Ni wakati wake tukumbushane jambo katika haya maisha kuna kitu kinaitwa wakati yaani time yako imefika na wengine muda wao hupita, hapa hua tunachanganya sana na kushindwa kutofautisha zama na nyakati. watakuita chawa, potelea mbali.

Tuseme ukweli kwasasa katika ligi yetu tumeletewa mwenye wakati wake kiungo fundi na mwenye kujua mpira tena kwenye viwango vya juu sana. tusibishane tulete fact. facts zangu ni namna Pacome Zouazoua alivyotuonyesha kwa vitendo namna ya kucheza na kushinda mechi.

Hesabu 23:23 inasema “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli. sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, ni mambo gani aliyokutendea mungu!” kucheza ligi kuu ya Ivory Coast kisha kuwa MVP siyo kitu rahisi, mwamba alipokuwa akiitumikia Asec Mimosas aliivusha timu na kwenda nusu fainali ligi ya mabingwa Afrika sasa unaweza kutumia lugha rahisi alipotoka alifanikiwa sana na timu yake hiyo ya Asec Mimosas na hapa Yanga sc napo anatuonyesha pia uwezo na ubora wake.

Kitendo cha Clatous Chama kushindwa kufanya kitu dhidi ya wajelajela ni ile ya kukuonyesha ni zama zimekwisha kwani ukiiondoa mechi dhidi ya Jwaneng galaxy hakuwa kwenye kiwango kile tulichokizoea lakini wanasema timu hua zinatofautiana na Tanzania Prisons wametujibu kwa vitendo.

Zama hizi ni za viungo wengine ni Pacome Zouazoua hata kama itawatoa roho baadhi ya watu lakini ukifika ukweli tunakubali tu. Yanga sc walikuwa na Haruna Hakizimana Niyonzima zama zake zilipita likaja jina la Clatous Chota Chama.

Ukiwatazama Simba sc waliwahi kuwa na Haruna Moshi Boban naye alipita kisha baadae alikuja marehemu Patrick Mutesa Mafisango na ni wakati wa kuwakumbusha kuwa tutunze kumbukumbu ndugu.

SOMA ZAIDI: Sitegemei Mapya Kwa Benchikha Kama Wachezaji Ni Hawa

1 Comment

  1. Pingback: Simba Wangeanza Na Huyu Anayeleta Wachezaji - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version