Pamba Jiji Football Club kurejea kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya Miaka 23 ni fursa kubwa sana katika sehemu tofauti ndani ya Jiji la Mwanza na nchini nzima kiujumla! Ni Miaka kadhaa tangu Mbao na Alliance FC zishuke kwenda Ligi Daraja la Kwanza na kupotelea huko chini bila kuwa na matumaini ya kurejea tena

Fursa kwa vijana wengi wenye vipaji ndani ya Jiji la Mwanza ni sehemu namba moja ambayo naiona kwa haraka katika urejeo huu wa Pamba FC ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kama utapita jioni ndani ya viwanja vya Nyamagana, CCM Kirumba, SAUT, Nsumba Secondary, Buswelu Secondary, Sabasaba, Mirongo Secondary na viwanja vingine basi utaona vijana wengi sana katika maeneo hayo

Pili ni eneo la biashara ambalo watu wengi sana watanufaika kuanzia wajasiriamali wadogo mpaka wafanya biashara wakubwa sababu kutakuwa na muingiliano wa Timu nyingi na wageni wengi ndani ya Jiji la Mwanza, eneo hili pia wafanya biashara kutoka nje ya Mwanza bado ni fursa kwao sababu watajitokeza na kusogea karibu na eneo hili ambalo lina fursa tayari

Uboreshaji wa baadhi ya miundombinu pia ni sehemu ya Jiji la Mwanza kunufaika katika eneo hili hasa sehemu za michezo ambapo fursa ya maboresho ya baadhi ya viwanja kama Nyamagana Stadium na CCM Kirumba ambayo itatumika kwa Asilimia kubwa! Fursa hii ya miundombinu itafunguliwa na uwepo wa Ligi Kuu ndani ya Jiji la Mwanza

Hivyo ni Miongoni mwa vitu vichache ambavyo Jiji la Mwanza vitanufaika navyo kutokana na uwepo wa PAMBA JIJI FOOTBALL CLUB ndani ya Ligi Kuu ya TANZANIA kuelekea Msimu wa 2024/25! The Time of Rock City to enjoy the beautiful game.

SOMA ZAIDI: Kibu Kuna Muda Ni Lazima Kukubali Kufanya Maamuzi Magumu

3 Comments

  1. Pingback: Je Yusuph Kagoma Ni Mbadala Sahihi Wa Khalid Aucho Yanga? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version