake aliutumia kufuta  chozi lililomiminika kwa wingi, moyo wake ulijawa na simanzi  ya hali ya juu sana. 

“Matilda tambua unanichanganya sana Mimi, sielewi hata nini  unataka kuzungumza. Nakuomba acha kulia sababu ukilia Mimi  siwezi kujua kilichokusibu” Alisema tena Mchungaji wakati huo  Matilda akiwa ameegemea Meza akiwa analia, hata Mchungaji  alilengwa na Mchozi kwa jinsi ambavyo Matilda alikua akilia  kwa uchungu, dakika tano zilikatika Matilda akishindwa kusema  chochote 

“Unasikia Matilda, kua na imani hakuna kinachomshinda Mungu  aliye hai, nijuze Mimi ili tujue tunakusaidia  

vipi….Unasikia….” Mchungaji alirudia kumbembeleza  Matilda, angalau kilio kilianza kupungua 

“Na hapo shavuni umekumbwa na nini?” Aliuliza Mchungaji,  shavuni Matilda alikua na alama ya kofi alilopigwa na James  kule Hospitalini. 

“Mchungaji napitia wakati Mgumu sana katika Maisha yangu,  Mtoto wangu yupo Hospitalini..” Matilda alijikaza akazungumza 

“Ulipotea kanisani kila Mtu akawa anajiuliza upo wapi  Matilda, kumbe ulijifungua….Enhee nini kinamsumbua Mtoto  wako?” Aliuliza Mchungaji ambaye alionekana kua na umri  mkubwa, ngozi nyeusi na mvi iliyokolea vizuri kichwani, akiwa  amevalia mavazi ya kanisa na msalaba mkononi. 

“Mtoto wangu ni Mlemavu, anasumbuliwa na Mapafu, anahitajika  kufanyiwa upasuaji na kibaya zaidi Baba yake Amemkana”  Alisema Matilda, kilio kilianza upya baada ya kumaliza  kumuelewesha Mchungaji ambaye alishikwa na butwaa, Matilda  alikua Muumini wa kabisa hilo sababu hata kwao alikotoka  alikua Binti wa kanisa hivyo alivyofika Dar alijiunga na  kanisa pia. 

“Yesu kristo! pole Binti yangu Matilda, hakuna linalomshinda  Mungu wetu aliye hai, yeye halali kwa ajili yetu, Mtoto yupo  Hospitali gani?” 

“JM Hospital, inahitajika Milioni nane aweze kufanyiwa  upasuaji, hapa nilipo sina hata senti tano na kadiri siku  zinavyozidi kwenda tumaini la Binti yangu kua hai linazidi  kupotea” Alisema Matilda akizidi kulia kaa uchungu sana. 

“Twende kwanza Hospitali kwa ajili ya maombi, baada ya hapo  kanisa litaangalia utaratibu wa kukusaidia” Alisema Mchungaji  akiwa ameshasimama,

“Asante Mchungaji George” Alisema Matilda, waliondoka hapo  kanisani kuelekea Magomeni Mapipa ilipo Hospitali ya JM,  waliondoka kwa gari maalum ya kanisa, Wakiwa barabarani  Mchungaji alimwambia Matilda 

“Hili jambo litaisha kwa namna nzuri Matilda, kua na imani  thabiti usitetereke. Kupitia Mtihani huu shetani anaweza  akajipenyeza na kukuingiza kubaya zaidi endapo  hautojiimarisha kiimani” Matilda aliitikia kwa kichwa kisha  alijishika tama. 

******** 

“Una uhakika?” lilikua ni swali aliloulizwa Neema, alikua  kituo cha polisi. 

“Ndiyo sababu yeye ndiye anayeishi pale” alisema Neema kwa  kujiamini kisha akatoa kitita kidogo cha pesa kwa siri sana,  Polisi akatabasamu sababu ilikua ni ishara kua alichokua  akikizungumza Neema kilihitaji kutengenezwa zaidi ili kiwe  kikubwa. 

“Jina lako?” Aliuliza Polisi akiwa anaandika jalada la kesi “Neema Ngushi, Miaka 32” 

“Mshtakiwa?” 

“Matilda John, Miaka 28” Alisema Neema 

“Vitu vilivyopotea vina thamani gani?” 

“Milioni 16” Alisema tena Neema 

Baada ya kumaliza kuandika maelezo marefu aliyoyatoa, alipewa  RB ya kumkamata Matilda, alichofanya Neema ni kwenda  kumfungulia kesi ya upotevu wa vitu kwenye nyumba anayoishi  Matilda, hakutaka kuendelea kumwona Matilda katika Maisha  yake, pembeni alikua amesimama Mwanaume mmoja ambaye kazi  yake ilikua ni kutingisha kichwa tu. 

