Ilipoishia 

“Sikia Jojo, ukiishi kwa kuhitaji huruma ya wengine utaishia  kuishi Maisha ya hovyo sana. Lengo la kukutoa mle ni kutaka  kufanya na wewe baadhi ya Majukumu kisha utaachiliwa huru”  Nilishtuka sana kusikia kuna majukumu nataka kupewa, nilifuta  chozi kisha nilimuuliza 

“Majukumu?” 

“Ndiyo! Kwasasa angalia Afya yako kwa mwezi mzima kisha  utakapokuwa sawa nitakuchukua tena” Hakunipa hata nafasi ya  kumuuliza chochote kile, aliondoka zake. Yule Mdada mwingine  alisogea akaniambia 

“Unapaswa kwenda Hospitali” Alininyanyua kisha alinitoa pale,  Ulikuwa ni usiku mwingi sana, nilipelekwa Kwenye hospitali ya  pale pale Magereza.   Endelea 

SEHEMU YA TISA

Nilitibiwa kwa muda wa wiki kama mbili hivi, afya yangu  ilikaa sawa, nilikula ninachokitaka. Mwili wangu ulirudi,  baada ya mwezi mzima wa kuwa pale Hospitali nilirudishwa  Ndani ya Gereza, nilirudi kwa akina Isabela ambao hawakuamini  kama Nimerudi nikiwa mzima tena mwenye afya. 

“Umewezaje Jojo? Tulijuwa huwezi kurudi tena kama wengine  walivyopotea hapa gerezani!” Alisema Isabela 

“Ni stori ndefu sana Isabela ila nimeambiwa nitapewa majukumu  ya kufanya” nilisema 

“Nje au ndani ya gereza?” Aliniuliza 

“Sijui Isabela, Baada ya afya kuimarika zaidi nitaambiwa” 

“Sikia Jojo yaani Mkuu wa hili gereza nasikia ndiyo mchezo  wake, anawachukua wafungwa aliowachagua kisha anawatumikisha  kazi za hatari huko nje kisha wanamletea pesa! Anayesimamia  ni Sarafina” Alisema Isabela. 

“Kiukweli sijui Isabela, ngoja tuone na kama nitapata hiyo  nafasi ya kutoka hapa sitotamani kurudi tena, sitotamani tena  kuendelea kubakia hapa Dar” nilisema 

“Unafikiria kufanya nini?” 

“Kurudi Tabora” Nilisema. 

Basi Maisha yaliendelea, nilikuwa sifanyi kazi yoyote ndani  ya Gereza zaidi ya kula chakula kizuri na kulala. Mwili wangu  ulijengeka sana, nikawa na Afya nzuri sana, Uzuri wangu ulirejea kwa kishindo sana tena nilizidi kunawiri na kuwa  mweupe. 

Mchana wa siku moja, Sarafina alikuja Kwenye chumba chetu,  nilikuwa peke yangu tu sababu niliambiwa nisifanye kazi  yoyote ile. Nilipomuona nilijuwa ndio alikuwa amekuja kunipa  hiyo kazi ya kufanya, nilikaa vizuri 

“Naona sasa Afya yako ipo sawa Jojo, unaweza kuongozana na  Mimi” Alisema kisha tuliongozana, tulienda hadi kwenye Ofisi  ya Mkuu wa Magereza. 

Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza namuona huyo Mkuu wa Magereza,  alionekana kuwa Mtu wa dili sana, basi tuliketi kisha Mkuu  huyo alisema 

“Sarafina hapa umecheza kama Pele, huyu ndiye niliyekuwa  namtaka. Nimeambiwa unaitwa Jojo, umefungwa kwa kosa la  kukamatwa ukiwa unajiuza, unapaswa kutumikia Kifungo cha  Miaka mitatu ila nataka kukupa ofa. Kuna kazi nataka kukupa,  ukiifanya nitakuachia huru” Alisema Mkuu huyo, niliposikia  kuwa nitaachiwa huru nilijawa na shahuku sana ya kutaka  kujuwa nilitakiwa kupewa kazi gani. 

