IlipoishiaKama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Milele  Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, siku  nikimaliza nitakuacha urudi kwenu” Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwa  haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi. 

“Unasema nini?” niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini. 

Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikua  mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwamba  sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu. Endelea 

SEHEMU YA SITA

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nikiwa kitandani, kichwa kilikua kizito sana. Macho yangu  yalikua hayafunguki kirahisi kutokana na Uzito wa Kichwa changu baada ya kupoteza fahamu  zangu wakati ule 

Kwanza nilihakikisha pumzi zangu zinarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kukumbuka  kilichokuwa kimetokea, chumbani hapakuwa na yeyote yule isipokua Mimi na maumivu yangu  ya Kichwa. Nilizivuta nguvu zangu hadi nikakaa kitako pale kitandani, nikawa nayasikia sasa  yale maumivu ya kuchanwa huku chini na wale Misukule 

Chozi likanitoka kutokana na ule unyama wa yule Mzee Mwinyimkuu, nikahitaji kuelekea  Bafuni kujikagua namna nilivyoumia maana misukule walinifanya kwa fujo tena kwa Mpigo  wote Watatu. Niliishusha miguu vizuri hadi Sakafuni, hapo nikahisi maumivu mengine makali  mguu wa Kushoto 

“Agggh‼” niligugumia, nikapeleka macho yangu Mguu niliouhisi una maumivu, Mungu wangu  yule Mzee alinifanyia kitu kibaya sana. Alinikata kidole kimoja. Aisee‼ nililia kwa uchungu  sana, sikuwa na kidole cha mwisho halafu damu ilikua imetapakaa mguuni, Hii siku nililia  kuliko siku zote. Yaani nibakwe ma wale Misukule halafu nikatwe kidole kimoja hebu fikiria ni  maumivu kiasi gani 

Chozi lilinibubujika nikajikuta nikisema  

“Mama yangu nateseka Mwanao, nakufa huku Mimi” Haki sikua na cha kufanya maana tayari  Nilishatiwa kilema. Nikajivuta hivyo hivyo hadi nikafika Bafuni, sikujua nianze kujikagua mguu  wangu au niukague Uchi wangu ambao ulikua ukiwaka moto kutokana na jasho lilivyokua 

likipita. Nilivua kaniki nikaanza kuoga ili angalau nipate nguvu japo moyo ulijawa na ganzi  sana.  

Hiyo ilikua siku nyingine ya pili baada ya tukio la kubakwa na kukatwa kidole maana matukio  haya yote yalifanyika siku moja tena Usiku. Nilifungulia maji hadi mwisho maana palikua na  bomba la mvua, nikakaa sakafuni huku maji yakishuka mwilini kwa kasi sana. Nililia kuanzia  moyoni mwangu hadi mwili mzima. Likaja wazo la kutaka kuondoa uhai wangu maana mateso  niliyoyapata yalinikatisha tamaa ya kuendelea kuishi 

Wakati wazo hilo likiwa limekolea kichwani pangu nilihisi kumwona Mtu pale Bafuni,  nilishutuka nikajivuta pembeni mahali ambapo yale maji yalikua hayanipigi tena, macho  yalinitoka kama fundi saa aliyepoteza nati. Mapigo ya moyo yalinidunda mithiri ya moyo  unataka kutoka ndani, Mtu yule hakuonekana kuwa Binadamu wa kawaida, alikua na nywele  ndefu zinazo buruza hadi chini, alivalia gauni jeupe lenye damu. Kibaya zaidi alikua ni Mtoto wa  kukadiriwa kuwa na Miaka 6 hadi 8 hivi. 

Hakunionesha sura yake iliyofunikwa na nywele hizo ndefu nzito na zenye uchafu wa kutosha.  Alisogea hadi nilipo kisha akayafunga yale maji halafu akanisogelea zaidi na kisha nilimsikia  akisema 

“Kukata tamaa ni sawa na kuuza utu wako, usijione unapigana kwa ajili yako bali unapigana kwa  ajili ya wengi. Amka ukashinde vita ili kuwaweka huru walio wengi ndani ya nyumba hii”  alisema yule Mtoto kwa sauti ya Kukaza sana, alikua ni Mtoto wa kike, mkononi alishikilia  mdoli fulani wenye manyoya. 

