IlipoishiaWaliomba sana, kuna wakati mimi nilihisi kuchoka lakini wao waliendelea tu hadi moyoni nikasema kweli ni watu wa Mungu.

Ghafla nilianza kuona moshi mweusi ukitoka chini ya milango yote ya wale ndugu, mlango wa sebuleni kama sikikosei na mlango wa chumbani. Moshi ulikuwa mzito kiasi kwamba, kuna wakati nilihisi kupaliwa na kukohoa kwa nguvu lakini wao hawakuonesha dalili ya kusumbuliwa na moshi huo ” 

Endelea

SEHEMU YA TISA (09)

Mara, milango yote miwili ikaanza kufunguka yenyewe polepole huku maombi yakiendelea kwa kasi na nguvu ya ajabu. Milango hiyo ilifunguka hadi ikafika mahali ndani kukaonekana.

Cha ajabu sasa, vyumba vilikuwa vyeupe, ndani yake hakukuwa na kitu chochote, hata karatasi. Ilikuwa kama chumba kilichopigwa deki au kufagiliwa kwa ajili ya maandalizi ya kuingia mkaaji mpya.

“Ha! Oneni jamani,” nilijikuta nikisema hivyo. Nilibaini kwamba, wale watu hawakuona wakati milango inafunguka kwa vile walipokuwa wakiomba walifumba macho na walikuwa wakijipigapiga kwenye viganja kwa kutumia ngumi.

Yule mzee alipoona vile akasema:

“Katika jina la Yesu.”

“Amiiin.”

“Sasa tushushe uwepo wa Bwana mahali hapa, kwamba akapafanye pawe mahali salama, penye amani na utulivu wa hali ya juu, kila mmoja sasa amwombe Bwana hivyo.”

Wakaanza kuomba tena, safari hii si kwa kukemea kama mwanzoni, ilikuwa sauti yenye upole na utii, mara nikasikia mlango mkubwa ukigongwa kwa nguvu.

“Ngo ngo ngo ngoo.”

“Ingia,” nilisema lakini huku nikienda mlangoni, nikaufungua! Mbele yangu alisimama yule dalali.

“Karibu bwana.”

“Ee bwana nini umefanya sasa?” ndilo swali lake hata kabla ya salamu.

“Kwa nini?”

“We hujui umefanya nini? Si wako watu humo ndani, wamekuja kufanya nini hapa? Hujui kama kuna watu umewaumiza? Wewe ungefanyiwa hivyo ungekubali kweli?”  

“Kaka unajua ukija kwangu njoo kwa heshima zako zote na hoja zenye msingi, usije kama mwendawazimu mpya, wewe unachokisema mimi sijakisema kwako? Ulichukua hatua gani wakati naumia mimi?”

“Lini umeniambia?”

“Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari kwa hilo…”

“Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana.”

“Sina haja, mimi ndiyo najua.”

Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba ile.

Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto, akasimama, akawa kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda kushoto na kuanguka puu!

Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa moja na matukio yote ya ajabu mle ndani. Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.

Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo alisema mambo ya ajabu sana. Alisema mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala kujulikana na mtu.

Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna ila alikuwa anasikia raha.

“Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu yeye hajui.”

Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila kulisema kwa mtu.

Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe, walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua, walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.

Yule mzee mkubwa wa wale waombaji akamuuliza:

“Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko wapi?”

Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.

Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi:

“Sasa watu wanasema majini wana uwezo mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli ni kwa nini aliamua uwe dalali?”

Dalali akajibu: “Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa sababu mimi na mke wangu tulipenda kuwachezea watu wanaoishi ndani.

“Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya maisha wala ya fedha.”

Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka. Hata siku ya kwanza nilipokutana naye nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi nikapata nguvu ya kumuuliza swali:

“Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje kusababisha mimi nipate namba yako ya simu kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf Mwamba?”

“Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na kukifanyia kazi. Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf.”

Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema tumwingize ndani maana watu waliokuwa wakipita walianza kukodolea macho pale nje.

Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna mtu amebandika jiko la mkaa.

“Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia matendo yako ya nyuma,” alisema yule mzee aliyenisaidia.

“Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine. Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu.”

Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali akasema atakwenda kesho yake mapema.

Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi ulinishika lakini nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba nimsamehe kwa yote yaliyopita.

Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta dalali ameshafika.

Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya wiki mbili, dalali alimleta mke wake  na mtoto mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado nasali kulekule Magomeni na yule dalali.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania mpaka kutoka katika nyumba ile. Ile mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu. Nadhani shetani alipanga nife katika nyumba ile lakini ameshindwa katika jina la Yesu. Amina.  MWISHO 

Tafadhali Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako Simulizi Ijayo Iwe Ya Kitu Gani? MAPENZI UJASUSI au UCHAWI?

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

45 Comments

  1. Stori zote tatu mwishoni huwa zinatoka kwenye uhalisia zinaishia kistori stori
    Jitahid ijayo kuwe na improvement plz

  2. Amina admin. Hii Stori ituhamasishe watoto wa Mungu kumtumainia katika yote. Up next, ujasusi itakuwa poa Sana

  3. Kwakweli hii ilikuwa hadith tamu mnoooo. Asante sana admin. Ukipata stori zingine zenye mauzauza usisite kutuletea.

Leave A Reply


Exit mobile version