Ile siku ambayo huwa na hisia tofauti kwa mashabiki wa soka wa Tanzania lakini pia na wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga ndio leo ambapo ni wazi Gamondi muda huu atakua anakuna kichwa kuona jinsi ambavyo wachezaji wake watatekeleza vipi zile mbinu ambazo waliziandaa kuelekea mchezi wao dhidi ya CR Belouizdad.

Tumeona namna ambavyo Okrah amerejea na ile kasi ambayo wengi walikua wanasubiri kuiona kutoka kwake tangu asajiliwe na wengi wamekua wakiibuka na maoni yao kama ambavyo imekua kwa mashabiki wa soka wa Tanzania ambao kila mmoja huzungumza vile ambavyo anaona kwakwe ni sahihi.

Unaweza kujiuliza ni nani aanze kati ya Max Nzengeli au Okrah Magic lakini kwangu mimi nadhani ni heri akaanza Max japokuwa namheshimu sana Okrah kwa kiwango chake alichonacho kwanza kabisa ukimtazama Nzengeli anacheza nafasi zaidi ya tatu anapokua uwanjani ambapo nacheza namba 8,6,11,7 na 10 hii ni tofauti kabisa na Okra Magic ambaye anacheza winga ya kushoto na kulia tu ina maana anacheza namba 7,11 ni mzuri zaidi winga ya kushoto.

Nzengeli anauwezo mkubwa wa kukaba tofauti na Okra Magic timu inapokua haina mpira kwani  huwa anarudi pande zote za uwanja kutafuta mpira na kukaba wakati Okra mpira ukipotea siyo mkabaji Kama Max.Naweza kusema kosakosa za magoli kwa Max Nzengeli asishushwe ubora wake awapo uwanjani

Iwapo Kocha hatochanga karata zake vyema, akaingia mkenge kushawishika kupanga kikosi kupitia mtandaoni japokuwa siamini hilo naona akienda kufeli kwani kuna wachezaji ambao baadhi ya mechi wanaweza kwenda kuigharimu timu siku ya jumamosi.

Yani kama mchezaji wenu hakuwahi kuonesha Quality ya kuridhisha kwenye mechi tough, then muanze kum-rate na kumpimanisha mchezaji huyo na mwengine kupitia performance ya jana dhidi ya timu ya Championship basi hamtapata kipimo sahihi.

Lakini kwa upande mwingine, Max anauwezo wa kucheza eneo finyu lililo banwa na wapinzani kwa kua ana flexibility na mobility, Okra ana uwezo mzuri wa kucheza kwenye eneo kubwa kwakua ana spidi kubwa kwaiyo inategemea na aina ya mpinzani anavyo cheza.

Ningekuwa Gamondi naanza na Okrah na Guede/Musonda mechi ya waarabu halafu second half naweka silaha nzito Max na Mzize lazima mwarabu namuua haraka sana

SOMA ZAIDI:Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga

1 Comment

  1. Pingback: Yanga Mmeniziba Mdomo, Mpira Ni Uwekezaji Sio Uchawi - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version