Kiukweli sikua na ujasiri wowote wa kuongea chochote mbele ya yle Mtoto nisiyemfahamu,  halafu nilihisi huwenda ni mawazo yangu tu.  

“Nimesema amkaaaaa‼” yule Mtoto alipaza sauti kali ya kutisha, hadi nilijikuta nikipiga yowe  la kutosha kwa hofu, niliziba masikio yangu na kufumba macho yangu, sikutaka kuendelea  kuisikia sauti ya yule Mtoto wa ajabu, sijui alitokea wapi na kwanini aliyaongea yote yale.  Nilipofumbua macho yangu nilikutana na Mzee Mwinyimkuu akiwa amesimama mbele yangu,  kibaya zaidi nilikua uchi wa Mnyama, niliivuta ile kaniki na kuivaa 

“Kwanini unapiga kelele?” aliniuliza yule Mzee, nilimeza funda zito la mate nikiwa sakafuni  kule bafuni, huwa hapendi akikuuliza kitu halafu usimjibu kwa wakati.  

“Hapana Baba, labda..” nilijikuta nikibabaika nisijuwe namjibu nini 

“Nakuonya Binti, Maisha ya Wazazi wako yapo mikononi mwangu. Kama unataka waendelee  kuishi basi fuata niyatakayo, kila utapofanya mapenzi na misukule nitakukata kidole kimoja cha  Mguu, hadi nitakapo maliza kuondoa vidole vyote vya miguu nitakuacha huru lakini kwa aharti  la kukaa kimya” alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa tu ili aondoke lakini sikuafiki eti  anikate vidole vyote vya Miguu yangu.

Alipoondoka ndipo nami nikapata unafuu wa kupumua vizuri, nikarudi chumbani mara moja,  wazo la kujiuwa halikurudi tena kwa wakati huo, wazo likawa moja tu nitawezaje kuondoka bila  wazazi wangu kudhurika? Halafu kingine nilichowaza ni kuhusu yule Mtoto kule Bafuni,  aliyoyaongea yalikua maneno mazito ambayo nilihitaji kuyatafakari. 

Ndiyo, sikupaswa kukata tamaa, sikupaswa kulia kila siku maana machozi yangu ni sawa na  machozi ya Samaki baharini huenda na maji mara zote. 

Nilishinda na maumivu makali sana na nilipaswa kumpikia Mzee Mwinyimkuu na Misukule  yake, siku hiyo aliniambia nipike Ugali mwingi na Maharage. Ningefanya nini, nilifanya hivyo  nikiwa natembea kwa maumivu makali sana hata hamu ya kula iliniisha.  

Nikiwa jikoni mchana, nilisikia Mtu akibisha hodi. Sikujali sana sababu nilishaanza kukata  tamaa, fikiria naambiwa nikatwe vidole vyote ndio ataniacha huru, maana yake nitakuwa kilema.  Nikamsikia akitembea kuelekea nje kumwangalia mgongaji, sijui walizungumza nini. Halafu  nikamsikia akiniita 

Nilijikaza hadi nikafika Mlangoni, nikamkuta Akiwa na Mwanaume mmoja mnene mwenye  kitambi na ndevu zilizozagaa 

“Saida Binti yangu, sogea” alisema Mzee Mwinyimkuu, aliongea kwa bashasha na tabasamu juu  halafu akaniita Binti yake, hadi nilishangaa nikasogea 

“Huyu ni Mwenyekiti wa Mtaa. Msikilize” Alisema kisha yeye akasogea kwa nyuma ili mimi  ndiyo nifanye mazungumzo na Mwenyektii, sikujua anataka kusikia nini na kwanini niitwe  Mimi. 

“Majirani wanasema jana usiku na leo asubuhi zimesikika sauti za yowe kama vile kulikua na  tatizo. Nimemuuliza Baba yako anasema binti pekee uliye humu ni wewe, Je, Ulipiga yowe?”  aliniuliza Mwenyekiti, moyo ulinilipuka. Nikageuka kumtazama Mzee Mwinyimkuu,  akanionesha ishara ya kunionya kwa kutumia macho yake. Basi nikarudisha macho kwa  Mwenyekiti, nikameza mate nikamjibu 

“Sikupiga yowe na wala sijui chochote kile Kaka”  

“Au kuna Binti mwingine anaishi humu?” 

