Ilipoishia “Fanya haraka” Akaelekezwa mahali ambapo angemwona Matilda,  japo dakika mbili zisingetoshea kuzungumza naye ila alihitaji  kumwona na kupata uhakika kua ana Mtoto na Bosi wake,  akapelekwa chumba kimoja ambacho kilikua rasmi kwa ajili ya  kuonana na Mahabusu, akasubiria hapo Matilda aletwe, sekunde  chache Matilda akafika hapo akiwa ameongozana na yule Polisi 

Hakumkumbuka Jack sababu alimwona kwa Mara ya kwanza pale  ofisini kwa James hivyo ilikua rahisi kwake kukubali kuonana  na Jack, akaketi huku akiwa anamtazama sana Jack 

“Samahani na pole Matilda, Naitwa Jack” Alijitambulisha Jack 

“Unanifahamu Mimi?” akauliza Matilda akionekana alikua  ameteswa sana, uso ulikua na majeraha kadhaa 

“Ndiyo nakufahamu japo si sana”  Endelea

SEHEMU YA SITA 

“Mbona Mimi sikufahamu?” akauliza Matilda 

“Mimi ni mfanyakazi wa James, nimekuja nahitaji kujua baadhi  ya vitu kutoka kwako” Akasema Jack 

“Kwahiyo James amekutuma uje kwangu unilaghai kwa kutegemea  kua nitakubali si ndiyo, sikia nikwambie kitu kimoja,  Nimeamua kuishi Maisha ambayo sitaki kuitwa Msaliti na Mtoto  wangu, nitasimama naye hadi mwisho na kama unafikiria utaweza  basi nakwambia katu hautoweza kunishawishi kwa chochote kile,  nenda kamwambie James, kama Mtoto wangu atakufa basi atabeba  msalaba na kamwe sitakubali” Alisema kwa hasira sana Matilda  hadi yule polisi akaona ni bora amrejeshe Mahabusu maana  kusingezungumzika kabisa 

“Sina nia hiyo Matilda nakuomba unisikilize” akazungumza  lakini Matilda aliondolewa hapo, kisha baadaye yule polisi  akamfuata Jack 

“Usirudi tena, hii ilikua nafasi pekee” 

“Lakini sikua na nia ya kumkasirisha kabisa, nilihitaji  kumsaidia” Akasema Jack 

“Hayo hayanihusu Mimi, nimetenda wema niliopaswa kukutendea,  utamsaidiaje ni juu yako” Akasema Polisi huku akimtaka Jack  aondoke Kiunyonge sana tofauti na alivyoingia kituoni, Jack  alionekana akishusha ngazi kwa kutumia kiatu chake kirefu,  Macho yake yakatua waliposimama Mchungaji na Mama Naomi, Mara  moja wakasogea karibu kumpokea 

“Vipi umefanikiwa kumwona?” akauliza Mchungaji 

“Anaendeleaje?” akauliza Mama Naomi huku nyuso zao zikionesha  shahuku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea huko ndani 

“Hataki kuzungumza na Mimi, inaonesha ana maumivu makali  sana” Akasema Jack akiwa anasogea karibu na gari yake,  Mchungaji na Mama Naomi wakiwa wanamfuata 

“Yupo salama?” akauliza Mchungaji, Jack akatikisa kichwa kama  ishara ya kua Matilda hayupo salama. 

“Niambie Matilda amekuaje?” alihoji Mchungaji, yeye ndiye  aliyempokea Matilda kanisani kwa mara ya kwanza. hivyo  Matilda kwake ni sawa na Mtoto wa kumzaa. 

“Siwezi kuzungumza nahitaji kutuliza akili kuona ninamsaidia  vipi, Tutawasiliana” akasema Jack kisha akaingia kwenye gari  yake na kuondoka hapo haraka sana, akawaacha Mchungaji na  Mama Naomi wakiwa hawajui kilichoendelea kati ya Jack na  Matilda. 

