Hivi sasa matarajio ya wengi pale ambapo kunafanyika usajili ni kwamba anayesajiliwa awe na kiwango kama cha mchezaji aliyeachwa au kuuzwa au kiwe juu yake zaidi na ndipo hapo unapowaibua mashabiki wa soka wa klabu ya Yanga kuhusu usajili wa mshambuliaji ndani ya kikosi chao na kuanza kumkumbuka Mayele.

Ukiyataja mafaniko ambayo klabu ya Yanga wameyapata katika misimu kadhaa iliyopita huwezi kuacha kumtaja mshambuliaji Fiston Mayele ambae walimuuza kwenda klabu ya Pyramids kutoka nchini Misri na baada ya kumuuza wakamsajili Hafiz Konkon kutoka pale ligi kuu ya Ghana.

Nadhani matarajio ya wengi yalikua Konkoni afanye kilicho bora zaidi ya kile ambacho alikifanya Mayele lakini mambo yakaenda ambavyo hayakutegemewa na wengi ambapo klabu ikaona imtoe kwa mkopo kwanza ili waweze kusajili mchezaji mpya mshambuliaji na hapa tumeona namna ambavyo magoli mengi ya klabu ya Yanga yakitoka kwa viungo wa klabu hii.

Unaweza kusema kilichomtoa Konkoni ni ule mzimu wa Mayele ambao kila shabiki alikua nao wa kuamini kuwa watapata mchezaji ambaye atakua na ile nguvu aliyokua nayo Mayele ya upachikaji wa mabao na kuonesha kuwa anataka na ana kitu kikubwa cha kufanya kuisaidia timu.

Kilichotokea kwake cha kutolewa kwa mkopo nadhani kila mmoja alikitegemea kwa sababu hakua na kiwango ambacho licha ya kutomshawishi kocha lakini pia mashabiki hawakua na Imani naye.

Baada ya kuondoka yeye amesajiliwa Joseph Guede ambaye tayari ameshacheza mechi kadhaa akiwa hana bao na huyu tusemeje? Ni kwamba mzimu ule ule uliomtesa Konkoni utamtesa na Guede? Tumpe muda zaidi au ndo ile kusema kwamba nyota njema huonekana asubuhi? Kila mmoja atakua na jibu lake kwa namna ambavyo anaona itafaa lakini kutokana na namna mechi kadhaa ambazo amecheza ni wazi ameonesha ana kitu na ni muda sasa wa mashabiki wa Yanga kuamini kuwa wanatakiwa kumpa nafasi ili aweze kufanya vyema zaidi katika kikosi cha Yanga.

SOMA ZAIDI: Kila Nikimuangalia Kibu Denis Namkumbuka Robertinho

 

1 Comment

  1. Pingback: Huwezi Kumchukia Kayoko Kama Unaupenda Mpira - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version