“Hapana, naishi Mimi na Baba. Mume wangu amesafiri” nilisema ili kuondoa ngoma juani japo  nilikua nautonesha moyo wangu kwa kiasi kikubwa sana. 

“Basi samahani sana, pia Samahani Mzee Mwinyimkuu huwenda Majirani walisikia tofauti”  alisema Mwenyekiti lakini wakati anaongea akajikuta akipeleka macho yake kwenye Mguu  wangu akaona sina kidole, halafu kibaya zaidi kidonda kibichi. Yule Mzee hakunifunga chochote  na wala hakukuwa na dawa yoyote ile hata Mimi ningetia ili pakauke 

“Kidole chako kimeenda wapi?” akauliza, nikashtuka

“kidole?” nikajikuta nikiuliza kwa mshituko nilioupata, laiti kama angelijuwa siyo kidole tu bali  hata huku chini nilichanwa na Misukule wa Mzee Mwinyimkuu sijui ingekuwaje. 

“Ndiyo ina maana hujui kama huna kidole, ona kinatoa maji maji” alisema huku akianza kutilia  shaka kuwa huwenda kelele walizo zisikia zilitokana na kukatwa kidole. 

“Mh…Aaaah..” kigugumizi kikanijaa maana sikujiandaa na swali hilo gumu. 

“Ana kisukari hivyo tulishauriwa akatwe kidole” alidakia Mzee Mwinyimkuu, yule Mwenyekiti  akashusha munkali wake, akaachia kicheko fulani na katabasamu 

“Aaaah! Samahani tena jamani, si unajuwa ni jukumu langu kuhakikisha Wananchi wangu  wanakuwa salama” alisema. 

“Hakuna shida Mwenyekiti, karibu sana. Saida si umpe Mwenyekiti hata chai?” aisee aliongea  Mzee Mwinyimkuu kama vile ni Mtu mwema na kwamba tunaishi vizuri sana Mimi na yeye 

“Hapana nina majukumu mengine, basi Mimi naenda” aliaga akaondoka zake, tukabakia  mlangoni Mimi na Mzee Mwinyimkuu, akanikata jicho fulani la ukatili hadi nikachechemea  kuelekea ndani mwenyewe. Akanifuata huko huko ndani kisha akanishika shingoni kwa nguvu  hadi nikawa nashindwa kupumua vizuri 

“Narudia Ole wako ujifanye una mdomo mrefu, hiyo hurka itakuponza” akasema halafu  akaniacha nakohoa kwa nguvu. 

“ Siku nyingine ukipiga kelele zako ndio utakuwa mwisho wako humu ndani. Halafu kuna Kaka  yako anaitwa Hamidu?” aliniuliza, nikaitikia kwa kutumia kichwa 

“Amepewa namba yangu na wazazi wako, amesema anapitia hapa kukuona anatokea Mbeya  kisha ndio aende Dar. Sasa hakikisha hajui chochote kile hadi anaondoka, nina uhakika  ametumwa kukuangalia unaishije sababu haupatikani kwenye simu wala Salehe hapatikani”  Nilishtuka, sikutaka ndugu yangu yeyote yule aingie ndani ya ile nyumba ya kishetani. 

Hamidu ni Kaka wa Mama Mdogo na Mkubwa hivyo ni Mtoto wa Dada yake Mama yangu.  Kiukweli sikutaka Kaka Hamidu aje kwa sababu kuu mbili 

Huyu Mzee siyo Mtu wa kumwamini, muda wowote anaweza akabadilika. Pili, kama itatokea  Kaka Hamidu akatilia mashaka kuhusu Maisha yangu itakuwaje, si familia yangu itakuwa  kwenye matatizo? Tumbo liliniwaka moto yaani kila nilivyofikiria nilihisi kuhara, hata maumivu  ya kubakwa na kukatwa kidole hayakuweza kuyafikia maumivu ya kufikiria kuhusu ujio wa  Kaka Hamidu. 

