IlipoishiaJua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.  Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vile  vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yangu  niteseke. 

Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuona  Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikua  nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawa  anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguo  akampa Mzee Mwinyimkuu. Endelea

SEHEMU YA SABA

Walionekana kupiga stori za hapa na pale kana kwamba walijuana muda mrefu, nilijua hii ilikua  ni tabia yake Kaka Hamidu kupenda kuongea sana na Watu tofauti tofauti pasipo kujua kua  aliyekua anaongea naye alikua katili sana na laiti angelijua hata asingelikanyaga mguu wake  ndani ya hii nyumba. Taratibu nilirudi ndani nikaingia chumbani, nikafunga mlango huku chozi  likinibubujika  

Hapakuchukua muda mrefu mlango uligongwa, halafu uligongwa taratibu sana na hapo hapo  sauti ya Mzee Mwinyimkuu ikasikika ikiniita 

“Mkwe” yaani nilizidi kukereka lakini kwa kuhofia uhai wa Kaka Hamidu ikanilazimu kuitikia  japo kwa shingo upande 

“Abee Baba” nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango, ghafla akanisukumiza hadi ndani kisha  akaufunga mlango na kunishika shingoni 

“Nilikuonya lakini unaonekana hutaki kusikia si ndiyo, sasa kwa taarifa yako hakuna  utakachofanya nisikijue. Ulichojaribu kukifanya leo sokoni kinaweza kukugharimu, subiri Kaka  yako aondoke nitakuonesha rangi yangu halisi na yule Mtu wako anakufuatilia sasa naye  arobaini yake imefika” alisema kisha akanitupa pembeni, kwakuwa nilikua mwembamba ikawa  rahisi sana kwake kunisukuma, nikawa nakohoa ila nikawa nimejua kua nilichokusudia kwa yule  Mwanaume kule Buchani kilifanya kazi ila sasa nikawa naogopa sababu ni lazima atadhurika tu. 

“Jiandae uje uonane na Kaka yako, kumbuka nilichokwambia ukifanye la sivyo naye ataishia  humu” alisema kwa sauti yenye mikwaruzo huku akimalizia na ishara ya kuweka mkono 

shingoni kuwa atamuuwa. Lugha ya chozi ndiyo Lugha pekee ambayo nilikua naizungumza kila  wakati, umri wangu na yote ninayoyapitia vilinizidi kabisa 

Ili kumlinda Kaka Hamidu nililazimika kuigiza kuwa kila kitu kipo sawa, nilifunga vizuri  kitambaa mguu ambao ulikatwa kidole kisha nikavalia na soksi, Nikanawa usoni ili kujipa  utulivu wa sura yangu iliyochoka mateso na manyanyaso ya Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama  mbele ya kioo huku kwa mbali nikisikia namna ambavyo Mzee Mwinyimkuu na Kaka Hamidu  walivyokuwa wakichekeshana 

Nilipohakikisha nimejiweka vizuri, nilitoka chumbani nikaenda sebleni ambapo Kaka Hamidu  alikuwepo, niliizima hisia ya majonzi nikaingia sebleni, Kaka Hamidu alifurahi sana sababu  hakuwahi kuhudhuria harusi yangu na pia ilipita kitambo pasipo kuonana, nilimkaribisha kwa  furaha ya kuigiza na kumtaka ajisikie yupo nyumbani kisha nilimuacha na kwenda kumuandalia  chakula. 

Niliporudi nilimpa chakula akaanza kula huku akinisifia kuwa mapishi yangu hayajabadilika,  yeye alionekana kuwa na amani na furaha ya kweli sababu hakuna alichokuwa anakifahamu hadi  muda huo, isipokua mimi niliyejiona nilikua ndani ya shimo refu lililoenea giza zito nisione pa  kutokea, tabasamu lilitanda kote usoni pangu ili tu kumlinda Kaka Hamidu, na jinsi muda  ulivyokuwa umeenda niliogopa sana kama atalala ndani ya nyumba hii ya Kutisha, nilitamani  aondoke baada ya kumaliza kula tu. 