“Ni bora angeeleza kiilichotokea kuliko kukaa kimya, hapana  shaka amemwona Matilda, roho inaniuma sana” Alisema Mama  Naomi akionekana kujawa na uchungu, chozi lilimlenga, alikua  hajatulia tokea asubuhi kwa ajili ya Matilda 

“Naomba urudi nyumbani giza linaanza kuingia, pesa hii  itakusaidia. Mimi narudi kanisani kwa ajili ya  maombi….Najua shetani yupo mahali anafanya kazi yake”  Akasema Mchungaji kisha akampatia noti ya Elfu Kumi Mama  Naomi 

“Lakini Mchungaji natamani nilale hapa ili nijue Matilda  anapitia wakati gani, naona kama tunamzika Matilda bila  kusikia kilio chake” Akasema Mama Naomi akiwa ameshika noti  mkononi huku chozi likianza kuvuja 

“Usilie..Hakuna marefu yasiyo na Ncha, kua na imani kua Mungu  atatenda na Matilda atatoka”

“Sawa Mchungaji” Alisema Mama Naomi, akaita Bajaji kwa ajili  ya kurejea anapoishi maana kwa muda huo ingekua shughuli pevu  kupata daladala, kwa wanaoishi Dar wanajua liingiapo giza  vurugu za kugombania usafiri zinavyochukua sura tofauti. 

Mchungaji alisubiria hadi Mama Naomi alipoondoka ndipo naye  akaondoka kituoni. 

******** 

Mawazo chungu mzima yalikua yakipita kwenye kichwa cha  Bilionea James, alikunywa pombe ili kuondoa mawazo yaliyokua  kichwani pake, moyo wake haukua na pingamizi kua Mtoto Patra  alikua ni damu yake lakini Neema alikua na ujauzito ambao  aliamini wazi ni wake. 

Alikua na tumaini kubwa la kupata Mtoto ambaye angekuja kua  Mrithi wa utajiri wake uliokithiri, hakupokea simu ya Neema  wala Mama yake Neema, alizidi kuchanganikiwa, licha ya  utajiri alio nao lakini alijikuta katika wakati mgumu sana  kisa Mtoto, akifikiria namna Matilda na Mtoto wanavyoteseka  anajikuta akikuna kichwa chake, alitamani sana kumsaidia  Matilda lakini pia wazo la kua Mtoto afe lilikua likimtawala,  kauli ya Matilda kua atahakikisha anamfilisi ilianza kumyima  raha, akamtafuta Chilo ili apate ushauri 

“Yupo sahihi sababu ana Mtoto ambaye akipimwa DNA  itagundulika wazi ni wako, akikufungulia kesi unafikiria  utatokea wapi Kaka? Hii serikali haiangalii una pesa kiasi  gani, kwa kifupi alichosema ana uhakika nacho James” Alisema  Chilo wakiwa wameketi mahali wakipeana Ushauri 

“Sasa nifanye nini, Nimhudumie Mtoto kisha nimtoe Matilda?” 

“Kama amekataa kurejea kwao hata kama utafanya yote bado  atakugandamiza James, Kama nilivyokwambia serikali ipo macho  sana kwa kesi za namna hii” 

“Sasa unanishauri lipi Kaka” 

“Kubali kua Patra ni Binti yako, mlee kama Binti yako, mfanye  Matilda aone mpo pamoja kisha mfanye wa siri ili Neema asijue  chochote hadi pale atakapojifungua” 

“Ushauri wako ni mzuri sana, nimetafakari usiku kucha  nawezaje kumaliza hili jambo katika namna ambayo itaniacha  salama” 

“Ikishindikana njia hiyo Kaka juwa kua hilo jambo ni gumu  kuliko ufikiliavyo, hapana shaka Matilda ana hasira nawe  kwasababu anahisi wewe umeshilikiana na Neema ili kumweka  yeye ndani” Alisema Chilo 

“Naamini Patra akipatiwa matibabu hilo haliwezi kua shida kwa  Matilda, ikibidi nitamtibia nje ya Nchi ili Matilda aende na  Mtoto huko, hadi wao watakaporejea Nchini nitakuwa  nimejipanga vizuri kuhakikisha hakuna kinachoharibika” 

