Ilipoishia Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana. 

“Kunywa Maji” alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikua  ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuuliza 

“Mnanimalizia lini nikapumzike?” Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chache  nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambia 

“Kifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwaje” alisema kisha akanipa maji, sikuwa  na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai. Endelea 

SEHEMU YA NANE

Niliyafakamia yale maji kwanza hadi yalinipalia, halafu nikahema. Akanitolea vidonge vya  kunituliza maumivu. Sikusita kumeza kiukweli maana nilikua na maumivu makali sana kisha  nilimshika mkono nikamuuliza 

“Ningekuwa mdogo wako ungenifanyia hivi, unajua najisikiaje Kaka?’’ Chozi lilikua  linanibubujika bila kuacha, akaniondoa mkono wangu kwa kutumia mkono wake mwingine  kisha akasimama, akaniambia 

“Kula upate nguvu” hakuzungumza tena, alisimama kisha alipiga hatua lakini alipofika mlangoni  alisimama. Kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini alighaili, hakujibu swali langu aliondoka na  kuufunga mlango kwa funguo, unajua hata kama angeuacha wazi sikuwa na nguvu ya kukimbia  kwa namna nilivyokua sina nguvu.  

Nilisikia akiondoka, nililia sana Mimi. Hakuna siku inapita bila kudondosha chozi langu,  nilimpoteza Kaka Hamidu na nilijiona ni mkosaji, nilijilaumu sababu bila kuolewa na Salehe  basi Kaka Hamidu angekuwa hai hadi sasa. Kidogo zile dawa zilipunguza maumivu ya mwili  lakini siyo maumivu ya Moyo wangu  

Haikuchukua hata dakika nyingi nilisikia yowe la Mwanaume mmoja, yowe lile lilisikika moja  kwa moja kutoka kwenye ile nyumba niliyohifadhiwa Mimi. Moyo ulinilipuka, niliamini ilikua  ni nyumba ya Mateso makali zaidi hata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama hata  nguvu sikujuwa ilitokea wapi 

Nilisogea mlangoni ili kuisikia zaidi ile sauti, ndiyo! Ilitoka ndani ya moja ya vyumba vya ile  nyumba, nilitamani kupaza sauti ila sikujua alikua akifanywa nini. Nilijiuliza

“Nani yupo ndani ya hii nyumba, anamfanya nini huyu anayepiga yowe” Ilikua ni sawa na  kujitekenya kisha kucheka mwenyewe, jibu lingetokea wapi ikiwa hata mimi mwenyewe sijui  nipo wapi 

Yule Mwanaume baada ya kupiga yowe alianza kusema 

“Msaada,Nani yupo ananisikia?” aliendelea kusema hivi, nikapata picha huwenda hata yeye  mwenyewe hajui amefikaje na Nani amemleta ndani ya hii nyumba. Kupitia dirishani nilianza  kuona jua namna lilivyokuwa likifanya safari ya kwenda kupumzika baada ya kuipiga ardhi kwa  siku nzima. 

Namna nyumba hii ilivyo ilionekana kujengwa kwa ajili ya kazi ya kuhifadhi Binadamu, hata  dirisha lake lilikua kama la Mahabusu, lilikua dogo lanye nondo,hapakuwa na taa ndani ya  chumba kiasi kwamba giza litakapoingia basi patakuwa giza tupu. Nilijikuta nikikaa mwenyewe  bila hata kuambiwa, kwa namna ilivyo hata ukipiga kelele vipi huwezi kupata Msaada wowote. 

Kwanza sikujuwa Mtu yule alikua ni Nani, sauti yake haikufanana na ya Kaka Hamidu. Wala si  ya Mtu niliyehisi kuwa niliwahi zungumza naye.  

