Mchezo wa raundi ya tano kundi B ligi ya mabingwa kati ya Asec Mimosas na Simba SC utapigwa Ijumaa Februari 23 katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny moja ya viwanja vilivyotumika katika michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika AFCON2023 iliyomalizika hivi karibuni Ivory Coast

Ni katika uwanja huo Simba SC inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali kwani itamaliza mechi ya mwisho kundi B dhidi ya Jwaneng Galaxy katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo alama moja huko Nchini Ivory Coast inaweza kutosha na Simba SC kuhitaji ushindi katika mechi ya mwisho nyumbani.

Asec Mimosas tayari wametinga robo fainali wakijikusanyia alama 10 katika michezo minne iliyocheza na pengine mchezo unaofuata watahitaji kujihakikishia kumaliza kinara wa kundi ambapo sare itatosha kuwahakikishia nafasi hiyo.

Nani atafuzu hatua ya robo fainali na Asec Mimosas katika kundi hili?

Simba SC, Jwaneng Galaxy na Wydad Casablanca ndio waliobakia ambao nao wanapambania kufuzu hatua ya robo fainali ambapo kila timu inayo nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika kama itachanga karata zake vyema na kufanikiwa kuungana na Asec Mimosas ambaye tayari ameshakata tiketi ya kuendelea katika hatua nyingine katika mashindano hayo

Simba SC ina nafasi kubwa ya kuendelea hatua inayofuata endapo itamfunga Asec Mimosas au kutoka sare katika mchezo huo ambapo itahitaji kushinda katika mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy na Jwaneng  itafanikiwa kufuzu hatua inayofuata endapo itamfunga Wydad AC katika mchezo utakaopigwa nyumbani kwao Botswana na itahitaji kushinda katika mchezo wa mwisho dhidi ya Simba SC.

Wydad AC itafuzu hatua inayofuata endapo itashinda mchezo wake wa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy huku ikihitaji pia kushinda mchezo wao wa mwisho wakiwa nyumbani dhidi ya Asec Mimosas.

SOMA ZAIDI: Kiburi Cha Chama Kinalindwa Na Mashabiki Wa Simba

Leave A Reply


Exit mobile version