“Tena hapo utakua umeuwa ndege wawili kwa jiwe moja Kaka,  Acha Neema aamini kua Matilda amerudi kwao lakini upande wa  pili unapambana kuhakikisha anatibiwa, naamini utashinda” 

Haikua rahisi kwa Jack kupata Usingizi usiku huo, taswira ya  Patra namna anavyoteseka Hospitalini iliendelea kujirudia  katika Ufahamu wake wa akili, alijikuta akiwa katika nyakati  ambayo kila alichokiwaza kilizidi kuibomoa akili yake, ikawa  ngumu kuukubali ukweli kua Bosi wake James alikua ametenda  unyama ule. 

***** 

Asubuhi mapema, Jack akaondoka katika makazi yake, alifunga  safari kuelekea kwa Mama yake James. Naam! alihitaji zaidi  kujua baadhi ya mambo ambayo yangemfanya apate njia ya  kulianza jambo hilo ambalo aliona wazi lilimhitaji kwa kiasi  kikubwa, alipahafahamu kwa Mama yake James, hata Mama yake  James alikua akimfahamu sana Jack, alipomwona alimkaribisha  ndani. 

Jua lilikua tayari limeshaanza kuchoma na kuunguza ngozi,  chai ikawa tayari, wakaketi mezani kwa ajili ya kuzungumza,  Mama James alishagundua kua kuna jambo lililomleta Jack pale 

“Karibu sana Jacklin” Alisema Mama yake James 

“Ahsante Mama” 

“Umenisusa sana Mwanangu” 

“Aaah Mama unajua majukumu ni mengi nakosa hata muda wa kuja  huku siku hizi” 

“Wala usijali naelewa” 

“Mama kuna jambo linanitatiza sana katika akili yangu,  limekua ni jambo lililobadili kabisa mtazamo wangu juu ya  James” Alisema Jack kisha alimtazama Mama yake James ambaye  alikaa vizuri kumsikiliza huku chai ikiwa inatoa mvuke

“Jambo lipi hilo mbona unanitisha Jack” 

“Mama….sijui hata nianzie wapi, naomba kujua, James ana  watoto wangapi?” aliuliza Jack, Mama James akashusha pumzi  baada ya kusikia swali hilo 

“James hana Mtoto..” 

“Una hakika Mama?” 

“Jack, Mimi ndiye Mama Mzazi wa James, akiwa na jambo ni  lazima anishirikishe……Hajawahi niambia chochote kile  kuhusu kua na Mtoto, isipokua yupo Msichana anayetarajia  kumzalia Mtoto, huyu namfahamu sababu alishawahi kumleta  Hapa, zaidi ya hapo hakuna Jack…sijui ni kwanini umeuliza  hilo swali” 

“Mama naomba nikwambie hili jambo, pengine nitatua mzigo  fulani kichwani pangu, James ana Mtoto ana miaka mitatu sasa  anaitwa Patra” Alisema Jack, Mama James akashtuka kidogo 

“James ana Mtoto? hilo haliwezekani Jack, hawezi kua na Mtoto  alafu anifiche Mimi, angeniambia tu” akasema Mama James 

“Hata Mimi nilishtuka na sikuamini kama wewe ambavyo huamini,  Mama,,James kua na Mtoto siyo tatizo ila tatizo ni kwanba  amemkataa huyo Mtoto kwasababu ni Mlemavu, na Hapa  ninapozungumza Mtoto huyo yupo Hospitali Magomeni hali yake  siyo nzuri, Mama wa Mtoto yupo polisi kwa kesi ambayo  inaonekana wazi kua James ameitengeneza…” 

“Jack hivi unajua unazungumza maneno mazito sana ambayo  hayaingii akilini mwangu, James hajawahi niambia kua ana  Mtoto. Hili jipya kulisikia.” 