Haki, nguvu ziliniisha Mimi. Sikuwa na simu labda ningemueleza Kaka Hamidu asije ili kuokoa  uhai wake na wa wazazi Wangu. Jasho lilinivuja, moyo ulinienda kasi sana, kibaya zaidi Mzee  Mwinyimkuu alinitaka niigize kuwa naishi Maisha ya furaha sana ili kuwatoa hofu ndugu zangu. 

Nilifuta kwanza jasho langu kisha nilikubaliama na hali halisi kuwa ni lazima niwe muigizaji  mzuri zaidi ya Monalisa, nikarudi zangu chumbani nikiwa nachechemea kisha nikavalia baibui  langu na mtandio, nikakaa mbele ya kioo ili nijiweke sawa. Nikajilazimisha kutabasamu ilihali  moyoni ninalia, nilipohakikisha kuwa naweza kuigiza vizuri nilikaa kitandani nikiendelea  kutafakari mambo mengine yaliyonijia akilini mwangu. 

Mara baada ya muda mrefu kupita Mzee Mwinyimkuu alikuja chumbani, hakuwa na heshima  wala adabu na Mimi aliingia kama anaingia chooni nami wala sikushtuka sababu niliyoyapitia  yalianza kunipa ukomavu. Akanipa hela, halafu alikuwa akinipa hela mpya tupu 

“Ukitoka hapo nje kuna Pikipiki, atakupeleka sokoni kisha atakurudisha. Muandalie Kaka yako  chakula anachopendelea, nasistiza, makosa yoyote yale yatakugharimu” mara zote anapoongea  ananinyooshea kidole na kunikazia macho yake mekundu kama mvuta Bangi, nilipokea na  kuitikia kwa kichwa tu. Mdomo wangu ulijawa na uzito usio kawaida sababu nilizoea kukaa  kimya. 

“Tabasamu” alininasa kibao na kunitaka nitabasamu, basi nikaachia tabasamu la hovyo huku  chozi likinibubujika, Nyakati hizi niliona ni namna gani Mungu niliyehangaika kumuabudu  akiwa amenikalia kimya akiniangalia ninavyoteseka Mimi. Nilifuta chozi na kuchapa mwendo  nikiwa na kapu mkononi, moyo ulinijaa chuki. Niliyachukia Maisha yangu, nikajichukia mimi  mwenyewe na zaidi nilimchukia yule Mzee.  

Nilitembea kwa kuchechemea halafu kichwa kilikua kinaniuma sana, nilipofika nje nikaigiza  kutembea vizuri lakini maumivu niliyokuwa nayapata hayakuwa ya kawaida. Basi, nilimuona  Bodaboda akiwa amesimama na Pikipiki yake, nami nikaidandia bila hata kumsalimia kisha yule  Bodaboda akaongoza kuelekea mbele kama Mtu anayejuwa nilikua naenda wapi. 

Ilikua ni mara yangu ya kwanza naenda mbali na nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, sikuacha  kuhuzunika ndani yangu. Niliwatazama watu wakiwa wanafanya shughuli zao kwa uhuru kabisa  tofauti na Mimi mfungwa kwenye nyumba ya Misukule. Ilituchukua wastani wa nusu saa hivi  hadi kufika sokoni, palikua pamechangamka vya kutosha na palikua na kila aina ya Bidhaa. 

Kaka Hamidu alikua mpenzi wa ndizi za Rosti na samaki wabichi, hela ilitosha kabisa kununua  vyote. Nilihakikisha namuacha yule Bodaboda mbali ili nipate nafasi ya kuomba simu nimpigie  Mama yangu ili nipate namba za Kaka Hamidu kusudi nimzuie asije, mwanzo yule Bodaboda  alikua akinitupia jicho kama vile alipewa maagizo ya kunichunga lakini baadaye nilimpoteza  kwa makusudi kabisa. 

“Samahani kaka naomba nitumie simu yako, ni muhimu sana niwasiliane na Mama yangu”  nilisema haraka haraka mbele ya Muuza Samaki wabichi, akanitazama bila kunielewa nahisi  alijawa na maswali mengi yasiyo na majibu 

“Simu yangu?” aliniuliza kama Mtu asiyenielewa kabisa, chozi lilianza kunidondoka.

“Ndiyo kaka ni muhimu sana naomba niongee na Mama yangu japo dakika moja tu Mimi”  nilisema huku chozi likinibubujika. Bado yule Mkaka alikua amepigwa na Butwa halafu dakika  zilikua zinakatika.  

