Ujio wa mchezaji Augustine Okrah katika kikosi cha Yanga unaelezwa unahitimisha maisha ya beki wa kati kutoka Uganda, Gift Fred ambaye tangu asajiliwe hajapata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana.

“Kutokana na kanuni ya wachezaji wa kigeni kutakiwa kuwa 12, tunalazimika kumfyeka mmoja kati ya wachezaji ambao wameshindwa kuonyesha uwezo kikosini akiwamo Gift Fred, huyu tutaachana naye wakati tunaendelea kuangalia wengine wa kuwatoa ili kupisha majembe mapya kikosini,” alisema mmoja wa vigogo wa Kamati ya Usajili ya Yanga.

Mbali na Gift wengine wanaoelezwa huenda wakafyekwa katika dirisha dogo kumpisha Okrah  Yanga itakapomalizana na nyota inayowasaka kwa sasa ni Hafiz Konkoni na Jesus Moloko, mbali na nyota wazawa wanaoelezwa watatolewa kwa mkopo kama Dennis Nkane na Crispin Ngushi.

Endelea kufuatilia zaidi taarifa zetu na vidokezo vya ubashiri kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version