IlipoishiaSikujuwa hata mtandio wangu niliudondoshea wapi, nilikuwa  kama Chizi maana wakati nalia nilitimua sana nywele zangu.  Nilikaa hapo kama Bubu, niliwaza sana hadi kichwa kiliacha  kufikiria tena, Sikujuwa niende wapi maana Sikuwa na namba ya  Mtu yeyote yule Kichwani, sikuwa na kumbukumbu ilipo Ile  kumbi ya Sterehe maana nilienda mara moja tu, kingine sikuwa  na kumbukumbu pale nilipokuwa naishi na Shonaa palikuwa  panaitwaje maana napo nilikaa kwa siku mbili tu, nilikuwa  Mgeni Dar, Nilimkumbuka sana Shonaa hadi Chozi likawa  linanidondoka tu. Endelea

SEHEMU YA TANO

Laiti kama Shonaa angekuwepo asingeruhusu napata tabu,  nilijilaumu hata kwanini nilishuka kwenda kujisaidia, Maisha  yangu yaliingia kwenye Dunia nyingine ngumu zaidi tofauti na  Mwanzo, niliivua ile Rozali kisha niliitupa kwenye mtaro  mdogo ulio mbele yangu, niliona Mungu amenisahau katika  Hesabu zake au alikuwa akinifanyia makusudi 

“Sasa kwanini ulimchukua Mama yangu, hukujuwa kama  nitateseka? Kama Mungu una nguvu nitoe hapa nipae hadi  Tabora” Nilisema maneno ambayo hata Kichaa hawezi  kuyafikiria, niligumia kwa nguvu sana hadi Watu walio karibu  walisimama kuniangalia kwa muda kisha waliondoka zao. 

Nilikaa pale kwa zaidi ya Masaa matatu, baadaye alikuja  Mwanaume mmoja alikaa kando yangu, alikuwa bize na simu yake  hata hakunisalimia. Nilipata akili ya kumsalimia 

“Mambo Kaka?” Nilisalimia nikiwa namtazama 

“Powa” Alijibu bila hata kunitazama Usoni, niliona potelea  mbali nimuombe msaada tu hata kama anaonekana ana dharau 

“Naitwa Jojo, Kaka yangu naomba msaada nilikuwa nasafiri  naenda Tabora bahati mbaya nimeachwa na gari, sina ndugu hapa  Mjini wala sijui leo nitakula nini na nitalala wapi”  Niliposema hivi alinitazama, nililiona jicho lake la  kunichunguza 

“Una shida kweli wewe?” Aliniuliza kwa sauti kavu sana,  mkononi alikuwa na tatuu, alikuwa na kifua cha kujaza alafu  alikuwa mweusi hivi, nilimjibu

“Ndio” 

“Subiri kuna mzigo napokea” Alisema yule Mkaka, niliona kama  ngekewa vile maana nilishakata tamaa kabisa, kusikia Mtu  atanisaidia ilikuwa faraja kubwa kwangu. Ilituchukua nusu saa  tukiwa kimya huku yeye akiendelea kuchezea simu yake. 

Alikuja Mwanaume mwingine aliyefanana na yeye, alimpatia  Boksi hivi dogo kisha aliondoka jamaa yule alafu yule Mkaka  akaniambia 

“Twende” alisema kikauzu sana, unafikiria nilitilia shaka  msaada wake? Wala sikuwa na mashaka hata kidogo, nilimfuata  kwa nyuma. Kumbe alikuja na Pikipiki yake aliiacha nje,  alinipa lile boksi dogo kisha aliniambia nipande kwa nyuma.  Nilipanda kisha safari ya kuelekea nisipopajua ilianza,  angalau chozi lilikuwa limekauka, niliona mwangaza mpya  katika Maisha yangu. 

