IlipoishiaJames, ni wazi bado unampenda Matilda, ni wazi kua ipo siku  utakuja kunitelekeza na Mimba yangu kitu ambacho sipo tayari  kitokee” akasema Neema akiwa anamsogelea James 

“Neema sikutegemea kama ungekua katili kiasi hiki, hukupaswa  kumtesa Matilda kiasi hiki hata kama lengo lilikua aondoke..” 

“Ishia hapo hapo, James ulinipa ruksa ya kufanya kila jambo,  inaonekana kua moyo wako umerudi nyuma, umerudisha mapenzi  kwa Matilda si ndiyo?” akauliza Neema lakini James hakujibu  chochote huku macho yake akiwa ameyapeleka kwa Matilda ambaye  alikua njia panda sababu aligundua kua James alikua na nia  njema kwake na wala hakushiriki kumtesa kiasi kile. 

“Vizuri James, niliyajua yote haya pale niliposikia kua  ulienda polisi kumwona Matilda, Sasa James inabidi uchague  kitu kimoja, ilipofikia siko tayari kupoteza chochote” James  akasimama baada ya kusikia Hivyo 

“Unamaanisha nini?” 

“Nitamwacha Matilda endapo utakubali kufunga ndoa nami”  Akasema Neema 

“Najua hilo lazima likupe wakati Mgumu sana sababu tukiachana  tutalazimika kugawana Utajiri ulio nao, kama hilo ni ngumu  kwako basi Nitamuuwa Matilda” James hakua na jibu lolote la  kumpa Neema. 

Hadi kufikia Usiku hakukua na taarifa yoyote kuhusu Matilda  ni wapi alipo, Mtu pekee aliyefanikiwa kujua alikua ni James,  hilo lilimpa mawazo sana, alikunywa pombe huku akitafakari  yale aliyoambiwa na Neema, achague moja, kumwoa Neema au  kukubali Matilda afe, kingine kilichompa mawazo ni kwamba  Neema ni Mjamzito, kiu yake kubwa ilikua ni kupata Mtoto japo  alikua na Mtoto na Matilda lakini Mtoto huyo alimkataa sababu  alikua ni Mlemavu, Usiku huo hakutaka kuzungumza na Mtu  yeyote zaidi ya kunywa pombe akiwa nyumbani kwake. Akajikuta  akichanganikiwa kabisa, alikua na pesa nyingi lakini hakua  mwenye furaha, sababu kubwa iliyopelekea kutokua na furaha ni  maamuzi yake ya kumkataa Mtoto wake. 

Siku iliyofuata, bado Matilda aliendelea kutafutwa bila  mafanikio yoyote yale huku Mtoto wa Matilda akipatiwa  matibabu Muhimbili kwa hisani ya Mama yake James,  wakahangaika kila kona kumsaka Matilda, polisi bado  wakaendelea kushikilia msimamo kua Matilda aliachiwa huru

Upande wa James aliamua kuelekea Hospitali ili amwone Patra  kabla hajafanya maamuzi yoyote yale, akaambiwa kua Mtoto  alisha hamishwa hapo siku tatu zilizopita, akapewa anuani ya  Muhimbili, haraka akaelekea huko hadi kwa Daktari ambaye  alikua na jukumu hilo la kumtibia Patra 

Akapelekwa hadi kwenye Wodi ambayo alikuwepo Patra, moyo  wangu ukaingiwa na uchungu sana, akalia ndani ya moyo wake,  ni kweli Patra ni Mtoto wake lakini kilichomfanya amkatae ni  ile aibu kua Mtoto huyo ni mlemavu, Bilionea kama Yeye awe na  Mtoto mlemavu hakutaka kabisa kukubali ndiyo maana akaweka  nguvu kwa Neema kuhakikisha anamzalia Mtoto, mambo yakaanza  kwenda kombo huku tumaini la furaha likiingia huzuni 

“Mbona unalia, una uhusiano gani naye?” akauliza Daktari,  maana James alijitanbulisha kama Mfadhili, chozi likiwa  linamtoka akimtazama Binti yake ambaye alikua ameshafanyiwa  upasuaji, kilichomliza zaidi James ni kuhusu Matilda ambaye  alikua akipewa mateso na Neema. 

“Nimeguswa tu na Maisha yake, pengine anastahili kilicho bora  zaidi” Akasema James huku akiwa anafuta chozi lake, kwa mara  ya kwanza alijisikia vibaya sana kuhusu Patra. 

“Usijali hali yake itaanza kuimarika kadili siku zitakavyokua  zinasonga, tatizo lililokua likimsumbua tayari  tumeshaliondoa” Akasema Daktari huyo. 