** 

Usiku ulipoingia ndiyo nililiona joto la jiwe, niliandamwa na ndoto za ajabu hadi niliamka, siyo  Mimi tu hata yule Mwanaume alikua akigugumia nahisi naye alikua kwenye hali kama yangu.  Niliamka na kukaa kitako nikaegemea ukuta 

Nikiwa hapo nilianza kuona nuru ya mwanga, ikianza taratibu hadi ikaenea chumba chote, hapa  nilikua na uhakika kuwa haikuwa ndoto tena bali ni tukio halisi. Nilimuona tena yule Mtoto  mdogo anayetisha, safari hii alinionesha sura yake, nilikua kwenye Mshangao wa hali ya juu  sana 

“Umeshindwa kutoka hapa, umeshindwa kujaribu kufanya chochote. Wewe ni Mtu wa aina gani,  unataka kila Mtu afe kama Kaka yako Hamidu” Ooh! Jamani nilishtuka, kama ningekua nina  presha kwa haya yote ningekuwa tayari nimepotea kwenye uso wa Dunia, namna alivyokua  anaongea alionesha alikua na tumaini na Mimi kwenye jambo fulani hasa la kuokoa uhai wa  wengine lakini Mimi mwenyewe nilikua nimeshajikatia tamaa. Japo nilijawa na woga lakini  nilimuuliza 

“Wewe ni Nani, umetokea wapi?” nilipomuuliza alidondosha chozi la damu, alikua Mtoto wa  ajabu sana 

“Mimi ni Ashura Mtoto wa Mama Muuza chapati. Nenda kamwambie Mama yangu kuwa bado  naishi kwenye nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, Mimi sijafa” alisema kwa kupaza sauti kali  ambayo ilinifanya nishindwe kuhimili zile kelele, pale pale nilijikuta nikiishiwa nguvu na  kupoteza fahamu. Kitu pekee kilichobakia kwenye akili yangu ni ,kumbukumbu juu ya yule  Mama anayeishi nyumba jirani na Mzee Mwinyimkuu, Mama aliyekuwa akiniuzia Chapati

Ndiyo‼ yeye ni Mama Ashura, nakumbuka alinitajia jina hili lakini sikuwahi kumuuliza huyo  Ashura yupo wapi, huyu Mtoto wa ajabu alijitambulisha kwangu kama Ashura na alinitaka  nimwambie Mama yake kuwa anaishi ndani ya nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. 

*** 

Baba yangu aliendelea kuumwa, Mama alikua anamuuguza huku akinitafuta Mimi kwa simu  lakini aliendelea kutonipata, zilipita wiki mbili bila kupata mawasiliano yoyote yale. Salehe  hakupatikana, hata Mzee Mwinyimkuu hakupatikana, Kaka Hamidu naye ilikua kama ndiyo  

kichocheo kipya cha hofu kwa Familia yangu. Mara ya mwisho aliwaeleza anakuja kuonana na  Mimi lakini baada ya hapo hawakujua kilichomfika na kupelekea kutopatikana kwenye simu  kwa wiki mbili. 

Vikafanyika vikao vya kututafuta Mimi na Kaka Hamidu maana hawakujua naishi Rukwa  sehemu gani na pia Kaka Hamidu alikutwa na nini. Ni Mimi pekee ndiye niliyekuwa najua Kua  Kaka Hamidu alikua ameuawa. 

Familia ikamtuma Mjomba wetu aliyeitwa Kambona, alikua Mtu mzima na mwenye busara  zake.  

Akasafiri kutoka Dar-es-salaam hadi Rukwa akiwa na picha yangu, akaanza kunitafuta bila  mafanikio kwa zaidi ya siku kumi. Mwishowe akaenda kituo cha Polisi maana sasa hakuna  aliyekua na amani bila kujua tupo wapi, wote waliamini wakinipata Mimi watajua mahali alipo  Kaka Hamidu maana mara ya mwisho aliwaambia anakuja kwangu. Polisi wakaanza kunitafuta  kila kona ya Rukwa lakini hakuna aliyeweza kujua niko wapi, lakini kupitia jina la Mwinyimkuu Ambalo Salehe alilitaja alipokua ananichumbia, ikawawezesha kufika hadi nyumbani kwa huyu  Mzee. 