“Sarafina utampa mpango wenyewe kisha utamuandaa kuifanya  kazi” Alisema Mkuu huyo kisha Mimi na Sarafina tulitoka,  tulienda mahali ambapo kulikuwa na Bustani ndogo nyuma ya  kantini ya Askari. 

“Jojo, ubaya wangu ndiyo uzuri wangu inategemea unanitazama  vipi, nilikuwa na uwezo wa kukuacha ufe mle kwenye chumba  lakini nilikutoa sababu nilitaka uwe huru” Alisema Sarafina  kisha aliendelea kusema 

“Kuna mfanyabiashara wa Madini anaitwa Vitalis Kyando, ni  Bilionea wa madini. Anakuja hapa Dar kesho kutwa kwa ajili ya  mauzo ya Madini, ni Mtu mwenye ulinzi mkali sana. Atafikia  Hyat Hotel, ataishi hapo kwa siku mbili kabla ya kukutana na  Waarabu kutoka Moroco ambao ndiyo Wateja wake. Tutakuingiza  hapo kwa kazi moja tu, kutumia uzuri wako kumnasa kabla  hajafanya Biashara. Tunayataka hayo Madini ambayo yanatajwa  kuwa na thamani ya Bilioni 20 za Kitanzania, unapaswa  kuyaiba. Ukishafanikisha utaachwa huru utaendelea na Maisha  yako” Alisema Sarafina 

“Huuuuh!” Nilishusha pumzi zangu, jukumu hilo lilikuwa zito  sana kwangu, nilimwambia Sarafina 

“Sidhani kama nitaweza Sarafina”

“Utaweza tu sababu unahitaji kuwa huru haraka iwezekanavyo”  Alikazia msumari 

“Nenda, Usiku tutaondoka hapa” Alisema Tena Sarafina 

“Kabla ya kazi hiyo naomba kuonana na Shonaa, nimesahau  anapoishi, nahitaji kumshukuru kwa wema alionifanyia”  Nilisema kisha nilimuona Sarafina akifikiria 

“Sawa! Lakini hupaswi kufanya ujanja wowote sababu ukifanya  hivyo utatajwa kuwa ulitoroka Gerezani, utakamatwa na  kurudishwa huku tena utaongezewa miaka ya kukaa hapa, Shonaa  hapaswi kujuwa chochote kile” Alisema Sarafina 

“Sawa nimekuelewa” nilimjibu kisha alinirudisha kwenye chumba  cha gereza, nilikuta wenzangu wakiwa wamerudi kutoka kwenye  kazi ngumu 

“Ulikuwa wapi Jojo!” Aliniuliza Isabela 

“Nipo Usijali Isabela, asante kwa ukarimu na moyo wako, usiku  wa leo nitaenda kutekeleza jukumu zito sana. Kama nitarudi au  sitorudi usiache kuniombea” Nilisema, Isabela aliendelea  kuniuliza maswali lakini sikutaka kusema kingine. 

Basi, Usiku ulipoingia Alitumwa Mtu kuja kuniita, nilienda  kuonana na Sarafina kisha tulitoka na gari la Mkuu wa  Magereza. Alienda kutuacha kwenye ghorofa moja karibu na  kanisa la Azania Front mjini Posta. 

Tulipanda juu kulikuwa na chumba kimoja ambacho  kilitengenezwa ili tuishi humo hadi tutakapo maliza mpango  huo. Tulilala hapo Mimi na Sarafina, asubuhi nilimkumbusha  kuhusu kwenda kumuona Shonaa, aliniambia nijiandae sababu  baada ya kwenda huko tutaenda kariakoo kutafuta nguo za  kuvaa, wakati huo nilikua nimevalia nguo zake. 

Alinipeleka Sinza majira ya saa tatu asubuhi, tulikuwa kwenye  gari nikapata kumuona Shonaa kwa mbali akiwa anacheka na  baadhi ya Wateja, Chozi lilinibubujika sana. 