“Mama hiyo ndiyo hali halisi, Mtoto amefanana sana na James.  Nimekuja hapa sababu sitaki Mjukuu wako azidi kuteseka,  sikujua kama James hakukwambia kuhusu hili, Mama nakuomba  fanya jambo katika hili vinginevyo Mtoto anaweza kufariki  kule Hospitalini” Akasema Jack akiwa na uso ulio poteza nuru,  alihitaji huruma ya Mama James kuingilia kati huku akiamini  fika kua si rahisi kumfikia James ambaye ndiye Bosi wake 

“Jack nahitaji kwanza kumwona huyo Mtoto ” 

“Kama tunaweza ongozana Hospitali muda huu itakua vizuri  Mama”

“Sawa!!” Mama James na Jack wakakubaliana kua waelekee  Hospitali kwa ajili ya kumwona Patra. 

Asubuhi hiyo, Neema akaelekea kituo cha polisi, akazungumza  na yule polisi ambaye alishapewa pesa ili kumshikilia  Matilda, wakazungumza kwa dakika kadhaa kisha Neema akaondoka  hapo, kitendo cha kupokea simu ya polisi kua James alienda  Polisi kilimfanya atengeneze mpango mwingine kwa ajili ya  kutekeleza takwa lake kwa Matilda ambaye kadili muda  ulivyokua ukienda alikua akiendelea kuteseka pale kituo cha  polisi, yule polisi akarudi ndani ya kituo maana maongezi  yalifanyika ndani ya gari ya Neema. 

Masaa matatu yakapita baada ya polisi kuzungumza na Neema,  Mchungaji George alikua nje ya kituo hicho huku akimpa Mama  Naomi jukumu la kushinda kule Hospitali, gari ya polisi  ikatoka. Mchungaji akaitazama sana gari hiyo pasipo kujua  kulikua na mpango ambao Neema alikua amepanga kuufanya.  Matilda alikua akihamishwa hapo kituoni muda huo huku ndani  ya kituo cha polisi kukiwa na jarada la kuachwa huru kwa  Matilda, nje kidogo ya kituo Neema aliingia kwenye gari baada  ya kuliona gari la Polisi likitoka hapo, akalifuata kwa  nyuma. 

********* 

“Dada, huyu ni Mama yake James” Ilikua ni sauti ya Jack, Mama  Naomi alimuona Mama James kwa mara ya kwanza, akamsalimia kwa  heshima sana 

“Mama huyu ni kama ndugu kwa Matilda ndiye anayeshinda hapa  Hospitali kuangalia hali ya Mjukuu wako” Alisema Jack, Mama  James hakutaka kuyaamini maneno ya Jack hadi pale  atakapomwona Patra, wakapewa ruhusa na Daktari kisha  wakaingia ndani ya wodi, Mama James akamwona Patra kwa mara  ya kwanza, alikua katika Mshangao Mkubwa sana, sura ya Patra  ilikua imefanana sana na sura ya James, Chozi la Mama James  likaanza kutiririka kila alivyozidi kumwangalia Patra, siyo  tu kwasababu ni Mjukuu wake bali kilichomliza ni jinsi  ambavyo Patra alikua juu ya kitanda akipigania uhai wake,  Mashine pekee ndizo zilizokua zikimpa uhai Mtoto huyo 

“Kwanini hukuniambia James?” aliuliza Mama yake James akiwa  ameshikilia kitanda kwa uchungu mkubwa sana, Jack akasogea na  kumshika Mkono Mama James akimtaka atulize hasira zake 

“Mama hiyo ndiyo hali halisi, jinsi unavyoumia wewe ndivyo  ambavyo Mama wa Mtoto huyu anaumia akiwa kituo cha polisi”  Alisema Jack huku Mama Naomi akiwa ametulia kimya

“Jack, miaka yangu 65 katika huu uso wa Dunia, sikuwahi  kuumia kama ambavyo leo naumia, hili ni Pigo Takatifu kwangu,  najiuliza kwanini James hakutaka kusema juu ya ujauzito hadi  Mtoto anazaliwa, Sina Mtoto mwingine zaidi ya James, pengine  sina Mjukuu zaidi ya huyu aliyelala hapa, lazima nipiganie  uhai wake” Alisema Mama yake James. 

