Utamu wa michuano ya mataifa barani Afrika unarejea tena hii leo katika dimba la Felix Houphouet-Boigny mchezo wa robo fainali kati ya Nigeria dhidi ya Angola kumtafuta mshindi wa kwenda hatua ya nusu fainali ya AFCON.

TAKWIMU:

Angola walifuzu katika hatua hii baada ya kumfunga Namibia mabao 3:0 huku Nigeria wao ni kawaida kufika hatua hii kwani katika michezo 10 ya 16 bora katika michuano ya AFCON wameshinda michezo 9 na wamefuzu kwa kumfunga Cameroon bao 2:0.

Hapa anatafutwa atakayeingia hatua ya Nusu fainali ingawa Angola hajawahi kufuzu hatua ya nusu fainali kabisa na mara ya mwisho kufika robo fainali ilikua mwaka 2010 ambapo walitolewa na Ghana katika michuano hii.

Kumbuka kuwa mshindi wa mechi hii anakutana na Afrika Kusini au Cape Verde katika hatua ya nusu fainali wiki ijayo.

  • Hii ni mara yao ya 12 kukutana ambapo Nigeria ameshinda mara 3 huku Angola akishinda mara 2 na zinazobakia zote ni sare.
  • Nigeria katika michezo yao 6 ya mwisho ukijumlisha na zile mechi za kirafiki hawajafikisha mabao 3.
  • Angola hawajafungwa katika mechi 8 za mashindano wakishinda mara 4.
  • Nigeria wamefunga katika mechi 11 kati ya 12 za AFCON zilizopita.
  • Angola huu ni moja kati yam waka waliokua na mafanikio makubwa sana kuanzia hatua ya makundi ya michuano hii ya AFCON.

TUNABETIJE?

Ukiachiilia mbali vimbwanga ambavyo vimekua vikijitokeza katika michuano hii ya AFCON katika mchezo huu ni bora kutumia kampuni yako ya kubashiri na kuchagua soko la To Qualify na ukachagua mmoja kati ya Nigeria vs Angola kwamba nani anafuzu nusu fainali.

Kumekua na kutolewa kwa kadi sana kuanzia hatua ya makundi katika michuano hii nadhani sasa ni wakati wa kubashiri kadi ambapo unaweka kuwe na kadi chini ya 6 kipindi cha kwanza 1st Half Under 5.5 Bookings

SOMA ZAIDI: Ukibeti Hivi Robo Fainali AFCON Una Uhakika Wa Kushinda

1 Comment

  1. Pingback: DR Congo vs Guinea AFCON Tunabeti Hivi - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version