Bila shaka leo ndie ile siku ambayo mashabiki wengi wa soka Tanzania Bara wanasubiri kutazama mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii kwa mwaka 2023 inayowakutanisha JKT Queens dhidi ya Simba Queens katika uwanja wa Azam Complex , Chamazi.

Fainali hiyo inakuja baada ya klabu ya Simba kumuondosha mtani wake wa jadi kwa penati 5 kwa 4 huku JKT Queens wao wakimfunga Fountain Gate mabao 5:0.

Katika mchezo wa mapema zaidi utawakutanisha Yanga Princess dhidi ya Fountain Gate Princess ambao utakua ni mchezo wa kumtafuta mshindi wa 3 wa ngao ya jamii.

Kumalizika kwa Ngao ya Jamii ndio kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya wanawake ambapo bingwa mtetezi ni JKT Queens aliyechukua msimu wa 2022/2023.

Unawajua wachezaji waliofunga magoli ya mapema zaidi ligi kuu Tanzania Bara? Wasome Hapa Sasa

Leave A Reply


Exit mobile version