Mzee Mwinyimkuu alikua ameketi anasikiliza maongezi yetu, akawa ananikumbusha stori za  zamani na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa nilipokua mdogo nilikua na tabia ya kulialia,  kwake alichukulia kama ni sehemu ya mazungumzo mazuri lakini kwangu niliona anapoteza  muda badala ya kula akamaliza mapema aondoke, baadaye akaniuliza kama naweza kupokea  simu kutoka kwake 

Huwezi amini alininunulia simu ndogo ili nisikae bila simu kwa wakati ambao nilimwambia  Mama kuwa namsubiria Mume wangu Salehe akirudi aninunulie simu mpya. Niliitaka sana ile  simu lakini jicho alilonikata Mzee Mwinyimkuu nikajikuta nikimwambia 

“Asante Kaka, muda siyo mrefu Salehe atarudi atanunua simu ni wajibu wake. Hiyo kampe Wifi  yangu” nilisema kanakwamba nilikua kwenye utani lakini moyoni nilitamani angenipa kisiri ile  simu ila sasa alikua hajui kuwa napitia mateso makali sana na vitisho vya kila aina. Mzee  Mwinyimkuu akajikoholesha, jasiri haachi asili yake nikashtuka lakini nikajishtukia na kurudi  kwenye hali ya kawaida 

“Saida, Muandalie mgeni sehemu ya kulala. Apumzike akimaliza kula maana anaonekana  amechoka” alisema Mzee Mwinyimkuu, nilishtuka sana sikutaka Kaka Hamidu asikie vitimbi  vya Usiku vya hii nyumba, nikaitikia kwa wasiwasi sana 

“Njoo Mama” akasema Mzee Mwinyimkuu, mbele ya Mtu mwingine hujionesha ni Mtu mzuri  lakini tukiwa wawili ananitendea unyama na ukatili wa kutisha sana. Nilitabasamu nikiwa 

namtazama Kaka Hamidu ambaye naye alikua akitabasamu huku akinitazama, ndani ya moyo  wake aliiamini hii picha ya nje kuwa nina amani na furaha lakini niliamini kama atalala hapa  basi ataiona picha ya ndani ya Maisha yangu kitu ambacho kitahatarisha Maisha yake. 

Niliongozana na Mzee Mwinyimkuu hadi kwenye korido, akairudisha ile sura yake ya Mbuzi  ambayo niliizoea japo inatisha, kwa sauti ya chini nzito akaniambia 

“Chumba cha mwisho kushoto, muandalie mazingira ya kulala.” Alisema, sijui kwanini alisistiza Kaka Hamidu alale wakati alikuja bila begi lolote lile akionekana amekuja Mara moja tu, licha  ya yote sikutaka alale pale ila sikujua nawezaje kumshawishi aondoke. 

“Sawa” hakunipa onyo lolote lile baada ya kuitikia aliondoka na kurejea sebleni, nilienda moja  kwa moja kwenye chumba nilichoelekezwa ambacho Kaka Hamidu atalala. Sikuwahi  kukifungua kile chumba wala kukisogelea, ilikua ndiyo mara ya kwanza nakifungua 

Nilipoingia ndani nilianza kuona vitu vilivyoniacha mdomo wazi, huyu Mzee alitaka makusudi  nione pia. Palijengwa kitu kama kaburi katikati ya kile chumba, halafu palikua na mifupa mingi  sana ya Binadamu, mafuvu ukutani, halafu nikasikia sauti ya kutisha ikisema 

“Hiki ni Chumba cha Hamidu” sauti hiyo ilinipa kiwewe nikajikuta nikipiga yowe nikakimbia  kuelekea sebleni, Kaka Hamidu akawa Mtu wa kwanza kunidaka na kuniuliza kuna nini. Hapo  akili ikanikaa sawa kuwa sikupaswa kupiga kelele namna ile, nikajitahidi kujikaza lakini tayari  

nilikua nimezua taharuki halafu cha ajabu Mzee Mwinyimkuu alikua akitabasamu tu kitu  ambacho kilizidi kunipa maswali yasiyo na majibu. 