Hapa ndipo mahali ambapo nilikuwepo kabla ya kuhamishwa, nyumba hii ndimo alimouawa  Kaka Hamidu tena kikatili sana na Mzee Mwinyimkuu. Walipofika walimkuta tena wala  hakuwa na wasiwasi kabisa, najua alitumia akili sana kunihamisha vinginevyo polisi  wangenikuta mle 

“Wewe ndiye Mwinyimkuu?” aliuliza polisi baada ya salamu fupi 

“Mnasemaje?” aliwauliza, alikua haogopi chochote wala Mtu yeyote yule, jeuri na katili mno “Saida anaishi hapa?” akauliza Polisi mmoja. 

“Yeye ni Nani?” akawauliza 

“Unajibu kwa dharau kiasi hicho Mzee, Saida ni Mpwa wangu Mimi. Ameolewa na Kijana  anaitwa Salehe, upelelezi umeonesha kuwa ni Kijana wako huyo Salehe halafu unauliza ni  Nani?” akaingilia kati mjomba Kambona na kumshika shati Mzee Mwinyimkuu, Polisi  wakaokoa

“Unanivunjia heshiam si ndiyo?” akauliza Mzee Mwinyimkuu kwa hasira 

“Siyo heshima tu, ntaivunja hata hii nyumba kama hutonipatia Saida wangu” Mjomba Kambona  hakupoa kabisa, alijawa na hasira sana. 

“Huyo Salehe unamfahamu?” Polisi wakamuuliza Mjomba Kambona 

“Ndiyo, nimeozesha mwenyewe. Picha si hii hapa ya ndoa” akatoa picha, ile picha akapewa  Mzee Mwinyimkuu. 

“Umemtambua mtajwa pichani?” akauliza Polisi mmoja, Mzee Mwinyimkuu akaangua kicheko  kisha akaita kwa sauti 

“Salehe, hebu njoo uone maajabu ya Dunia” akaitikia Mtu kutokea ndani na kuwafanya Polisi na  Mjomba Kambona wakae mkao wa kula kumuona Salehe. Ikachukua kama sekunde kadhaa tu  Kijana mmoja akatoka ndani, Kijana aliyekuja hakufanana na Salehe wa kwenye picha.  

“Unamfahamu Saida?” akauliza Mzee Mwinyimkuu akimuuliza huyo Kijana aliyemtambulisha  kama Salehe, kiukweli hakuwa yule Salehe aliyeniowa kabisa yaani sura tofauti. 

“Hapana, kuna nini?” akauliza huyo Salehe, kiukweli Mjomba Kambona alinywea. Lakini Polisi  mmoja akasema 

“Ongozana na Mimi Kijana” akamshika mkono Salehe na kwenda naye nje. Lengo la Polisi ni  kutaka utambuzi kwa Majirani maana Upelelezi wao uliwaambia Salehe wa kwemye picha  anapatikana kwa Mzee Mwinyimkuu. Wakafika hadi nyumbani kwa Mama Ashura maana ndipo  palikua na Watu nje 

Walipomuona Yule Kijana akiwa na Polisi vijana walikimbia hadi yule Polisi akashangaa, hata  Mama Ashura naye alikua anataka kukimbia ila Polisi akamzuia Mama Ashura na Kumwambia  asikimbie ana maswali kadhaa anataka kumuuliza, ndipo Mama Ashura akabakia lakini kwa hofu  sana 

“Unamtambua nani pichani?” Yule Polisi akampa picha yule Mama, Mama Ashura akaipokea  picha japo kwa wasiwasi lakini alipoiangalia ile picha alishtuka sana, akameza funda la mate.  

“Hapana’’akajibu lakini kwa hofu sana kiasi kwamba yule polisi akahisi pengine kuna jambo  analificha. Kilichomshtua Mama Ashura ni kuniona Mimi kwenye ile picha ya ndoa ambayo  Mjomba Kambona aliwapatia polisi 

“Na huyu Kijana hapa?” akauliza Polisi, Mama Ashura akamtazama yule Kijana. Akaachia  tabasamu la hofu kisha akajibu 

“Ni Salehe, anaishi pale” akaonesha na kidole kabisa. Majibu haya yakamuacha yule polisi  kinywa wazi, basi akarudi hadi nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Hakuna ushahidi wa  anachosema Mjomba Kambona. Lakini Mjomba akawaaambia

“Nina namba ya huyu Mzee alikua anawasiliana na Mama yake Saida, hii namba nimepewa na  Mama Saida. Jina ni hilo la Mwinyimkuu” akasema Mjomba japo kwa sauti ya kupoa, ikabidi  Polisi waipige ile namba. 

