Ilipoishia Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo  kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa  hapa.  

“Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?” 

“Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na  Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe  akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku  dimpozi zangu zikionekana . Endelea 

 

SEHEMU YA PILI

Ilikua ni ndoto yangu siku moja nifanye ibada na Mwanaume aliyeniowa, moyoni nilimshukuru  Mungu kunipa Mume kama Salehe anayejua wajibu wa Mke na Dini yake. Basi tuliongozana  hadi chumbani kujiandaa, haikuchukua muda mrefu tukawa tumeshapata udhu kwa ajili ya Ibada. 

“Twende sebleni, Baba naye anatusubiria” alisema, sikuacha kutabasamu. Kwangu niliiona ni  Familia bora sana, Baba alitusalisha sote hadi tulipomaliza kisha tukarudi Chumbani Mimi na  Mume wangu 

“Mume wangu, sijui jiko liko wapi, sijui chochote. Mimi ni Mwanamke raha yangu ni kupika  chakula mle nyote” nilisema nikiwa nalivua Baibui langu na kulitupa kitandani 

“Usijali, leo pumzika sote tunaelewa. Kuanzia kesho utaanza kupika na kufanya kazi nyingine,  subiria nakuletea Chakula” alisema Salehe kisha aliondoka zake, aliniacha natabasamu kwa raha.  Nikajisemea moyoni tu 

“Kumbe ndoa ni tamu kiasi hiki” kicheko cha raha kilinitoka Mtoto wa kike, nikabdilisha nguo  kisha nikawasha simu na kuzungumza na Wazazi wangu maana tokea nimefika sikuwajulisha  sababu simu ilikua imezima chaji. Wazazi wangu walifurahi sana na kunisihi niwe mvumilivu. 

Salehe alikuja na chakula kinachotoa mvuke kuashiria kuwa kilitoka jikoni muda huo huo, pilau  la nyama ya Mbuzi na kachumbari yenye pilipili nyingi kama nipendavyo, alinipatia na  kunifanya macho yanitoke. Nilimeza mate kwa uchu 

Sikutaka kuuliza alikitoa wapi na kama alikipika alipika saa ngapi, nilikifakamia kama kilivyo  bila hata aibu. Sasa nimwonee aibu Mume wangu jamani si nitachekwa na Dunia nzima, sasa  baada ya kushiba ndio nikakumbuka kumuuliza

“Hivi hiki chakula kimetoka wapi Mume wangu au umenunua maana kusema kimepikwa hapa ni  Uwongo, pilau nishindwe kusikia harufu yake wakati kinapikwa Mmh‼” Salehe alitabasamu tu,  akaninawisha Maji halafu akaniuliza 

“Umeshiba eeh?” 

“Saaaana, asante kwa Chakula Mume wangu” nilisema nikiwa namwachia tabasamu Mume  wangu. Tulikuwa chumbani wawili tu 

Akaondoa vyombo bila kunipa jibu lolote lile, sikujali sana. 

*** 

Usiku ulipoingia nilikua na uhakika kuwa Ndiyo utakuwa usiku wetu wa kwanza kama Mume na  Mke, nilikua tayari kuiondoa bikira yangu kwa ajili ya Mume wangu. Sasa nikae na Bikira hadi  lini na nimeshaolewa, nilijifanyia Usafi nikamsubiria Mume wangu amalize mazungumzo na  Baba yake Mzee Mwinyimkuu kisha tuzagamuane kwa mara ya kwanza. 

Masaa yalienda hadi nilihisi Usingizi unaninyemelea, nikajiegesha kidogo maana Jumbe zote  nilizomtumia hakuzijibu. Nilikuja kushtuka nikakuta kuna Mwanaume ananikula, sikuweza  kujizuia nilimpa ushirikiano. Nilijua tu ni Salehe awe nani mwingine, alikua fundi haswa na  alinikula haraka haraka kama mwizi vile, nilikua nimezima Taa hivyo palikua giza tupu na  sikuweza kuona taswira yoyote isipokua raha ya ajabu sana 

Nilitolewa Bikira yangu kwa mazingira hayo, kisha baada ya kumaliza alikimbilia bafuni nami  kwa haraka nikawasha taa kuangalia kama kuna damu inatoka ili nisichafue shuka. Hapakua na  Damu yoyote ile, lakini nilikipata cha moto nikawa natabasamu tu. Nikiwa hapo nilikua  namsuburia Salehe aniambie kwanini amenikula guzani tena nikiwa Usingizini hadi nimeshtuka  wakati mimi ni Mke wake  

Siyo kwamba aliniudhi, la hasha ila tu si unajuwa asijeniona kama Napenda sana  kuzagamuana.basi nilisubiria kwa kitanbo kidogo kama dakika ishirini hivi hadi nikajiuliza 

