IlipoishiaNajuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwa  kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,  sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi” 

Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwa  akinikagua, nilionesha lile tabasamu feki 

“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibana  kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononi 

“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamu  lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamu  lililotoka moyoni 

“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengine  walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.

Endelea 

SEHEMU YA TATU

“Vumilia Jojo utakuwa sawa tu” Alisema tena Shonaa kisha  alinyanyuka akatoka ndani, alikuwa na moyo wa peke yake, kuna  wakati nilijiona nipo sawa pindi ninapozungumza na Shonaa. 

Nilijilaza kitandani, kutokana na ule uchovu nilijikuta  nikipitiwa na Usingizi, niliamka mishale ya saa tatu usiku,  nilimuona Shonaa akivaa nguo, alivalia Baibui hadi  nilishangaa, nilihitaji kumuuliza anaenda wapi? 

“Shonaa unaenda wapi tena?” Nilimuuliza nikiwa ninatabasamu,  kiufupi alipendeza sana 

“Naenda kwa Bwana wangu” Alijibu akiwa anajipodoa,  nilinyanyuka kwanza ili niseme kitu 

“Bwana wako? Ina maana umeolewa?” 

“Hapana ni Boyfriend tu, vipi mbona unanishangaa?” 

“Umependeza sana unaonekana ni mwenye Heshima kubwa snaa  Shonaa” Nilisema, nilimfanya acheke 

“Ndio nina heshima kwani naonekana sina heshima?” Aliniuliza 

“Hapana…ninachomaanisha yale mavazi ya kazini yanakufanya  uwe tofauti sana na jinsi ulivyo sasa” Nilisema 

“Jojo Maisha haya yatakufundisha vitu vingi sana, yatumie  vizuri uone kile ambacho macho yako ya kawaida hayawezi  kuona” 

“Una maana gani Shonaa?” 

Shonaa hakunijibu chochote, alipomaliza kujiandaa aliondoka  zake, nilipata muda wa kuwa peke yangu, usiku huo niliona ni  bora niwasiliane na Msonjo ili anipe mrejesho wa kile  alichozungumza na Bosi Muntaza, nilipiga simu lakini  haikupokelewa hadi baadaye kidogo aliponipigia yeye 

“Griii! Grii!” Ulikuwa ni mlio wa simu yangu, ilikuwa tayari  nimepitiwa na Usingizi, niliamka na kuipokea 

“Hallo Msonjo” Nilisema kwa sauti ya uchovu 

“Mambo Jojo” Alisema Msonjo 

“Mambo mabaya Msonjo vipi umeshaongea na Bosi anipe nauli?”

“Nimeongea naye ila kasema hawezi kupoteza pesa yake kwa Mtu  ambaye hajafanya kazi yoyote” Alinijibu Msonjo, moyo uliniuma  sana 

“Sasa Msonjo….huwezi kuazima sehemu nikifika nitakurudishia  tafadhari” 

“Mmh! Jojo nisikuongopee hapa sina wa kumuazima pesa,  ninachoweza kukushauri ni kwamba fanya kazi kwa muda ili  uweze kuipata hiyo pesa”. 

“Yaani Msonjo katika vitu nimebugi katika Maisha yangu basi  ni kuja huku Dar, naona kama nipo kwenye chumba chenye giza  na joto kali, najiona mwenyewe tu na sina Mtu wa kunisaidia”  Nilisema, Chozi lilianza kunilenga, Msonjo aligundua kuwa  nakaribia kulia kutokana na jinsi sauti yangu ilivyokuwa  ikitoka. 

“Jojo huna sababu ya Kulia, pambana huko Dar….pengine  baadaye unaweza ukabadilisha kauli baada ya kuona mambo  yanakunyookea, cha Msingi sasa hivi kaza Buti” Alisema Msonjo  kwa maneno rahisi sana, niliona siwezi kuupata Msaada  niliokuwa nautaka kutoka kwake nilimuaga 

“Msonjo….nakutakia Usiku mwema” Nilisema kisha  jilisikikizia jibu la Msonjo lakiji hakujibu chochote kile,  nilikata simu na kuanza kulia, niliona kama Msonjo alikuwa  ameniuza Jiji Dar, nililitazmaa Begi langu, nilikumbuka nina  elfu kumi tu tena hata Jiji silijui kabisaa. 

“Eeh Malaika wa Mama yangu naomba Mniongoze, nahisi kushindwa  na kukata tamaa kabisa, Mungu unaniona?” Nilisema huku chozi  likinibubujika, ilikuwa mishale ya saa nne za Usiku. Mlango  uligongwa tena mgongaji aliita jina la Shonaa, ilikuwa ni  sauti ya Mama wa Makamo aliyeonesha kuwa na jazba ya jambo  fulani mana jinsi alivyoita Mmh!! 

