IlipoishiaMh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi wa  Elfu Kumi” alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumi  ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani. 

“Usicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hata  beseni zima nakua namaliza mapema” Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanisha  anachoongea, nikasema

“Sawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ila  nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mama” nilisema nikiwa  nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwa  nigeuke . Endelea

SEHEMU YA TATU 

Alikua ni Baba Mkwe wangu, Basi yule Mama alipomwona Baba Mkwe akafurahi sana 

“Afadhali nimekuona Bosi wangu, siku hizi ndio mmeamua msiniungishe si ndiyo?” aliyatupa  maneno kwa Baba Mkwe 

“Ah! Mama mboga mboga huyo, basi fanya kama kawaida. Saida hebu leta beseni” alisema  Baba Mkwe, nilishangaa sana lakini sikutaka kuonesha chochote. Nikaelekea ndani kisha  nikarudi na Beseni.  

Huwezi amini yule Mzee alichukua Mchicha wote na nyanya zote ambazo yule Mama alikua  nazo kwenye beseni, nilihisi kama naota vile maaana mchicha wote ule tule wawili? Halafu  akatoa pesa yake mfukoni na kulipia kisha yule Mama akaondoka zake, Yule Mzee akabeba  Beseni hadi jikoni halafu akaniambia 

“Unapaswa kupika Mchicha wote, ukimaliza nitakuelekeza cha kufanya” Uwiii, nilihisi  nachanganikiwa. Msomaji unaweza usinielewe lakini Jaribu kununua Mchicha wa Elfu Kumi  halafu kaa hapo uuchambue na uupike, nakwambia utamaliza usiku mgongo ukiwa unauma, sasa  fikiria tupo wawili tu halafu nipike Mchicha wote ule, haki nilihisi yule Mzee ana mapungufu  fulani ndani yake.  

“Sawa Baba” jinsi alivyonitazama ilinifanya niitikie tu na siyo vinginevyo ili nisije  nikamkasirisha tena, halafu kwa madoido alielekea sebleni kuendelea kunywa chai, nilibaki  nimejishika kiuno. Beseni la Mchicha naanzaje kuchambua Jamani halafu nipike tule wawili tu,  sikuwahi kusikia kwa Watu kuhusu visa vya Baba Mkwe mara nyingi nilisikia kuhusu Mama  Mkwe ila anachofanya Mzee huyu ni zaidi ya Ukatili. 

Sikutaka kupoteza muda hata hamu ya Chai iliniishia, nilianza kuchambua Mchicha haraka  haraka na uzuri Mungu alinipa Mkono mwepesi sana, hilo hata Mama yangu alikua akilisifia  sana. Hata niwe na kazi kubwa kiasi gani nitaifanya kwa muda mfupi sana, sikutaka hata  kunyanyua simu na kumpigia Mume wangu Salehe kumweleza anayonifanyia Baba yake sababu  sikutaka kuwagombanisha. 

Tokea saa Nne asubuhi nilimaliza Kuchambua saa kumi kasoro nikiwa nimechoka na hapo bado  sijapika, halafu Baba Mkwe alikua akija kunikagua jikoni kama nimemaliza au vipi huku  akinitaka kifanya haraka kupika. Nilijaribu kumwambia kua nimpikie yeye cha Mchana kidogo  ili apoze njaa huku mimi nikiwa naandaa huo Mchicha wa Elfu Kumi. 

Baada ya kumaliza alinionesha sufuria kubwa ambalo hupikiwa kwenye mashuhuli ili nipikie  humo, halafu akaniambia

“Ukimaliza kupika usiipue sufuria hadi niwepo” Unafikiri aliongea kimzaa? Hapana alinikazia  sura yake mbaya 

“Sawa Baba” nilimjibu kwa sauti ya chini iliyojaa hofu kubwa, sikutaka kupoteza muda nilianza  kuupika ule mchicha mwingi huku nikitamani kucheka na kulia kwa wakati Mmoja, ni vile  niliambiwa mambo ya kwenye ndoa ni siri ya ndoa siyo vizuri kuyatoa nje ila nilitamani nipige  picha niwatumie rafiki zangu waone kichekesho nilichokutana nacho Rukwa. 

