MSHAMBULIAJI wa Girona, Valentin ‘Taty’ Castellanos amefichua kuwa Lionel Messi ni sanamu yake na anaipenda Barcelona kuliko Real Madrid baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Los Blancos kwenye La Liga katikati ya wiki.

Castellanos alimsifu nyota wa zamani wa Barcelona Lionel Messi kama sanamu yake baada ya onyesho la kihistoria katika ukumbi wa Estadi Montilivi.

Mshambulizi huyo wa Argentina, ambaye alijiunga na Girona kwa mkopo kutoka New York City FC, alifunga mabao yote manne wakati timu yake ikiwachabanga mabingwa hao watetezi 4-2 siku ya Jumanne.

Muargentina huyo, ambaye alikiri kuvutiwa na nyota huyo wa Paris Saint Germain, amefunga mabao 12 katika michezo 31 katika mashindano yote akiwa na Girona msimu huu.

Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alisema kupitia kituo cha Uhispania cha JijantesFC, “Siku zote nimekuwa nikiipenda Barca zaidi kuliko Madrid kwa sababu ya Leo. Yeye ni sanamu kwangu.”

Leave A Reply


Exit mobile version