Sehemu Ya Kwanza

“KAMA kuna watu hawayajui haya nitakayoyaongea basi nawataka kuanzia sasa wajue kwamba, hapa Dar kuna mambo makubwa sana ambayo ukisimuliwa unaweza kusema si kweli, lakini wale wanaoyapata hayo mambo wanajua na wewe usiombe yakukute hata siku moja,” ndivyo alivyo anza kusimulia Bw. Humuli Samaki (43), mkazi wa Buguruni (kwa sasa) ambaye alipata mkasa mzito akidai alipanga nyumba moja na majini Magomeni, Dar es Salaam.

“Si zamani sana mkasa huu uliponitokea, ilikuwa mwaka 2009 tu, kwa hiyo naweza kusema ni juzijuzi.  Kwa sasa naishi hapa Buguruni, baada ya kuhama kutoka Magomeni ambako nilipata mkasa huo mzito na wa kuogopesha. Nilipanga nyumba moja na majini.”

Awali nilikuwa nikiishi Mwanyamala Mwanjuma, jirani kabisa na Makao Makuu ya Bendi ya TOT, hata Kapteni John Komba nilizoeana naye kwa kuonanaonana pale CCM-Mwinjuma, ingawa jina langu najua hakuwa akilifahamu.

Ile nyumba niliyokuwa nikiishi Mwananyamala iliingia kwenye mgogoro wa mirathi, familia ilifika mahakamani. Hukumu ilipotoka ikaamriwa iuzwe kisha ndugu wagawane fedha.

Kwa maana hiyo, mimi na wapangaji wenzangu watano, tulipewa notisi ya kuhama baada ya mteja kupatikana. Huyu mteja anaitwa Masawe anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini sijui ofisi za wapi.

Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine, niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala mtoto, hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa mke wangu huyu.

Rafiki yangu mmoja anaitwa Mohamed Kombe alinipa namba ya dalali kwani yeye anaishi Magomeni hata sasa. Nilimpigia simu dalali wake, anaitwa Yusuf Mwamba, akaniita Magomeni pale kwenye nyumba wanayosema aliwahi kuishi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikwenda mpaka pale, nilimkuta amesimama nje ya nyumba hiyo, tukasalimiana, akaniuliza nataka nyumba yenye sifa gani, nikamweleza.

Akasema nyumba ya aina hiyo ipo moja mitaa ya katikati kama unatokea pale tulipokuwa kuelekea kwa Sheikh Yahya Hussein (marehemu).

Tulikwenda kuiona hiyo nyumba. Wakati tukiwa tunaifikia, nilishangaa kuwaona majirani wakitukodolea macho, sikushangaa nikijua ni mambo ya mjini kitu kidogo tu watu kibao.

Yule dalali alifungua mlango, tukaingia ndani. Tulipita sebuleni, tukaenda kwenye vyumba viwili, tukaelekea  jikoni, chooni na kumalizia na bafuni. Ni nyumba iliyojitegemea kwa maana kwamba, ilikuwa na ua wake na mtu akiwa uani hakuna aliyeweza kuona kwa nje. Mlango wa kuingilia ndani ni mmoja tu.

Kulikuwa na vyumba vingine viwili ambavyo toka mwanzo alishaniambia kuna mtu anaishi na mkewe, kimoja wanalala, kingine wamekifanya sebuleni, lakini hawana watoto kama mimi.

Nilijiridhisha kwamba ni pazuri, dalali akaniuliza kuhusu malipo, nikamwambia tuongozane nikachukue fedha Magomeni Mapipa kwenye benki ya Barclays, akasema wakati mimi nakwenda kutoa hizo fedha, yeye anakwenda Dawasco tawi la Magomeni.

Tukiwa tunaelekea Magomeni Mapipa, nilimuuliza wenye vile vyumba wanafanya kazi wapi? Akajibu wafanyabishara, lakini hata yeye hajui ni wapi. Nilimuuliza imekuwaje ana funguo, wale wapangaji wengine wakirudi je, akajibu wana funguo yao na ile yeye alipewa na mwenye nyumba kwa ajili ya kutafutia mpangaji mwingine. Nilikubaliana naye.

Baada ya nusu saa nilitoka benki nikiwa na fedha, nikampigia simu, akasema na yeye alishatoka Dawasco na wakati huo alikuwa anakunywa soda kwenye Hoteli ya Shibam, ipo palepale Mapipa. Nilimfuata pale, nikampa fedha, akatoa mkataba, nikajaza kwani yeye ndiye aliyepewa jukumu lote na mwenye nyumba.

“Kwa hiyo upo huru kwenda kuhamia,” dalali aliniambia huku akinikabidhi funguo.

“Sawa, nitahamia usiku wa leo.”

Nilirudi nyumbani kwa awali na kupangapanga vitu tayari kwa usiku kuhamia makazi mapya, Magomeni. Niliwaambia wapangaji wenzangu wote, nao wakanitakia maisha mema huku wakisema tukumbukane kwani hata wao walikuwa kwenye mchakato wa kuhama kwenye nyumba ile.

Saa mbili usiku nilikuwa juu ya lori tukipeleka mizigo makazi mapya, lakini moyoni nilikuwa na maswali mengi ambayo mpaka leo hii siyakumbuki na yalikosa majibu. Pia, nilijikuta nakosa amani ya moyo na sikujua ni kwa nini!

Nje, nilikuta taa inawaka, ndani pia taa inawaka, lakini si sebuleni bali kwenye korido. Hii iliashiria kwamba, wale wapangaji wenzangu walisharudi kutoka kwenye biashara zao.

Nilishusha vyombo kwa kusaidiwa na wasaidizi wa dereva wa lile lori, lakini nilishangaa sana kuona kila nikiingia na mizigo, wale wapangaji wenzangu wanacheka sana chumbani kwao. Maana yangu ni kwamba, kwa kawaida walitakiwa hata watoke na kunisalimia ili tufahamiane. Tena kwa wengine, mume angetoka na kunisaidia kubeba hata stuli tu.

Mambo yameanza.. Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILI Ila Niambie Hapa Uliwahi Kukutana Na Jambo Gani Kwenye Nyumba za kupanga likakushtua?

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

46 Comments

  1. Oyaa tunao lala pekeyetu tuna ruhusiwa kusoma kwanza maana nimeona picha tu nika sita

    Oya hivi vitu vya kutisha naomba vije kwa wingi kabisa😆😆

  2. Ila nyie watu hawa,, Duh🤔🤔🤔
    Et “lakini nilishangaa sana kuona kila nikiingia na mizigo, wale wapangaji wenzangu wanacheka sana chumbani kwao.”
    Mbn ni Kamzozo

  3. Upcoming Billionaire on

    Admn siku ya yanga kuchukua ubingwa utatuuliza kama tumeflai afu uweke LIPA NAMBA we jamaa unajua kujiongeza 🤣

  4. “Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine, niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala mtoto, hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa mke wangu huyu.”

    “Kulikuwa na vyumba vingine viwili ambavyo toka mwanzo alishaniambia kuna mtu anaishi na mkewe, kimoja wanalala, kingine wamekifanya sebuleni, lakini hawana watoto kama mimi.”

    Hii umejitungia tuu au!!?

    Mwanzo hukua na familia mara hawana watoto kama yeye ndio nini sasa?

Leave A Reply


Exit mobile version