Nilipiga moyo konde nikawa napika hadi ulipoiva, nilihakikisha chumvi iko sawa kisha  nilimwita Baba Mkwe ili kabla sijaondoa sufuria jikoni aone. Alipofika aliniambia 

“Tia hii” alinipa karatasi yenye Unga mweusi ninyunyize kwenye mchicha, sikusita nilifanya  hivyo halafu akaniambia baada ya dakika Kumi epua kisha acha upoe halafu kapumzike.  Alisema akiwa anatabasamu hadi nikajiuliza  

“Huyu Mzee ni Mzima kweli, sekunde kumi ananuna sekunde kumi anacheka” Sikummaliza,  nilimtazama hadi alipozama chumbani kwake. Basi nilipomaliza niliepua kisha nilifanya kama  alivyonielekeza kisha nikaenda zangu chumbani kulala maana nilikua nimechoka sana yaani hata  njaa iliacha kuuma. 

** 

Niliamka kama saa moja na Nusu hivi Usiku, kitu cha kwanza kilikua kuangalia simu yangu  kama Mume wangu amenitafuta. Hapakua na ujumbe wala Missed Call yake, nikajaribu  kumpigia lakini nikaambiwa simu yake haipatikani niache Ujumbe wa Sauti, nikaitupa simu  pembeni kisha nikausikilizia mwili wangu namna unavyowaka moto kwa maumivu 

Pale pale nikaanza kujisikia hali ya kutapika, nikaelekea Bafuni nikatapika vitu vya Kijani mfano  wa mlenda hivi. Baada ya kutapika nilianza kujisikia vizuri kiasi, nikahisi huwenda labda  nilibadili mazingira. Sasa wakati namalizia kunawa mdomoni nikaona kitu kama hirizi nyekundu  imeangukia chini, nilishtuka sana maana siku zote hirizi ni ishara ya Uchawi. 

Nusura nipige kelele lakini nilijizuia, nikafikiria nifanyaje nimwambie yule Mzee lakini  nikahofia anaweza sema mimi Mchawi, pia nikafikiria nimuulize Mume wangu Salehe atakapo  rudi ila nikahisi hivyo hivyo, sikujua nifanye nini na ile hirizi. Nikaisukuma kwa mguu na  kuisweka nyuma ya bomba mahali ambapo siyo rahisi kwa Mtu yeyte kujua kuwa kuna hirizi ili  nione ni ya Nani na kwanini ipo Bafuni. 

Kama ni ya Mume wangu basi ataitafuta na kama ni ya yule Mtu niliyefanya naye mapenzi  Usiku halafu akatoweka katika mazingira ya kutatanisha ni lazima atarudi tena, nilijiona kama  askari aliye vitani. 

Muda huo njaa ilianza kuniuma, nikaiwaza chai yangu jikoni, basi nikavaa dera na kuelekea  jikoni. Hapo giza lilikua tayari limeingia, nilitafuta zile chapati lakini sikuziona popote pale  nikahisi huwenda Baba Mkwe alizichukua na kuzila. Nikawaza nipike ili nile, lakini nikapata 

wazo la kumuuliza Baba Mkwe atakula nini, nilimuita sana lakini hakuitika, nikamtazama kote  bila mafanikio yoyote yale 

Wakati wazo la kwamba atakua ametoka liliponijia ndipo nilipoanza kusikia sauti fulani ya ajabu  sana ikitokea chumba kimoja kilicho katikati, kama vile palikua na mnyama anayekula nyama  ndani ya hicho chumba.  

Sauti ya kuunguruma kabisa kama vile simba anakula nyama, nilishtuka sana halafu mapigo ya  moyo yakaanza kunienda mbio huku nikiwa ninatetemeka, nilijiuliza ni nini kinaendelea ndani  ya nyumba ya Mume wangu Salehe maana tokea nimefika ni mauzauza tu, shahuku ya kutaka  kujuwa kuna nini ilinianza. 

Palikua kimya hapakuwa na dalili ya Mtu yeyote kuingia ndani isipokua sauti ya ajabu ya  kutafuna na kuunguruma humo ndani, pumzi za nguvu zilinitoka huku kifua changu kikipata  shida ya kuzisukuma pumzi hizo zilizojaa hofu sana. Nikapata wazo jipya la kuchungulia badala  ya kuufungua mlango huo, basi nilimwomba Mungu kwanza kabla ya kulianza zoezi hilo.  

Taratibu nilipeleka jicho langu kubwa kwenye tundu la kitasa cha Mlango, ile sauti bado  ilikuwamo lakini kilichonishtua ni kuliona lile sufuria la Mchicha likiwa tupu ndani ya kile  chumba. Weee‼ nilishtuka hadi nikaacha kuchungulia, kimbelembele chote kiliniisha haraka  sana. 

