Nadhani watu wa Simba kipindi hiki mngetulia kwanza kwani naona kila siku mnazidi kutengeneza sintofahamu kwa watu wa mpira. Sasa kama hiyo kauli ya kununuliwa kwa Simba SC kupitia Rais wao wa heshima Mo Dewji sidhani kama wanachama wanalifahamu hili.

Pengine alitaka kumaanisha kitu kilichomlia pesa zake zaidi ni klabu ya Simba, sawa hapo angeeleweka tofauti na hapo sidhani kwasababu hata zile Bilioni 20 haieleweki zilikwenda wapi. Je zipo kwenye akaunti benki au ni vipi.

Hii pia inaweza ikawa inachagizwa na maendeleo ya watu wengine ambao hawakuwahi kufikiriwa kama siku moja wangekuja na kuyafanya hayo yanayoendelea kwa hivi sasa. Watu watulie, viongozi wapunguze munkali lakini na wanachama wao pia.

Kama kufuzu Robo bila shaka Simba itaenda kufanya hivyo lakini hizi mambo mengine tusiibue mijadala ambayo haina manktiki yoyote Katika mpira wetu. Simba ni klabu ya Wanachama ambao wanatambulika kwa hisa zao asilimia 51% kama unataka kuwakeza nenda kanunue hizo 49%.

Kauli ya Tajiri Mo binafsi niseme sijaona kama ina tija kwa maana imetawaliwa na unafiki mwingi nani hajui kuwa Mo aliinunua Simba kama hawajui mbona timu inapofanya vibaya humsakama huyuhuyu tajiri wasijisahaulishe vichekesho vyao wenyewe.

Kama tajiri amemaanisha kununua hisa ambazo ni 49% kuna vitu vya kujiuliza pia na hapa.

  1. Mfumo wa mabadiliko ambao ndani yake ndio kuna hayo mauziano ya hisa na kutafsirika kama uendeshaji wa timu kisasa huo mfumo wa mabadiliko umekamilika? Jibu ni Hapana

  2. Kama bado, hizo hisa 49% unazinunua kwa utaratibu upi?

Kwa faida tu.

January 18 Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria wa Simba, Wakili Hussein Kitta alisema maboresho ya rasimu ya Katiba ya Simba yaliyofanywa kama wanachama watapitisha, basi mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo utafanikiwa ndani ya muda mfupi, maana yake ni kwamba mchakato wa mabadiliko haujakamilika.

Nukuu

“Maboresho ambayo tumeyafanya na vitu ambavyo tulivyoviboresha kwenye rasimu ya Katiba ikitokea wanachama wameipitisha, mchakato wa mabadiliko utafanikiwa ndani ya muda mfupi tofauti na ambavyo mchakato huo wa mabadiliko ulikwama kwa zaidi ya miaka mitano.”

Tarehe 18 hiyo hiyo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa nchini Ivory Coast, alitolea ufafanuzi mchakato wa katiba mpya ya Simba na alisisitiza sheria na kanuni ziheshimiwe akaongeza kwa kusema wizara haijapitisha katiba ya Simba.

Nukuu

“Wizara haijapitisha katiba ya Simba,katiba ya Simba ilikuwa na mapungufu na ilikiuka sheria za ushindani wa haki, RITA na BMT ! maelekezo ambayo wamepewa Simba ni kwamba lazima waheshimu sheria”

Tafsiri yake sasa ni kwamba kama katiba bado maana yake mchakato wa mabadiliko pia bado kama mchakato wa mabadiliko bado mauziano ya hisa pia bado kama hisa tu mauziano bado Tajiri ameuziwaje hii timu?

Hizi kauli ni za January 2024, Tajiri anasema ameinunua hii timu mwaka wa tano sasa.

 

SOMA ZAIDI: Klabu Zilizowahi Kushinda Mataji Ya Ligi Kuu Tanzania Bara

1 Comment

  1. Pingback: Simba vs Jwaneng Galaxy Wachezaji Hatari Ni Hawa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version