Alipohakikisha amemfungulia kesi, walitoka na Mwanaume huyo  wakaingia kwenye gari, wakaondoka kituo cha polisi. 

“Unajua huyu Mwanamke anaweza kua kikwazo kikubwa sababu  James alikiri kua Mtoto ni wake lakini anaona aibu kulea  Mtoto ambaye ni kiwete, sasa hofu yangu ni kwamba akili ya  Matilda ikifunguka alalfu akaenda kudai haki, huwenda James  akajirudi kwake sababu atatakiwa kumtunza Mtoto kwa lazima na  pengine akachukuliwa hatua za kisheria alafu Mimi  nikahangaika” Alisema Neema akiwa anaendesha gari 

“Hapo usiwe na huruma hakikisha unamsotesha hadi akili imkae  sawa, James akijua itakuaje?” 

“Hata akijua hawezi kufanya chochote sababu nimeshamwambia  kua nataka nitengeneze mchezo ili Matilda akubali kurudi kwao  Njombe” Alisema Neema 

“Bingoo!!! Sasa tunaenda wapi?” 

“Naenda kukuacha kwako Sadam alafu Mimi nirudi nyumbani,  kesho tunamkamata Matilda, naamini kitisho hiki kitamfanya  akubali kurudi kwao” 

“Umetisha sana hakika wewe ni jembe la kujivunia Neema”  Alisema Mwanaume huyo kisha akaweka Mkono wake kwenye paja la  Neema ambaye alikua na Ujauzito wa Miezi mitatu tu. 

***** 

Saa 12 Jioni, Gari ya kanisa ilikua ikiingia kwenye geti la  Hospitali ya JM Magomeni Mapipa, Matilda alikua amelia sana  hadi macho yalimvimba, wakashuka na kuelekea Nje ya chumba  ambacho Patra alikua amelazwa, Macho ya Mchungaji na Macho ya  Matilda yaligongana na macho ya Daktari ambaye alikua akitoka  ndani ya Chumba hicho. 

“Dokta samahani hali ya Mwanangu inaendeleaje?” aliuliza  Matilda kwa presha. 

“Matilda Mtoto anaendelea vizuri kwasasa, aliamka kisha  akalala hadi sasa hivi” 

“Tunaweza kumwona?” 

“Ndiyo lakini hampaswi kumsumbua” Alisema Dokta akiwa  anaondoka 

“Asante Dokta, Mchungaji twende” Alisema Matilda kisha  alifungua mlango wa chumba hicho 

“Mwanangu!!” Alisema Matilda baada ya kumwona Binti yake  akiwa anapumulia Mashine, Roho ilimuuma sana.

“Oooh Jesus” Alisema Mchungaji, Chozi likaanza kumbubujika  tena Matilda, alikua Mtu wa kulia kila dakika kwa namna  ambavyo hali ya Binti yake ilikua, Mchungaji akamwambia  Matilda 

“Kulia hakusaidii chochote, ngoja tufanye kwanza Maombi ili  tumkabidhi Mtoto huyu na hali yake mbele za Mungu” Alisema  Mchungaji George 

Alianza kufanya Maombezi kwa Mtoto Patra, aliomba kwa imani  kubwa sana, Matilda naye alizama kwenye Maombi akisaidiana na  Mchungaji huyo, maombi yalifanyika kwa sauti ya chini sana  ili wasimsumbue Mtoto kama ambavyo Daktari alikua amewaambia.  Zilitumika dakika arobaini na tano hadi kumaliza kumwombea  Patra, Jasho lilikua likimvuja Mchungaji huyo ambaye kila  alivyomwangalia Patra alijiskia vibaya sana kwa jinsi hli ya  Mtoto huyo ilivyokua. 

“Mungu amepokea Maombi Matilda, anaenda kutenda kwa ajili  yako na Mtoto, atafungua minyororo ya mateso kwa Mtoto huyu,  amini kua amekwisha kombolewa” Ilikua ni kauli ya kutia moyo  ya Mchungaji huyo ambaye alikua amemshika bega Matilda, mara  aliingia Daktari akawaambia Muda umeisha. 

“Baby leo nimefanya kitu ambacho kitakuondolea hasira sana”  Alisema Neema akiwa anakula embe bichi, alikua akimwambia  James wakiwa chumbani Usiku. 

“Jambo gani hilo?” 

“Ni kuhusu Matilda” 

“Sitaki hata kumsikia huyo Mwanamke Neema, katika Maisha  yangu sijawahi pata ona Mwanamke King’ang’anizi kama Matilda”  Alisema kwa hasira James, alionesha wazi hataki kusikia  kuhusu Matilda ambaye alitoka kumpiga Kule Hospitalini. 