“Anakinawa kitu gani hadi sasa hatoki bafuni?” Bafu lilikua mle mle chumbani. Basi  nikaikusanya shuka ili nijifunge nimfuate bafuni, mara ghafla mlango wa chumba ulifunguliwa.  Nilipatwa na Mshangao mkubwa sana, eti Salehe ndiyo alikua akiingia Chumbani tena akiwa na  nguo zake zilezile alizoondoka nazo kuelekea kuzungumza na Baba yake 

Niliyapeleka macho bafuni huku nikijiuliza ni Nani niliyekuwa nafanya naye mapenzi muda  mchache uliopita, hata Salehe alinishangaa akaniuliza 

“Vipi mbona umepigwa na Butwaa unashangaa nini?” sikujua nimjibu nini, nikakimbilia bafuni,  sikukuta Mtu yeyote yule na hapakua na dalili hata ya Maji pale chini, Uwii niliishiwa pozi huku  mwili ukitetemeka. Salehe alinifuata Bafuni huku akiniuliza 

“Wewe una nini?” 

“Mh Mh niko sawa tu, ndio umemaliza muda huu kuzungumza na Baba?” nikajibalaguza kwa  hofu sana kumuuliza swali hili ila moyo wangu uliniambia kuwa ndani ya ile nyumba palikua na  manbo ya mazingaombwe sababu haiwezekani nifanye mapenzi na Mtu ambaye alipotea ghafla  Bafuni 

Huu siyo mkasa wa kujitungia, nimkasa wa kweli wa Maisha yangu. Nataka ujifunze kuhusu  ndoa na Mtu usiye mjua, unaweza fikiria ni mambo ya kusadikika lakini yalinikuta haya mambo  Rukwa kwenye ndoa yangu ya kwanza, sitakuja kusahau. 

Basi tulirudi hadi kitandani, wenge zito likiwa limeigubika sura yangu. Wasiwasi ulizidi kutanda.  Ningewezaje kumweleza Mume wangu Salehe, angemiamini? Hapana isingelikua rahisi kiasi  hicho 

“Mke wangu nataka tuzungumze jambo” alisema Salehe alipomaliza kuvua nguo zake, nilitikisa  kichwa changu ili aniambie tu maana kichwa kilinijaa mambo mengi na maswali magumu  yanayohitaji majibu ya haraka. Siku ya kwanza Rukwa ilianza kwa ugumu sana na ndiyo kwanza  ni Usiku wa kwanza 

“Kesho naenda Sumbawanga, kuna jambo Baba amenitaka nikalifanye ndiyo maana  nimechelewa sana” alisema Salehe 

“Ooh! Sawa Mume wangu, utarudi lini?” nilijikaza sana hadi kuunganisha sentensi hii na  kumuuliza swali, kigugumizi cha ghafla hakikuniacha kabisa. Halafu kwa mbali nilianza kuhisi  homa kali ila nilijikaza tu.  

“Baada ya siku tatu, sikuweza kumkatalia. Nimekubali ili Baba aridhike tu ila kukuacha Mke  wangu siyojambo rahisi kwangu” Alisema, siyo kwamba nilikua namsikiliza Salehe bali niliwaza  ni Nani yule nilifanya naye mapenzi 

Haikua ndoto kabisa sababu niliushika mwili wa yule Mwanaume aliyepotelea bafuni. Usiku  ulikua mrefu kwangu, maswali hayakuniisha Mimi hadi kulipo pambazuka, kama kawaida ya  Salehe hakunigusa kabisa. Kwanza nilishukuru sababu nisingefurahia kutokana na msongo wa  mawazo niliokuwa nao 

Niliamka mapema kuagana na Mume wangu Salehe, alipoondoka nilienda tena bafuni kukagua  huku nikijikumbusha Usiku wa jana, kwa hakika yule Mtu alikimbilia bafuni lakini kwanini  hakuwepo nilipoenda lilikuwa ni swali nililojiuliza sana bila kupata jibu lolote lile. Nilibakia  nimesimama mlangoni nikilitazama lile bafu 

“Sasa nilikua nafanya Mapenzi na Nani mbona sielewi Mimi?” sikuwa na budi bali kukosa  majibu tu, nikajiwekea moyoni kuwa ipo siku nitaufahamu ukweli.  

Jua lilipo chomoza nilivalia nguo za kufanya shughuli za nyumbani, kwakuwa tayari Mume  wangu alinionesha mahali lilipo jiko nilielekea huko, nilikagua vitu vya jikoni kama mpishi 

nikaanza na kuweka chai jikoni huku nikifikiria ni vitafunwa gani Baba Mkwe angependelea  asubuhi hiyo 

Nilipaswa kumuuliza kwanza hivyo nilienda kumgongea mlango huku nikiwa na hofu asije  akanifokea kama alivyofanya jana, alifungua mlango haraka  

“Shikamoo Baba” nilimsalimia kwa haraka sana tena kwa heshima zote huku nikipeleka na  magoti yangu uelekeo wa chini kisha nikarudi juu, nilimfanya atabasamu kidogo 

“Marhaba Saida, umeamkaje?” 

