Ilipoishia  “James una hakika kuwa hii ni Mimba yako?” Lilikua ni swali  aliloulizwa James, walikuwa chemba na Mama yake wakimuacha  Neema akiwa sebleni 

“Ndiyo Mama kwanini unauliza hivyo?” Alihoji James akiwa  anamtazama Mama yake, alikua ameenda kumtambulisha Neema kwa  Mama yake huko Kiwalani 

“Nimekuuliza tu sababu imekuwa ghafla sana James”  Endelea 

SEHEMU YA PILI

“Ha!ha!ha! Mama hilo lisikupe presha kabisa nilipanga  kukufanyia sapraizi Mama yangu sababu najua ulikua na hamu ya  Mjukuu. Baada ya kutafuta pesa nyingi niliona furaha pekee  kwako ni Mjukuu Mama” Alisema James akiwa anatabasamu, Mama  yake akachungulia sebleni akamtazama Neema kisha macho  akayarudisha kwa James 

“Sawa Mwanangu, sijui kwanini Moyo wangu unaniambia tofauti,  ila Usijali Baba” Alisema Mama yake James 

“Basi Mama uchangamke ili Mgeni asijisikie vibaya sawa?” “Sawa Baba” 

Baada ya Maongezi walirejea Sebleni, Neema hakujua chochote  kile, aliona mambo yakiwa kawaida, Mama yake James akaongeza  uchangamfu kwa Neema 

“Karibu Mkwe wangu, nimesikia taarifa kuwa una kichanga cha  Mwanangu” Alisema Mama yake James akiwa anatabasamu, hata  James alitabasamu 

“Ndiyo Mama, nategemea kupata Mtoto kwa Majaliwa yake Mungu”  Alisema Neema akiwa anatabasamu pia, furaha ikawa kubwa sana.  Baada ya muda waliopanga kuwa hapo kuisha iliwalazimu warudi  wanapoishi kwenye jumba la Kifahari la James. 

Kutokana na furaha aliyokua nayo James alimuahidi vingi Neema  kama atamzalia Mtoto mzuri wa kiume, alimuhesabia vitu  ambavyo angempa ni pamoja na kampuni yake ya kuuza Magari,  Jengo la Ghorofa lililopo Kurasini na Gari jipa aina ya BMW  X6. James Kyando alikua na pesa nyingi lakini hakubahatika  kupata Mtoto katika Maisha yake hivyo alihitaji Mtoto aje kua  Mrithi wa mali zake. 

Neema aliishi Maisha ya kifahari sana, akaahidiwa ndoa endapo  Mtoto atazaliwa, James akahakikisha anamuajiri daktari Maalum  kwa ajili ya kuchunguza afya ya Mtoto na Neema mwenyewe, kila  alichotaka Neema alikua akikipata sababu furaha ya James  

ilikua ni Mtoto tu. 

“Baby Naamini utaniheshimisha sana, nitapata heshima kubwa  kuliko hivi sasa. Mtoto akizaliwa wa Kiume nitamwita Lameck”  alisema James akiwa amelishika tumbo la Neema 

“Kama atazaliwa wa kike?”

“Akizaliwa Malikia wa kike nitamwita Princes Ana” Alisema  James 

“Waoooh Jina zuri sana James wangu” Alisema Neema. Pale pale  simu ya James iliita ikakatisha maongezi yao, aliangalia  aliyekua akipiga akaona ni Matilda 

“Eeeh huyu Mwanamke Usiku huu anataka nini tena?” aliuliza  James Kyando, haraka Neema akaipora simu ya James 

“Unamuendekeza baby, si umfukuze pale jamani? ningekua Ni  Mimi yaani wala nisingemuendekeza kiasi hiki hadi anisumbue  Usiku kama huu” Alisema Neema, James akaipokea simu hiyo 

“Unasemaje Matilda huoni kama ni Usiku mwingi sasa hivi?”  alihoji James, hakujua kua Matilda alikua katika nyakati  ngumu sana ya kumpambania Mtoto Hospitalini, sauti ya kilio  ikasikika, Matilda akaongea akiwa analia 

“James Mtoto yupo Hospitali anatakiwa kufanyiwa upasuaji  kusafisha Mapafu..” Alisema Matilda huku kwikwi ikiwa  imemshika 

“Kwahiyo unaniambia hivyo kwani Mimi ni daktari, ina maana  kupiga simu usiku wote huu ni kwa ajili ya ndondocha wako?”  alisema James 

“James usiwe mkatili namna hiyo, Patra ni damu yako,  usimuache akaangamia kisa Mlemavu” Alisema Matilda akizidi  kulia 

“lengo la kunipigia ni nini?” 