Ikapokelewa na Mtu mwingine kabisa tena Mwanamke akimuuliza yule Polisi Nani wewe?  Yalikua kama maigizo ya Filamu lakini lilikua tukio la kweli, nyakati zote hizo Mzee  Mwinyimkuu alikua akitabasamu akiwa anamtazama Mjomba Kambona.  

“Mnaona anavyo nitazama, huyu anajua kila kitu” akasema Mjomba lakini hakuwa na ushahidi,  maneno yake yalikua ni sawa na kuupaka upepo rangi. Muda wote Mzee katili alikua  akitabasamu kwa mpango fulani ulio kichwani pake 

Polisi walikosa ushahidi, ikaonekana kuwa Mjomba Kambona aliyakosea maelezo yake. Kibaya  zaidi hata picha aliyowaonesha Polisi kuwa ndiye aliyeniowa ilikanwa kwa kuoneshwa Salehe  mwingine na kilichotia nguvu kukosekana ushahidi ni maneno ya Mama Ashura. Angefanyaje  Mjomba wangu zaidi ya kutoa kitambaa na kujifuta jasho ila moyoni aliamini Mzee  Mwinyimkuu alikua anajua wapi nilipo, pia hapakua na ushahidi mwingine sababu Mzee  Mwinyimkuu hakuhudhuria ndoa yangu  

Polisi wakamwambia Mjomba Kambona 

“Tutaendelea na Uchunguzi, kwasasa wewe liachie jeshi la Polisi. Tutakupa taarifa ya Uchunguzi  juu ya Saida pia huyo Kaka yake” haikua kauli yenye matumaini, ilimvunja moyo sana Mjomba  Kambona. Akamwambia Mzee Mwinyimkuu 

“Saida hawezi kutoweka kirahisi, lipo unalolijua. Siondoki Rukwa hadi nihakikishe nampata  Mpwa wangu” alisema hivyo kisha aliongozana na Polisi kuondoka, Salehe feki na Mzee  Mwinyimkuu wakatazamana kisha wakawa wanawatazama namna Polisi na Mjomba Kambona  walivyokuwa wanaondoka.  

Wala hawakufika mbali, kabla hata hawajapanda kwenye gari ya Polisi. Mjomba Kambona  alianguka na kufariki papo hapo akitokwa na Mapovu mdomoni. Licha ya jitihada za jeshi la  polisi kumkimbiza Hospitali lakini alikua tayari amefariki 

Taarifa ikarudi Dar-es-salaam kuwa Mtu waliyemtuma kuja kututafuta Mimi na Kaka Hamidu  alikua tayari ameshafariki. Yalikua ni majonzi juu ya Majonzi, taarifa hii ilipomfikia Baba yangu  alifariki pia kwa presha. Bundi aliizingira familia yangu, misiba miwili ndani ya siku moja,  Mzee Mwinyimkuu akashinda tena kwa kishindo kikubwa sana. 

** 

Nilihesabu siku ambazo nilikua ndani ya ile nyumba ya mateso, zilitimia siku saba ngumu.  Nilikonda nikawa kama Mtoto mdogo, niliishiwa nguvu. Kilichokuwa kimebakia kwangu ilikua  ni kufa tu. Kila nilipoamka nilijikuta nimeshaondolewa kidole kimoja, pumua yangu ikawa ya 

shida sana. Nikakosa uwezo wa kuwatambua Watu kirahisi, yule Bodaboda aliendelea kuniletea  chakula kila siku lakini pia sauti ya Mwanaume mmoja kugumia ilikua ni sauti ya Kila siku 

Lilikua ni jambo la kawaida sana yeye kupaza sauti, sikuwahi kufahamu alikua akipitia mateso  gani, ila dakika za mwisho niligundua kuwa naye alikua akipelekewa chakula na huyu huyu  Bodaboda anayeniletea Mimi chakula. 