“Eti Babu huyu ana nini?” akauliza Kaka Hamidu akiwa amenishika bega huku macho yake  akiyapeleka kwa Mwinyimkuu aliyeketi bila hata kujitingisha 

“Saida Bwana, sasa nini kinakufanya unamshtua Kaka yako, hadi leo hujaizoea hii nyumba tu?”  Aliniuliza Mzee Mwinyimkuu lakini swali lake lilijaa dhihaka sana kitu ambacho sikukipenda  kabisa wakati alijuwa alichokua amekifanya. Bumbuwazi niliyonayo ilinifanya nishindwe kujibu  swali lolote lile 

“Hamidu hebu twende ukaone kilichomshitua huyu” akasema Mzee Mwinyimkuu, Moyo  ulifanya kama unataka kusimama hivi kwa namna nilivyoshituka, nikajiuliza kama Kaka Hamidu  ataenda kule atakiona kile chumba cha kutisha chenye kaburi ndani na hapo kizaa zaa kitaanza  kwake, nikajitahidi nimzuie nikamwita 

“Kaka Hamidu…” alikua tayari ameongozana na Mzee Mwinyimkuu, walikuwa wameshafika  kwenye korido wakiwa wamebakisha hatua chache sana kukifikia kile chumba cha kutisha,  macho yalinitoka nikiwaangalia walivyokuwa wakienda kisha walisimama mlangoni  wakatazamana kwa mshangao 

Halafu Kaka Hamidu akaangua kicheko huku akigeuka na kunitazama nikiwa nimesimama  mlango wa kuingilia sebleni, alicheka kama Mtu aliyepandwa na wendawazimu, hapo hapo 

nikaisikia simu yake ikiita maana aliiacha kwenye kochi, nikatamani kurudi niipokee ili nitoe  taarifa kusudi akipotea kila Mtu ajue pa kuanzia lakini sikupata hata hiyo nguvu mara akaniita 

“Saida hebu njoo” aliniita Kaka Hamidu, alikua tayari ameacha kucheka. Akaniita tena kwa  kunisitiza kuwa niende, nikajikuta bila kujiuliza mara mbili naanza kupiga hatua kama Mgonjwa,  kumbuka hapo nna maumivu ya Uchi wangu pia kidole kilichokatwa halafu nilishakata tamaa  

Nilisogea taratibu huku nahesabu hatua zangu kama mwendawazimu, nilijua naenda kuona nini  sababu nilichokiona mwanzo ni kile kile. Nilipofika nilishangaa sana, Jamani eti kile chumba  chenye kaburi na mafuvu na mifupa ya Binadamu kilikua hakina chochote zaidi ya kitanda kizuri  kilochotandikwa shuka safi sana na zaidi kilikua kinanukia ila chini palikua na paka aliyetulia  zake. 

Kaka Hamidu akanishika bega akaniuliza 

“Ni lini utaacha kuogopa paka Mdogo wangu? Wewe ni Mtu mzima sasa pia ni Mke na huwenda  ukawa Mama baadaye, unaogopa Paka kweli?” aliniuliza, haikuwa siri ni kweli nilikua naogopa  paka lakini nilichokiona mwanzo wala hakuwa paka, sasa nikajiuliza ni mawazo yangu tu au  nilichokuwa nimekiona kilikua halisi na hiki tunachokiona ni kiini macho tu. 

Nilihema mfululizo kama vile moyo ulishusha pumzi na kuamua kurejea kwenye mapigo ya  kawaida, basi nilikaa kimya sikusema chochote kile. 

“Utalala hapa, si ulisema kesho asubuhi unarudi Mbeya?” aliuliza Mzee Mwinyimkuu 

“Eeeh asubuhi narudi ili nijiandae halafu kesho kutwa niende Dar” alijibu Kaka Hamidu,  akanishika mkono tukarudi sebleni nikiwa kimya. Nilimhurumia sana Kaka Hamidu maana  nilianza kuwa na wasiwasi kuwa Mzee Mwinyimkuu kuna mpango fulani ameupanga dhidi  yake. Muda huo huo Mzee Mwinyimkuu akapokea simu halafu akatuacha pale akaelekea nje  kuzungumza ikionekana kama kuna Mtu aliyemtarajia alikua amefika nje. 

Nilipanga kumshawishi Kaka Hamidu asilale ndani ya ile nyumba lakini sikujua naanzia wapi  Mimi. Nikiwa natafakari Kaka Hamidu akaniuliza 

“Huonekani kuwa sawa Saida, kuna tatizo gani hapa?” aliuliza kama Mtu aliyeanza kuonesha  wasiwasi wa ghafla japo muda wote huo alikua akionesha kutokuwa na wasiwasi kabisa.  Kwakuwa alionesha kuwa na wasiwasi nikaona ni bora nimueleze ili aokoe uhai wake sababu  uhai wa Wazazi wangu ulikua mikononi mwangu. 

