Wapo watu wengi sana ambao wamekua wakikutana na option hii wakati wanasuka mikeka yao ya kila siku na wameshindwa kufahamu ikoje na unachezaje ili uweze kushinda kwenye mkeka. Usiwaze sana kwani sisi tumekuandalia ufahamu nini maana ya “match result and both teams to score” ili uweze kuitumia katika mikeka yako.

Ukizungumzia Match Result kwanza kabisa maana yake ni kwamba una bashiri matokeo ya moja kwa moja ya mchezo husika ambapo ni Ushindi au Sare na hii ni kwamba kama kwenye betslip unakuta kuna timu ya nyumbani au ugenini na sare. Mfano : Mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam Fc ukisema matokeo maana yake ni Simba ashinde au Azam ashinde au kupatikane sare katika mchezo husika.

GG ambavyo ni kifupi lakini kubwa yake ni kuwa timu zifungane sasa katika soko hili la “match result and both teams to score” maana yake ni kuwa unabashiri timu ipate ushindi au kutokee sare na zifungane katika mchezo huo.

Zipo ambazo baadhi ya kampuni hutumia kwa jina la Full-Time results na zipo ambazo hutumia jina la match result ila namna yake ya ubashiri inakua ni ile ile tu.

Kwa upande wa GG ni muhimu kufahamu kuwa unaweza kukubali au kukataa kwani huwa ni kama swali tu kwamba GG ukasema YES, au kwamba GG ukasema No.

Mfano mzuri ni huu hapa:

Maana yake ni kuwa hapa unachagua katika mchezo huu kati ya Liverpool na Real Madrid kuwe na matokeo halisi ya mechi lakini pia timu zifungane isipotokea hivyo basi ujue kuwa mkeka wako umechanika.

Ukitazama jinsi palivyo hapo ni kwamba unaweza kuchagua option hizo ambazo zinakua kwa upande wa soko hili la matokeo na kufungana hivyo maamuzi ni yako tu kuusuka vyema mkeka wako kwa jinsi ambavyo unadhani itakua vyema na kukupa ushindi.

SOMA ZAIDI: Nini maana ya 1 | x | 2 katika betting? 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Exit mobile version