Ilimchukua msimu mmoja na nusu kuhudumu kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo na baada ya hapo nyota yake ilianza kung’ara akianzia kwenye kikosi cha timu ya vijana na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo, ni kama ilionekana anaweza na ana kitu licha ya kuwa bado alikuwa akicheza kwenye kikosi cha vijana ila nyota nzuri iling’ara kwake.

Kocha mkuu wa kikosi hicho alimuona na kuamua kumoa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha timu ya wakubwa na alipoingia kwenye mfumo basi Kocha mkuu wa kikosi hicho kwa wakati huo aliamua kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya mchezo mmoja wa Ligi kuu akitazama akiwa kwenye benchi jambo ambalo kadri muda ulivyokuwa unaenda kijana huyo akapata nafasi ya kuingia kwenye moja ya mchezo wa timu hiyo na kilichobaki ilikuwa ni historia tu kwake na jamii yote.

Kwa sasa kijana huyo amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Yanga SC na siyo kwa bahati mbaya bali kwa kile anachoonyesha akiwa na kikoai chake cha Yanga SC kwa misimu miwili sasa na kupelekea kuwaweka benchi wachezaji wa kigeni anaocheza nao nafasi hiyo.

Huyu siyo mwingine ni Clement Mzize kijana ambaye maisha yake ya mpira muda mwingi yalikuwa mkoani Iringa eneo la Semtema, miguu yake ikicheza sana kwenye uwanja wa Kihesa, Kigonzile na Samora pia. Ila kwa sasa kijana huyo miguu yake imekuwa ikicheza viwanja vikibwa ndani ya nje ya Tanzania

Clement Mzize ni kijana ambaye ameonyesha ubora wake kwa muda mfupi licha ya kutopita kwenye misingi bora ya mpira wa miguu ukilinganisha na vijana wengine kama Dickson Job, Israel Mwenda, Kibwana Shomari. Licha ya yote hayo bado ameonyesha ubora jambo ambalo linapelekea kuibua tetesi mbalimbali kuhitajika na baadhi ya vilabu vikubwa ndani ya nje.

Kitendo cha Azam FC kuhitaji huduma ya kijana huyo tena kwa kuweka kiasi kikubwa sana cha pesa mezani ili kupata saini yake ni dhahiri kuwa kwa sasa thamani yake ipo juu na ni wakati wake sasa. Licha ya yote hayo ila kijana huyu amekuwa bora sana akiingia kwenye mifumo mbalimbali ya makocha, kivipi ?.

Wakati wa kocha Nasredine Nabi, alikuwa akitumika zaidi akitokea katikati zaidi na alikuwa akionyesha ubora wa hali ya juu akiungana (aki link) vizuri na viungo wa ushambuliaji kwa kutengeneza magoli na kufunga pia. Ila kwa sasa chini ya Miguel Gamondi amekuwa akitokea katikati ila mara nyingi amekuwa akitumika zaidi kama mshambuliaji ila akitokea pembeni zaidi akitengeneza nafasi na ndiyo sababu ya kuwa mshambuliaji pekee kwenye Ligi aliyetengeneza (Assist) magoli mengi akiwa nazo 5 mbili nyuma ya kinara wa (Assist) Ligi kuu.

Anaweza kuingia kwenye mfumo wa Azam FC? Jibu ni ndiyo kwani namna wanavyocheza Azam FC wamekuwa wakitumia mawinga zaidi na kwa nmana anavyocheza Clement Mzize ni dhahiri ataingia kirahisi sana na hiyo inabebwa na uwezo wake wa kutokea pembeni na katikati pia.

Ni ipi njia bora kwake kubaki Yanga SC au kwenda Azam?. Kwa mujibu wangu sioni shida kwa yeye kwenda Azam FC au kuamua kubaki Yanga SC na sababu ni kuwa vyote ni vilabu vikubwa. Ila kwenye upande mwingine ni angalie upande ambao utampa zaidi mafanikio kwenye uoande wa maokoto nikimaanisha malipo kuanzia usajili hadi mshahara wake kwani maisha ya wacheza mpira ni mafupi mno hivyo ni vyema akaanza kutengeneza njia nzuri sasa.

Kiasi walichoweka Azam FC ni kikubwa sana na kimeonyesha kumpa thamani mchezaji huyo na hiyo ni faraja sana kuona mzawa anapewa thamani kubwa hivyo, ila yote ya yote Azam FC kuna nafasi kubwa kwake yeye kucheza zaidi tena kwenye kikosi kinachoanza.

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga 

11 Comments

  1. Tobias Mzopola on

    Azam fc ndiyo chaguo lake Kwa sasa. Hauhitaji kufikiria mara mbili kufanya maamuzi hayo hata kama wewe ndo ungekuwa mzize.

    • Mashaka Lugoma on

      Ulaya hapawezi kuwa sawa na Chamazi wala Kariakoo bila kufikiria ni namna gan ataweza kufanikiwa au kutofanikiwa ila Watford ni miongoni mwa timu kubwa kwa level ya wachezaji kutoka kwenye taifa kama letu (Tanzania)

      So kama Watford wapo serious kwel basi Mzize na watu wanaomsimamia hawatakiwi kupepesa macho kwenye deal hilo kwani kucheza championship ya England ni tayar profile ya mchezaji inaanza kukua na kuanzisha safari nyingine ya soka kwa mchezaji yeye binafsi na Taifa letu

  2. Agripina mwang'onda on

    Me nadhani Clement mzize ni wakati wake wa kuchagua Azam au Abaki yanga Ila wanayanga bado tunamhitaji Sana na kwakuwa Ana uwezo mkubwa ni bora tumpeleke Ulaya kipaji kikukue zaid

  3. Collins collinho on

    Kupata offer ya kwenda ulaya then ukatae uende azam itakua ujinga yatakua kama ya ibrahim ajibu kapata offer kwenda tp mazembe akagoma et anaipenda simba nini kilimkuta sasa yupo costal union mzize anatakiwa kukaa na kufikilia kwa makini sana

  4. Baxeo Africa on

    Mm Kama mhanga wa maendeleo ningependa kumshauri kijana huyu chipukizi alinganishe uwiano wa mambo mawili kabla ya kufanya maamuzi ambayo ni;
    1.upande wa maokoto kwa manufaa yake binafsi
    2.ni uwezekano wake kucheza katika kikosi Cha kwanza kwa AJILI ya kipaji chake

  5. Rumbyambya Jr on

    Wenyewe wanamuita waridi Mzinze. Ipo hivi Clement yampasa atumie busara kubwa sana kufanya maamuzi ambayo yatamletea manufaa yafuatayo;
    1.kutokupotea katika rada za Soka
    2.Kujitengenezea nafasi za kuwa bora zaidi ili kwenda Katika soko la Football
    Kwa upande wangu ni bado mapema saana kwa mzinze kwenda Ulaya .
    Bora zaidi akienda kwa Wana lamba lamba mwisho wa Msimu kwa sababu Yanga watasajili na hope atakuja mtu atakempa Mzinze wakati mgumu sana kuwika mitaa ya Jangwani

  6. Abaki Yanga kwa kua bado chipkiz akienda huko mambele ataishia kupigwa sub na ku under performe ni bora achezee yanga kwa msimu mwingine aivee vizuri kisha ndo atembee mamble ila sio Azam . maana atakua anajishusha kutoka juu kwenda chini

Leave A Reply


Exit mobile version