Wakati huo Mama yake James na Mama Naomi wakiwa wanakuja hapo  Hospitalini, Baada ya kushuka kwenye gari Mama James  akamwambia Mama Naomi 

“Sikulala usiku wa jana, japo sijamwona huyo Binti aliyezaa  na James lakini nimejikuta nikimuwazia sana, sijui  anafananaje” Alisema akiwa anafunga mlango wa gari 

“Mama hata Mimi sipati usingizi tokea alipokua polisi, wakati  mwingine nachoka lakini nikifikiria kuhusu yule Mtoto  najikuta napata nguvu ya kuja hospitalini” Akasema Mama Naomi  wakiwa wanaanza kutembea kuelekea wodini 

“Hongera hakika wewe ni miongoni mwa wanadamu wachache ambao  wana mioyo bora sana hapa Duniani” 

“Mama Usijali sana namchukulia Matilda kama Mdogo wangu hivyo  chochote chake ni changu pia” Maongezi yaliendelea wakiwa  wanasogea wodini wakati huo James akiwa anamwambia Daktari

“Nitasimamia matibabu kuanzia sasa, kadi yangu ya Mawasiliano  ni hii hapa, kwa chochote nijulishe” Akampatia kadi Daktari 

“Mungu akuongoze ukaguse Maisha ya wengine wenye uhitaji Mr.  James” Akasema Daktari bila kujua kua aliyekua mbele yake  ndiye Baba wa Mtoto, Basi James akamuaga Daktari kisha  akatoka wodini wakati huo Mama yake akiwa anafika hapo,  wakapishana kidogo tu, James anageuza kisogo Mama naye ndiyo  anaingia akamkuta Daktari Daktari akiwa ameshikilia kadi 

“Karibu Mama, karibuni sana” Akasema Daktari huyo kisha  akaitia kadi mfukoni 

“Hali ya Mtoto inasemaje?” akauliza Mama James huku Mama  Naomi akiwa anatabasamu kwa namna mashine zilivyokua  zikionesha hali ya Patra 

“Hali yake Mungu anasaidia sana tena ashukuliwe zaidi na  zaidi sababu pasi na yeye hakuna Uhai wa Binadamu yeyote”  Wote wakatabasamu kwa maneno ya Busara ya Daktari 

Mchungaji George akawatangazia waumini wa kanisa lake juu ya  Mwenendo mzima wa Matilda na Binti yake sababu baada ya  mchango ule hakusimama Madhabauni na kuzungumza, akawaambia  hali halisi ya kinachoendelea huku akiwataka waumini kutoa  taarifa endapo watasikia au kumwona Matilda, kila mmoja  alisikitika sana, ikawa gumzo kanisani hapo 

“Ikibidi tufunge na kusali ili Mungu atuoneshe ni wapi alipo  Matilda” Akasema Mchungaji 

“Ameen” Waumini wakaitikia 

Mchungaji George akaanza maombi pamoja na waumini wote ili  Matilda apatikane popote alipo, pia hali ya Mtoto wa Matilda  iimarike zaidi na zaidi. 

“Mama, ilipofikia naona kama naenda kushindwa” Akasema Neema  mbele ya Mama yake, macho ya Mama Neema yakagongana na ya  Binti yake kisha akamtazama Masudi 

“Kwanini unasema hivyo?”

“James amerudi kwa Matilda. Nimefanya kama ulivyoniagiza  lakini inaonekana wazi kua ameanza kurejea upande wa Matilda”  Akasema Neema huku akiketi kwenye sofa 

“Kwa dawa ambazo ulikua ukimpa kwa kipindi chote sidhani kama  anaeza akathubutu kufanya hivyo, maisha yetu yamebadilika  Neema, hii ni ishara kua dawa zinafanya kazi. Cha Msingi ni  kuvuta subra ili aamue jambo letu” 

“lakini Mama anachosema Neema kina ukweli sababu jamaa  haeleweki sasa hivi, si kama zamani…” Akadakia Masudi 

“James hawezi kubadilika isipokua ni hofu zenu tu,  tulishamtengeneza vya kutosha, kala limbwata za kutosha  inawezekana vipi ndani ya muda mfupi mseme amebadilika?  kumbukeni huu ni mpango wa kufanikisha kupata pesa kwake,  kama ni hivyo basi Ujauzito hauna maana tena” Akasema Mama  yake Neema 

“Bado namshikilia kwanza Matilda ili nione msimamo wa James  utakua vipi, alafu pili nataka nijue Hospitali aliyolazwa  Mtoto wa Matilda, hiyo inaweza kua karata nyingine sababu  Hospitali ya Mwanzo hayupo” akasema Neema huku akiangalia  Ujauzito wake ambao ulianza kukua 

“Neema nafikili ulifanya makosa pale mwanzo, ulipaswa kumuuwa  Mtoto akiwa tumboni na siyo kumfanya azaliwe kilema, haya  yote yasingejitokeza sasa hivi, huu mvutano unatokana na yule  Mtoto, sasa inabidi tumuuwe tu hakuna njia nyingine” Akasema  Mama yake Neema 

