Timu zote mbili kwa nyakati tofauti walionekana kuwa watulivu sana hususa ni kikosi cha Simba SC licha ya kuwa nyuma kwa goli 0-0 ila walikuwa watulivu sana kwa dakika 90 za mchezo huo. Utulivu huo uliifanya Simba SC kuendelea kucheza kwenye mbinu yake na hata goli walilopata lilichangiwa na utulivu wao kuanzia nyuma kwenda mbele kufanya shambulizi.

Licha ya kujaribu mara kadhaa wa kadhaa kucheza mipira ya juu ila Geita walionekana kuimudu vizuri mipira na muda mwingi wa mchezo walikuwa wakiiondoa kwenye eneo lao. Kuingia kwa Nassoro Saadun kwa upande wa Geita Gold FC kuliipa balance upande wa kulia wa Geita Gold na kulimnyima Mohamed Hussein “Zimbwe” kupanda mara kwa mara kama alivyokuwa anafanya kipindi cha kwanza, hii ndiyo Sub iliyoleta tofauti zaidi kwa timu zote mbili.

Luis Miquisone pamoja na Saido Ntibazonkinza iliongeza kasi ya mashambulizi kwa upande wa Simba SCna sababishi wa goli la Simba SC.

Mchezo ulichezwa zaidi na upande wa Simba SC utulivu wa Beki Che Malone Fondoh pamoja na kiungo Fabrice Ngoma uliendelea kuifanya Timu ya Simba SC kutulia mipira mingi iliyokuwa ikitua eneo lao walitulia na kuipeleka eneo sahihi.

Mbinu kubwa ya Geita Gold FC waliyoitumia ni kujilinda zaidi kipindi cha kwanza waliingia na 4-4-2 mbele akibaki Ramadhani Kapera pamoja na Edmund John huku wachezaji wengi wa Geita wakiwa eneo lao na kuziba mianya mingi ya mpira kupita.

Kipindi cha pili walibaki kwenye mbio yao ile ile ila Saadun alibaki kama mchezaji anayepanda na kushuka pamoja na Eric Mwijage wakisaidia mashambulizi pamoja na mshambuliaji Tariq Seif aliyechukua nafasi ya Ramadhani Kapera, hivyo iliongeza kasi kidogo ya kishambulia hususa mipira ikitokea pembeni kwa Mwijage pamoja na Saadun.

Upande wa Simba SC waliingia na 4-3-3 ambapo Clatous Chama, Kibu Denis pamoja na Pa Omar Jobe wakitumika kwenye eneo la ushambuliaji, mabadiliko ya kimfumo yalikuwa yakitokea kuna wakati Simba SC waliamia kwenye mfumo wa 4-2-3-1 na Jobe alibaki kwenye eneo la mwisho Chama pamoja na Kibu Denis wakiungana na Sadio Kanoute kwenye kiungo zaidi kwenye kuipandisha timu huku Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma wakibaki zaidi eneo la ukabaji.

Kipindi cha pili kwa Simba SC kilibadilika na walitumia zaidi maeneo yao ya Pembeni na hiyo ilifanya kumuingiza Luis Miquissone na Saidi Ntibazonkiza wakiwa wanatokea pembeni muda mwingi wa Mchezo na hata goli pekee la mchezo huo lilitokea upande wa pembeni.

Kongole kwa waamuzi wa mchezo wa leo walijitahidi na mchezo ulikuwa na maamuzi sahihi kwa muda mwingi wa mchezo huo.

 

SOMA ZAIDI: Mayele Ana Laana Ya Ligi Kuu?

Leave A Reply


Exit mobile version