Moja ya kitu ambacho wana Yanga wengi hawaombei ni majeraha ya kiungo Pacome Zouzoua, na kupona haraka kwa Khalid Aucho na kama ikitokea hawatorejea mapema basi wataenda kutia ugumu kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns. Sitaki kusema Yanga SC wanakikosi finyu hapana ila katika ushindi wa Yanga kwenye michuano ya kimataifa basi Pacome na Khalid Aucho wana mchango mkubwa zaidi.

Naamini kama ungekutana na kocha Miguel Gamondi na ukamuuliza ni kitu gani ulikuwa ukihitaji Kwa sasa?Nadhani kubwa atakalokuambia ni kupona kwa wachezaji wake ambao ni majeruhi mnaona namna wachezaji wa Yanga SC wanavyocheza Kwa tahadhari kubwa wakikwepa majeraha lakini wachezaji wa Azam wao wanaamini hawana cha kupoteza.

Kabla ya kwenda kuwalaumu waamuzi wetu na sisi turejee nyuma kwenye zile ajenda mfu kwani hampaswi kusahau haraka namna hiyo.

Kabla ya huu mchezo mtakumbuka vizuri propaganda zilivyotembea kuwa Yanga wakishinda dhidi ya Azam FC unakuwa siyo ushindi wa kweli. Yaani kama kuna namna ambayo inafanyika ili Yanga ishinde.

Sasa katika mazingira ya kawaida kama mwanadamu unafikiri utafanya kitu gani kama siyo kuingia kwenye mchezo na presha kubwa watasema yule Heri Sasii ni Yanga kabisa au Simba wakutupwa na ikitokea hivyo refalii anaingia uwanjani na anashindwa kutekeleza majukumu yake.

Ukweli ni kwamba mpira wetu unachezwa sana Instagram zaidi kuliko sehemu nyingine ile, yaani kalamu zinatumika zaidi na tunaacha kuufanya mpira uchezwe.

Leo mashabiki wa Yanga wanatoka mbele na kuanza kumlaumu Kocha wao Miguel Gamondi amekosea kupanga kikosi chake lakini wanasahau namna ratiba ilivyo ngumu mbele yake, siku 17 mechi 5 wewe kuwezaaaa. Nakuuliza wewe ungeweza wapi.

Sawa wanasema ratiba imepangwa lazima wachezaji wacheze lakini na wao ni binadamu na wakati mwili nao unachoka na majeraha ya hapa na pale. Tatizo hapa kwetu kama wewe siyo Yanga SC basi Simba SC Mnyama. Ukweli unafichwa na unafki unatembea.

SOMA ZAIDI: GUEDE Amemponza GAMONDI Kwenye Mfumo Wa Azam Na Sababu Kubwa 

Leave A Reply


Exit mobile version