“Una nusu saa pekee ya kwenda kwa Shonaa kisha urudi ndani ya  gari tuondoke” Alisema Sarafina 

“Asante Sarafina” nilisema kisha nilifuta chozi langu 

Nilitembea taratibu kisha nilisimama karibu na Shonaa nikiwa  ninamtazama jinsi alivyokuwa anacheka, nilikumbuka jinsi  alivyojitoa kunisaidia hadi alinipa nauli ya kurudi Tabora ila Bahati mbaya yalitokea ya kutokea nilishindwa kuondoka  hadi kujikuta kwenye matatizo makubwa mno. 

Basi nilijitoa pale kisha nilimkimbilia na kumkumbatia kwa  nyuma, chozi lilinibubujika. Alishangaa ni nani  aliyemkumbatia 

“Nimekumis sana Shonaa” nilisema, aliitambua sauti yangu  haraka akaniita 

“Shonaa” kisha haraka akageuka, akanishika mkono akanipeleka  nyuma ya Jengo. 

“Nimekutoa sababu Bosi yupo sitaki aanze kuniuliza maswali  kuhusu wewe, siamini Jojo kama nimekuona tena leo” alisema  kisha alinikumbatia tena 

“Za siku nyingi Jojo, umependeza sana. Ndiyo maana  nilikwambia urudi nyumbani si unaona ulivyo nawiri” Alisema  Shonaa bila kujuwa kuwa sikuwahi kuondoka kwa kipindi chote  hicho 

“Ndio maana siwezi kukusahau Shonaa, ushauri wako umenisaidia  sana. Nimerudi kukushukuru” 

“Basi nilisubiria sana simu yako hadi nikapatwa na mashaka  umekumbwa na nini?” Basi nilicheka tu ili kumfanya Shonaa  asiingiwe na hofu 

“Yaani simu ile niliipoteza ndio nikapoteza na namba yako  kabisa” 

“Masikini pole sana Jojo, unaishi wapi kwa sasa?” 

“Nimekuja tu kwa Dada yangu mmoja hivi wa kule Tabora”  Niliangalia saa yangu niliona muda wa kuwa pale ulikuwa  umeisha, ili nisiharibu mambo nilimwambia Shonaa 

“Dada yangu ananisubiria kwenye gari kule kwahiyo ngoja  nirudi tutaonana siku nyingine” 

“Ngoja nije kumuona Dada yako basi” Alisema Shonaa 

“Hapana usijali Shonaa, utamuona siku nyingine” Basi  niliondoka zangu pale kwenye gari 

“Hujamwambia Chochote?” Aliuliza Sarafina

“Hapana sijamwambia chochote” nilimjibu, safari ya kutoka  Sinza kuelekea Kariakoo ilianza, nililikariri lile eneo  ambalo tulienda ili kama kitatokea chochote basi nimtafute  Shonaa. 

Tulienda kwneye maduka yanayouza nguo nzuri za kiarabu,  nilichagua na zingine alinichagulia Sarafina ili kesho yake  niende Hyat Hotel. Niliambiwa paliandaliwa sherehe fulani ya  kuadhimisha miaka kadhaa ya Hoteli hiyo hivyo miongoni mwa  watakaokuwepo atakuwa ni huyo Bilionea wa madini. 

Tulirudi kule kwenye ghorofa la Tancot House ambapo ndiyo  tulilala usiku uliopita, Nilijaribu nguo zote ikapatikana  moja tu ambayo ilionekana kuwa nzuri sana na yenye  kunipendeza zaidi 

“Wow!! Hii ndiyo yenyewe Jojo, nina uhakika hawezi kuchomoka,  sasa unapaswa kuwa makini sana sababu ni lazima akuchukue  kama kimada wa kulala naye Usiku, ndipo utakapo iba hayo  madini, utachunguza kujuwa yalipo, baada ya kufanikisha  zoezi, utafungua dirisha sababu chumba chake kipo mashariki  mwa jengo hilo, utayatupa madini kwa kutumia kifaa ambacho  kitakuwa kimehifadhi kisha utayachukua baada ya kushuka, kuwa  makini sana vinginevyo unaweza ishia huko Hotelini, pia ni  lazima ukamilishe zoezi ili uwe huru” alinieleza Sarafina 

Nini Kitaendeea?  Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST? 

Usikose SEHEMU YA KUMI ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

 Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx 

 

5 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version