Utulivu ndani ya klabu ni timu kutwaa mataji kama hilo likikosekana lazima mchafuko utokee tu na ndio hicho ambacho kinawatafuna klabu ya Simba kwa sasa. Mo Dewji anatolewa Mbuzi wa kafara eti hatoi pesa tena siyo sehemu ya kuhudumia timu lakini maswali ni machache tu, mbona Viongozi walinyamaza kimyaa walisubiri mambo yatokee vibayaa waanze kuvujisha Siri za namna hiyo. Hii imetoka ndani humo hakuna mwingine wakutambua kama tajiri hatoi hizo huduma.

Huu siyo muda wakuyaanza haya mambo siyo nyakati nzuri za kupopoana wenyewe kwa wenyewe, timu ikishinda mshinde wote na ikipoteza mmpoteze wote baadae Viongozi mnaketi na kujitafakari upya.

Hakuna unafki mbaya kama hapa sasa watu wanatoka pembeni na kuanza kusengenya atasemwa yule na kusemwa huyu Sasa kwanini msiseme ukweli kuwa usajli ndio ulioidondosha timu, si lilikuja dirisha dogo je kipi kilifanyika cha maana zaidi ya kuleta wachezaji ambao nao walihitajika kuvumiliwa.

Kwa Simba SC ilipofika ilihitaji wachezaji wa kuvamiliwa? Tena ambalo liliwashangaza wengi ni kuwaacha wachezaji ambao wangeendelea kuisaidia timu na wakaletwa wachezaji ambao msaada wao haujakidhi mahitaji ya timu.

Lazima tukubali hapa ni sahihii sana kuwa wavumilivu msimu umalizike na kurudi kwenye uwanja wa usajli kucheki mapungufu ni yapi na kuyafanyia kazi hii itasaidia sana kuliko hili la kuanza kumtafuta mchawi kwangu hakuna afya.

Ukweli mtupu wachezaji wengi waliopo Simba SC umri umeshawatupa mkono na wengine wametumika miili imechoka kwaiyo wanashindwa kutoa kitu kipya. Mfano mdogo Saido Ntibanzokiza yule unataka akupe kipi zaidi, mchezaji ameshamaliza saizi ni Kama anajisukuma tu sasa unahitaji uchawi au Elimu ya Chuo kuliona hili.

Mimi nimemaliza, Mchawi wa Simba ni Wanasimba wenyewe.

Unaweza kutuma andiko au chapisho lako ili lisomwe hapa KIJIWENI kupitia editor@kijiweni.co.tz

SOMA ZAIDI: Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda

6 Comments

  1. Baxeo Africa on

    Wajifunze kutoka kwa uongozi wa yanga,viongozi ambao wana jitoa kwa AJILI ya team na wanajenga uzalendo na hisia za uzalendo kwa wachezaji wao wote

  2. Zeyy Tabasamu✨🥰 on

    Nikweli kbsa🙌Usajili haukulipa hatuna wachezaji Hatuna Timu 🥺Wasianze kuchafuana ila hata Uongozi nao Mbovu sababu wao ndo wanaotulea Onana Na Yule Mtoto mwenye Kwashakooo jobe 💔Pesa zinatoka wananufaisha mitumbo yao

Leave A Reply


Exit mobile version