Ilikuwa ni safari ndefu kutoka Ubungo, nilisoma vibao vya  Njiani ili kujuwa tupo wapi, niliona tupo mwenge kisha  baadaye niliona Mbezi Africana, hapo ndipo safari yetu  ilipoishia kwenye nyumba moja hivi ambayo ilikuwa kimya sana.  Aliniambia nimpe Boksi lake baada tu ya kushuka, kisha  aliekelea kufungua geti, tuliingia humo. Ilionekana ni nyumba  ambayo haikuwa na Mtu kabisa maana alifungua milango yote  hadi tulipofika sebleni kisha alisema 

“Karibu” Alisema alafu alijitupa kwenye kochi, akawa  analifungua Boksi lile alilopewa na yule jamaa kule Ubungo. 

Alitoa vitu kama Unga fulani hivi ila hata sikutaka sana  kujiuliza maswali mengi, akaingia chumba kimoja alafu akatoka  akiwa ameshikilia kisu, nilihofia sana maana nilikumbuka lile  tukio la Kutaka kubakwa kule kwa Shonaa. Yule Mkaka alikuja  karibu yangu akavuta kiti kisha akakaa mbele yangu, hofu  ilianza kunijaa 

“Umesema unaitwa Nani?” Aliniuliza 

“Naitwa Jojo” nilijibu kwa woga sana 

“Jojo…sasa Jojo, mimi najuwa kama wewe ni Askari na kwanini  uko hapa, umetumwa kunipeleleza si ndiyo?” Aliniuliza yule  Mkaka ambaye hata Jina lake sikulifahamu, stori ya Maisha  yangu ilianza kunichanganya maana kila nilipoenda nilikutana  na kikwazo kikubwa zaidi.

“”Mimi siyo Polisi Kaka yangu, Nahitaji msaada wa Mimi kurudi  Tabora kama hauwezi kunisaidia basi niruhusu niondoke”  Niliona ni bora hata kuondoka kuliko kuendelea kuwa pale 

“Wengi waliotumwa kwangu walipotea kama ambavyo wewe unaenda  kupotea,”. 

“Unamaanisha nini?” Niliuliza kwa hofu kubwa sana, niliona  sasa Maisha yangu yanaenda kufika kikomo 

“Mimi ndiye Juma Baro, najua nini nafanya” alinivamia,  nilijitahidi kupiga kelele kuomba msaada, alinikamata vizuri  kisha aliniweka unga kwenye pua yangu, sikuchukua raundi,  nilihisi mwili hauna nguvu kisha niliona giza zito, sikujuwa  kilichoendelea. 

Niliporudisha fahamu zangu nilijikuta kwenye chumba chenye  giza, ghafla taa iliwashwa, Yule Mkaka aliyejitaja kuwa ni  Juma Baro alisimama kando yangu. Nilikuwa nimechoka sana,  nilikuwa nahema juu juu, alinimwagia maji ya Baridi, angalau  alifanya mwili wangu uanze kuwa sawa. 

“Kaka yangu naomba uniruhusu niomdoke Mimi siyo Polisi”  Nilisema. 

“Najuwa wewe siyo polisi, dakika chache nimelitambua hilo,  lakini bahati mbaya ni kuwa umejuwa baadhi ya vitu na wapi  yalipo makazi yangu, sitokuruhusu kwenda popote badala yake  utaishi hapa” Alisema, nilishtuka nikamwambia 

“Sijui chochote kuhusu wewe Kaka yangu, naomba tafadhali sana  uniache niende nikatafute msaada sehemu nyingine, nakuomba  Kaka yangu nipo chini ya Miguu yako” Nilisema, alikuwa  amenifunga kamba mikononi na miguuni. 

“Hutoweza kutoka hapa tena utaishi hapa kama Mke wangu”  Alisema Juma Baro 

“Tafadhali Sana Kaka yangu nakuomba usifanye hivyo, nina apa  kwa Mungu wangu kuwa sijui chochote, ninachotaka ni kurudi  Tabora tu” 

“Mungu? Kumbe Mungu wako yupo? Yupo wapi sasa? Basi huyo  Mungu amekusahau, angekuwa anakukumbuka angekutoa hapa kwenye  hiki chumba” Alisema Juma Baro kisha aliondoka na kufunga  mlango kwa nje, kamba zilikuwa zimeniumiza mno mikononi,  kauli moja ya Juma Baro ilijirudia katika akili yangu kuwa  “MUNGU AMENISAHAU” Ndiyo niliitafakari sana, niliona ina  ukweli ndani yake sababu kama angekuwa ananikumbuka basi  angenitoa kwenye matatizo na kuniweka salama, kwanini  anazamisha Maisha yangu kila wakati. 