“Mama, Kwasasa nakusikiliza wewe tu. Chochote ambacho  utakiamua nitakifwata sababu naona mambo yanataka kuniendea  kombo” 

“Basi mpigie simu Babu yako, Mwambie amuuwe Mtoto usiku wa  leo ili asubuhi kuwe na habari nyingine, kama ulivyosema  karata pekee inayoweza kutufanya tukatimiza adhma yetu ni  kumuuwa yule Mtoto kwanza” Akasema Mama Neema kisha akaketi  pia huku Masudi akifuatia kuketi 

Mpango mpya mbele yao ukawa kwanza kujua Mtoto amelazwa  Hospitali gani, kama alivyosema Mama yake, Neema akampigia  simu Babu yake ambaye alikua Mchawi haswa na ndiye  aliyesababisha Matilda akazaa Mtoto mlemavu. Babu yake alikua  haishi mbali sana na Jiji la Dar, alivyopata simu ya Neema,  haraka akaingia Dar akitokea Kiluvya – Kibaha.

Babu yake Neema aliyeitwa Mzee Mapinduzi, akajaribu kuangalia  namna ya kufanya lakini ikawa ngumu kujua Mtoto mahali gani  alipo, Maombi ya Mchungaji George yalionekana kuzuia jambo  hilo kufanyika, akawaambia 

“Simwoni Mtoto, Mna hakika yupo hai?” akauliza Mzee Mapinduzi  wakiwa sebleni 

“Babu, Mtoto yupo hai, Hospitali ya mwanzo alihamishwa”  Akasema Neema 

“Simwoni ndiyo maana nauliza, kuna kitu gani kinachozuia  hapa?…” 

“Basi Babu, nitafanya jitihada za kujua yupo Hospitali gani,  kesho tutajua Hospitali ambayo Mtoto amelazwa” Akasema Neema 

Wakati Neema na familia yake wakipanga namna gani wafanye,  Usiku huo Mama yake James akamwita James nyumbani kwake,  Haikumpa Mshituko James sababu alijua Mama yake hafahamu  chochote kile kinachoendelea, Mama yake James hakutaka  kumwonesha chochote kijana wake kua anajua kinachoendelea,  akamuuliza 

“Hivi Neema anaendeleaje, Maana tokea ile siku umemleta hadi  hivi leo sijamtia machoni, nawe husemi chochote kile” Sura ya  James ikapoteza Uchangamfu kidogo baada ya kusikia swali la  Mama yake, akamjibu 

“Neema anaendelea vizuri tu Mama, ni majukumu ya hapa na pale  ndiyo maana unaona kimya, hata hivyo nilipanga kuja naye ila  nikaona ni usiku nikamwacha apumzike” 

“Hivi James, katika pitapita zako hauna hata Mtoto wa  kusingiziwa kweli Mwanangu?” akauliza Mama yake kwa utani  hivi huku akitabasamu, James naye akatabasamu kidogo lakini  moyoni swali hilo lilimpa pigo takatifu 

“hapana Mama, sitaki litokee hilo, unajua ukishakua na hela  basi kila Mwanamke atataka kusema hivyo, siwapi nafasi  kabisa, Mjukuu pekee yupo kwa Neema, tarajia mazuri” Akasema  na kujichekesha, 

“Haya Mwanangu, Nami Mama yako natarajia mazuri kutoka kwako  na Neema, natamani sana kuitwa Bibi..”

“Usijali Mama yangu, muda siyo mrefu utapata Mjukuu wako…”  Wakazungumza kwa dakika kadhaa kabla ya James kuondoka. 

Maisha ya James yalibadilika hasa kutokana na kile kilichokua  kikiendelea, akahisi labda ni Mkosi wa kumkana Mtoto ndiyo  umepelekea kuingia katika nyakati ngumu ambayo kuingia kwake  ilikua rahisi lakini kutoka ikawa ngumu sana, alipewa siku  tatu na Neema ili atoe jibu kama yupo tayari kwa ndoa,  akilini mwake alishajua Mwanamke huyo alikua na tamaa ya  kuupata Utajiri wake lakini hakua na njia ya kumkwepa sababu  aliamini ana Mtoto wake tumboni, aliendesha gari kwa spidi  sana hadi nyumbani kwa rafiki yake Chilo 

Mara nyingi alipokwama alipewa ushauri na Chilo lakini siku  hiyo ilikua tofauti sana, Chilo alikua na Mke wake, aliziona  simu za James zikiingia lakini Mke wake akamwambia 

“Mwache Dunia imfunze, hiyo ni laana ya kumkataa Mtoto, usiku  huu akusumbue Mume wangu Akhaaa” Alisema akiwa anamkumbatia  Chilo ambaye aliyakubali maneno ya Mke wake, James alipiga  sana honi bila mafanikio yoyote yale kitu ambacho hakikua  kawaida, akashuka na kugonga geti kwa nguvu lakini hakuna  aliyefungua geti, akajaribu kumwita Chilo lakini hakupokea  jibu lolote lile, akazidi kuchanganikiwa, akarudi kwenye  gari, akaketi kumsubiria Chilo akiamini huwenda hajarudi  Usiku huo, akajikuta amepitiwa na Usingizi Mzito sana. 