Sikuweza kusimama tena, vidonda vilianza kutoa funza sababu sikuwa na dawa yoyote isitoshe  joto la mle ndani liliniathiri kwa kiasi kikubwa, Mwenzenu niliwahi kufika Jehannam nikiwa  Hai. 

Basi siku moja yule Bodaboda alikuja, siku yenyewe palikua na mvua kubwa. Aliingia akiwa  ameloa sana anatetemeka kwa Baridi, japo nilikua katika nyakati za mwisho kabisa za uhai  wangu lakini niliweza kugundua kuwa Baridi lilikua tatizo kubwa kwake. Alikua akiniandalia  chakula huku akitetemeka nikagundua anasumbuliwa na tatizo linalo sababishwa na Baridi. 

Akajikaza, akaniwekea chakula. Alipaswa kunilisha sababu Mimi nilikua siwezi tena hata  kushika kijiko, nilikonda mno hadi mishipa ya Damu ilikua ikionekana. Akajitahidi kuniinua ili  kunikalisha kitako niweze kuegemea ukuta anilishe vizuri, siku hii nilipanga kuacha kula ili nife  mapema maana mateso yalinizidi kabisa, Jamani naposema nilikonda basi ujue nilikonda nikawa  na kilo chache sana halafu kichwa kikawa kikubwa. 

Nilitamani kumuuliza ana shida gani, huyu Mtu hakuwahi kunitesa wala hakuwahi kunisemea  jambo baya isipokua alikua hajibu maswali yangu yote niliyokuwa namuuliza. 

Hali yake ilianza kuwa mbaya, akashindwa hata kunishikilia akaanguka chini na kuanza kugala  gala kwa maumivu Makali sana, mlango ulikuwa wazi hakuufunga sababu alipoingia alikua  tayari ana hiyo hali ya Maumivu, niliona ni nafasi ya kutoroka lakini sikuwa na akiba yoyote ya  nguvu iliyobakia 

Nikatamani kuendelea kuishi ghafla tu, namna pekee ya kuendelea kuwa hai ni kutoroka. Huko  nje mvua ilikua ikinyesha na kusababisha kelele kubwa sana kwenye Bati. Sikuwa na nguvu ya  kusimama, nikaona ni bora nijiburuze nione kama naweza kufika nje 

Yule Bodaboda alipoona naanza kujiburuza akajua nataka kumtoroka, akili yake ikatamani  anizuie lakini mwili ulimsaliti, nguvu zilimwisha akiwa sakafuni anapumua kwa shida sana.  Nikaendelea kujivuta taratibu huku nikiwa ninasali Mungu niliyemkatia tamaa azidi kunipa  nguvu, unajua kwanini niliamini naweza kuondoka pale? 

Kwasababu hapakua na mtu mwingine aliyekuwa anakuja isipokua yeye, hivyo hakuna tena wa  kunizuia, halafu niliwaza kufika chumba ambacho yule Mwanaume anagumia ili kama yeye ana  nguvu tusaidiane kutoroka. 

Nilijiburuza kama nyoka hadi nilipotoka nje ya chumba kile, palikua na funguo kwenye kitasa.  Nikapata akili ya dharura kuwa huwenda funguo ile inaweza nisaidia kufungua milango mingine 

maana ilikua na funguo tatu zilizowekwa sehemu moja, naipataje Funguo ni lazima nisimame  niichomoe 

Kivumbi kilianzia hapo, nilikonda Mimi kiasi kwamba upepo unaweza nipeperusha, Malaika  Mtoa roho alikua amenisimamia akiniuliza nasimama au achukue roho yangu, sijui nguvu  zilitoka wapi nikasimama kwa kuyumba huku nikitetemeka. Nikachomoa funguo, ile nataka  kupiga hatua nikaanguka 

Basi nikagugumia kwa maumivu, nilihitaji kufanya haraka maana kama yule Bodaboda atapata  nguvu basi sitaweza tena kuondoka, nikamkumbuka Mama na Baba yangu, nikamkumbuka Kaka  Hamidu. Ghafla nguvu zikaamka 

Nikajikaza na kuanza kujiburuza sakafuni kama nyoka vile, kwa mwendo huo huo nilijikuta  nikikiacha chumba kwa mbali kidogo, sikuufunga ule mlango wa chumba nilichomuacha  Bodaboda.  