“Lakini Mama pamoja na yote, sitaki James agundue kua Mimi  ndiye niliyekupa hizi taarifa” 

“Hilo usijali Jack, kikubwa ni huyu Mtoto awe salama,  atahamishwa hapa na kutibiwa kwa siri, kwakua James alimkataa  huyu Mimi nitalifanya hili kwa siri sana, pia nipo tayari  kuandaa wakili kwa ajili ya huyo Msichana aliye polisi,  nitalimaliza hili bila kuharibu upande wowote ule” Akasema  Mama yake James 

Muda wote huo Mama yake Naomi alikua akilia kwa furaha baada  ya mzigo huo kutuliwa, mzigo ulikua mzito upande wao maana  ilikua ni ngumu sana kupata pesa za matibabu ya Mtoto. 

Mama James akazungumza na uongozi wa Hospitali kwa ajili ya  kumhamisha Patra kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya Upasuaji,  jambo hilo likafanyika haraka sana, Gari maalum ya wagonjwa  ikaondoka na Patra na Mama Naomi huku Jack na Mama James  

wakielekea Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda, hadi  kufikia muda huo hakuna aliyajua kua Matilda alikua  ameondolewa kituo cha polisi huku mpango huo ukisukwa na  Neema. 

Safari ya gari ya polisi ilikua ni nje kabisa ya Jiji la  Dar-es-salaam, palikua na jumba moja lililo kando ya Msitu,  Matilda akaingizwa ndani ya jumba hilo lililoonekana kutulia  sana, Neema akaingia pia. 

“Kua Makini nimefanya kwa upande wangu, nahitaji hicho kiasi  kabla ya kupambazuka ili kama kuna kitakachotokea nisife kama  Mzoga” Akasema Polisi ambaye alicheza mchezo huo wa  kumhamisha Matilda na kuaandaa Jarada kua aliachiwa huru 

“Ndani ya Masaa 12 kuanzia sasa kiasi kitakua ndani ya  akaunti yako, ondoa shaka. Ahsante kwa hili, nikwambie tu kua  kazi yako imeishia hapa lakini si mwisho wa Mimi na wewe, huu  ni mwanzo mzuri” Alisema Neema kisha akatoa bahasha ambayo  ilikua imetuna akampatia Polisi huyo, Polisi akachungulia  akaona alichokiona ambacho kilimfanya atabasamu, kisha  akaondoka hapo mara moja.

Matilda hakujua amepelekwa wapi, Nani aliye nyuma ya mchezo  huo, mara akasikia mlango ukifunguliwa katika chumba ambacho  alikuwepo, akamwona Neema akiingia, aliongozana na Wanaume  wawili ambao walijazia vizuri, Matilda hakusema chochote  baada ya kumwona Neema 

“Ulihisi natania Matilda, pengine hujui wewe ni kikwazo kiasi  gani katika mipango yangu, uwepo wako ni tatizo kubwa kwangu”  Alisema Neema 

“Mimi sijakuzuia kumzalia James, lakini siwezi kuishi  mafichoni kisa wewe” Akasema Matilda, akapigwa kofi 

“Hivi unajua unazungumza nini wewe Mshenzi? James ana Mtoto  mmoja tu, huyu aliye tumboni na si vinginevyo, kwanini unakua  king’ang’anizi, sasa utakua hapa na Dunia itakutafuta sana  Matilda, hakuna atakayekuja kukusaidia hapa, na kama  utaendelea kuleta ubishi basi nitamuuwa Binti yako” Alisema  Neema, alionesha wazi kua hakua Mtu wa masiala kabisa 

“Unasemaje….Umuuwe Mtoto wangu? laiti kama kitamkuta  chochote Patra basi nitakulipiza” 

“Hata haumaanishi, utatokaje hapa hilo ni suala unalopaswa  kujiuliza kisha ndiyo uwaze utanizuia vipi…” Neema akatoa  simu yake kisha akamwonesha video ambayo ilivuruga akili ya  Matilda, video hiyo ilimwonesha Neema akiwa katika wodi  ambayo Patra alikua amelazwa, ilimdhihirishia wazi Matilda  kua Neema anaweza akafanya chochote kwa ajili ya kumdhuru  Patra. 

