Kwenye soka imezoeleka kuwa kila mchezaji ana nafasi yake anayoimudu vyema lakini huwa inatokea mara chache kuona Mchezaji wa ndani anakuwa kipa. Ndio yaani yule labda beki anaenda kuvaa gloves za kipa na kisha kuanza kunyaka na hii hutokea mara chache sana na sababu kubwa ni pale ambapo kunatokea wachezaji wa mabadiliko kumalizika na kipa kuumia au kutolewa kwa kadi nyekundu na mambo mengine mbalimbali.

Wafuatao ni Wachezaji wa ndani waliobadilishwa kuwa makipa kwenye mechi na sababu ambazo zilipelekea wao kwenda kucheza nafasi hiyo:

01.CHAKER AHLADHUR (Comoro vs Cameroon)

Chaker ambaye kiasilia ni beki wa kushoto kwa MAPENZI yake binafsi kwa Wa-Comoro alisimama Kama golikipa kwenye mchezo wa kufuzu Hatua ya Robo Fainali za Kombe la AFCON Kati ya Comoro na Cameroon

Kwenye mchezo huo Alhadhur aligusa mipira Mara 52 na kufanikiwa kupiga pasi 42 huku akiokoa mipira hatari (saves) 4 za maana (Kama za MOUSA CAMARA wa Simba au DIARRA wa Yanga )

CHAKER anabaki kuwa alama (ICON) ya Wapambanaji wote duniani kuwa Mpambanaji hachagui KAZI ya kufanya

02.RIO FREDNAND (Man United vs Portsmouth)

MWAKA 2008 aliyekuwa Beki wa Manchester United,Rio Ferdinand alivaa gloves baada ya kipa namba moja,Edwin van der Sar kuumia huku kipa namba mbili akipewa kadi nyekundu. Kazi ya kwanza ya Rio ilikuwa kuokoa penalti ya Sulley Muntari kwenye mchezo wa Robo Fainali ya FA lakini hakuweza kuokoa licha ya kwenda uelekeo sawa na Mpira ulipopigwa. Man United ikatolewa kwenye kombe la FA kupitia Penati hiyo.

03.JOHN TERRY (Chelsea vs Reading)

ZIKIWA zimesalia sekunde 29 za mchezo,Mshambuliaji wa Reading Stephen Hunt aligongana na golikipa wa Chelsea,Petr Cech na kumsababishia kipa huyo maumivu makali kichwani. Kipa namba 2,Carlo Cudicini aliingia na kutolewa sekunde chache Kabla ya mchezo kumalizika. Kutokana na hilo,Terry ilimbidi aende golini. Mechi hiyo iliisha kwa Terry kutoruhusu goli. Tangu siku hiyo,Cech amekuwa akivaa kofia ya kujikinga kichwani mpaka alipostaafu soka.

4DANI ALVES (PSG vs SOCHAX)

Akiwa na kimo cha futi 5, Alves alikubali kwenda kuwa kipa baada ya Kevin Trapp kuonyeshwa kadi nyekundu.Wakati anakwenda kuwa kipa tayari PSG ilikuwa inaongoza 4-1 lakini alikumbana na changamoto kadhaa ikiwamo kukabiliana na mipira ya adhabu.

05.HARRY KANE (TOTTEHAM VS ASTERAS)

MECHI ni kama ilikuwa imekwisha kutokana na Spurs kuongoza goli 5-0 dhidi ya Asteras huku Kane akifunga Hat Trick kwenye michuano ya EUROPA. Kane atakumbukwa zaidi kwenye mchezo huo baada ya kugeuka kuwa kipa kufuatia kipa namba moja Hugo Lloris kuoneshwa kadi nyekundu na huku Spurs wakiwa wamemaliza Sub zote. Mechi hiyo ilimalizika kwa Spurs kushinda goli 5-1 baada ya Kane kushindwa kuokoa mpira wa adhabu wa Jeromino Barrales.

06.OLIVIER GIROUD (AC MILAN VS GENOA.)

Bingwa wa Kombe la dunia na UEFA,Olivier Giroud alijikuta akiongeza CV kwenye Career yake baada ya kuoongoza kuipa ushindi AC Milan dhidi ya Genoa na kuibuka Mchezaji bora wa mechi. Kipa namba moja,Mike Maignan alioneshwa kadi Nyekundu huku Sub zikiwa zimekwisha.