“Shonaa hayupo” Nilijibu nikiwa chumbani 

“Njoo wewe” Alisema Mama huyo kwa shari sana, sikumjuwa na  wala hakuwa akinijuwa, basi niliingiwa na woga sana nilitoka  ndani. 

“Shikamoo Mama” Nilimsalimu kwa adabu sana 

“Shikamoo mwenyewe, kama unaona hiyo shikamoo Mali basi ikate  iweke kwenye sufuria igeuke nyama ya Mbuzi…hivi nyie  mnatuchukuliaje humu ndani?” Aliuliza kwa shari ile ile

“Kwani kuna nini Mama yangu” Nilimuuliza maana woga ulikuwa  umenishika 

“Hebu twende” Alinishika mkono kwa nguvu akawa ananipeleka  njia ya Chooni, aliniingiza hadi chooni 

“Nini kile?” Alionesha kidole kwenye karo la Choo, Aah yaani  kulikuwa na haja kubwa iliyokuwa haijamwagiwa maji 

“Hizo pombe mnazokunywa sisi tumekunywa kitambo na tukaziacha  sababu hazina faida yoyote, wenyewe mnaona Ujanja si ndiyo?  Sasa safisha hapo haraka sana nataka kuoga” Alisema Mama huyo  kwa hasira sana 

“Lakini Mama mimi ni mgeni hapa na sijui chochote kile”  Nilijitetea kwa sauti ya chini sana, mkononi nilikuwa  nimeshikilia simu yangu ndogo, sasa yule Mama alinisukumiza  nishike Fagio, simu ikaangukia kwenye shimo la choo 

“Simu yangu” Nilisema kwa maumivu makali sana, simu ile  ilikuwa ndio msaada mkubwa kwangu kuwasiliana na Msonjo na  Watu wengine ambao walikuwa Tabora. 

“Nyooo! Usinilegezee sauti, hebu fanya Usafi fastaa” Alisema  Mama huyo, kwa jisni alivyochukia ilinilazimu haraka sana  kushika fagio, Mama huyo alitoka nje. Macho yangu yalijaa  machozi ya maumivu makali sana niliwaza ndani ya akili yangu 

“Haya ndiyo Maisha gani jamani ni Bora ningekufa njaa Tabora,  Mama umeniacha unaona sasa yanayonikuta Mwanao” Nilijisemea  huku chozi likizidi kunibubujika, nilifanya Usafi nikiwa  ninalia hadi nilipomaliza kisha nilitoka 

“Subiria hapo hapo niangalie Kama umesafisha vizuri” Alisema  Mama huyo kisha aliingia chooni kuangalia, baada ya sekunde  chache alitoka 

“Bahati yako, haya sepa” Alisema, nilimuogopa mno, ilinibidi  haraka nishike njia ya kurudi ndani, nyuma nilisikia sauti  yake akicheka kisha alisema 

“Mjini shule” Jamani niliumia sana, moyo ulimwaga chozi la  damu lenye Maumivu, nilikuwa Msichana mpole sana ambaye  sikuweza kujibizana na Mtu yeyote yule. 

Nilipofika chumbani niliongeza kilio, Chozi lilinimwagika  nikiwa nimejitupa kitandani. Jiji la Dar liligeuka kuwa  chungu sana kwangu, kabla hata sijatulia nilisikia tena  Mlango ukigongwa, niliogopa sana nilijifuta chozi haraka  kisha niliuliza

“Nani?” Niliuliza kwa sauti ya upole mno tena iliyojaa woga 

“Fungua wewe” nilisikia sauti ya Mdada mmoja ambaye  tulimuacha akiwa amelala asubuhi, ilikuwa ni sauti  iliyoambatana na Ulevi. 

Mara moja nilienda kumfungulia, ile nafungua tu nilikutana na  tusi la nguoni, tena aliyetukanwa alikuwa ni Marehemu Mama  yangu Masikini 

“Malaya wewe! Unajiona mzuri ndio hufungui mlango eeeh?”  Alisema yule Mdada, nilichukia sana kisha nilienda chumbani  wala sikutaka kubishana naye. Alikuwa ameongozana na  Mwanaume, wote walikuja chumbani. 