Nilisogea na kupiga magoti mbele yake nikashika na miguu yake huku chozi likinibubujika. 

“Kaka Hamidu, usilale ndani ya hii nyumba na kama utafanya hivyo basi kifo chako kitakuwa  karibu zaidi na wewe” nilimwambia chozi likizidi kunibubujika, hata sauti iliyonitoka  iliambatana na kilio kisicho na sauti Kubwa 

“Unamaanisha nini?” 

Nikavua soksi na kmwonesha Kaka Hamidu nilivyokatwa kidole ili ayaamini kwa haraka  maneno nitakayo mwambia, alishtuka sana. 

“Huyu Mzee siyo Mtu mzuri Kaka yangu, okoa Maisha yako bado una muda wa kufanya hivyo.  Hii nyumba imejaa uchawi na mateso makali, hata kile chumba unachoambiwa ulale ni chumba  chenye kaburi ndiyo maana nilishtuka. Ondoka bado una muda” Nilimueleza Kaka Hamidu,  haikuhitaji elimu ya chuo kikuu kujua kua Kaka Hamidu alikua ameshanielewa. 

Akajawa na taharuki na hasira sababu alikua ananipenda sana na isitoshe hakuna ndugu  anayeweza kumuacha ndugu yake kwenye shida kiasi kile.  

“Saida siwezi kukuacha hapa, nitamfundisha adabu huyu Mshenzi” akasema Kaka Hamidu,  kimwili Kaka Hamidu alikua amejazia jazia hivyo kama utamuweka mizani moja na Mzee  Mwinyimkuu basi yeye ndiye atazidi. Akanishika mkono kwa nguvu akasema 

“Tunaondoka wote”  

“Kaka nenda wewe tu, mimi niache hapa ili Wazazi wangu wawe salama” nilisema, sasa Kaka  Hamidu akaanza kupaza sauti kitu ambacho sikukitaka kabisa. Nilichotaka ni siasa zaidi ili Kaka  Hamidu aondoke pasipo Mzee Mwinyimkuu kujuwa chochote kile. 

Mara tukasikia mlango ukifungwa tena siyo kufungwa kawaida ni kule kufungwa kwa kufuri  kabisa halafu ni Mlango wa kuingilia nyumba kubwa, Kaka Hamidu akanipa ishara ya kukaa  kimya. Alidhamilia kuomdoka na Mimi, nami niliona ni bora niondoke naye kuliko kubaki tena  kwa Mzee Mwinyimkuu  

Akaingia Mzee Mwinyimkuu pale sebleni, alikua amevalia suruali, singlendi na Balaghashia  kama kawaida yake, hakututazama kabisa akalisogelea kabati na kuiweka funguo kwenye droo  kwa mbwembwe sana huku akiwa anapiga zake mluzi. 

Ilikuwa ndiyo nafasi pekee ambayo Kaka Hamidu alikua ameipata, akachukua jagi la kioo lenye  maji kisha akasogea taratibu hadi nyuma kwa Mzee Mwinyimkuu, akampiga na lile jagi kisogoni  kwa nguvu hadi Mzee Mwinyimkuu akagugumia kwa maumivu na damu zikaanza kutoka  alipopigwa akaanguka chini huku akionekana kutaka kusema jambo lakini alikua akishindwa.  

Kaka Hamidu alikua akimuangalia Mzee Mwinyimkuu alivyokua anatapa tapa, kwa sekunde  kadha tu zilitosha kumnyamazisha akawa ametulia tuli pale chini kama maji ya Mtungi, ikawa ni  nafasi ya dhahabu sana kuondoka ndani ya ile nyumba.  

“Twende” akasema kaka Hamidu akiwa amenishikilia mkono kwa nguvu tukawa tunaelekea  mlangoni ili tuondoke. Tulipofika Mlangoni tukapata akili ya ile funguo, ndiyo! Palikua na  kufuri mlangoni, funguo aliiweka kwenye droo kule sebleni,. 