07.JOHN O’SHEA (Totteham vs Man United)

Kwenye mechi hiyo Man United ikiwa ugenini ilikuwa inaongoza kwa goli 4-0 lakini dakika za mwishoni kipa wake,Edwin van der Sar alivunjika na wakati huo Sub zikiwa zimekwisha. O’shea ndiye aliyeenda golini kudaka.

08.NIALL QUINN (Man City vs DerbY)

Mshambuliaji huyo akiwa ametoka kufunga goli alijikuta akibadilika kuwa golikipa baada ya kipa wao,Ton Coton kuoneshwa kadi nyekundu. Quinn akiwa kipa aliokoa penalti ya Dean Saunders na kuisaidia City kushinda dhidi ya Derby.

09.KYLE WALKER (Man City vs Atalanta)

Novemba 6, 2019 Walker alifanikiwa kuwa kipa wa nne ghali zaidi duniani wakati beki huyo wa kulia wa pauni milioni 47 alipojitolea kuwa golikipa wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Man City dhidi ya Atalanta mwaka 2019 Baada ya kuchukua nafasi ya Éderson wakati wa mapumziko, Claudio Bravo naye alipewa kadi nyekundu katika mechi hiyo, Walker kisha akashikilia mechi kuanzia dakika ya 81 na hata kufanya save kali kuliko wote Bravo na Ederson walikuwa wamefanya hapo awali wakati wa mchezo.

10.SERGE AURIER (Ivory Coast vs Sierra Leone)

Beki wa Ivory Coast Serge Aurier alichukua glovu baada ya golikipa wao kutolewa nje kwa machela baada ya kuumia wakati  Sierra Leone wakitafuta bao la kusawazisha huko AFCON. Hakuruhusu goli lolote hivyo rekodi zinaonyeshe alimaliza mechi na Clean Sheet safi kwa Beki huyo mkongwe

11. PELE. (Santos vs Gremio).

WAKATI Gwiji huyo akibadilishwa kuwa kipa alikuwa tayari amefunga hattrick kwenye mechi dhidi ya Gremio kabla ya kipa Gilmar kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mshambuliaji huyo alijitolea kuchukua nafasi hiyo na alikuwa bora katika nafasi hiyo.

12.JAN KOLLER (Borussia Dortmund vs. Bayern Munich)

Jan Koller alikuwa tayari ameshawahi kuwa golikipa wakati akicheza utotoni kabla ya kubadili na kuwa Mshambuliaji. Baada ya golikipa wa Dortmund,Lehman kupewa kadi nyekundu,Koller alikumbushia kudaka na karibia dakika 24

13. PHIL JAGIELKA (Sheffield United vs Arsenal)

JAGIELKA alichukua nafasi ya Paddy Kenny aliyejiumiza wakati akianzisha mpira. Kwenye mechi hiyo Jagielka alitoka na Clean Sheet huku akikumbukwa kwa kufanya save matata iliyopigwa na Robin can Persie.

14.EDMUND TAPSOBA (Bayer Leverkusen vs Dortmund)

Baada ya Lukáš Hrádecký kutolewa kwa kadi nyekundu kwa mpira wa mkono katika dakika ya 92 ya mechi ya Bundesliga dhidi ya Borussia Dortmund, Tapsoba alibadilishwa kuwa golikipa kwenye dakika za mwisho ambapo mechi iliisha kwa Bayer Leverkusen kupoteza 1-0, Wakati Tapsoba anaenda golini Bayer Leverkusen walikuwa tayari wameshamaliza Sub za wachezaji wake wote watano wa akiba

15.ROBBIE SAVAGE (Derby County vs Reading)

TUNAMALIZIA Orodha yetu na Robbie Savage baada ya kipa wa Derby County,Saul Deeney kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.Licha ya Derby kupoteza kwa goli 4-1 na Savage kuruhusu magoli mawili ila bado alifanya saves 2 za hatari.

Timu unayoshabikia NBCPL Mchezaji Gani Unaona Kabisa Ikitokea Hakuna Golikipa Nje Anaweza Kudaka Yeye?

Unaikumbuka Mechi Ipi Kati Ya Hizi? Au tukio gani sijaliweka hapa ila wewe unalikumbuka?  

SOMA PIA : Hii Ndio Michezo 8 Hatari Zaidi Duniani

wachezaji xx wachezaji xx wachezaji xx wachezaji xx

4 Comments

  1. Afcon comoro vs Cameroon,chacker alikuwa anachekeshaha Sana,Kuna wakati mpira unapigwa kweye box ye anaweka mikono nyuma😂😂anasahau kama ni goalkeeper

Leave A Reply


Exit mobile version