“Namshukuru Mungu nimeamka Salama Baba” 

“Usiku wako wa kwanza Rukwa umeendaje!” Nilianza kuonesha tabasamu kabla ya kumjibu 

“Mungu ni Mwema Baba, samahani Baba nilikua nauliza unatumia kitafunwa gani asubuhi ya  leo?”  

“Ooh! Chochote tu mpendwa wangu, maandazi, chapati, mkate Mimi nakula tu” alisema,  niliweka mikono yangu mbele kwa heshima muda wote nilipokua naongea naye. Niliachia  katabasamu kisha nikamwambia 

“Basi sawa Baba, naomba nikakuangalizie” 

“Haya Mama, ukitoka tu hapo nje mkono wa Kulia kuna Mama anatengeneza Chapati nzuri sana  unaweza kwenda hapo”  

“Sawa Baba” Basi nilimwacha Baba Mkwe akiufunga mlango wake kisha mimi nilirudi  Chumbani kuchukua pesa ambayo Mume wangu aliniachia halafu nilielekea nje kununua  chapati, japo nilikua natembea lakini mwili ulikua na maumivu makali kama homa fulani hivi.  

Nilijikaza hadi nilipofika kununua Chapati nilipoelekezwa, nilimsalimia vizuri maana ndiyo  majirani wenyewe hao, nikachukua chapati za kututosha Mimi na Baba Mkwe wangu lakini  wakati naondoka yule Mama Muuza chapati akaniita, nilikua nimeshampa mgongo hivyo  niligeuka na kurudi maana nilishapiga hatua kadhaa mbele 

“Abee Mama” Niliitika wito, yule Mama akanitaka nisogee zaidi kanakwamba kuna jambo  analotaka nilisikie Mimi tu, basi nilisogea na kwa uzuri tulikua wawili japo kwa pembeni palikua  na vijana wengine wakiwa wanatia zogo masuala ya Mpira 

“Samahani Binti, ndiyo mara ya kwanza nakuona. Wewe ni Mgeni hapa mtaani?” aliniuliza ila  nilianza kuhisi pengine ana jambo fulani lisilo la kawaida pengine anataka kusema, nilisita  kidogo lakini nikajikuta nikiachia tabasamu kama ilivyo kawaida yangu  

“Ndiyo, Mimi ni mgeni” 

“Unaitwa Nani?”

“Naitwa Saida” 

“Hayo maua mwilini ni ishara kuwa umeolewa siku chache zilizopita si ndiyo?” Jamani yule  Mama simfahamu lakini alinidadisi ndani ya muda mfupi na kugundua yote hayo. 

“Ndio, nimeolewa na Salehe wa nyumba ile pale” sikutaka kona kona maana nilijua angeniuliza  naishi wapi nikaona nirahisishe maongezi tu.  

“Mh! Sawa Mwanangu nisikucheleweshe” alisema halafu muda huo huo akapoa mwili mzima  kama siyo yeye aliyekua akinichangamkia. Nilitamani kumuuliza kwanini ameguna ila nilihisi  nitazidi kuchelewa maana niliweka chai kwenye jiko la Gesi. Haraka nikamuaga yule Mama  kisha nilirejea nyumbani kuepua chai. 

Nilikuta tayari chai ilikua imesha chemka niliiweka kwenye chupa, nakumbuka nilikua  nimenunua chapati Nane, siyo kwamba mimi nilikua mlaji sana ila hofu yangu ilikua kwa Baba  Mkwe sikuujua uwezo wake.  

Nilipomaliza tu kuweka chai ndani ya chupa papo hapo Mlango uligongwa, nikapaza sauti 

“Nakujaaa” Niliamua kwanza nimuwekee Baba Mkwe chai Mezani, nilimtengea chai sebleni na  kumwekea chapati tano kisha nikamgongea mlango na kumueleza chai ipo tayari Sebleni, basi  nikaelekea moja kwa moja hadi Mlangoni kuitika wito 

Nilipofika nilikutanaa na yule Mama muuza mboga mboga wa jana, niliachia katabasamu  nikamsalimia. 

“Vipi na leo hamchukui? Jamani nyie ni wateja wangu wakubwa sana wa Mboga mboga. Tokea  mmeacha kununua Biashara imekua ngumu mno” alisema yule Mama, nilicheka tu  nikamwambia 

“Mwenye nyumba alisafiri Mama, basi naomba Mchicha wa Elfu moja” nilisema maana  niliamini ungetosheleza kwa Watu wawili 

“Wa elfu Moja?” 

“Ndiyo mbona umeshtuka?” 

“Mh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi wa  Elfu Kumi” alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumi  ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani. 

“Usicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hata  beseni zima nakua namaliza mapema” Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanisha  anachoongea, nikasema

“Sawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ila  nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mama” nilisema nikiwa  nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwa  nigeuke …… 

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

18 Comments

    • Afrasiambise@gmail.com on

      Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .

  1. Afrasiambise@gmail.com on

    Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .

Leave A Reply


Exit mobile version