“Wewe umetokea wapi?” naye akaanza kunihoji badala ya kunisaidia, niliihitaji hii nafasi  kuokoa uhai wa Kaka Hamidu. 

“Kaka nisaidie kwanza mengine utayajuwa tu, samahani nipo chini ya Miguu yako” nikasema  tena, halafu pale Buchani palikua na Wateja wengine wawili ambao waliweka umakini kwangu  kusikiliza, mmoja akadakia 

“Bro, si umsaidie huoni Mtu hadi analia bado unamuuliza maswali?Hebu chukua ya kwangu”  akasema Kaka aliyekuwa akisubiria kuhudumiwa, yaani maongezi yalichukua dakika tano za  thamani ambazo zingenisaidia kumpata Mama kwanza kabla ya Kaka Hamidu. Akanipa simu  

yake nikaanza kujaza namba ya Mama yangu haraka na kwa pupa hadi nikawa nakosea kosea na  kurudia rudia huku mkono ukitetemeka sana hadi mwenye simu akaniambia 

“Nipe simu nikusaidie” basi nikampa na kuanza kumtajia Namba. Kabla hata sijamalizia namba  za mwisho nikaguswa begani, nikashtuka. Nikafuta chozi haraka, nilipogeuka nikakutana na yule  Bodaboda 

“Dada unafanya nini, muda unaenda?” alisema, sikuwa na la kufanya pale wala sikutaka  kuendelea kuwasiliana na Mama yangu, nikatoa pesa nikampa muuza samaki, kila mmoja  akajawa na bumbuwazi la kufa Mtu. Sababu ghafla tu Mtu aliyekuwa analia na kuomba msaada  nikawa na nguvu ya kusema 

“Kaka nipimie kilo moja nachelewa Mimi” nilisema kama Mtu mwenye haraka, cha ajabu  hakuna hata aliyeongea tena pale isipokua kunitazama kwa mshangao, nikapimiwa samaki kisha  nikageuka na kuongozana na yule Bodaboda, nikageuka kumtazama yule Kaka aliyekuwa na nia  ya kunisaidia simu nikamtazama kwa huzuni huku chozi likianza kunibubujika. Nilikua kama  nimemtumia Ujumbe kuwa nimeshikiliwa nahitaji msaada.  

“Nyie mmemuelewa yule Msichana?” aliuliza yule Kaka akiwa pale Buchani, kila mmoja  alionesha kutonielewa mimi. 

“Usikute anapitia magumu sana yule Msichana, siyo bure aombe simu halafu ghafla tu ajikaushe  baada ya yule Mtu kuja” akasema Muuza samaki. Yule Kaka akawaambia 

“Ngoja niwafuatilie” aliongea kisha haraka akatoka pale kutufuatilia Mimi na yule Bodaboda.  Binafsi niliamini asingeliweza kuelewa chochote lakini nahisi Malaika wake walimuonesha kitu  juu yangu. Wakati huo Mzee Mwinyimkuu alikua akieelekea kituo cha Daladala kumpokea Kaka  Hamidu ambaye alimwambia kuwa anakaribia kufika.  

Nilikuwa nimeshamaliza kununua mahitaji, nikapanda kwenye pikipiki bila kuzungumza na yule  Bodaboda maana nilijuwa wapo timu moja na Mzee Mwinyimkuu hivyo sikutaka hata kuongea 

chochote kile. Aliendesha kwa mwendo wa kasi sana kurudi nyumbani, sikuogopa mwendo wake  sababu nilijiona kama Mfu anayeishi. Nyuma yetu yule Kaka alikua akitufuatilia na Pikipiki,  Mimi wala sikujua hata yule Bodaboda hakujua kama kuna Mtu anatufuatilia hadi tunafika  nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu 

Yule Bodaboda alisimama na kunisindikiza kwa macho hadi naingia ndani, lakini nami sikusita  kumfuatilia maana nilipoangalia mlangoni sikuviona viatu vya Mzee Mwinyimkuu hivyo nikawa  na uhakika kuwa alikua ametoka, nikabana mlangoni na kumchungulia yule Bodaboda 

Wasiwasi wangu ulikuwa wa kweli, akapiga simu na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa  amenifikisha nyumbani halafu akasuburia kwa dakika kadhaa ndipo akaondoka, nilihema kwa  nguvu kisha nikaegemea ukuta kwanza ili kumiminisha chozi langu ambalo lilikua likibisha hodi  kila sekunde iendayo kwa Mungu, siyo tu kububujisha chozi bali nililia sana Mimi Saida. 