Niliishi pale kwa Juma Baro kama Mfungwa ndani ya Chumba  chenye giza, nilililaani Jiji la Dar-es-salaam, nilimlaani  Msonjo kwa kunileta katika Jiji hili lenye kila aina ya  ukatili. Alikuwa akija kuniletea chakula, alikuwa akija kwa  siku mara mbili, sikujuwa ilikuwa ni siku gani, sikujuwa  ulikuwa ni wakati gani, chumba hicho kilitengenezwa mfano wa  chumba cha Kulala maabusu, hakikuwa na Choo, dirisha lake  lilikuwa juu sana hata sikuweza kuangalia nje. 

Nilikuwa najisaidia kwenye ndoo kisha anakuja kuchukua,  anaenda kumwaga, sikujuwa nilikuwa kwenye ile nyumba ya  mwanzo au alinipeleka kwenye nyumba nyingine, Basi niliishi  Maisha hayo. 

Usiku mmoja alikuja, alinifungua kamba mikononi kisha  alinitoa humo akiwa amenifunga kitambaa usoni, alinipeleka  kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kizuri sana, kilikuwa  na kila kitu akaniambia 

“Kuanzia leo utakuwa unaishi hapa” 

“Kwanini unanifanyia hivi Kaka yangu, unajuwa ni kiasi gani  nateseka Mimi?” Nilisema kwa maumivu makali sana ndani ya  moyo wangu. 

“Unayajua mateso wewe? Katika watu nimeishi nao vizuri wewe  namba moja, unajuwa kwanini?” Aliniuliza akiwa amenisogelea,  nilitikisa kichwa changu ishara kuwa sijui 

“Kwasababu wewe ni Mzuri sana Jojo, ni hasara kubwa kuishi na  wewe katika mateso makubwa ndiyo maana nimekuleta hapa”  alisema, kusema ule ukweli woga uliniisha kabisa sababu  sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kile. Alianza kunishika  shika kitu ambacho kilinifanya nichukie, nilimpiga kofi 

“Ukiendelea kunishika nitakufanya kitu kibaya” Nilisema, Juma  Baro alipandwa na hasira akanitandika kofi na Mimi kisha  alinitupa kitandani, alitumia nguvu zote aliniondoa nguo  zangu na kunibaka. 

Ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuingiliwa na mwanaume,  tena kwa kubakwa, nilipata uchungu na maumivu makali sana  katika sehemu zangu za siri, roho iliniuma sana. Damu  zilinitoka lakini hata hakujali aliondoka zake na kufunga mlango, katika mateso ambayo yaliniumiza moyo na akili yangu  ni pamoja na kubakwa, nilijiona nimeondolewa thamani yangu,  nilijiona nimepoteza kila kitu katika Maisha yangu 

Nililia sana, mwili ulishika moto vibaya mno. Baadaye alikuja  akanipa dawa za kutuliza maumivu kisha aliondoka zake 

Hayo yalikuwa ndiyo Maisha yangu nyumbani kwa Juma Baro,  niligeuzwa kuwa Mtumwa wake wa ngono, alinifanya apendavyo  tena bila kujali kuwa nilikuwa ninaumia sana kuingiliwa bila  ridhaa yangu. Nilipiga sana kelele lakini sikuuona msaada  wowote ukija mle ndani, nilienda mwisho nilikata tamaa ya  kutoka kabisa. 

Niliishi hapo kwa miezi miwili nikiwa sijui siku wala muda,  niliona jua likizama na kuchomoza. Madirisha yalikuwa  yamewekwa nondo ngumu na kioo hivyo hata ningefanyaje  nisingeliweza kufungua na kutoka, niliishia kufungua dirisha  na kuangalia mwanga wa jua tuu. 