“Upasuaji unahitaji Milioni 8 nami sina hiyo pesa James”  Alisema Matilda 

“Tuwasiliane asubuhi” Alisema James kisha alikata simu ya  Matilda, akamtazama Neema ambaye alikua amenuna 

“Baby ina maana umekasirika?” aliuliza Neema 

“Unaongea na Mwanamke mbele yangu alafu unataka nifurahie si  ndiyo? Hivi james kwanini unataka kunipa presha isiyo na  msingi wakati unajua fika kuwa Mimi ni Mjamzito?” aliuliza  Neema. 

“Nalijua hilo ndiyo maana nimemwambia anipigie asubuhi  nimsikilize anataka kusema nini?”

“Unaniona mimi Mtoto si ndiyo James, si nimesikia hapo kua  Mtoto amelazwa Hospitali, hivi James yule Mtoto ni wako au si  wako?” 

“Nawezaje kuwa na Mtoto mlemavu na pesa zote hizi Neema? Si  Mtoto wangu yule isipokua huruma yangu kwake ni kwasababu  alikubali kutoroka kwao Njombe na kuja Dar kwa ajili yangu,  kuna wakati naingiwa na Moyo wa huruma sana” 

“Nitaamini vipi kama si Mtoto wako? Unajua sitaki Mtoto wangu  atakapozaliwa akute marumbano, sitaki aanze kusikia kuna  mtoto mwingine tena mlamavu” 

“Unataka nifanye nini Neema?” 

“Mfukuze pale, mpe pesa arudi kwao. Napata kichefu chefu kila  saa anakupigia na kukulilia, ona sasa hivi tulikua  tunazungumza mambo ya Maana matokeo yake anapiga simu na  kuanza kujiliza kisa Mtoto ambaye si wako” Alisema Neema,  James hakujibu chochote kile. 

***** 

“Mtoto akiendeela kuwa katika hali ya usaidizi wa Mashine ni  gharama pia Neema” Alisema Daktari ambaye alikua akimhudumia  Patra Hospitalini 

“Dokta hali yangu unaijua, nahangaika huku na kule ili kuokoa  uhai wa Binti yangu, tusubirie hadi kesho asubuhi pengine  naweza kupata tumaini lolote juu ya hali ya Binti yangu”  Alisema Matilda, ulikua ni usiku akiwa ameketi nje ya chumba  cha uangalizi maalum ambacho Binti yake alikua amelazwa 

“Kwani Baba yake anasemaje?” Aliuliza Daktari, Tayari Matilda  alikua ameshadondosha chozi, akalifuta 

“Baba yake amemkataa sababu ni mlemavu Dokta, roho inaniuma  sana, katika vitu ambavyo namuomba Mungu katika hii Dunia  basi ni kuhusu Binti yangu kupona sababu najua huu mzigo ni  wangu peke yangu” Alisema Matilda akiwa analia, Dokta akaketi  ili amsikilize vizuri 

“Usilie Matilda, hebu nieleze ilikuwaje?” Aliuliza Dokta,  Matilda alianza kumsimulia Dokta namna ilivyokua japo alikua  analia lakini alimudu kueleza

Wakati Matilda akiwa shule huko Kijijini Njombe alikutana na  James kwenye Mashamba ya Maparachichi, James alikua akilima  Maparachichi huko, walipokutana kwa mara ya kwanza Matilda  alipokua akiomba kazi ya kuvuna Maparachichi, James alivutiwa  sana na Matilda 

Alimpatia kazi katika Shamba hilo kubwa la kisasa ili awe  kibarua ili tu apate kua karibu naye, akamueleza jinsi  alivyovutiwa naye siku moja wakiwa shambani 

“Mmh!! Mimi masikini hivi nije kuwa na wewe, haitowezekana  tafuta Msichana mnayelingana kifedha” Alisema Matilda 

“Mapenzi ni upofu Matilda, moyo hauna macho wala hauoni,  popote hutua kama ndege kwenye Bustani nzuri ya Maua” Alisema  James, maneno ya James yalimuingia Matilda akawa anatabsamu  tu 

“Ukikubali kua na Mimi na ukanizalia Mtoto nitakupa nusu ya  Mali zangu Matilda, utajiri huu utakua wako na nitakuowa,  pamoja na hela zote nilizo nazo Mimi sina Mtoto hata wa  kusingiziwa” Alisema james 

Matilda aliomba muda wa kutafakari jambo hilo, hakutaka  kukurupuka sababu bado alikua mwanafunzi wa chuo cha ufundi  veta, Baada ya siku tatu alimpa jibu James 

“Najua kwanini inakua ngumu kwako, sababu unaogopa wazazi  wako lakini nataka kukwambia kitu Matilda, endapo utakubali  basi utaokoa Maisha ya familia yako itaondokana na Umasikini  kabisa” Alisema James wakiwa ndani ya gari ya James 

“Nataka uje kuishi na Mimi Dar, nitakutunza kama Malkia  Matilda” Maneno ya James yalimshawishi sana Matilda, James  aliporudi Dar baada ya kumaliza mavuno, aliwasiliana na  Matilda kupitia simu ambayo alimnunulia,,Matilda akatoroka  kwao Njombe akaenda kuishi Dar na James. 

