IlipoishiaAsante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja na  kumwinua 

“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji George  alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti.  Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umati  ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa Matilda  Msichana wa miaka 28 

Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikua  kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpa  ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisani. Endelea

SEHEMU YA NNE

“Asanteni kwa wote, asanteni sana. Nilikata tamaa kabisa  lakini roho mtakatifu ameniinua kupitia nyie” Alisema  Matilda, Chozi lilimbubujika kilio kikamzidi maarifa akaweka  kipaza sauti huku akimpa ishara Mchungaji kua hawezi  kuzungumza kabisa.

Kanisa kikazizima, hadithi ya Maisha ya Matilda ikawaliza  wengi, bahati nzuri muda huo wataalam wa kuhesabu pesa  walikuwa tayari wamemaliza, Mchungaji akawatangazia kua  wamepata Milioni tano, Matilda hakuamini masikio yake 

“Sikutegemea kabisa kama kwa taarifa hii iliyo ghafla  tungeweza kukusanya kiasi kikubwa namna hii, pesa hii itaenda  moja kwa moja Hospitali muda huu ili Mtoto aanze matibabu”  Alisema Mchungaji, Akawaambia waumini waendelee na ratiba  zingine, yeye, Mama Naomi na Matilda wakaingia kwenye gari ya  kanisa, safari ya kuelekea Hospitali ikaanza. 

“Mama Matilda, napata hisia mbaya juu ya Mtoto wetu” Alisema  Baba Matilda akiwa ameketi kwenye Mkeka, Mama Matilda alikua  akimalizia kuweka kuni jikoni, kauli ya Mume wake ikamfanya  aache alichokua anakifanya, akapiga hatua za taratibu huku  sura yake ikijawa na Mshangao akamsogelea Mume wake,  akajishika kiuno 

“Kwanini unasema hivyo Baba Matilda?” 

“Jana usiku nimeota ndoto mbaya sana kuhusu Matilda, sina  hakika kama Atakua hai na kama yupo hai basi anaishi kwa  Mateso ya Golgota” Akasema Baba Matilda huku akikunja vizuri  goti lake wakati huo Mama Matilda akivuta kigoda na kuketi  huku macho yake yakiwa bize kwenye sura ya Mume wake 

“Mungu amuepushe Binti yetu na majaribu yoyote yale, hujui  jinsi roho yangu inavyouma Baba Matilda” Akasema Mama Matilda  huku akifuta chozi lake 

“Tokea nikiwa shambani leo sijisikii vizuri kabisa,  nimeliweka jambo moyoni kama Mwanaume lakini Mwisho wa siku  nimeshindwa nimeona ni bora nilitoe, Huu wasiwasi sijui  utaondoka lini” 

“Baba Matilda Mtoto yupo hai, na anatukumbuka sana. Ewe  Yehova tenda kwa ajili ya Binti yetu popote alipo, mpe roho  ya kurejea nyumbani ili sisi tuwe na Amani” Akasema Mama  Matilda mikono ikiwa juu, Hakika familia hii ilikua yenye  misingi thabiti ya dini. 

“Kama siyo huu umasikini basi ningeenda Mjini kumtafuta  Matilda, hatuna Mtoto mwingine sisi” Jinsi Baba Matilda  alivyokua akilalamika alizidi kumfanya Mama Matilda adondoshe  chozi lake. 

“Baba Matilda moyo unaniuma sana tena zaidi ya sana, nikiwa  kama Mama naumia kuliko unavyofikiria” Alisema Mama Matilda  kisha akaingia ndani akiwa analia, alimuacha Baba Matilda  akiwa amejishika tama. 

Mchungaji, Matilda na Mama Naomi walikua kwenye kordo la  Hospitali tayari kuelekea kwa daktari kwa lengo la kukabidhi  pesa ili upasuaji uanze. Ghafla polisi waliwasimamisha,  sintofahamu ikatawala 

“Sisi ni Maafisa wa polisi, Matilda upo chini ya ulinzi  kuanzia sasa..” Alisema askari mmoja, Matilda alishtuka

“Mimi?” 

“Ndiyo” Akasema polisi 

“Afande…huyu Binti amefanya nini?” alihoji Mchungaji George  kwa Mshangao Mkubwa sana. 