Basi nilipofika kama chumba cha tano hivi nikasikia Mtu akiugonga mlango kwa nguvu huku  akisema 

“Njoo unitoe humu Mshenzi wewe, mtauwa wangapi. Siku ikifika mtakufa kama Kuku” alisema  kwa hisia sana lakini hakujuwa kuwa Mimi nilikua tayari nipo mlangoni. Mlango ulikua  umefungwa, korido lilikuwa refu halafu vyumba vilikua mbali mbali. Nilijitahidi sana kusimama  nifungue mlango lakini nilikua nakosa nguvu, nilijaribu kama mara tatu lakini niliishia kuanguka 

Wakati nikiwa nimeanguka nikageuka nyuma, ndipo nilipomuona yule Bodaboda akijikongoja  kwa maumivu kuja nilipo, alikua amelishikilia tumbo lake. Hapo sasa yule Malaika mtoa roho  nikamuona kama anachukua koleo kwa ajili ya kuichukua roho yangu. 

Sauti ya yule Mwanaume ilizidi kusema, kibaya zaidi Mimi ndiye mwenye funguo halafu sauti  yangu ilikua haitoki. Nikasema kama sisimami basi siondoki. Yule Bodaboda akawa anazidi kuja  upande wangu kwa kasi akionekana kuanza kupiga hatua za nguvu. Nikamtaja Mungu nikasema 

“Mungu nipe nguvu niishinde hii vita” nikajivuta haraka nikasimama nikiwa ninayumba,  nikaanza kusaka tundu la kuweka funguo maana nguvu yenye ilikua sifuri, nikawa najitahidi  huku nikiwa natetemeka. Mara naingiza mara nakosea, huku yule Bodaboda akizidi kunisogelea,  hata nilipopaatia nilikua nimeingiza funguo isiyo yake. 

Akawa karibu zaidi kiasi kwamba akipiga hatua tatu anakuwa amenifikia na kunizuia kuufungua  mlango, nikapapasia kwa bahati nzuri nikapatia funguo nikavuta nguvu za mwisho nikatekenya  kitasa lakini tayari Bodaboda alikua ameshanivaa na kuniangusha chini, Bahati nzuri ule mlango  ulikua tayari umeshafunguka 

Akatoka mwanaume mmoja na kuanza kumkita mateke yule Bodaboda hadi akamtupilia mbali  huko akiwa hoi sana anatokwa na damu mdomoni, eneo la Korido lilikua linawaka taa isipokua 

vyumbani tu. Sikuamini macho yangu Mtu ambaye nilikuja kumuona na kumtambua japo  nilimuona mara moja tu  

Alikua ni yule Mwanaume niliyemuazimaga simu kule Buchani, Ndio! Ni Abuu, masikini naye  alikua mateka wa Mzee Mwinyimkuu baada ya kujulikana ananifuatilia Mimi, kwa muda mfupi  naye alikua amepungua sana japo alikua na nguvu. 

Hakuniuliza chochote zaidi ya kuninyanyua na kuweka mkono wangu kwapani kwake tukawa  tunaelekea nje, mvua bado ilikua inanyesha. Tulipokua tunakaribia kutoka kabisa tukamuona  Mtu anakuja Mbio, tena akikimbia kwenye mvua, ikatubidi tujifiche nyuma ya Mlango wa  kutokea 

Yule Mtu alipofika, breki ya kwanza ilikua vyumbani kisha akamrudia yule Bodaboda aliyekuwa  anagala gala. Akamuuliza kwa hasira 

“Umefanya nini Mpuuzi wewe?” aliuliza kwa sauti ambayo niliitambua, ilikua ni sauti ya Mzee  Mwinyimkuu. Nilishtuka na kupata nguvu, nilipokumbuka kuwa yeye ndiye mtesi wangu basi  mkojo ulinibana. Ghafla tu nikajiona ni Binadamu ninayehitaji kujitetea 

“Nenda, hatuwezi kuondoka wote. Kaiambie Dunia kuhusu huyu Mzee, kama nitarudi tutakutana  na kama nitafia hapa basi Roho yangu itakua salama” alisema Abuu, roho iliniuma. Sikua na  uwezo wa kuzungumza. Mdomo wangu wa juu na chini nilihisi kama vimeungana sababu nilikua  na vidonda mdomoni hivyo kukaa kimya ndiyo yalikua maisha yangu. 

