Umbali wa takribani masafa 4,270 kutoka Ardhi ya Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Namibia Robert Shimooshili na msaidizi wake Jakobus Markus akiwa makamu hadi kwenye udongo wa Yacine Idriss Diallo Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast, safari ya kumbukumbu bora kwa Namibia anakabidhiwa Collin Benjamin raia wa Namibia.

Magurudumu ya ndege yanaanza safari na hatimaye yanaingizwa ndani kuashiria kuwa mruko huo umeshaagana na “nyonga” na nyonga yenyewe ni ardhi ya Namibia inayoshiriki kwa ufugaji mkubwa.

Maono ya timu ya taifa ya Namibia yanakuwa chini ya Kocha Mnamibia Collin Benjamini mwenye miaka 45, akiwa ni mchezaji wa zamani wa taifa ilo pamoja na vilabu kadhaa kama Hamburger SV na 1860 Munich vya Ujerumani ambapo maisha yake mengi ya kucheza mpira kwa vilabu yalikuwa hapo akicheza kama Kiungo.

Safari yake ya kukinoa kikosi cha Namibia ilianza rasmi mwaka 2018 akiwa kama Kocha msaidizi wa Namibia ikiwa ni baada ya miaka sita ya yeye kustaafu kucheza soka na hapo sasa safari ya kumbukumbu na ya kihistoria kwa Namibia ndani ya Soka la Mataifa Afrika ilianza hapo, pale ambapo mwaka 2022 alikabidhiwa kijiti cha kuwa Kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa ya Namibia.

Ilimchukua takribani mwaka mmoja kuifanya timu hiyo ya taifa kuingia kumi bora ya timu za taifa zilizofanya vizuri ikiwa pamoja na mabingwa Senegal na Morocco. Hakuishia hapo bali aliliwezesha taifa hilo kufanikiwa kutinga Fainali ya COSAFA 2022 na kufungwa mchezo wa fainali dhidi ya Zambia kwenye dimba la Moses Mabhida.

Ilikuwa kama njia kwa iliyotengenezwa kwa mbinu na hamasa ya Collin Benjamini, Kocha huyo aliwezesha Namibia kufuzu AFCON akiwa kundi C pamoja na Cameroon, Kenya na Burundi kwenda nchini Ivory Coast na kumbukumbu bora ya kwanza inawekwa kwenye AFCON 2023 ambapo taifa hilo linafanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo tena kwa taifa kubwa la Morocco. Huku ikifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza na hiyo ikiwa ni mwaka mmoja na miezi 7 ya Kocha huyo kuanza kuinoa timu ya taifa ya Namibia.

Tujifunze kupenda kuthamini na kuvipa imani vitu vyetu, Senegal imepata mafanikio kupitia mzawa Aliou Cisse, Algeria ilichukua ubingwa wa AFCON 2019 na Kocha mzawa Djamel Belmadi hayo ni baadhi ya mataifa yaliyowaamini wazawa na kufanikiwa.

SOMA ZAIDI: Huwezi Amini AFCON Imepita Na Vichwa Vya Makocha Hawa

1 Comment

  1. Pingback: DR Congo Kumtoa Egypt Haijanishangaza Nilitegemea - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version