“Utajua ukifika kituoni, ruhusa ya kukamatwa kwake hii hapa”  Alionesha 

“Polisi nimefanya nini Mimi jamani, tafadhali msinifanyie  hivyo. Binti yangu ni mgonjwa sana anahitaji matibabu”  Alisema Kwa kilio Matilda lakini tayari pingu zilikua  zimeshafungwa kwenye mikono yake, pesa zilikua mkononi mwake,  haraka Mchungaji akataka kuzichukua lakini polisi wakazuia 

“Chochote mtakachokifanya hapa kitatumika kama Ushahidi  Mahakamani” 

“Vijana, tafadhari sana hizo ni pesa kwa ajili ya matibabu ya  Mtoto, kama mnamkamata Matilda basi hizo pesa hazihusiani na  sababu yoyote ile ya Kumkamata, hizi ni pesa kutoka kanisani”  Alisema Mchungaji George akitaka pesa ziachwe lakini polisi  hao walikua tayari wameanza kumchukua kwa nguvu Matilda  ambaye alikua akipiga mayowe ya kutaka aachwe ili akamtibie  Binti yake Patra. 

Aliyeucheza mchezo huu alikua amejibanza mahali akiangalia  namna mpango wake unavyofanikiwa, Neema akashangilia baada ya  Matilda kutupwa kwenye difenda ya polisi, gari hiyo ikaondoka  haraka sana. Mchungaji na Mama Naomi wakatazamana kwa  mshangao mkubwa hawakujua waende wapi, waingie kwa daktari  bila pesa au waelekee Kituo cha polisi ambacho walikua  wametajiwa. 

“Mchungaji nenda Polisi Mimi naenda kwa Mzazi mwenzake”  Alisema Mama Naomi huku taharuki ikizidi kuwa kubwa ndani yao 

“Kwa Mzazi mwenzake wakati amemkataa Mtoto? Twende pamoja  polisi kujua nini chanzo cha kukamatwa kwake” 

“Na vipi kuhusu hali ya Mtoto Mchungaji?” Aliuliza Mama Naomi 

“Oooh hapa sasa nachanganikiwa Mimi, basi baki hapa  ukiangalia hali ya Mtoto, wacha Mimi nikimbilie Polisi”  Alisema Mchungaji, akakimbilia kwenye gari na kuondoa gari  kwa kasi sana, Mama Naomi alipoona Mchungaji ameondoka naye  akaondoka kuelekea kwa James kumpa taarifa.

Neema akajitokeza kisha akajinasbu kua ni lazima Matilda  aondoke Dar. 

******** 

Mchungaji George alipofika kituo cha polisi alipaki gari  kwenye maegesho, kisha akashuka haraka haraka na kukimbilia  ndani ya kituo hicho cha polisi. Akapandisha ngazi kabla ya  kukutana na polisi 

“Afande nimekuja haraka sababu bado sijajua sababu ya  kukamatwa kwa huyu Binti” Alisema Mchungaji akiwa  anamwangalia Matilda ambaye alikua amekalishwa chini 

“Nifuate” Alisema polisi huyo kisha akamnyanyua Matilda  wakaelekea kwenye chumba kimoja ambacho kilionekana wazi  kilikua chumba cha mahojiano, Mlango ukafungwa, ndani kulikua  na askari wawili wengine ambao waliwakuta humo 

“Huyu Binti ni mwizi, mahali anapoishi siyo pake kuna Mtu  amemweka akae hapo lakini mwenye nyumba amelalamika juu ya  upotevu wa vitu vyenye thamani ya Zaidi ya Milioni 10”  Alisema polisi huyo akiwa na sura kavu sana. 

“Ameiba?” 

