Mchezaji mashuhuri wa Manchester United, Rio Ferdinand ameshangazwa na uamuzi wa Erik ten Hag wa kutomuanzisha Fred katika mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Newcastle United mwishoni mwa wiki iliyopita, akisema hii ilikuwa ni kosa la kocha.

Manchester United walipoteza kwa 2-0 katika uwanja wa St. James ‘Park, baada ya magoli kutiwa wavuni na Joe Willock na Callum Wilson.

Ferdinand haielewi kwa nini kocha huyo Mholanzi aliamua kumuanzisha Marcel Sabitzer na Scott McTominay badala ya Fred katika kiungo pamoja na Bruno Fernandes ambaye alicheza nafasi ya No.10.

“Nilishangaa sana kwa nini Fred hakucheza. Kuelewa nini kinachohitajika katika mechi hii, Fred ana nguvu, miguu, na uwezo wa kupigania mpira,” Ferdinand alisema kwa FIVE.

“Unaweza kumkosoa Fred kwa kitu chochote lakini nishati, kujitolea na kujituma hazijawahi kuwa kitu unachoweza kusema ni hasi kwake. Hivyo nilikuwa kweli nimeshangaa aliposhindwa kuanza mechi. Lakini nafikiri kwa ujumla hakuna mtu ambaye alikabiliana na hali hiyo. Hawakuwa tayari kwa mechi hiyo.”

Leave A Reply


Exit mobile version