Hapakuwa na ujanja isipokua Kaka Hamidu kurudi sebleni kuchukua funguo, alipofika Sebleni  hakumuona tena Mzee Mwinyimkuu pale sakafuni wala sebleni kote, ni kama aliyayuka mithiri 

ya Barafu juani. Akaniita, nikakimbilia sebleni nami nikawa shuhuda wa kutoweka kwa Mzee  Mwinyimkuu, tulitazama kwa mshangao mkubwa. 

Tusingeweza kurudi nyuma tena, Kaka Hamidu akafungua droo na kuikuta funguo, akaichukua  kisha akaniambia tuondoke. Cha kushangaza ambacho kilitufanya tugande kama Barafu ni  kuukuta ule mlango tuliohangaika kuchukua funguo ukiwa wazi kabisa, halafu nje tukisikia sauti  ya Mtu kama akichakata kuni hivi.  

Sote tukawa na hofu sana, Nani ameufungua ule mlango bila kusikila sauti yoyote? Hakuna  aliyekua na jibu la moja kwa moja, Kaka Hamidu akaona ni bora apige simu ili aombe msaada,  alishaona siyo rahisi kuondoka ndani ya ile nyumba ya kutisha, halafu ilikua mishale ya usiku  mchanga kama saa 3 hivi lakini matukio yaliyotokea na ukimya uliokuwa umetanda na giza  ilionesha kama vile ni Usiku mnene. 

Akajipapasa na kukumbuka simu aliiacha Kwenye kochi, kabla hata hajapiga hatua kurudi  sebleni, pale pale taa zote zikazima. Pakawa giza tupu hata nuru moja isionekane, pakawa kimya  kabisa, sikumsikia tena Kaka Hamidu isipokua sauti ya kugugumia ambayo aliitoa kwa nguvu,  papo hapo nikasikia kitu kikianguka kama Mzigo ‘Puuh’ 

“Aaaaah‼” niligumia kwa hofu lakini ghafla nikabanwa mdomo wangu halafu sauti ya Mzee  Mwinyimkuu ikagonga ngoma za Masikio yangu, nilishtuka sana.  

“Shiiiii‼!” akanitaka nikae kimya. Nilikuwa nahema juu juu, mara papo hapo taa zikawaka.  Nilichokiona jamani sitakuja kusahau Maisha yangu yote, nilihisi uchizi, nilihisi wendawazimu.  Mwili ulipoa kama nimemwagiwa maji ya Baridi. Kaka Hamidu alikua sakafuni, damu nzito  ilikua imetapakaa kila mahali.  

Alitenganishwa kichwa na kiwiliwili chake, damu zilikua zinaruka kwenye shingo yake. Hata  Mzee Mwinyimkuu aliponiachilia sikua na nguvu nilianguka chini nikakalia damu. 

“Nilikuonya hukusikia” akasema Mzee Mwinyimkuu, alisema. Mkononi alikua ameshikilia kisu  kikubwa chenye damu. Niliishia kudondosha chozi tu, mara akaingia Mwanaume mmoja na  kuanza kuuvuta mwili wa Kaka Hamidu kuelekea nje, Mze Mwinyimkuu akakichukua kichwa  cha Kaka Hamidu na kukipeleka kwenye kile chumba alichokua amekiandaa kwa ajili ya kulala  Kaka Hamidu. 

Sijui kilichoendelea baada ya hapo nilijikuta nikizidi kuishiwa nguvu, giza zito likatanda nikahisi  usingizi wa ajabu. Nikapoteza uwezo wa kujitambua. 

** 

“Saida,Mdogo wangu amka Unisaidie” ilikua ni sauti ya Kaka Hamidu, alikua amesimama  mbele yangu nikiwa nimekaa kitandani, alikua akivuja damu kila sehemu. Alikua ametisha kiasi  kwamba niligugumia hadi nikapaza sauti yangu kwa hofu. Hivyo ndivyo nilivyoamka kutoka  Usingizi wa kifo 

Nilikua na maumivu makali sana mguuni, ndoto hii mbaya iliniamsha. Eneo lile lile nililokatwa  kidole lilikua na maumivu makali sana. Niliusogeza vizuri Mguu wangu na kuangalia kidonda  kinaendeleaje, nilipoangalia niliona vidole viwili vikiwa vimeondolewa. Yaani jumla ya vidole  vitatu vinavyofuatana kuanzia cha mwisho vilikuwa havipo. 

