Tukiwa shule tulifundishwa nidhamu,nidhamu hiyo ilijumlisha na kuomba ruhusa maalum kwa mwalimu wa darasa endapo una tatizo lolote ambalo linakutaka wewe uende nyumbani,kama mwalimu wa darasa hayupo basi ruhusa hiyo ataifikisha viongozi wa darasa. Yeye ndie mtu wa pili baada ya mwalimu wa darasa,taarifa zote za mahudhurio ya mwanafunzi hutoka kwake kwenda kwa mwalimu wa darasa.

Endapo utapata tatizo ukiwa nyumbani mzazi wako atalazimika kwenda shuleni kukuombe ruhusa kwa mwalimu wako. Misingi ilizingatiwa,ilikuwa ni utaratibu tu ambao lazima ufatwe kwani bila hivyo shule ingekuwa kijiwe cha bangi ukiamua uende au usiende,ingekuwa kama kilabu cha pombe uamue kwenda kunywa au usiende.

Kama hutafanya hivyo basi utakapoenda shuleni utaadhibiwa tu hata kama ilikuwa unaumwa,mwalimu bado atakaumbia nakuadhibu kwa kosa la kutoomba ruhusa kwangu au kwa viongozi wa darasa (Monitor s). Walikuwa sahihi walimu,sijui utaratibu wa sasa kwa sababu hapa mjini ambapo mimi sikusoma naona wanafunzi hata shule wanaenda muda wapendao.

Uwezo wa soka hautafutwi Google,uwezo wa soka hauazii miaka 20,mbinu za utoto wa kutumia mipira ya tambala ndio kipaji huibukia hapo. Hili ni suala ambalo kila mdau wa soka anapaswa kulitambua na kuelewa ipasavyo.

Soka ni idara kubwa unapomtazama under seven wa kijijini unaweza ukacheka akifuma mpira kwa kutumia mifuko na matambala lakini ndipo akili ya kuupenda mchezo inanzia hapo.Unaweza ukajiuliza huyu mtoto anashindwa kusoma anacheza na milaironi hii baada ya dakika kadhaa utaona kaingia kucheza peku tena kwa furaha sana.

Aah!,nimewaza tu yule mtoto anayehangaika kufuma mpira ili aonyeshe uwezo wake kama angeonyeshwa njia vilabu vyetu vingekuwa wapi kwa sasa katika utawala wa soka la wazawa.

Kwa miaka mingi sasa vilabu vyetu vimekuwa na vikosi vya timu za vijana ambako pia kwa kiasi fulani wanatumia gharama kuwalea lakini kwa asilimia kubwa tumeona wakikosa kula matunda ya gharama hizo kwa kutotambua umuhimu wao.

Kuna vijana wengi ambao wanalelewa na vilabu vya Yanga Sc na Simba Sc lakini huishia kuwaacha tu na mwisho wa siku hao ndio wamekuwa wakiwaadhibu pale wanapokutana na ndio wanaonekana kufanya vizuri na vilabu vingine.

Nimefikiria zaidi na mbali zaidi kama vilabu hivi vyote vya ligi kuu vingeweza kuwathamini wachezaji wa timu za vijana na kuwapandisha wa kutosha kupata uzoefu na wakubwa ni kwa kiasi gani wangekuwa wamepunguza gharama hizo za usajili wa wachezaji wa ndani.

Kuna ulazima mkubwa sana wa kukwepa adhabu ya vijana hawa kwani wengi wao ndio wanageuka fimbo za kuwachapa pale wanapokutana,kuna ulazima mkubwa wa kuonyesha nidhamu kwa kuwa na maumivu ya gharama wanazotumia kulea hawa vijana,kuna ulazima mkubwa kwa mashabiki kutambua vijana wanaoshinikiza waondolewe ndio wanakuwa fimbo nzuri za kuchapia vilabu vyao.

Mashabiki wanatakiwa kutambua baada ya muda mfupi tu vijana hao hao wanaotoka kwenye timu zao ndio hao hao wanakuwa wanawanyoshea vidole vya kutaka timu zao ziwasajili na kujikuta wakitumia gharama huku wakijua kabisa wao ndio waliwalea kabla ya kutotambua thamani yao. Naimani kama watalelewa vyema watawasaidia bila tatizo.

Tukienda mbali zaidi ya hapo sio lazima wawatumie wao lakini inawezekana ikawa biashara nzuri zaidi ya kujipatua uchumi na kuimarisha timu.

Nidhamu ni pamoja na kuheshimu matumizi yasiyo ya lazima pale panapowezekana.

SOMA PIA: Heritier Makambo Kitabu Cha Simulizi Walichokataa Wazawa

1 Comment

  1. Pingback: Jean Charles Ahoua,Je Simba Imepigwa Kwenye Huu Usajili?

Leave A Reply


Exit mobile version