“Ndiyo” 

“Afande Mimi siyo mwizi na sijawahi kuiba chochote kile,  nimeishi pale kwa zaidi ya mwaka mmoja iweje leo ionekane  Mimi ni Mwizi? James anakosea sana” Alisema kwa uchungu sana  Matilda 

“Kaa kimya hupaswi kuongea chochote kile hadi pale  aliyekushtaki atakapofika hapa” Alisema polisi huyo 

“Jamani kuweni na huruma, huyu Binti ana Mtoto mdogo ambaye  ni mgonjwa sana na yupo Hospitalini, hizo pesa mlizomkamata  nazo ni michango ya kanisa kwa ajili ya Matibabu” Alisema  Mchungaji 

“Kwakua umeshafahamu nini kilichopelekea akakamatwa basi ni  vema ukakaa kimya huku ukisubiria uendeshwaji wa kesi hii,  kama unahitaji kuwa shahidi wa hili basi tukutane mahakamani”  Alisema Polisi huyo ambaye alishapewa Hongo na Neema ili kesi  hiyo iwe hai 

“Nenda nje” Akasema polisi huyo akimtaka Mchungaji aondoke

“Afande kua na moyo wa utu japo hata kidogo, Mtoto wake  anaangamia kule Hospitali kwa kukosa matibabu, ninaomba sana  na nipo chini ya Miguu yenu ikibidi hata kua Mdhamini wa  hili, hizo pesa nazihitaji zikamtibie Binti yake” Alisema  Mchungaji George akishinikiza apewe pesa hizo lakini polisi  wakamtoa Nje Mchungaji George 

Matilda alikua Mtu wa kulia muda wote huku akiomba kwa Mungu  kuhusu hali ya Binti yake, dakika chache baadaye aliingia  Neema akiwa ameambatana na yule Mwanaume anayeitwa Masudi,  akavuta kiti na kuketi, Matilda alishtuka baada ya kumwona  Neema 

“Matilda, kama ulifikiria unaweza ukachomoka kwenye hili basi  sahau kabisa” Alisema Neema, polisi wakatoka ili kuwaachia  wazungumze 

“Kumbe ni wewe ndiye uliyenifungulia hii kesi isiyo na kichwa  wala Miguu, wewe ni Mzazi mtarajiwa si ndiyo? utajisikiaje  ukitendewa namna nitendewavyo Mimi…Kumbuka Binti yangu yupo  Hospitalini na anahitaji Matibabu…” alisema kwa uchungu  Matilda huku chozi likimvuja, alishindwa kufuta chozi sababu  alifungwa pingu mikononi 

“Kumbe inaumiza eeeh? basi hivi ndivyo ambavyo Mimi pia  naumia ninapokuona mbele ya macho yangu, una chaguo moja la  kufanya, nalo ni kukubali kurudi kwenu kabla hujafikishwa  mahakamani, ukikubali hii kesi naifuta haraka sana, sitaki  kukuona ukiendelea kuwa karibu na James kwa lolote lile”  Alisema Neema 

“Dada yangu kama unafikiria Mimi ni dhahifu kwenye hilo  naomba usahau kabisa, ikibidi mniuwe lakini siwezi kuidhurumu  haki ya Mwanangu Kumjua Baba yake” Alisema Matilda, akapigwa  kofi na Neema 

“Mshenzi mkubwa wewe, sasa endelea kujifanya Mjuaji kwenye  hili, mwisho wako unakuja” Alisema Neema kisha aliondoka hapo  akiwa na Masudi, walipofika kwenye gari Neema alionekana kua  na hasira sana sababu lengo halikua kesi bali ni kumtisha tu  Matilda 

“Usiwe na hasira, huu ni mwanzo tu Naamini mateso  atakayoyapata atakubali kuondoka mwenyewe” Alisema Masudi,  Mwanaume ambaye alionekana kua karibu sana na Neema

“Kama kuteswa inabidi ateswe haswa, kwasababu amekataa  kuondoka kwa uhuru basi ataondoka kwa shari kama atakavyo”  Alisema Neema kisha aliondoa gari haraka sana. 

“Nikusaidie nini?” lilikua ni swali aliloulizwa Mama Matilda  baada ya kufika ofisini kwa James, hakukaribishwa ofisini  bali aliachwa getini azungumze 

“Ni kuhusu Matilda” Alisema Mama Naomi akiwa anahema “Amefanyaje?” 

