Kuna wakati unaweza kujiuliza wana shida gani na wanakosa nini lakini ukiona namna ambavyo wanaishi na jinsi ambavyo walivyo katika mazingira mazuri kabisa kimpira unashangaa na kujiuliza hivi ni hawa ambao wanapata kila kitu? Azam wamekua na mchezo mzuri na kukosa nafasi nyingi sana za wazi ambazo kwa timu ambayo ina malengo ya ubingwa haiwezi kufanya na kukosa nafasi namna hiyo ambayo wamekua wakikosa.

Ukiangalia kwenye matokeo ya hivi karibuni ni kama Simba wanapata shida kupata ushindi mbele ya Azam fc msimu uliopita kwenye ligi Azam ameondoka na alama 4 huku Simba akiambulia alama moja, lakini pia Simba alipoteza kwenye mechi ya nusu fainali FA kule Nangwada sijaona.

Msimu huu Azam tayari walishajipata na wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu na kabla ligi haijasimama walikuwa kwenye kiwango bora kuliko Simba ambayo ilitoka kupoteza kocha na kuwa chini ya kocha mpya ambaye ndo anaijenga Simba.

Tangu ligi imerudi Azam hawajacheza mechi hata moja ya kiushindani kulinganisha na Simba ambao wamecheza mechi mbili na kupata alama zote sita jambo ambalo uanweza kusema kuwa wachezaji wa Simba tayari wapo kwenye ushindani na tayari wamepata ile namna ya kupambana ingawa Azam nao walikua na mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu jambo ambalo nililitegemea hata kwenye hata mechi ya leo ambayo Azam walikua vizuri ingawa Simba walikua na kujiamini sana kutokana na  morali ya kushinda mechi mbili lakini tayari wachezaji washacheza mechi ngumu na utimamu wa miili yao unaonekana kuwa sawa.

Hii ilikua  ni mechi ambayo ilikua inatoa taswira ya msimamo wa Ligi kwa timu tatu zinazowania ubingwa [Yanga, Azam FC na Simba] huku tuliona kuwa Azam haitaki kuachwa mbali na Yanga wakati Simba inataka kuendelea kuisogelea Yanga na kuongeza ushindani kwenye mbio za ubingwa.

Ushindi wa Yanga dhidi ya Mashujaa pia uliongeza presha kwenye mchezo wa Simba vs Azam, kwani kila timu ilikua inahitaji alama tatu. Timu yoyote ambayo ingepoteza mchezo mchezo wa leo basi ingepata kuongeza tofauti ya alama dhidi ya Yanga ambao ndio vinara wa Ligi.

Nilitarajia mechi itakuwa ngumu kwani Simba imefanya mabadiliko kwenye baadhi ya maeneo kupitia dirisha dogo la usajili hususani kwenye eneo la ushambuliaji na tayari washambuliaji wao wameshafanikiwa kufunga kwenye mechi iliyopita lakini katika mchezo huu wamekutana na wakati mgumu sana japokua wamepata bao kutoka kwa kiungo Chama.

Tumeona namna ambavyo Azam pia imefanya usajili wa wachezaji kadhaa kupitia dirisha dogo lakini kitu kizuri kwao wachezaji wapya katika mchezo huu wamekua hawana presha kubwa ya kuingia moja kwa moja kikosini kwa sababu wachezaji wengi muhimu bado wapo na wanafanya vizuri.

SOMA ZAIDI: Simba Wamefikiria Alama 3 Au Mapato CCM Kirumba?

1 Comment

  1. Pingback: Utata Wa Penati Na Uchambuzi Wa Kina Simba vs Azam - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version