Yaani kilichonikausha kilio changu kilikuwa ni kitendo chao  cha kuondoa nguo zao zote kisha kuanza kufanya mapenzi mbele  yangu bila hata Aibu, sikuweza kuwavumilia nilitoka chumbani,  kelele zao zilikuwa juu hata sebleni niliona hapakuwa salama  kwangu, nilienda nje kabisa. Ndani ya muda mfupi nilikutana  na matukio yaliyoniacha kinywa wazi, mambo ambayo nilikuwa  nasimuliwa na Watu kuwa wameona katika filamu ndiyo nilikuwa  nikiyashuhudia kwa macho yangu, nilitamani sana kumpigia simu  Shonaa nimueleze maana angalau yeye tulikuwa tukiiva chungu  kimoja lakini ndiyo hivyo tena simu ilikuwa imeingia Chooni. 

Nilikaa nje kwa zaidi ya Masaa mawili nikiwa ninalia, baadaye  nilirudi ndani, palikuwa pametulia, basi nilifunga mlango  kisha nilijilaza kwenye kochi nikiwa nimevalia zangu dera. 

Sijui hata ilikuwa ni saa ngapi, nilishtuka tu nilihisi mkono  ukinichezea makalio yangu, nilipoamka nilimuona yule Mwanaume  ambaye alikuja na yule Mdada. Nilimuuliza 

“Wewe ni Nani na Unataka nini?” Niliuliza huku nikiwa  nimejaza woga kwenye kifua changu, nilijisogeza nyuma kabisa  ya Kochi 

“Shiii” Alinipa ishara kuwa sipaswi kusema chochote kile,  alitoa kisu akaniambia 

“Ukipiga kelele Nakuchoma kisu sasa hivi” Alisema akiwa  ananionesha na ishara kabisa jinsi atakavyo nichoma hicho  kisu. 

Kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliona Mungu  amenitazama, yule Mdada alikuwa ameamka hakumuona Mtu wake  hivyo akaja sebleni na kukuta yule jamaa akiwa amenishikilia  kisu, aliposikia sauti ya Mwanamke wake alikitupa kile kisu. 

Bahati nzuri taa ilikuwa inawaka maana nilikuwa siwezi kulala  bila taa, alikiona kile kisu 

“Unaniacha chumbani unakuja kwa huyu Malaya si ndiyo?”  Alisema yule Mdada, nilihema juu juu 

“Unafanya nini hapa?” Alihoji yule Mdada, alimshushia kipigo  yule Mwanaume hadi nilishangaa, Mwanamke anaweza vipi kumpiga  Mwanaume namna ile? Hadi niliingilia kati maana alishamtoa  damu kinywani 

“Wewe malaya hayakuhusu haya, una kesi na Mimi kwahiyo subiri  hivyo hivyo” Alisema yule Mdada, basi aliendelea kumpiga,  alipochoka alimwambia 

“Tembea nisikuone tena hapa Shwaini Mkubwa wewe” Alisema yule  Mdada, yule Jamaa aliposikia hivyo aliona kama vile alikuwa  ametembelewa na Malaika mtoa roho alafu akamuacha basi  alijipigiza kwenye mlango akafungua na kukimbia zake,  nilijikuta nikicheka japo kwa sauti ya chini maana Yule Mdada  naye alicheka kidogo kisha aliacha kucheka alafu akaniangalia  kwa jicho kali 

“Ukijilegeza utaliwa!” Alisema yule mdada kisha aliongoza  kuelekea chumbani 

“Samahani”nilisema kwa woga, alisimama 

“Unaitwa Nani?” Nilimuuliza, alicheka kisha alinijibu “Sarafina” Alijibu na kuingia chumbani. 

Japo mambo yale yalikuwa mageni kwangu na yenye kuniumiza ila  yalinifundisha vitu vingi sana ambavyo hata kama ningesoma  hadi ngazi ya digrii nisingeliweza kujifunza. Usingizi  haukuja kabisaa nilikaa macho hadi niliposikia adhana  wakiazini msikiti wa jirani ndipo nilipofahamu kuwa palikuwa  pamepambazuka. 

Tulikuwa na zamu ya kwenda kule Dar City Mimi na Shonaa,  nilijiandaa. Muda ulienda nikiwa ninamsubiria Shonaa, Jua  lilipoanza kutua Shonaa alirudi akiwa mwenye furaha,  alinionesha kiasi cha pesa alichokiingiza. 

Kilikuwa ni zaidi ya laki moja, niliitamani pesa hiyo maana  kama ningeliipata basi ingenitosha kwa Nauli ya kuelekea  Tabora, aliketi lakini aliniona nikiwa sina fruaha kabisa. Nini Kitaendelea

Usikose SEHEMU YA NNE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

 Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx

6 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version