Tayari Mama James na Jack walikua wamefika kituoni, wakatoa  maelezo kua wanahitaji kumwona Matilda, wakaambiwa kua  Matilda alikua ameachiwa huru muda mchache uliopita,  iliwashangaza sana sababu kama angelikua ameachiwa huru basi  wangemwona 

“Afande Mimi nimekaa hapo nje kwa takribani masaa matano,  kama angekua ameachiwa basi ningemwona lakini sikumwona hebu  angalia vizuri” Akadakia Mchungaji George 

“Jarada lake hili hapa, sisi tunafanya kazi kwa maandishi,  tayari ameachiwa huru. Hatukuona sababu ya kumshikilia kwani  Mlalamikaji alikuja na kusema kua haitaji kuendelea na kesi”  Alisema tena yule polisi 

“Polisi Mimi ni Mama wa mlalamikaji, nimekuja kwa ajili ya  kumwona huyo Binti tafadhali” Alisema Mama James

“Jamani nimeshawaambia kua Msichana ameachiwa, jukumu la  kujua yupo wapi ni la kwenu sababu kwetu ameshatoka”  Akasistiza polisi huku akionekana haitaji kuendelea kubishana  nao 

Taratibu watatu wakashusha ngazi hadi chini, Jack akapiga  simu Hospitali ambako walikua wameenda kwa ajili ya Matibabu,  wakapata taarifa kua Matilda hakwenda huko. Taharuki ikawa  kubwa, hakuna aliyejua mahali ambapo Matilda alikua ameenda 

“Sasa atakua ameenda wapi au ameelekea kule Hospitali ambako  Mtoto amehamishwa?” akauliza Jack, akili zao zikawaza kwa  pamoja kua huwenda Matilda akawa ameenda huko, mara moja Mama  James na Jack wakaelekea Magomeni ilipo Hospitali ya JM. 

Wakati wao wanatoka kituo cha polisi, gari nyingine nyeusi ya  kifahari ikaingia hapo, akashuka James, yaani kama angewahi  kidogo tu angekutana na Mama yake na Mfanyakazi wake hapo  Kituoni, James alihitaji kuzungumza na Matilda, hakujua kua  Matilda alikua ameondolewa hapo na Neema, akaingia na  kujitambulisha, akapewa maelezo yale yale ambayo Akina Jack  walipewa, haraka akatoka hapo akajaribu kuipiga simu ya Matilda lakini haikuita, akampigia  simu Neema 

“Neema Nahitaji kuongea nawe sasa hivi, nieleze mahali ulipo”  Akasema James, akaelezwa mahali ambapo Neema alikuwepo,  akawasha gari kuelekea huko. 

Ilikua ni nje kabisa ya Mji, kitu ambacho kilianza kumpa  Mashaka James, akasogea hadi kwenye jengo ambalo Neema  alikuwa amemuelekeza James aende, Palikua ni msituni. Jengo  hilo lilikua katika eneo la peke yake kabisa, James  aliposhuka macho yake yakawa kwenye jengo hilo lililo kimya  sana, James akasogea kama alivyoelekezwa na Neema 

Alipoingia alisikia sauti ya Matilda ikiita, akashtuka sana  akaenda hadi kwenye hicho chumba akamkuta Matilda akiwa  amefungwa kamba 

“Matilda?” akaita James kisha akamkimbilia Matilda alipokua  amekaa, Chozi lilikua likimbubujika Matilda, James akamwambia  Matilda 

“Nataka nikutoe hapa sawa?” Akawa anafungua kamba lakini  akasikia Watu wakija kwenye chumba hicho, James akashtuka,  alipogeuka akamwona Neema, Masudi na wanaume wengine wawili 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

9 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version