Wakati Matilda anamsimulia Dokta, mara ikaja taarifa kuwa  hali ya Patra imebadilika, Dokta akakimbilia chumba cha  Uangalizi kwa ajili ya kuangalia hali ya Patra. 

Matilda alikesha akimuomba Mungu asimchukue Binti yake kwani  bado anampenda sana, asubuhi ilimkuta akiwa macho. Mama Naomi  alikuja Hospitalini asubuhi hiyo kwa ajili ya Kumjulia hali  Patra 

“Hali ya Patra ilibadilika Usiku, hata hivyo hadi sasa hakuna  taarifa yoyote ile Mama Naomi” Alisema Matilda

“Mungu atampigania Binti yako, Usijali sana Matilda, wewe ni  Jasiri sana” Alisema Mama Naomi, akampatia Matilda chupa ya  chai na Chapati ili apate kifungua kinywa maana tokea jana  hakula chochote zaidi ya kulia. Mara simu ya Matilda iliita,  aliyekua akipiga alikua ni James, akafuta chozi kisha  akapokea haraka sana. 

“JM hospital, Magomeni Mapipa” Alisema Matilda kisha simu  ilikatwa 

“Nani huyo?” 

“James” 

“Anakuja?” 

“Ndiyo Mama Naomi” 

“Asante Mungu pengine huu mzigo atakutua Matilda, nilikwambia  Mungu yupo macho anaona” Matilda aliitikia kwa kutumia kichwa  huku akivuta pumzi kubwa, chozi lilikua likimbubujika muda  wote hata alipokua akilifuta halikuacha kudondoka, Mama Naomi  aliona ni jinsi gani Matilda alikua katika wakati mgumu sana 

Mama Naomi aliketi kando kisha akamnyonyesha Naomi maana  alikua bado Mdogo, kilichokua kinamsukuma zaidi Mama Naomi  kumsaidia Matilda ni kwasababu hata yeye amepitia Maisha hayo  bada ya kujifungua, Baba Naomi alimtelekeza na kwenda kuishi  na Mwanamke mwingine, alimuacha akiwa hajui atakula nini wala  ataishi vipi, alishawahi mwambia Matilda kua atasimama naye  bega kwa bega hadi pale Mambo yatakapokua sawa. 

******** 

“Umemwambia Maimuna?” Aliuliza Baba yake Matilda 

“Ndiyo huwenda ameenda Njombe Mjini kama atafanikiwa kumwona  basi amueleze kua sisi tunamtafuta sana, arejee tu wala  hatuwezi kua na hasira naye” Ilikua ni kauli ya Mama yake  Matilda 

Familia ilikua katika nyakati nzito zilizojaa maumivu ndani  yao, walikua masikini waliotegemea vibarua katika Mashamba ya  Parachichi. Matilda alikua ni Mtoto pekee kwao. 

Yalipita masaa matatu, James aliwasili JM Hospital akiwa na  gari yake ya kifahari, jinsi alivyo ilitosha kukwambia kua 

alikuwa na kila kitu katika Maisha yake, aliposhuka  hakuhitaji kuhangaika akavuta simu akampigia Matilda, Mara  moja Matilda alifika alipo James, 

Chozi lilikua likimbubujika, James alifanana sana na Patra  kila alipomuangalia alizidi kuumia ndani ya nafsi yake,  alisimama mbele ya James aliyekua akitabasamu, ilionekana  wazi kua alikua akimdhihaki Matilda, akavua Miwani kisha  akamuuliza Matilda 

“Utaendelea kuishi kwenye kivuli cha Patra hadi lini?” “Unasemaje James?” 

“Umenisikia, sikia nikwambie Matilda, ni bora urudi kwenu  sababu muda utafika na hautokua na sehemu ya kuishi, nitakupa  pesa umtibie Mtoto wako na pia uondoke hapa Mjini” Alisema  James 

“James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni Mtoto  wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”  alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibu  walishtuka 

“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanya  kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni Mtoto  wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyo  vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”  alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua na  hasira sana. 

Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, Mama  Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakini  ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James naye  aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,  aliondoa gari haraka sana. 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

10 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version