“Amekamatwa na Polisi muda mchache uliopita, hadi sasa  hatujui sababu ya kukamatwa kwake. Nakuomba James, hunijui  lakini Mimi ni jirani wa Matilda kule anakoishi, fanya  uwezalo ili aachiwe” 

“Usinichekeshe ndugu yangu,, yaani umetoka kote huko hadi  hapa ili kuniambia hicho tu? unaonekana kama Mwanamke mwenye  busara zako lakini sikutegemea kama mwisho wa siku ungesimama  na Mwizi” Alisema James akionekana hana wasiwasi kabisa 

“Mwizi? nimeishi naye kwa siku zote hakuwahi kuonekana na  tabia hiyo ya wizi, hata kama akawa mwizi lakini ana haki ya  kuokoa Maisha ya Binti yake, fanya kwa ajili ya Patra ni  Binti yako yule James” Alisema Mama Naomi, kofi likatua  kwenye shavu lake la kulia 

“usirudie tena hiyo kauli, hakuna unachojua kuhusu  Mimi…..Ondoka” Alisema kwa hasira sana James 

“Laiti kama ungelijua Maisha anayopitia Matilda sasa hivi  wala usingethubutu kunipiga, basi siyo Mtoto wako lakini  kumbuka wewe ndiye uliyemtoa kwao basi thamini utu kama  Binadamu wa kawaida” Alisema Mama Naomi kwa uchungu sana huku  Mtoto akiwa analia mgongoni 

“Nini ambacho hujanielewa?” Alisema James kwa hasira akiwa  anamsogelea Mama Naomi, kelele hizo zikamtoa Sekretari hadi  nje 

“Bosi kuna nini?” aliuliza 

“Simjui ananilazimisha nimsaidie, amekua king’ang’anizi sana  Jack!”

“Halafu kama alikuja jana huyu na Mdada mwingine, sura  nishaikumbuka kumbe walikua wanahitaji msaada? kwanini  usiwasaidie Bosi?” aliuliza Jack 

“Hujui kitu hakuna msaada unaotolewa kwa kung’ang’ania namna  hii, Kutoa ni moyo, sikia nenda ofisi zingine hapa hatusaidii  omba omba” Alisema James kisha akarudi ofisini 

Jack akamtazama Mama Naomi. Akiwa kama Mwanamke alimuonea  huruma Mama Naomi na Mtoto aliye mgongoni, akatoa noti ya  elfu tano akampa 

“Chukua hii itakusaidia” Alisema Jack 

“Asante lakini huu siyo msaada ambao Mimi niliutaka kutoka  kwa Bosi wako” Alisema Mama Naomi 

“Ulikua unahitaji msaada gani?” Jack akapata shahuku ya  kutaka kujua zaidi maana hakuna ombaomba ambaye anaweza  kukataa shilingi elfu tano, akasogea 

“Bosi wako James amezaa na Msichana yule ambaye nilikuja naye  jana, James amemkataa Mtoto sababu ni mlemavu, Mtoto yupo  mahututi Hospitalini, Yule Msichana amekamatwa na polisi muda  siyo mrefu ndiyo maana nilikuja hapa ili kumpa taarifa  akamsaidie hata Mtoto sababu anahitaji matibabu, hakuna pesa  ya kumtibia” Alisema kwa uchungu Mama Naomi huku akikaribia  kudondosha chozi, Jack aliumia sana 

“Sikia chukua hii kadi yangu, kwa lolote naomba unipigie,  nenda sababu James ana hasira sana” Alisema Jack, kila  alivyomtazama Mama Naomi akiwa anaondoka alisikitika kisha  akarudi Ofisini, akamkuta Bosi wake akiwa anataka kutoka 

“Yaani Watu wengine Bwana kutaka kuharibiana siku tu, kwani  ni lazima kumsaidia Ombaomba….Mimi natoka sijisikii kufanya  chochote kwa sasa, siku nyingine usiruhusu Omba omba katika  ofisi yangu” 

“Sawa Bosi” Aliitikia Jack 

Jua lilikua kali lakini Mchungaji George alihitaji kujua  hatma ya Maisha ya Matilda, Mateso yalianza upande wa  Matilda, alipigwa bila kosa lolote lile. Lengo lilikua ni  kumtaka aondoke Dar ili asiwe kero kwa James, ndicho  alichokipanga Neema.

Baada ya Saa nzima aliingia Mama Naomi akamkuta Mchungaji  George akiwa anachomwa na jua la Mchana 

“Eeeh kulikoni Huko Hospitali kuna usalama?” aliuliza  Mchungaji George kwa Mshtuko sababu alimuacha Mama Naomi  Hospitali 

“Sijui Mchungaji lakini natumaini hakuna kitakachoharibika,  Mungu aliye hai anapigana vita nzito muda huu, vipi kuhusu  Matilda?” 