Alipokuja kushtuka palikua tayari pamepambazuka, alishtuka,  hakuamini Bilionea kama yeye alale ndani ya gari, Mara Mke wa  Chilo akafungua geti wakati James akiendelea kujikagua,  haraka akashuka kwenye gari huku akipiga mihayo ya Uchovu 

“Habari Shem, mbona asubuhi mapema hivi kuna tatizo?”  aliuliza Mke wa Chilo kama vile siyo yeye aliyesababisha  James akalala kwenye gari, James alipoona Mke wa Chilo hajui  kama yeye alilala hapo akajifanya kuzuga 

“Nilikua na Mihadi na Chilo, ndiyo nimekuja lakini kama  hajaamka, basi kuna mambo naenda kuweka sawa kisha  nitawasiliana naye” akasema James kisha akarudi kwenye gari,  akaondoa gari hapo huku Mke wa Chilo akitabasamu tu 

“Na bado. wanaume wa namna hii wanaishia kuishi Maisha ya  Kimasikini sababu ya laana za kujitakia” Akasema huku  akilisindikiza kwa macho gari la James 

Mahali ambapo Matilda alihifadhiwa alihamishwa na kupelekwa  sehemu nyingine sababu James alikua ameshapajua, mpango ulio  mbele ni kumuuwa Mtoto wa Matilda ili James akose nguvu. 

Akatumwa Masudi kupeleleza ni wapi ambapo Mtoto amepelekwa,  Akaelekea Magomeni Hospitali, akaambiwa kua Mtoto yupo  Muhimbili, haraka akampigia simu Neeema na kumpa taarifa, 

Taarifa hiyo hiyo ikamfikia pia Mzee Mapinduzi, akamwambia  Neema 

“Chukua hii, katupe Muhimbili, katikati ya Hospitali,  inaonekana kuna nguvu inayonizidi ndiyo maana simwoni Mtoto”  Akasema Mzee Mapinduzi, akampatia Neema kitu mfano wa pipi  tena akamsistiza 

“Hakikisha mahali hapo Mtu hawezi kuokota wala kuigusa, ikae  hapo ili nimshughulikie” Haraka Neema, akaingia kwenye gari  akawaacha Mama yake na Babu yake wakiendelea kuzungumza huku  wakisubiria Neema akafanye tukio hilo. 

Ndani ya Hospitali, mambo yalikua shwari kabisa sababu hali  ya Patra ilianza kukaa sawa, maombi ya Mchungaji na Matibabu  ambayo Mama James aligharamia yaliimarisha afya ya Mjukuu  wake japo alifanya kwa siri James asijuwe, Patra alikua  akitabasamu huku akitazama walio mzunguka, alionekana  kuhitaji kuuliza ni wapi alipo Mama yake lakini Mtoto huyo  alizaliwa akiwa hajui kuzungumza kutokana na Uchawi ambao  familia ya Neema ilimfanyia, Mbele ya Patra alikua amesimama  Mama James ambaye ni Bibi yake, Mama Naomi, na Mchungaji  George 

“Hakika Mungu aliye hai ametenda miujiza” Alisema Mchungaji  George kwa Furaha kubwa kutokana na hali ya Patra ilivyokua  ikiimarika 

“Asante sana Mchungaji, maombi yako yamesaidia sana, mara ya  kwanza nilivyomwona Mtoto huyu roho yangu iliumia sana,  Malaika asiyejua chochote alikua akiteseka sana, hadi kua  hivi leo ni Miujiza tu” Alisema Mama Yake James 

“Itakua siyo busara kama tutasahau kumshukuru Mama Naomi, ni  ngumu Dunia ya sasa kupata Jirani kama Mama Naomi hasa katika  Jiji hili ambalo kila Mtu yupo bize” Akasema Mchungaji 

“Ni kweli kabisa, Asante Mama Naomi, Mjukuu anaendelea  vizuri. Sasa kilicho mbele yangu ni kuhakikisha tunampata  Matilda ili ashuhudie Muujiza huu” Akasema Mama yake James 

Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwa  kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua ni  James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee Hospitali  kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. Akaketi 

kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namna  mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari ya  Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini James  alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepaki  sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingia  akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. Endelea 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

14 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version