Ni Pale Unapoona Kwamba Jeraha lingine halitoweza kutokea, Ndipo Hutokea..!

Paul Labile Pogba aliyezaliwa tarehe 15 Machi 1993 ni mchezaji wa soka la kulipwa wa Ufaransa anayesakata kabumbu katika klabu ya Juventus, Ligi ya Serie A na timu ya taifa ya Ufaransa. Anacheza kama kiungo wa kati, lakini anaweza kutumika pia kama mshambuliaji wa pembeni akitokea upande wa kushoto, kiungo mshambuliaji, kiungo wa ulinzi na kiungo mchezeshaji.

Paul Pogba alianza kazi yake ya soka katika klabu ya Le Havre ya Ufaransa kabla ya kuhamia kwenye timu ya vijana ya Manchester United mwaka 2009. Alicheza kwa muda mfupi katika timu ya kwanza ya Manchester United kabla ya kuhamia Juventus ya Italia mwaka 2012.

Akiwa Juventus, Pogba alionyesha uwezo wake mkubwa wa kucheza soka na alifanikiwa kushinda taji la Serie A mara nne mfululizo kati ya mwaka 2013 na 2016. Alijiunga tena na Manchester United kwa rekodi ya dunia ya uhamisho wa pauni milioni 89 mwaka 2016.

Pogba amecheza kwa mafanikio makubwa katika timu ya taifa ya Ufaransa, ambapo aliisaidia kushinda Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2018 na pia alikuwa mchezaji muhimu kuifika fainali ya Euro 2016.

Pogba aliendelea kufanya vizuri katika klabu ya Manchester United, ambapo alikuwa mchezaji muhimu wa timu na ameshinda tuzo kadhaa za Mchezaji Bora wa Mwezi wa klabu hiyo kabla ya Kutimkia tena kwa matajiri wa Turin, “La Vecchia Signora”, Juventus

Katika kipindi chake chote ambacho Pogba amekua akicheza soka la Kulipwa, Majeraha yamekuwa sio jambo geni kwake, kwani mara kadha wa kadha amekua nje ya uwanja kwa vipindi tofauti tofauti. Katika misimu yake mitatu ya mwisho huko Manchester, Paul Pogba alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha mara nane tofauti, na aina mbalimbali ya matatizo ya kiafya. Mchezo wake wa mwisho akiwa na  Manchester United ulikuwa mwezi Aprili mwaka jana, ambapo alitoka uwanjani akiwa majeruhi katika kipigo cha 4-0 dhidi ya Liverpool.

Hizi ni rekodi zake za majeraha akiwa Manchester United.

Msimu wa 16/17:  Majeraha ya Kifundo cha mguu, Machi 16, 2017 – Aprili 3, 2017, Mechi alizokosa ni 3

Msimu wa 17/18:  Kuvunjika kwa misuli ya paja, 14 Septemba, 2017 – 16 Novemba, 2017 , Mechi alizokosa ni 12

Msimu wa 18/19:  Mshtuko wa Misuli ya Paja, 3 Januari, 2019 – 14 Januari, 2019 , Mechi alizokosa ni 2

Msimu wa 19/20:  Majeraha ya Mshipa wa Mgongo, 1 Agosti, 2019 – 12 Agosti 2019 , Mechi alizokosa ni 1

Msimu wa 19/20:  Majeraha ya Mshipa wa Mgongo, 29 Agosti, 2019 – 26 Septemba, 2019 , Mechi alizokosa ni 5

Msimu wa 19/20:  Majeraha ya Mshipa wa Mgongo, 30 Septemba, 2019 – 23 Disemba, 2019 , Mechi alizokosa ni 19

Msimu wa 19/20:  Majeraha ya Mshipa wa Mgongo, 26 Disemba, 2019 – June 8, 2020 , Mechi alizokosa ni 20

Msimu wa 20/21:  Majeraha ya Mshipa wa Mgongo, 16 Novemba, 2020 – 3 Disemba, 2020 , Mechi alizokosa ni 4

Msimu wa 20/21:  Majeraha ya Kifundo cha mguu, 4 Februari, 2021 – 18 Machi, 2021, Mechi alizokosa ni 12

Msimu wa 21/22:  Majeraha ya Kifundo cha mguu, 8 Novemba, 2021 – 3 Februari, 2022, Mechi alizokosa ni 14

Msimu wa 21/22:  Majeraha ya Kisigino, 18 April, 2022 – 23 Mei, 2022, Mechi alizokosa ni 6

 

Pogba amerudi, Hakika..! Amerudi tenaTurin. Aliondoka kama mtoto na amerudi kama mtu mzima na bingwa, lakini kuna kitu ambacho hakijabadilika, hamu ya kuandika kurasa na historia ambazo hazitasahaulika klabuni hapo tena. Tangu kurejea kwake Juventus akiungana na Mastaa wengine waliopo kikosini, Paul Pogba ameshindwa kuwa na nyakati bora katika kiwango chake kisoka. Kwa kweli, kurudi kwa Pogba Turin kumeongeza Huzuni kubwa sana hadi sasa, ikiwa na majeraha mfululizo kila mara.