Juma alipojisikia kufanya mapenzi alikuja na kunitumia vile  apendavyo yeye hadi pale anapokuwa ameridhika ndiyo  anaondoka, nilizoea maisha hayo hata nikawa silii hovyo tena  sababu tumaini la kuondoka hapo halikuwepo kabisa, sikumtaja  tena Mungu katika Maisha yangu sababu niliona hanisikii tena. 

Kufanywa bila kinga kulisababisha nipate mimba, nilimueleza  Juma Baro kuwa Mimi ni Mjamzito, alichukia sana akawa  ananiambia kuwa nimefanya makusudi wakati anajuwa fika  alikuwa akinifanya Bila kinga. Roho iliniuma sana akaniambia  atanipa vidonge nitoe ujauzito, sikuwa na pingamizi istoshe  sikupenda kuzaa na Mtu katili kama Juma Baro, Basi jioni  aliniletea vidonge nikameza, cha ajabu mimba haikutoka kabisa  wala sikuhisi maumivu yoyote yale wakati nilikuwa nikisikia  kuwa Mtu anapotoa Mimba anapata maumivu ya Tumbo ila kwangu  haikuwa hivyo kabisa, nilirudia kumeza kwa hasira yani  sikutaka kuwa na kiumbe cha Juma Baro. 

Asubuhi nilipoamka niliona damu kidogo sehemu nyeti ila  ilitoka bila maumivu yoyote. Juma alipokuja aliniuliza 

“Hivi umemeza vidonge wewe?” Aliniuliza kwa dharau sana kama  vile mimi nilikuwa nataka kuzaa na yeye 

“Ndiyo” nilimjibu kwa kifupi sana 

“Yaani umeze vidonge na uwe sawa hivyo, unanitania si ndiyo?”  Aliuliza Juma Baro, nilinyanyuka nikamsogelea bila woga

“Unafikiri nataka kuzaa na Mwanaume katili kama wewe? Ungejua  jinsi ninavyo kuchukia hata usingenisemesha, natamani hii  Mimba itoke kimiujiza” Nilisema kwa hasira mbele yake 

“Ok! Ngoja” Alisema Juma kisha alisogea mezani akachukua  vidonge kama vitano kisha akaniambia 

“Meza hivi vidonge mbele yangu vinginevyo nitaitoa hiyo mimba  kwa mikono yangu” Alisema kwa jazba, nilivichukua vidonge kwa  hasira sana kisha nikachukua maji na kuvimeza vyote 

“Ungejua natamani kufa kuliko kuendelea kuwa hapa, kama kuna  sumu nipe ninywe nife, bora kufa kuliko kuishi maisha  yaliyojaa mateso kama haya” Nilisema, Juma alinisogelea kisha  akaniuliza 

“Unataka kufa?” 

“Ndiyo! Kama siyo kunifunga mikono na miguu ningekuwa  nimeshaondoa Maisha yangu” Nilisema huku chozi likinimwagika 

“Nakurahisishia kazi” Alisema Juma, aliacha mlango wazi kisha  alitoka, niliketi kitandani, alirudi na Madawa ya kulevya 

“Tumia haya, dakika chache utakuwa umefika kwa Mungu wako”  Alinipatia kifuko kidogo sana kilichofungwa Unga huo,  kiukweli nilisema tu yale maneno ila kufa sikufikiria kabisa  niliamini ipo siku nitatoka pale, hivyo nilibakia nikiwa  nimesimama tu na kumtazama Mwanaume huyo kwa jinsi alivyoamua  kuwa katili wa Maisha yangu. 

“Unasubiria nini?” Vuta huo Unga, natumaini nitakaporudi  nitakuja kutoa maiti yako na kwenda kuitupa” Alisema Juma  kisha aliondoka zake na kunifungia mlango. 

Nilichoka sana nilijitupa kitandani, sikuwa na ujanja wala  sikujua nafanya nini, nilisikia mlio wa gari yake kisha geti  kufunguliwa akawa ameondoka zake, ilikuwa ni ngumu sana Mimi  kujuwa nipo wapi sababu dirishani niliona ukuta mrefu,  sikuona nje. Hata hivyo nilijiuliza kwa kelele nilizokuwa  napiga kama nyumba ile ingekuwa kwenye makazi ya Watu basi  wangenisikia na kunisaidia haraka sana. 