Nikanyanyua miguu yangu kuelekea jikoni kuangalia kama lile sufuria lipo, nilipofika sikuliona  hivyo nikawa na Uhakika kabisa kuwa Sufuria lipo ndani ya kile chumba, lakini limeenda  kufanya nini na ule Mchicha unaliwa na Nani, ile sauti ni ya Nani?  

Sikupata jibu lolote lile, hofu ilizidi kunizonga huku mwili ukiniisha nguvu, nikakimbilia  chumbani ili nimpigie simu Salehe. Kiukweli woga mkubwa ulioambatana na kukosa nguvu  ulinishika sana, niliichukua simu haraka sana na kumpigia Salehe huku nikiomba simu  ipokelewe. Bahati nzuri safari hii simu ya Mume wangu iliita 

“Salehe Pokea simu tafadhali” nilisema huku sauti ikinijia ya kutaka kulia, kabla hata  haijapokelewa mara mlango ulianza kugongwa. Huo mshituko nilioupata ulinifanya nidondoshe  simu yangu ikaangukia chini na kupasuka kioo kabisa. Sikujali kuhusu simu nilijali kuhusu ni  Nani anaugonga mlango wa chumba changu. 

“Saida” niliisikia sauti ya Baba Mkwe wangu, jinsi nilivyokua namwogopa yule nilizidi  kutetemeka, akaita mara ya pili na tatu huku akizidi kukaza sauti yake ikabidi niitike kama Mtu  aliyeamshwa Usingizini 

“Njoo” alisema halafu nikasikia kama kaondoka pale mlangoni, nilishusha pumzi nzito  sana,pumzi ambayo kama pangelikua na karatasi basi ingelipeperukia mbali kutokana na  mshindo wa pumzi yangu. Nikaiokota simu, cha ajabu ni kuwa muda wote Salehe alikua anaitika 

ile simu yaani alikua akiongea na kuniuliza mbona siongei, wakati naiweka sikioni akakata simu.  Nikajaribu kumpigia lakini bahati mbaya nyingine simu ilikua haina uwezo wa kugusika na  kufanya kazi zaidi ya kuiangalia tu. 

Nusura chozi linibubujike lakini sikuacha kujipa moyo, nikajikaza ili Yule Mzee asigundue chochote kuhusu Mimi, papo hapo nikaelekea kufungua mlango huku nikiigiza kanakwamba  ndiyo nimetoka kuamka, sikujua yule Mzee ananiita wapi ikabidi Mimi ndiyo niite ili nijuwe  alipo. Ulikua usiku mgumu sana kwangu……Tuendeleeee‼ 

“Njoo” aliniita baada ya kusikia sauti yangu, aliniita kwenye chumba kile kile ambacho nilisikia  sauti ya ajabu na kuona lile sufuria la Mchicha.  

Taratibu na kwa hofu niliufungua mlango huku nikimwomba Mungu nisikutane na chochote  kibaya. Nilipofika nilimkuta akiwa amesimama. Chumba kilikua na sufuria chini lakini  nilipoingia niliusikia mwili wangu ukiwa unasisimka sana kitu ambacho kilinifanya nihisi  hapakuwa sehemu salama 

“Abeeh‼” 

“Ondoa halafu uje” aliongea kwa sauti kavu, huku kidole chake akikionesha kuelekea kwenye  sufuri lililo tupu halafu funiko lake likiwa pembeni, chini palikua na chembe chembe za Mchicha  kama vile kuna waliokuwa wanakula kwa Pupa sana, niliinama haraka ili nitoke pale chumbani.  Nilitoka haraka hadi nikajigonga mlangoni lakini sikusikia maumivu yoyote yale. Nilipofika  Jikoni nilijikuta chozi likinitoka, nilitamani kumpigia simu Mama niweze kuondoka maana  niliona yule Mzee alikua na mambo yasiyoeleweka, Mume wangu naye sikujua kwanini  aliniacha na Baba yake. 

Nilijikaza kikike hadi nikarudi tena chumbani mle na kufanya usafi kisha yule Mzee akaniambia 

“Halafu uje” nilihisi nitakuwa nimemaliza kumbe ndiyo kwanza alinihitaji tena, kibaya zaidi  alikua amevalia msuli mwekundu na Singlendi nyeupe iliyochanika, juu alikua na balaghashia  nyeusi ndogo. 

“Sawa Baba” nilisema kisha nilienda kuweka ule uchafu kwenye mfuko wa taka jikoni, moyo  uliniuma sana. Siku ya pili ya ndoa yangu lakini sikuwahi kujuwa maana ya hiyo ndoa ni nini.  Basi, nilirudi ndani ya kile chumba, yule Mzee akaniambia 

“Ulikumbuka kuja na gauni ulilofungia ndoa?” ilinichukua sekunde kadhaa kulijibu swali hili  maana sikujua anamaanisha nini.  