Maumivu yalikua makali, ni bora uyasome kwenye hii hadithi lakini yasikukute, mwili wote  ulipandisha homa ya ghafla, kichwa kilikua kinauma sana. Safari hii sikuwa na uhakika kama  ninaweza hata kutembea, eneo lenyewe nililopatia ufahamu sikulijua kabisa. 

Nilikua sakafuni, chumba kilikua kitupu isipokuwa mimi tu na maumivu yangu. Nilipiga sakafu  kwa uchovu nikasema 

“Kama uliniumba niteseke hadi nife basi nitakufa na kama huu ni mpango wa shetani basi  hawezi kukuzidi maarifa” nilipomaliza kusema hivi nilijikunyata, Nililia sana. Nilikua tayari  nimempoteza Kaka Hamidu na sijui walimpeleka wapi 

Eneo lile lilikuwa kimya sana tofauti kabisa na nilivyozoea, sikusikia sauti za Pikipiki wala  mazungumzo yoyote yale. Niliona ni bora nilikague eneo lile, nilichungulia dirishani, nililiona  Pori la Kubwa, nilishtuka. Nikagundua nilikua nimehamishwa kutoka kwenye nyumba ya Mzee  Mwinyimkuu. Nililia sana maana safari hii siwezi kukutana na yeyote yule nikapata msaada,  Mzee Mwinyimkuu alishagundua kuwa kama ataniacha huru naweza kutoroka, ilifika hatua  nilikua mkali nikajisemea 

“Kama kuokoa uhai wangu kutafanya wazazi wangu wafe ni sawa, napaswa kukwepa haya  mateso Makali. Mungu atapigana kwa ajili ya Wazazi wangu” hayo ndiyo yalikua maamuzi  yangu. 

Niliveshwa kaniki pekee halafu nilikua na alama fulani kwenye paja langu, ilikua alama ya ajabu  iliyochorwa kwa moto, palikua na maneno ya ajabu. Huu ndiyo wakati mgumu zaidi kuwahi  kuupitia katika Maisha yangu yote, haukuwa wakati rahisi kwangu, ulikuwa wakati ambao  nilipoteza tumaini la Maisha yangu lakini sikuweza kufanya chochote isipokua kuugulia  maumivu na kulia. 

Kilipita kitambo kirefu cha Ukimya, sijui ilikua ni saa ngapi, siku gani au lile eneo ni wapi.  Nilichojua ni kuwa bado naendelea kupumua, niliusikia Mlio wa pikipiki. Nikajivuta na  kuchungulia dirishani, niliiona pikipiki ikiwa imesimama kando kidogo kama mita chache tu hivi  kisha Mtu mmoja alisogea mbele kuelekea nyumba niliyopo 

Kumbuka hapo ni Porini, tokea nimezinduka sikuwahi kumuona yeyote yule isipokua sauti za  ndege zilizopita kwenye ngoma za masikio yangu yaliyochoka kusikia sauti za kutisha. Nilikua  nimekonda ghafla sana Mimi Saida 

Basi, yule Mtu sikuiona sura yake kwa haraka sababu hata nguvu ya kusimama kwa muda mrefu  ilianza kuniisha nikajikuta nikianguka chini, maumivu yalikua makubwa halafu nilikua na njaa 

sana. Nilisikia tu akifungua mlango ulioonekana kuwa na komeo nyingi, akaingia hadi chumba  nilichopo 

Yule Mtu nilimkumbuka kwa haraka sana, alikua ni yule Bodaboda aliyenipeleka sokoni siku ile  ambayo nilikutana na Abuu. Nilikua na wenge zito lakini sikuacha kumtazama kwa makini hadi  nikamtambua. Alikuwa amebeba chakula kwenye Hot-pot 

Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana. 

“Kunywa Maji” alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikua  ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuuliza 

“Mnanimalizia lini nikapumzike?” Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chache  nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambia 

“Kifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwaje” alisema kisha akanipa maji, sikuwa  na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai 

Comments zikiwa nyingi naachia ya NANE leoleo hapa

Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA NANE YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx 

15 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version