Ilikuwa ni wakati wa jua kuwaka, baadaye lilizima na giza  liliingia, mlio wa gari niliusikia kisha geti lilifunguliwa,  baadaye mlango wa chumba nilichopo ulifunguliwa, alikuwa ni  Juma Baro, aliponiona alinicheka, nilimtazama kwa hasira sana

“Nilijuwa utakuwa umeshakufa Jojo, nilijiandaa kukuchimbia  kaburi hapahapa nyumbani kwangu nikuzike, inaelekea una damu  kali sana hadi dawa hazikufanya kazi si ndiyo?” Aliuliza  nikiwa nimejilaza tu nikiwa namtazama, aliuchukua ule unga  wake kisha akaniambia 

“Ngoja nikuoneshe kitu” Alinifuata akanifunga miguu na mikono  yangu, yalikuwa ni maisha niliyoyazoea wala sikuwa mkorofi  hadi alipomaliza, nikawa siwezi kufanya chochote. Alitoboa  kifuko kisha akatoa unga kwa kutumia kidole chake 

“Usihangaike sawa?” Alisema, sikujuwa alikuwa anataka  kunifanyia nini, nilishtuka aliponikamata kichwa na  kunipakaza ule unga eneo la pua, nilihisi maluwe luwe ambayo  sikuwahi kuyahisi kabla, Niliona nyumba inageuka alafu mwili  ukawa unawasha sana 

“Unanifanyia nini Mshenzi wewe” Nilisema kwa sauti kavu  iliyotoka kwa nguvu sana nikaambatanisha na kelele 

“Shiii!” Alinitaka kunyamaza kisha aliniweka tena, basi  nililegea mno nikajikuta napoteza uwezo wa kufikiria. 

Alinifanyia huo mchezo kwa siku saba mfululizo hadi nilijiona  mdhahifu sana, kisha aliniacha. Cha ajabu ambacho  kilinishangaza nilijiona nakuwa na hamu ya kupakwa yale  madawa, nilikuwa nahisi mwili una baridi mno, nikawa  natetemeka mwili mzima na vipere vya msisimko vilikuwa  vikinitoka, kwa mara ya kwanza nilipata maumivu makali ya  tumbo kisha niliona mabonge ya Damu yakinitoka huku chini,  nilijisafisha ila mwili haukuwa na nguvu hata kidogo,  nilijuwa tu yale maumivvu yalitokana na mimba kuharibika. 

Aliponiletea chakula nilimwambia Juma Baro kuwa mwili wangu  ni dhahifu sana, alicheka tu kisha aliondoka zake, nahisi  alikuwa anajuwa alichokiwa akikifanya kwangu. Hali ile  iliendelea kwa wiki mbili mfululizo, siku moja alikuja  akanipa kifuko cha Madawa ya kulevya akaniambia 

“Tumia utakuwa sawa” Kutokana na jinsi nilivyokuwa natetemeka  na kuhangaika ilinibidi nikubali kutumia madawa ya kulevya,  basi nikawa naweka puani ndiyo najisikia unafuu na uchangamfu  wa hali ya juu sana. Nikawa na nguvu ila nikawa sipendi kula  chakula zaidi ya kupenda sana kuvuta yale madawa ambayo  alikuwa akiniletea kwa kunikadilia sana, siku nyingine  alikuwa haniletei hivyo nilishi kwa kuhangaika sana pale  chumbani na kuishiwa nguvu, nilikuwa napiga mlango kwa nguvu  ili aniletee madawa, nilijiona nimekuwa Mwanamke wa hovyo  sana.

••••••••••••••

Alitumia mwanya huo kunitumia kingono kisha ananiahidi kunipa  madawa ya kulevya, basi nilimpa penzi la kweli kabisa Juma  Baro kisha ananipa madawa ya kulevya na pombe, alipoona  nimekuwa Mtumwa akaniambia naweza kutoka na kwenda sebleni  kukaa, basi nikawa natoka chumbani naenda sebleni nakaa hapo  kwa muda fulani kisha narudi chumbani kwangu. Nilianza kuwa  mlevi wa pombe na madawa ya kulevya, siku nyingine Juma  alikuja chumbani kwangu na kuvuta pamoja na Mimi, tukawa  marafiki mno 

Nilijiona nimekuwa wa hovyo kuanzia mwili na akili yangu,  nikawa nawaza pombe, madawa ya kulevya na kufanya mapenzi tu.  Alikuwa akileta zile pombe kali sana! 