“Ndiyo…‼” 

“Kalivae uje, kuna mila za kwetu kwa Mwanamke aliyeolewa” alisema yule Mzee, niliitikia kwa  kichwa safari hii, halafu niliondoka taratibu hadi chumbani kwangu. Maswali hayakuisha.  Nikaufunga kwanza mlango kisha nikajaribu kuwasha ile simu nione kama itafanya kazi  niwapigie wazazi wangu. Nilihitaji msaada zaidi na moyo wangu uliniambia hivyo

Simu iliwaka lakini haikukubali kubinyika , lakini muda huo huo simu iliita. Salehe alikua  akinipigia, nilihangaika kuipokea lakini haikukubali hadi ilipokata, mara baada ya kukata simu  ukaingia ujumbe, niliweza kuusoma kidogo sana lakini haukumalizika sababu simu ilikua  imelock 

“Saida nisamehe Mimi, yote ni Makosa yangu. Baba yangu…” Ujumbe uliishia hivyo, sikuelewa  alitaka kusema nini kuhusu Baba yake. Nikiwa natafakari mara mlango uligongwa na sauti ya  yuke Mzee niliisikia ikisema “Nakusubiri wewe muda unaenda huu”  

“Nakuja Baba namalizia” nilisema kwa sauti isiyo na shaka kwake halafu nikaitafuta ile gauni,  sikuwa na budi bali kuivaa tu ili nione atasema nini yule Mzee. Nilipata hisia mbaya dhidi yake. Nilivalia lile gauni haraka haraka kisha niliificha simu yangu ndani ya gauni, sijui kwanini  nililipata wazo hili la kwenda na simu japo haifanyi kazi. 

Nilipoingia ndani ya kile chumba, Baba Mkwe aliniambia  

“Kaa katikati ya Chumba kisha jifunike huo mtandio hadi nitakaposema ujifunue” wakati  anasema alikua akiwasha udi, nikaikumbuka harufu ya Udi. Niliusikia kwa mara ya kwanza siku  ya kwanza naamka ndani ya nyumba hii 

Hakuishia hapo akaweka Udi ule kila pembe ya chumba kisha akaufunga mlango wa chumba na  kunikumbusha 

“nimekwambia ujifunike huo mtandio na ubugaze macho yako hadi pale nitakapokueleza nini  cha Kufanya” alisema kwa mkazo kidogo, kwakuwa tayari nilikua na woga basi nikafanya hivyo  mara moja. Zikapita dakika kadhaa pakiwa kimya kisha dakika iliyofwata akaniambia 

“Ondoa mtandio na ufumbue macho yako” aliposema hivyo nilipata hisia ya kuwa kuna jambo  nitaliona ndio sababu ya kunitaka niyafumbe macho yangu. Mwili ulizidi kusisimka Jamani.. 

Nilipofunbua macho sasa nilitamani nikimbie lakini haikuwezekana, nilitamani nife lakini  wakati ulikua haujafika, nikatamani ardhi ipasuke niingie lakini hiyo siyo rahisi na mwisho  nilitamni ingelikua ndoto niamke nikaendelee na shughuli zangu. Ilikua ni kweli nilizungungwa  na Wanaume walio Uchi wa Mnyama, wanaume hao walikua wamepaka vitu kama unga  mweupe usoni na mwili mzima halafu walikua wameinamisha vichwa vyao 

Nilikua natetemeka kwa hofu huku sura yangu ikizidi kuwa yenye kutaka kulia, Baba Mkwe  alikua ameshikilia kisu mkononi akinitazama kwa jicho kali. Yaani jinsi walivyonizunguka  wakiwa wamekaa ilinizuia kurudi nyuma wala kwenda mbele bali kutetemeka tu. Sijawahi  kupata woga kama ambao niliupata siku hii, moyo ulidunda kwa mapigo ya juu sana kiasi  kwamba niliyasikia mapigo kama vile mdundo wa Muziki kwenye redio kubwa (Sabufa). 

“Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisu  kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

“Leo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulani  nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lugha  nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaenda  kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi. 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNE YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

14 Comments

    • Afrasiambise@gmail.com on

      MUNGU wng . Hukumbuki ht kuswali jmn . Taja ht jina la YESU tu mbona wangesambaratika wote na hapo ungejua mume ni yupi

Leave A Reply


Exit mobile version