Nilipomaliza kulia nilielekea jikoni ili kuandaa chakula cha Kaka Hamidu, Mzee Mwinyimkuu  alikua mwenye kujiamini sana sababu aliyaweka dhamana Maisha yangu kwa ajili ya Wazazi  wangu. Nikaanza kupika kwa ajili ya Kaka Hamidu. 

*** 

Kumbe yule Kaka alikua amejificha mahali akiangalia kilichokua kinaendelea, alikua na uhakika  kabisa kuwa nilikuwa kwenye mateso mazito, baada tu ya yule Bodaboda kuondoka basi  akamfukuzia kwanza yule Bodaboda hadi Kijiweni. Akasimamisha pikipiki yake kando kisha  akavuka barabara hadi alipo yule Bodaboda. 

Akamwita pembeni na kuanza kuzungumza naye, kitu cha kwanza alichomuuliza 

“Samahani Bro, hunijui, wala sikujui lakini kuna jambo nataka kukuuliza. Kwanza  unanikumbuka?” akauliza, yule Mkaka alikuwa mweupe halafu alikua na rafudhi ya Kichaga.  Umri wake kwa makadilio ni kama miaka 33 hivi, kwangu ni mkubwa sana hata kwa Salehe pia.  

Yule Bodaboda akamtazama kwa umakini lakini hakumkumbuka kwa haraka “Sikufahamu bro, unashida gani na Mimi?”  

“Naitwa Abuu, nilikuona pale Bucha ya Samaki kule Mjini. Ulikua umemfuata Msichana mmoja  hivi ukaondoka naye” alipomuuliza hivi tu yule Bodaboda akaanza kutafuta majibu 

“Anhaa‼ inawezekana, sasa unataka nini?” 

“Yule Msichana aliniomba simu awasiliane na Mama yake, sasa hakufanikiwa ndiyo wewe ukaja  ila kwa namna nilivyomuona anaonekana yupo kwenye changamoto kubwa sana na anahitaji  msaada, unalifahamu hilo?” Si unajua Wachaga hawakwepeshi maneno yao, alimchapa moja  kwa moja na kumwacha Bodaboda akiwa anatafakari sana

“Kaka unajua yule ni Mke wa Mtu, mimi kazi yangu ni kumpeleka sokoni tu. Hayo mengine  mimi siyajui na wala sifuatilii kabisaa, sasa kama unataka kufuatilia ndoa za Watu haya, ila  nakutahadharisha sana. Hii ni Rukwa” alisema kwa kujiamini sana. 

Abuu alikosa cha kuongea zaidi akamshukuru tu yule Bodaboda lakini kichwani alikua na  maswali mengi sana, Basi yule Bodaboda alikua akitumika kweli na Mzee Mwinyimkuu hivyo  baada ya Abuu kuondoka akampigia simu Mzee Mwinyimkuu na kumueleza aliyoyasema Abuu  kuhusu safari ya Sokoni, Abuu akawa amejiweka matatizoni bila kujua alikua akifuatilia jambo  la hatari kiasi gani, wakamtazama Abuu kama kikwazo hivyo wakawa na mpango juu yake. 

Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.  Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vile  vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yangu  niteseke. 

Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuona  Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikua  nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawa  anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguo  akampa Mzee Mwinyimkuu. 

Comments zikiwa nyingi naachia ya saba leoleo hapa

Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA SITA YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx 

21 Comments

  1. Heee😓
    Makubwa yanamkuta Saida jamani
    Maskini oooh
    Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na maumivu na mazingatio maishani.
    Asante Admin ❤️
    Kaka Mkubwa
    Kwa burudani ❤️🌄

  2. Afrasiambise@gmail.com on

    Naona km Bado MUNGU yupo n ww Saida . Ni Wakati tu hujfika japo kweli unteseka . Ngoja tuone pengine kaka yako atakuwa anasali .

Leave A Reply


Exit mobile version