“Usikasirike sababu hili jambo litaenda kumfanya aondoke hapa  Dar bila kupenda Bby” 

“Nakusikiliza” 

“Hii hapa ni RB ya kumkamata kwa kosa la wizi wa vitu kwenye  ile nyumba, naamini akilala polisi siku moja akili itamkaa  sawa” Alisema Neema kisha alimpatia Karatasi kutoka polisi,  James akaisoma kwanza kabla ya kusema Chochote, kisha  akamtazama Neema

“Umemfungulia kesi?” 

“Ndiyo!! lengo langu apate kitisho kitakachomfanya aiyone Dar  chungu, nimefanya hivyo sababu sitaki kumwona Baba Mtoto  wangu mtarajiwa anakosa raha” Alisema Neema, James  alitabasamu sababu aliitwa Baba Mtoto, alihitaji sana Mtoto 

“Mbinu yako ni bora sana Neema, naamini kwenye hili  hachomoki, ataondoka hapa Dar atake asitake, tena kwa kuondoa  kero nitampatia na pesa ya kuanzia Maisha huko aendapo”  Alisema James kwa furaha 

“Umeona jinsi gani nakupenda, nakuhitaji na pia nakuthamini,  furaha yako ndiyo furaha yangu Mpenzi” Alisema Neema  akiendelea kula embe kwa chumvi. 

Neema alishajua udhaifu wa James, wala hakutumia nguvu nyingi  kumfanya James afurahi, ni kumweleza tu kuhusu ujauzito,  alichotaka alipewa bila hata kulazimisha. 

Siku iliyofuata, Neema alienda kituo cha polisi akaonana na  yule polisi ambaye aliandika jarada la kesi ya Matilda,  akaomba askari kwa ajili ya kwenda kumkamata Matilda, akapewa  askari polisi wawili akaenda nao moja kwa moja JM Hospital. 

Muda huo Matilda alikua kanisani, zoezi la kukusanya pesa kwa  ajili ya kuratibu matibabu ya Patra lilikua likiendelea  kanisani hapo chini ya uangalizi wa karibu wa Mchungaji  George ambayo alimwambia Matilda kua atasimama naye bega kwa  bega hadi Patra apone, Mama Naomi alikua miongoni mwa Watu  waliofika kanisani hapo baada ya kupewa taarifa na Matilda  kua litaendeshwa zoezi la Uchangiaji wa matibabu ya Patra. 

Chozi halikuacha kutoka kwenye macho ya Matilda baada ya  kuona uchangwaji wa pesa hiyo, muitikio ulikua mkubwa sana  kiasi cha kumtia moyo hata Mchungaji wa kanisa hilo ambaye ni  Mchungaji George. Nyimbo za kusifu zilikua zikiimbwa, kila  mwenye kua nacho alitoa kidogo alicho nacho kwa moyo wote  bila kujali 

Waumini waliungana kwa pamoja ili kurejesha furaha ya Matilda  ambaye alikua haamini macho yake jinsi kapu lilivyokua  linajaa noti. Mikono ya Matilda ilikua kwenye mdomo wake huku  chozi likiendelea kuvuja, tabasamu pana lilionekana kwenye  sura ya Mama Naomi ambaye alitoa wazo la Matilda kurejea  kanisani. Mchungaji George alimtia moyo sana Matilda katika  kila hatua ambayo walikuwepo, baadaye Mchungaji alikabidhiwa  kapu lenye fedha hizo.

Watu maalum wa kuzihesabu walianza kazi hiyo huku Mchungaji  George akitoa neno kanisani hapo 

“Hakika leo Bwana ameinuliwa, kwa moyo huu uliooneshwa hakika  roho mtakatifu yupo ndani yetu, kusimama na Mwenye matatizo  kunaongeza Baraka, hamjui ni kiasi gani Mungu anaenda  kuongeza kilichopungua kwenu. Mungu awabariki sana kwa jina  la yesu” Alisema Mchungaji huku kanisa likiitika haswa kwa  kusema 

“Aaameen” Matilda alizidi kulia kwa uchungu sana,  kilichomliza siyo tu kuumwa kwa Binti yake bali ni maisha  anayopitia baada ya kuitwa Mama, jinsi watu baki  wanavyosimama na yeye wakati Mwanaume aliyemfanya akatoroka  kwao hajigusi kwa lolote lile, alipiga magoti na kusema 

“Asante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja na  kumwinua 

“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji George  alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti.  Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umati  ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa Matilda  Msichana wa miaka 28 

Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikua  kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpa  ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisani 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

9 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version