Pogba alirudi rasmi Juventus tarehe 11 Julai 2022. Wiki mbili baadaye, aliumia wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya kirafiki ya msimu mpya dhidi ya Barcelona huko Dallas. Klabu ya Juventus ilieleza kwamba baada ya Paul kulalamika kuwa na maumivu kwenye goti lake la kulia, alifanyiwa uchunguzi wa radiolojia ambao ulionyesha tatizo kwenye kishikizo cha goti upande wa kulia na hivyo kufanya asiungane na Timu kuelekea mchezo huo jijini Dallas.

Baada ya taarifa iliyotolewa Oktoba 31 kuhusu Paul kutoungana na kikosi cha Timu ya taifa ya Ufaransa katika Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Nchini Qatar 2022, Tarehe 28 Januari, Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri aliweka wazi katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Pogba alikuwa tayari kupatikana tena kwenye kikosi, na akamjumuisha mshindi huyo wa Kombe la Dunia katika kikosi chake kwa pambano la Serie A dhidi ya Monza huko Turin siku iliyofuata laiki mambo bado hayakua shwari kwa Staa huyo wa Ufaransa baada ya Kupata tena kuumia tena Februari 1, 2023.

Jumatatu ya Machi 13, 2023 akitoka katika Kituo cha Matibabu cha Juventus, Sura ya Paul Pogba iliweka dhahiri kuwa hali si shwari na alifahamu hilo. Juventus ilisema kuwa Pogba alipata mshtuko mdogo wa kuumia misuli ya paja la kulia ambao ulitokea wakati akipiga “free kicks” mazoezini Jumapili asubuhi, kama ilivyoripotiwa na Romeo Agresti wa Goal Italia, na kwamba tayari wameanza mchakato wa matibabu ili kumrudisha tena katika ushindani wa Kisoka.

Kulingana na ripoti kutoka kwa Gianluca Di Marzio wa Sky Italia na Tuttosport, jeraha jipya la Pogba linaweza kumweka nje kwa muda wa mwezi mzima ambao, ikizingatiwa jinsi mambo yalivyo kwa msimu wake, na kwa kiasi kikubwa ni hali isiyoridhisha. Wakati kuna mapumziko ya kimataifa yatakayoanza wiki ijayo na kuchukua nusu ya kipindi hicho, ukweli ni kwamba hii ni jeraha jipya katika orodha ndefu ya majeraha aliyowahi kupata Paul na ni jambo linalosikitisha zaidi.

Pogba alionekana kuwa anapiga hatua ya kupona katika matatizo yake ya majeraha wakati alipoingia katika mchezo wake wa pili ndani ya Juventus wakati wa Derby della Mole dhidi ya Torino mwishoni mwa Februari Mwaka huu. Ulikuwa ni mchezo mfupi kwake wa dakika 20, lakini ilitakiwa kuwa ishara kwa Juventus kwamba Pogba yuko tayari kuchangia kwa njia fulani kwenye matokeo ya mechi hiyo.

Pogba aliingia tena kucheza katika mechi dhidi ya Roma, ambapo Kocha Allegri alisema kuwa Mfaransa huyo alikuwa anaonyesha dalili za kurejea polepole kwa kuonyesha uwezo wa kucheza dakika nyingi zaidi, Jumla yake, Pogba amekosa mechi takribani  zaidi ya 40 msimu huu.

Hizi ni rekodi zake za Majeraha tangu aliporejea Juventus;

Msimu wa 22/23:  Maumivu kwenye kishikizo cha goti, 25 Julai, 2022 – 22 Septemba, 2022, Mechi alizokosa ni 7

Msimu wa 22/23:  Upasuaji wa Goti, 5 Septemba, 2022 – 26 Januari, 2023, Mechi alizokosa ni 21

Msimu wa 22/23:  Mshtuko wa Misuli ya Paja, 21 Oktoba, 2022 – 18 Januari, 2023, Mechi alizokosa ni 7

Msimu wa 22/23:  Jeraha, 1 Februari, 2023 – 27 Februari, 2023, Mechi alizokosa ni 26

Msimu wa 22/23: Kipasuko katika misuli ya kiunoni, 12 Machi, 2023 – 2 Aprili, 2023, Mechi atakazokosa ni 4

 

Leave A Reply


Exit mobile version