Kama utakua ni miongoni mwa wale ambao hutazama masoko mbalimbali katika ubashiri na ambazo huwa na odds za juu basi lazima utakua umekutana na soko hili ambalo limeandikwa Player Specials.

Mara zote option kama hii hutafutwa sana na wale watu ambao wanakua wamechambua takwimu mbalimbali ambazo anakua nazo mchezaji katika baadhi ya mechi ambazo anakua amezicheza na hapa utaangalia vitu vingi sana kwa mchezaji binafsi pekee.

Katika soko hili utakutana na kuamua labda atapiga mashuti mangapi langoni au atapiga pasi ngapi katika mechi husika, lakini pia unaweza kuangalia atacheza rafu mara ngapi au kupata kadi katika mchezo huo husika nk.

Hizo ndio miongoni mwa option ambazo utakutana nazo katika kutumia soko hili kwenye ubashiri wa mikeka yako haswa kama utachagua option hii ya Upekee wa mchezaji katika mchezo.

Mfano: Mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Morocco uamue kubashiri kuwa Aishi Manula ataokoa mashuti zaidi ya 4 katika mchezo huo na ikatokea akaokoa mashuti 5 basi umeshinda, kumbuka kuwa ikatokea hajaokoa shuti hata moja basi umepoteza mkeka wako.

Wapo ambao huamua mara nyingi zaidi katika soko hili kuwapa mabeki kupiga pasi zaidi ya 20 au chini ya hapo kutoka katika kipindi husika cha mechi au kuwapa washambuliaji nafasi ya kupata shots on target hata zaidi ya 4 katika mechi husika.

Unaweza kuamua kubashiri nani apate kadi ya kwanza katika mchezo na hata nani apige kona ywa kwanza au ya mwisho au hata ya 2 ya mchezo.

 

SOMA ZAIDI: Nini maana ya Anytime Goalscorer katika betting?

 

4 Comments

  1. Pingback: Huu Hapa Mkeka Wa Leo Ijumaa - Kijiweni

  2. Pingback: Senegal vs Ivory Coast Mkeka Wa Ubashiri Tunausuka Hivi - Kijiweni

  3. Pingback: Mkeka Wa Leo Jumanne Wenye Odds 100 - Kijiweni

  4. Pingback: Mkeka wa Leo Jumatatu Anza Wiki Kibingwa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version