Moja Ya muhimili mkubwa sana kwenye timu ni Uongozi imara wa timu husika lakini mafanikio yote Ya timu yanabebwa na muhimili muhimu kikosini ambapo msingi huo ni Kocha mkuu wa kikosi cha timu hiyo. Mafanikio yote Ya timu yanaanzia nje ila eneo mama zaidi ni ndani Ya uwanja ambapo uimara wake uundwa na Kocha mkuu.

Klabu ya Simba SC hivi sasa inapitia kipindi kigumu sana na eneo Lao ni ndani Ya uwanja, kikosi kimekuwa na matokeo yasiyo na muendelezo bora wa kiuchezaji na kimatokeo pia na jambo ilo limepelekea kutokuwa na utulivu na kupelekea kubadilishwa kwa benchi la ufundi Mara kwa mara.

Mara zote hizo walizoamua kubadilisha benchi la ufundi wamekuwa wakiajiri zaidi makocha wa nje au makocha wa kigeni kuanzia Pablo Martin, Roberto Oliviera na sasa Abdelhak Benchinka. Hata hivyo moja Ya njia Ya mafanikio ya timu ni kuwa na muendelezo wa kusimamia falsafa zao kwa usahihi na hiyo inaanzia kwa kuwa na Kocha mwenye mbinu na mifumo ambayo iko au inaendana na falsafa ya timu husika na jambo la pili ni kuwa na wachezaji sahihi kwa ajili ya falsafa  hiyo.

Wapi Simba SC wanahitaji kuboresha kwa sasa? Jambo la kwanza kabisa ni kuwa na Kocha mkuu mwenye staili ya uchezaji ambayo inaendana na Faslafa ya timu hiyo. Simba SC chini ya Kocha Benchinka ni dhahiri kuwa Falsafa ya timu hiyo imekuwa haionekani kabisa, kwanini ? Falsafa mama ya Simba SC ni kucheza soka la chini la kuvutia kwa kuanzia chini huku wakiwa na utajiri wa kumiliki eneo la kiungo kama eneo mama la kuanzisha au kutengeneza mashambulizi na ndiyo maana wamepita wachezaji kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kuonyesha soka safi kama Clatous Chama, Rally Bwalya, Haruna Chanongo, Emmanuel Okwi, Ibrahim Ajibu, Ramadhani Singano, Amri Kiemba na wengine wengi.

Nani mtu muhimu kuirudisha “Style” ya uchezaji ya Simba SC kwa sasa ? Jibu ni Kocha ambaye ana uwezo wa kuisimamia Falsafa ya timu. Sasa swali lipo hapa ni wakati wa kumpa nafasi Kocha Mzawa ?

Jibu langu siyo tu wakati huu bali hata nyuma ilikuwa inafanyika hivyo na tumeona wamekuwa wakifanya vizuri kiuchezaji na mfano wake ni Kibadeni, Matola na Juma Mgunda. Hivyo jambo muhimu siyo wao kupewa timu bali kupewa imani, ushirikiano na mahitaji yote muhimu ambayo wanapewa makocha wageni na mengine ambayo kama Kocha ataona yahitaji kwenye timu.

Wako makocha wengi wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuziongoza timu ya Simba SC na namna yao ya uchezaji kwa vilabu mbalimbali walivyopita na kufundisha vinalandana na namna Simba SC wanavyocheza wakipata timu kubwa na kupewa mahitaji yote muhimu kwa wakati na kuaminiwa basi wanaweza kuifikisha mbali mfano wao ni kama Mecky Mexime, Juma Mgunda ni kati ya makocha ni naona wanaweza kama wataaminiwa.

Imani, matumaini, mshikamano na subra ni njia imara ya kuwapaisha wazawa wetu, kama tunaweza kuwaamini wageni na kuwapa nafasi wanaweza kufanya vizuri

SOMA ZAIDI: Akiondoka Benchika , Tutegemee Simba Gani Msimu Ujao?

6 Comments

  1. Kama kocha wa kigeni anapewa resources zote na anaaminiwa why sio mzawa. I think MGUNDA is man for the job aaminiwe, apewe usaidizi akaongeze ujuzi naimani anakitu. Best coach Best coach MGUNDA

  2. SUREBOY 🥸🤏 on

    Kocha hata awe wewe admn tukikupawachezaji wazurii unatamba mfano nkikupa kosi la gamondiii wewe utakwama wapiiii😂

    Unafikiri benchika ni mbovuuu mpeleke pale yanga uone,🪘🪘🪘

  3. Pingback: Tukiyafanya Haya Kiwango Cha Mpira Tanzania Kitapanda - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version