Nakumbuka siku moja ilikuwa Usiku, Juma alikuwa Chumbani  kwake na Mimi nilikuwa chumbani kwangu, alikuja haraka  chumbani kwangu akaniambia kuwa polisi wanakuja, nilishajenga  uadui na hao polisi kutokana na vitu nilivyokuwa natumia,  nilimuuliza 

“Tufanye nini sasa?” 

“Tuondoke hapa haraka” Alisema Juma Baro, mara moja alirudi  chumbani kwake na kuchukua Bastola yake, aliniambia nichukue  vitu muhimu. Tukaelekea getini, ikawa ndiyo mara yangu ya  kwanza kupunga upepo wa nje kwa zaidi ya mieizi mitano nikiwa  nafungiwa ndani tu, ile anafungua geti na kutoka alipigwa  risasi ya tumbo. Nilitupa vitu nilivyobeba kisha nikakimbilia  nyuma ya nyumba, huko nikapanda juu ya Ukuta huku majibizano  ya Risasi kati ya Juma Baro na polisi yakiwa yanaendelea,  nilichumpa hadi nje, niliangukia kwenye kifusi cha mchanga  ambacho kilinisomba kwa safari hadi chini ambako kulikuwa na  kama machimbo ya Mchanga hivi, eneo hilo lilikuwa kimya mno  alafu kulikuwa na pori, hakukuwa na nyumba yoyote eneo hilo,  taa zilikuwa zikiwaka kwa mbali sana. 

Niligeuka nilipotoka, nikaanza safari ya kukimbia kutoka pale  na kuzifuata taa ambazo zilionesha kuwa ni makazi ya Watu,  ujasiri ulinikamata kwa kiasi kikubwa ila tochi za polisi  zilinifuata porini, kelele za mbwa zilisikika huku ile milio  ya risasi ikiwa imekata kabisa nikajuwa tu lazima Juma Baro  atakuwa ameuwawa. 

Nilikimbia kwa umbali mrefu bila kupumzika ila baadaye  nilihisi nguvu zikiniisha, tochi za polisi sikuziona tena,  nilijitahidi kuendelea kukimbia ila baadaye nilianguka na  kujigonga kwenye mti. Nilipoteza fahamu zangu sikujuwa  kilichoendelea.

Fahamu ziliponirudia nilijikuta nikiwa kitandani, pembezoni  mwangu alikuwepo Baba mmoja na Mama mmoja ambao walikuwa  wakiniangalia sana. Sikujuwa hapo ni wapi na wale Watu ni  akina Nani, nilijaribu kujiinua ila maumivu ya kichwa  yalinizuia 

“Polepole Binti utakuwa sawa tu” Alisema Huyo Baba 

“Nipo wapi na nyie ni akina Nani?” Niliuliza huku nikiwa  ninawatazama 

“Upo sehemu salama sana, Naitwa Baba Nesha na Huyu ni Mama  Nesha” Alisema Baba huyo kisha Huyo aliyemtambulisha kama  Mama Nesha alisema 

“Jinsi ulivyokuwa katika hali mbaya sikutegemea kama ungeamka  na kujitambua, ulikuwa umepoteza fahamu kwa siku mbili”  Alisema, nilishtuka sana 

“Siku mbili?” Niliuliza kama vile sikusikia sawa sawa  alichokisema 

“Ndiyo, siku mbili” 

“Jumaa….” nilitaka kuuliza kuhusu Juma Baro ila  nilipokumbuka kuwa Mwanaume yule alikuwa Muuza Unga nikaacha 

“Leo ni Juma tatu Binti” alijibu Baba Nesha akihisi labda  nilitaka kuuliza ni Siku gani 

“Hapa ni Rufiji” 

“Rufiji?” 

