Hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa barani Afrika inaanza hii leo ambapo mchezo wa kwanza utawakutanisha Nigeria dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo utakaochezwa katika dimba la De La Paix.

Nigeria wanaingia katika hatua hii wakiwa hawajafungwa mchezo wowowte na wakitafuta kupata nafasi ya kuwa mabingwa mara 4 kwani wameshachukua mara 3 huku South Africa wao wakitafuta ubingwa wao wa 2 wa michuano ya mataifa barani Afrika.

TAKWIMU:

Nigeria wanaingia katika mchezo huu wakiwa hawajaruhusu bao lolote katika michezo yao 4 ya mwisho kucheza huku viungo na mabeki wao wakifanya kazi nzuri zaidikatika michuano hii huku wakikabiliana na Bafana Bafana ambao wana kikosi kipana chenye wachezaji wanaofahamiana sana.

Licha ya kutopewa matumaini makubwa ya kufika hatua ya nusu fainali lakini South Africa wameweza kuonesha kuwa nao wana uwezo wa kuchukua ubingwa wa mataifa ya soka barani Afrika.

  • Katika mechi 5 za mwisho dhidi ya South Africa kikosi cha Nigeria kimeshinda mchezo mmoja , sare 3 na kupoteza mara moja nah uku wakiwafunga South Africa katika michezo yao 3 ya mwisho ambayo wamekutana katika michuano ya AFCON.
  • Nigeria wamefunga mabao 8 na kuruhusu bao 1 pekee dhidi ya South Africa katika faianli hizi za mataifa ya barani Afrika.
  • South Africa wameshinda mabao 6 na kuruhusu mabao 2 pekee katika michuano yam waka huu
  • Katika michezo yao 5 ya mwisho Nigeria ameshinda michezo 4 na kusare mchezo mmoja huku South Africa akishinda michezo 3 na kupata sare mchezo mmoja na kupoteza mmoja.

 

TUNABETIJE?

  1. Kipindi cha kwanza kitakua na magoli chini ya 3 (1st Half Under 2.5 Total Goals)
  2. Kutakua na kona zaidi ya 7 katika mchezo (Total Corners Over 7)
  3. Kutakua na kadi zaidi ya 4 (Total Bookings Over 4)

SOMA ZAIDI: Mkeka Wa Leo Jumatano Odds Kibao

 

Leave A Reply


Exit mobile version