Nikaitikia kwa kutumia kichwa kisha nikasimama kama Mzimu, Mungu akaamua kunikumbuka.  Akanipa nguvu na ujasiri, alichotaka Abuu ni kumzuia Mzee Mwinyimkuu. Wakati naanza safari  Mzee Mwinyimkuu akaja mbio nahisi alikua anaanza kutusaka, sijui alijuaje kuwa tunatoroka.  Huyu Mzee alikua Mchawi haswa, aliponikaribia tayari Abuu alimdaka Mzee Mwinyimkuu  wakaanza kupalangana, muda huo nami nikaanza kujivuta kuondoka pale taratibu hadi nikaingia  kwenye mvua. 

Ulikua mchana lakini anga lilikua na wingu la kutosha kiasi kwamba palikua na giza fulani  isitoshe palikua Porini. Nilipopigwa na mvua nikapata nguvu ya kuanza kuchanganya Miguu  yangu vizuri. Nikaanza kukimbia huku nikiyumba kama mlevi 

Sijui nilikimbia umbali gani lakini nilikimbia bila kuangalia nyuma, nilikimbia sana hadi  nilichoka kabisa nikaanguka na kupoteza fahamu zangu. 

Nilirudisha fahamu na kuanza kujitambua nikiwa naburuzwa kwa kasi sana, watu walikua kama  vile wamenizunguka. Walikua na mavazi ya kufanana, nilikua kwenye kitanda kiendacho kwa  kasi mno, nikawasikia wakisema 

“Apelekwe ICU Haraka sana, kazi ianze mara moja” niligundua nilikua Hospitalini, wale  wauguzi walionekana kunikatia tamaa sababu nilikua na hali mbaya sana. Lakini mimi 

mwenyewe nilijiona ni mzima wa Afya zote, mahali nilipokuwepo palikua ni hatari zaidi ya  Kuzimu.  

Chozi lilinibubujika nikafumba macho yangu huku nikimshukuru Mungu. Madaktari walifanya  kazi yao kwa wiki tatu kuhakikisha najitambua zaidi, wakaniweka kwenye uangalizi maalum  kwa kipindi chote hicho hadi nilipokumbuka yaliyonisibu. 

Nikawaandikia jina Langu, mahali nilipotoka maana nilikua siwezi kuzungumza tena, Hospitali  ikasambaza jina na taarifa zangu ndipo Mama yangu alipokuja Mbeya akiongozana na Ndugu  wengine kunitambua. Mama alilia sana, sikuwahi kumuona Mama yangu akilia namna ile, yale  Maisha yaliniathiri sana kisaikolojia. Nikapoteza uwezo wa kuzungumza kabisa. Taarifa ya Kifo  cha Baba ilinihuzunisha mno, ikanitoa chozi. 

Polisi walipokuja niliandika maelezo yangu, ilikua baada ya wiki sita. Mwezi mmoja na siku  kadhaa, afya yangu ilianza kukaa sawa lakini sikuwa na Uwezo wa kuzungumza chochote  isipokua kuandika. Polisi walinichukua ili nikawapeleke mahali nilipoteswa yaani nyumbani kwa  Mzee Mwinyimkuu  

Mimi na Mama tulienda, palikua ni pale pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Namba ya nyumba ilikua  ni ile ile, mazingira yale yale, chozi lilinibubujika sana hadi Mama akashindwa kujizuia.  

