Baada ya hatua ya makundi ya Michuano ya Mataifa barani Afrika AFCON kutamatika na kujua timu 16 ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora na kujua ratiba kamili ya hatua hii kabla ya kwenda robo fainali kujulikana. Karibu sana tutazame tuzo za hatua ya makundi zimeenda kwa nani na nani?

1.MCHEZAJI BORA KIJANA HATUA YA MAKUNDI

Mpaka hatua ya makundi inatamatika tumeshuhudia vijana wengi wakifanya vizuri ila kijana mdogo kutokea kikosi cha Senegal Lamine Camara ameibuka kuwa Mchezaji bora wa hatua ya makundi.Camara ambaye ana miaka 20 tu akiichezea klabu ya Metz huku akitumia zaidi mguu wa kulia, amevaa jezi namba 18 kwenye AFCON hii na amecheza Dakika 179 sawa na mchezo mmoja na mchezo mwingine akitolewa dakika ya 89.

Hata hivyo amefanikiwa kufunga jumla ya goli 2 tu na yote dhidi ya Gambia na akipata kadi moja ya njano.Ikumbukwe kuwa Lamine Camara ndiyo Mchezaji bora wa AFCON U-20 iliyofanyika Misri. 

2.KIPA BORA HATUA YA MAKUNDI

Kipa wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea Jesús Owono ndiyo amekuwa kipa bora wa michezo yote ya Hatua ya makundi. Jesus Owono amefanikiwa kufanya jumla ya save 25 za Hatari katika michezo yote mitatu kwa ujumla, huku akiwa na pasi moja ya goli dhidi ya Guinea Bissau akimpa Josete Miranda akifunga goli la pili la mchezo huo. 

Ikumbukwe kuwa Jesus Owono anavaa jezi namba 31 kwenye kikosi chake cha Equatorial Guinea akiwa na umri wa miaka 22 tu akihudumu ndani ya Kikosi cha Deportivo Alaves ya Hispania na anatumia zaidi mguu wa kulia. 

3.KOCHA BORA

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Senegal Aliou Cisse ameibuka kuwa Kocha bora wa michezo yote ya makundi ya AFCON, huyu ndiye kiongozi wa benchi nzima la Ufundi la Senegal.Cisse ameongoza jumla ya michezo mitatu ya Makundi akifanikiwa kushinda michezo yote mitatu, wakifunga jumla ya magoli 8 na wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja tu, huku likiwa taifa pekee lililofungwa goli moja tu katika hatua ya makundi.

Kikosi cha Senegal ndiyo taifa pekee lililofanikiwa kushinda michezo yake yote ya hatua ya makundi na kukusanya jumla ya alama 9.Ikumbukwe kuwa Aliou Cisse ana umri wa miaka 47 na ni Nahodha wa zamani wa taifa hilo, na aliaanza kama Kocha msaidizi wa Senegal kwa miezi 10 na Marchi 2015 akateuliwa kuwa Kocha mkuu wa Senegal. 

SOMA ZAIDI: Mchezaji Huyu Yanga Kutinga Robo Fainali AFCON

1 Comment

  1. Pingback: AFCON Imepita Na Vichwa Vya Makocha Hawa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version