“Ndiyo kwanini umeshangaa? Tulikukuta Shambani kwetu ndiyo  tukakuleta hapa Binti” Alisema Baba Nesha, nyumba yao ilikuwa  nzuri sana na ilionesha walikuwa ni Watu wenye uwezo mkubwa  kifedha. 

“Unaitwa Nani Binti na nini kilikusibu?” Aliuliza Baba Nesha  akionesha kuwa na hamu kubwa ya kutaka kujuwa, niliwaangalia  ikanijia akili ya ghafla kuwa nisijimalize sana maana  wanaweza kunichoma kwa polisi 

“Naitwa Jojo” nilijibu 

“Nini kimekusibu?” Aliuliza yule Mama 

“Sikumbuki chochote” Nilisema kisha walitazamana

“Pole sana basi taratibu utakuwa unarejesha kumbukumbu”  Nilikuwa na kovu upande wa kulia lililotokana na vurugu za  kule nyumbani kwa Juma Baro kipindi cha nyuma nililishika,  nililetewa Chakula lakini nilipokula nilitapika kutokana na  ile hali ya kutumia madawa ya kulevya kwa wingi. 

Walihisi labda ninaumwa, wakanitengenezea vyakula vilaini  sana ambavyo angalau nilikula kidogo, niliishi hapo kwa Baba  Nesha na Mke wake, walinichukulia kama Binti yao. Baba Nesha  alikuwa ni Mtu wa kusafiri safiri kwasbabu alikuwa ni dereva  wa Mabasi 

Ile hali ya kuhitaji Madawa ya kulevya ilianza kunitesa,  bahati nzuri wenyeji walikuwa wanywaji wa pombe hivyo angalau  nilijituliza kwa kunywa pombe kali, lakini japo nilitumia  pombe ila nilihisi mwili unakosa nguvu, nashikwa na baridi  mara kwa mara. 

“Unaumwa Jojo?” Aliniuliza Mama Nesha siku moja tukiwa jikoni “Hapana Mama nipo sawa” nilimjibu 

“Nakuona ukiwa hauna amani, unatetemeka utasemaje upo sawa  Jojo? Kama unajisikia homa basi nikupeleke Hospitali maana  usije zidiwa usiku na Baba Nesha hayupo ikawa shida” Alisema  Mama Nesha akiwa anaendelea kupika, mimi nilikuwa nimekaa tu 

“Hapana Mama usijali nipo sawa tu” nilimwambia 

“Haya! Ila Jojo tunakutendea vizuri hapa nyumbani?” 

“Ndio Mama, siku 17 nilizokaa hapa naona nipo nyumbani,  nashukuru sana nina amani ya Moyo wangu” Nilimwambia huku  vipele vikianza kunitoka yaani vile vya msisimko wa kuhitaji  madawa na hivyo ndivyo nilivyokuwa nikijisikia. 

“Haya Nenda kapumzike” Alisema Mama Nesha ila kwa jinsi  nilivyokuwa najisikia niliona bila kupata Madawa ya kulevya  ningekuwa katika hali mbaya zaidi baada ya masaa kadhaa  mbele. 

“Mama naenda Dukani kununua Juisi” Nilisema 

“Haya Jojo” Alijibu Mama Nesha, ila akili yangu ilijuwa  nataka kufanya nini, kuna hela ambayo aliniachia Baba Nesha  kama Elfu 40 niliona ni bora niutumie muda huo kutafuta  Madawa ya kulevya. Nilikumbuka kuna sehemu Niliambiwa  nisipite na Mama Nesha kwasababu Watu wa hapo ni wahuni  wavuta Bangi hivyo nilijuwa tu nikienda huko nitapata madawa kirahisi mno, kingine nilishazijuwa mbinu na mameno ya  kuzungumza ambayo Wahuni wangemielewa kwa haraka sana. 

Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko,  kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada ya  kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayo  Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwa  kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza unga  pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadi  hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20  kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutuliza  kiu yangu. 

“Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlango  ukifunguliwa 

“‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisi  ili kusiwe na maswali  

Nini Kitaendelea?

Usikose SEHEMU YA SITA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM  

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

 

 Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx

5 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version