Nilikua natembezwa kwenye kiti cha Walemavu maana bado miguu ilikua haipo sawa pia sikua  na vidole nilikua najiuguza. Nikampa ishara Mama yangu kuwa anipeleke kwanza nyumba  jirani, pale kwa muuza chapati, nilimkuta Mwanamke mwingine kabisa akitengeneza chapati,  nikaandika kwenye karatasi 

“Mama Ashura yupo wapi?” nilikua na ujumbe wa Mtoto wake Ashura nilitaka kwanza nimpe  ujumbe, wakati huo polisi walikua wameizingira nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Mama  akamsomea yule Mwanamke, lakini cha ajabu eti akadai yeye ndiye Mama Ashura, nilishtuka  alafu kingine kilichonipa mshituko ni kumuona Ashura mwenyewe, alikua ni Ashura yule yule  niliyemuona Nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu 

Haya mambo yalinifanya nianze kuonekana akili yangu bado haiko sawa, nikajitahidi  kuwaambia kwa maandishi lakini niliishia kupewa pole tu, kisha nikapelekwa kwa Mzee  Mwinyimkuu. Nako nikakutana na stori mpya kabisa 

Kwanza ile nyumba si ya Mzee Mwinyimkuu, hawamfahamu. Wao wanaishi hapo Kwa Miaka  mingi, nilitokwa na Mchozi, nyumba ile ile mazingira yale yale lakini stori tofauti. Nikaomba  niingizwe ndani, nikapelekwa kwenye chumba nilichokuwa nalala 

Nikakuta magunia ya vyakula, tena kilikua chumba chenye makorokoro mengi sana na  hakikuonekana kua chumba cha kulala Mtu. Mama akaniambia 

“Saida, najua umeteseka sana huku lakini hukumbuki chochote tena. Siku ukikumbuka nakuahidi  tutarudi, yule Kijana na Baba yake watalipa” Kauli ya Mama yangu ilinimaliza akili yangu, 

nilifikia hatua nikakubali kuwa akili yangu haipo sawa, inawezekanaje kila kitu kibadilike kwa  haraka vile. Hakuna aliyeniamini 

Lakini sasa wakati natoka nikajikuta nikipeleka macho yangu jikoni, nikaiona ile sufuria kubwa  ambayo kwa mara ya kwanza nilipika mchicha mwingi, nikashtuka alafu nikauona Mchicha  mwingi ukiwa kwenye Beseni. Kilichonishtua ni kwamba nilimuona Msichana wa umri wangu  akiutengeneza. 

Nilijikuta nikipiga yowe kali sana. Hali ya afya yangu ikawa sio nzuri nikarudishwa tena  Hospitali. Tokea siku ile nilikua Msichana ninayekaa kimya hadi leo hii nawasimulia hiki kisa,  sikumpata Mzee MwinyiMkuu wala Salehe, lakini sitakubali. Siku moja nitarudi Rukwa ili  walipe kwa maumivu na mateso makali ninayoyapitia hadi sasa. 

Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa ya  Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa,  sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze. 

Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka cha  Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapata  ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changu  nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini. 

AHSANTE……….MWISHO

Comments zikiwa nyingi TUNAANZA MPYA Chaap

USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kutuma Message WhatsApp Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

22 Comments

    • Hatar sana,, mungu amekpgania pakubwa,, mm kama kijana ambae sjaoa hakka nmepata kitu kwa riwaya hii,, mungu akupe maisha mazur

  1. Hii ya leo machozi yamenibubujika sijui nisemeje lakin naamin Allah anajua zaid yaliyopo mioyon mwetu wanadamu

  2. Maskini Saida jamani 😥
    Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mazingatio makubwa jamani
    Uchawi upo
    Ila uchawi wa MwinyiMkuu ni zaidi ya Uchawi
    Mungu atunusuru maisha yetu na Wachawi
    Mungu AWAANGAMIZE WASHIRIKINA WOTE MOTONI.
    Ameen.

  3. 🥹nianze kwa kuhiluzunika ,ila mtu kuna sehem nmecheka dadeq, KWAMBA NYIE WASHENZ NIFUNGUENI MTAKUF KAMA KUKU , YAN MUUNI YUPO KWENY MATATZO ILA BADO AJAL, KWEL MAN IS STRONG NATURAL

Leave A Reply


Exit mobile version