“Bado yupo kituoni, hizo sauti unazozisikia ni zake,  anaonekana kua kwenye mateso makali” Alisema Mchungaji 

“Jamani sasa amewakosea nini?” 

“Wanasema ameiba vitu vyenye thamani kwenye nyumba anayoishi” 

“Ameiba? si kweli, Maisha anayoishi Matilda ni ishara tosha  kua hawezi kuiba, hawa Watu kwanini waneamua kumkatili Binti  wa watu jamani” 

“Hatuna namna Zaidi ya kusubiri muda utupe majibu sahihi,  Kama hakufanya hivyo basi ataachiwa tu ila kinachonipa hofu  ni kuhusu Binti yake, sijui itakuaje” 

“Mchungaji hapo ni pazito zaidi sababu uliponiacha Hospitali  nilitoka na kwenda kwa Mwanaume aliyezaa naye lakini huwezi  amini kamkana mbele ya Macho yangu, kanipiga kofi pia”  Alisema Mama Naomi akiwa anamweka vizuri Mtoto 

“Sijui hata tufanye nini, kwani wazazi wa Matilda wapo wapi?” 

“Wazazi wake wapo Njombe, pamoja na shida anazopitia lakini  alisema hawezi kurudi kwao wala kusema chochote kwa Wazazi  wake” 

“Oooh Mungu wangu, basi wewe ungerudi tu nyumbani Mimi  nitabakia hapa kwa masaa kadhaa kwa ajili ya kujua Hatma ya  Matilda” Alisema Mchungaji George 

“Sawa Mchungaji kwa chochote kile tuwasiliane” Alisema Mama  Naomi kisha akaondoka kituoni hapo. 

Upande wa pili, gari moja lilikua likiendeshwa kwa spidi  kubwa sana, ndani yake alikuwepo James akionekana  kuchanganikiwa, maneno ya Mama Naomi yaliendelea kujirudia  ndani ya Kichwa chake, akawa anapiga usukani kwa hasira,  alikanyaga mafuta hadi nyumbani kwake, akateremka haraka  kisha akaingia ndani

Kama akili yake ilivyomtuma ndivyo alivyokuta, Neema alikua  ameketi huku akitikisa miguu yake, pembeni kukiwa na embe  bichi ambalo lilikua linasukuma tabasamu lake, baada ya  kumwona James akiwa ameingia na taharuki akamuuliza 

“Kulikoni Baby mbona una taharuki?” aliuliza Neema akiwa  ameacha kula embe Bichi 

“Nenda kafute kesi inayomkabili Matilda” Alisema James kisha  akajitupa kochini kama Mtu aliyechoka sana 

“Unasemaje?” 

“Ulivyosikia ndivyo nilivyosema, hakuna sababu ya kuendelea  na kesi, tuangalie namna nyingine ya kumfanya Matilda aondoke  hapa Mjini” Neema akamtazama Kwa hasira James 

“James Mimi natarajia kua Mama wa Mtoto wako, siwezi kuzaa  Mtoto katika familia yenye migogoro namna hii, ikishindikana  nitoe ujauzito ili ulee Mtoto wako na Matilda” Alisema Neema 

“Sina maana hiyo Neema, Sina lengo hilo nawe huna sababu ya  kufanya hivyo, tambua kiu yangu ni Mtoto lakini naona Matilda  anateseka sana, Mtoto wake yupo Hospitalini” 

“Kwahiyo umeanza kua na huruma si ndiyo? Basi hakuna sababu  ya kujificha, jitokeze hadharani ujitangaze kua Bilionea  mwenye Mtoto Mlemavu, si una shida sana ya Mtoto basi hakuna  sababu ya Mimi kubeba huu mzigo wakati una Mtoto unaye muonea  huruma” Alisema Neema kwa hasira zaidi, akanyanyuka ili  aondoke lakini James akamshika mkono kwa lengo la kumzuia  asiondoke 

“Mpenzi hupaswi kua na hasira sababu wewe ni Mama mtarajiwa,  natamani haya mambo yaishe kwa namna nzuri, basi nitaenda  Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda ili aondoke hapa  Mjini” Alisema James lakini Neema akatoa Mkono wa James  akaelekea chumbani.  

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

5 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version