Nicolas Jackson ana kifungu cha kuvunja mkataba cha €35m (£30.1m) katika mkataba wake na Villarreal, Bournemouth walikubaliana kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwezi Januari lakini alishindwa vipimo vya afya kutokana na tatizo la nyama za paja.

Jackson alifunga mabao 13 katika mechi 38 kwa niaba ya Villarreal msimu uliopita, akizidi ufanisi wa washambuliaji wa Chelsea.

Nicolas Jackson amekamilisha vipimo vya afya kabla ya kuhamia Chelsea kutoka Villarreal.

Jackson amekuwa lengo muhimu kwa Chelsea msimu huu wanapojaribu kufanya mabadiliko katika safu yao ya ushambuliaji baada ya kumsaini Christopher Nkunku kutoka klabu ya Ujerumani RB Leipzig.

Katika mashindano yote msimu uliopita, Jackson alifunga mabao 13 na kutoa asisti tano kwa niaba ya Villarreal na uthibitisho rasmi wa uhamisho wake kwenda Stamford Bridge unatarajiwa katika siku zijazo.

Hata hivyo, Jackson si jina lenye mvuto kama wengi walivyokuwa wakitumaini msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alipandishwa kikosi cha kwanza cha Villarreal msimu uliopita, na angejiunga na Bournemouth mwezi Januari kama asingeshindwa vipimo vya afya.

Kwa taarifa zaidi za usajili tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version